COSTECH WAASWA KUHAKIKISHA TAFITI ZINAZOFANYWA ZIJIKITE KUTOA MATOKEO YANAYOTATUA MATATIZO.

August 23, 2016



Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
TUME ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeaswa kuhakikisha tafiti zinazofanywa zijikite katika kutoa matokeo yatakayoweza kutatua matatizo ya wananchi na kuendelea kutengeneza ajira ili kuinua kipato cha wananchi na uchumi wetu kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako wakati wa kuzindua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Katika Kutekeleza agizo la Uchumi wa viwanda tunategemea rasilimali watu yenye ufahamu, ujuzi, teknolojia na ubunifu ili kuzalisha kwa tija na kuhimili ushindani wa kimataifa. 

Profesa Joyce amesema kuwa Tafiti zilenge katika kuimarisha uchumi wa viwanda zikiwa ni muhimu katika kuinua tija na uzalishaji, 
 “Baadhi ya tafiti za Kilimo zilizofanywa na taasisi zetu kama vile Chuo Kikuu cha Sokoine zimefanikiwa kutoa matokeo mazuri. Hii inajumuisha mbegu bora zinazoongeza mavuno kama vile mbegu za mihogo, mahindi na mpunga ambazo zinavumilia ukame na zinaweza kukinzana na magonjwa”. Amesema Profesa Joyce. 

Aidha amewaomba wakamilishe mapema taratibu zinazohitajika ili watanzania wengi waweze kunufaika na chanjo hizo muhimu kwa wafugaji wa kuku.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan Mshinda amesema kuwa tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeweza kupata  chanjo inayozuia magonjwa ya kuku kama vile mdondo, ndui na mafua katika chuo Kikuu cha Sokoine .
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan Mshinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu  jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa sayansi wakati wa kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Tume ya Sayansi Afrika Kusini, Tami Mseleku akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako kulia akiwa katika ufunguzi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifujijini Dar es Salaam leo.







 Baadhi ya wanasayansi wakiwa katika kongamano la wanasayansi jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akitembelea maonesho ya wanasayansi mara baada ya kufungua  Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifujijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako  akipata maelekezo juu ya kifaa kinachopiga picha za Juuu(Drone) jijini Dar es Salaam leo mara baada kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako  akipata maelekezo katika  banda la wanasayansi jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
TFF YAIANDALIA SERENGETI BOYS KAMBI TULIVU

TFF YAIANDALIA SERENGETI BOYS KAMBI TULIVU

August 23, 2016
Baada ya kutekeleza ahadi ya mwanzo ya kuipeleka Madagascar kwa ajili ya kambi ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepanga kutekeleza ahadi yake nyingine kwa kuipeleka timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kwenye kambi tulivu, ikiwezekana nje ya nchi.
Rais Malinzi aliahidi na kutekeleza ahadi yake kuipeleka Madagascar Serengeti Boys baada ya kuitoa Shelisheli katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Madagascar, mwakani. Kadhalika aliahidi kuipeleka timu hiyo nje ya nchi ambayo hata hivyo haijateuliwa baada ya kuindoa Afrika Kusini. Ameahidi kambi hiyo itaanza Septemba mosi, mwaka huuu.

Serengeti Boys ilipiga kambi Hosteli za TFF, zilizo Karume kwa wiki moja kabla ya kuhamia Hoteli ya Urban Rose, katikati ya jiji la Dar es Salaam ambako ilivunjwa kwa muda jana Agosti 22, 2016 ambako vijana wamekwenda makwao kusalimia ndugu zao na itaitwa mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya maandalizi ya kambi ya nje ya nchi.
Serengeti Boys imebakiwa na mtihani mmoja kufuzu kucheza fainali hizo kwa kucheza na Congo – Brazaville na mchezo wa kwanza utafanyika Dar es Salaam, Septemba 18, 2016 kabla ya kurudiana Septemba 30, 2016, Oktoba 1 au Oktoba 2, 2016.
TFF imejipanga kwa ajili ya kambi hiyo, na kinachosubiriwa kwa sasa ni mapendekezo ya makocha ili shirikisho itekeleze hatua hiyo ya kambi ya utulivu.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi amesema kwamba anaamini kuwa mchezo ujao utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu nitajipanga kuvuka ili kucheza fainali hizo.

MBUNGE WA ILEJE JANET MBENE ATAKA WALIOKULA FEDHA ZA MRADI WA HOSPITALI WACHUNGUZWE

August 23, 2016
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene, akiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo  akikagua sehemu ya juu ya jengo jipya la Hospitali ya Wilaya ya Ileje Ksata ya Itumba inayojengwa kwa pesa za Serikali ya Tanzania

 Mganga mkuu wa Hospitali ya  Ileje akitoa maelezo kwa  Mbunge wa Jimbo hilo Mh Janet Mbene alipokuw akaikagua ujenzi wa jengo jipya la Hospitali hiyo
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akitoa pole katika wodi ya Wanawake amabao walibahatika kujifungua kwa Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje.
  Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akitoa pole katika wodi ya Wanawake amabao walibahatika kujifungua kwa Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje.

Tigo yaanzisha mkakati wa huduma kwa jamii nchi nzima katika msimu wa Fiesta 2016

August 23, 2016

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwiru Mkoani Mwanza wakiwa wamekalia madawati 60 waliyopewa na kampuni ya Tigo,wakati wa hafla iliyofanyika jana.



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(wa tatu kulia) akimpa mkono Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya,kwenye hafla ya kukabidhi madawati 60 kwa Shule ya Msingi Bwiru jana.



•Shule 9 za msingi Mwanza zapokea madawati 385
Mwanza, Agosti 19, 2016:   Kampuni ya Simu ya Tigo Tanzania leo  imeanzisha rasmi  mkakati wake wa nchi nzima wa kutoa huduma kwa jamii  kwa kuchangia madawati 385  yenye thamani ya shilingi milioni 64 kwa shule tisa za msingi mkoani Mwanza  ambayo  yatazinufaisha shule za msingi katika wilaya za  Ukerewe, Nyamagana, Ilemela na Sengerema wakati wa msimu wa tamasha la Fiesta 2016 mkoani Mwanza
Kukabidhiwa kwa madawati hayo mkoani Mwanza ni matokeo ya juhudi zinazoendelea za Tigo za kuwekezaq katika  elimu na hususani katika kupunguza uhaba wa madawati  katika shule za msingi za umma nchi ambapo  mikoa 18 itanufaika katika msimu wa Fiesta 2016. Ikumbukwe kwamba kwa mwaka huu  kampuni imeshachangia madawati 5,700 kote nchini na hivyo kuwa imewakalisha wanafunzi 17,000 ambao awali walikuwa wakikaa sakafuni.
Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’
Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo  zilizofanyika katika Shule ya Msingi Bwiru Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya, alisema  uhaba wa madawati katika shule za msingi unajulikana kama moja ya sababu zinazoathiri kujifunza  pamoja na ufanisi wa wanafunzi  katika  shule zetu nyingi za msingi.
“Tumejikita katika kuhakikisha kuwa mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi yanaboreshwa  na tunayofuraha  kwamba Tigo inabadilisha kizazi cha baadaye  am,bacho ni wanafunzi katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai chini tena. Tunaamini  kwamba msaada huu utaenda mbali katika kuwasadia wanafunzi kuzifikia ndooto zao za kuwa viongozi wa baadaye kutokana na kuondoka kwa bughudha  na hivyo kujikita katika masomo,” alisema Maswanya.
Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ambaye alisema kuwa madawati 385 yataboresha kwa kiwango kikubwa  mazingira ya kujifunza  kwa watoto katika mkoa huo  na kuwataka  watu wengine wenye mapenzi mema  kujitokeza  na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mkoa huo.
Mongela alizitaja shule zitakazopokea madawati hayo na idadi katika mabano kuwa ni  Nakoza (29), Uhuru (40), Busangu (41), Bukongo (30), Nansio (30), Namagubho (30), Mkuyuni (65) Chambanda (60) na Bwiru (60) .
“Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza kiasi cha uhaba wa madawati katika shule za msingi mkoani Mwanza. Tunaamini  madawati haya 385  yatatufikisha mbali  katika  kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio  katika elimu yao,” alisema Mongela.

Hati za viwanja vya Bayport zaendelea kutolewa kwa wahusika

August 23, 2016
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akimkabidhi hati mteja wao Mary Simon, baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinapatikana kwa njia ya fedha taslimu na mikopo maalumu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Kulia ni Meneja Mikopo wa taasisi hiyo, Nasibu Kamanda. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Wateja wa Bayport wafurahia hati zao za viwanja

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana imeendeleza utaratibu wake wa kugawa hati kwa wateja wao walionunua viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa njia ya mikopo na fedha taslimu.

Mradi huo wa Vikuruti ulizinduliwa mwaka jana, ambapo baada ya kufanikiwa kwake, taasisi hiyo ikaanzisha miradi mingine mitano ambayo ni Kigamboni, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha na Kilwa, huku ikiweka utaratibu rahisi na nafuu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, alisema kwamba kugawa hati kwa wateja wao ni mwendelezo wa huduma nzuri zinazotolewa na taasisi yao kwa ajili ya kuwakomboa wananchi katika suala zima la ardhi.

Alisema kwamba makubaliano yao ni kuhakikisha taasisi inasimamia sualaa la hati ili wateja wao wasisumbuke kutokana na mchakato mzima wa utendaji kazi wao unaotoa urahisi juu ya upatikanaji wa viwanja vyao vyenye hati.

“Tunaendelea na kutoa hati kwa wetu walionunua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, ambapo Watanzania wengi walichangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo, ambavyo ukiacha vya Vikuruti, wateja wetu pia wanaweza kukopa fursa hii ya ardhi kwa miradi yetu ya Kimara Ng’ombe (Bagamoyo), Msakasa (Kilwa), Tundi Songani (Kigamboni), Boko Timiza (Kibaha), Kibiki na Mpera (Chalinze) na Kitopeni (Bagamoyo).
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akizungumza jambo baada ya kumkabidhi hati mteja wao Mary Simon kushoto baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Mikopo wa Bayport Financial Services, Nasibu Kamanda.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services katikati akisisitiza jambo.
Mteja wa Bayport Financial Services Sixtus Kilenga kushoto akisaini kama sehemu ya kukabidhiwa hati ya kiwanja. Hati hizo kwa wateja walionunua viwanja vinavyopatikana kwa njia ya mkopo na fedha taslimu zinaendelea kutolewa kwa waliokamilisha taratibu zao.


Naye mteja wa Bayport aliyopewa hati yake, anayejulikana kwa jina la Mery Simon Anthony aliipongeza Bayport kwa kutoa huduma nzuri kiasi cha kumfanya amiliki kiwanja chenye hati, huku kikiwa hakina mlolongo wowote.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu nimepata hati yangu kwa haraka na sijapata usumbufu wowote, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi katika miradi hii ya viwanja vya Bayport kwa sababu ni rasilimali nzuri,” Alisema.

Naye Sixtus Francis Kilenga alisema kwamba amefurahishwa na utaratibu mzima wa kupata kiwanja chenye hati, huduma zinazotolewa na Bayport, ambapo mteja hana jukumu lolote la kufuatilia hati katika maeneo yanayohusika.

“Utaratibu wa kununua kiwanja kasha ukapewa hati bila kufuatilia wizarani ni mpya, hivyo binafsi nimeufurahia na unaweza kuifanya Bayport kuwa moja ya ofisi zenye kujali muda na gharama za kiutendaji wa wateja wao,” alisema.

Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo ya bidhaa ikiwamo viwanja pamoja na fedha taslimu isiyokuwa na amana wala dhamana, huku taasisi hiyo ikiwa na matawi zaidi ya 82 nchi nzima kwa ajili ya kuwapatia Watanzania huduma bora.