UKOSEFU WA MALEZI BORA UMECHANGIA MATUKIO YA UFISADI NCHINI

April 05, 2018


Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Baraza la Waislamu BAKWATA Mkoa wa Tanga Shk Hassan Kabeke wakati wa uzinduzi wakampeni ya baba bora iliyofadhiliwa na ubalozi wa Swedeni kwa kushirikiana na madhehebu ya dini nchini kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga akizungumza kwenye halfa hiyo kushoto ni Balozi wa Swedeni nchini Katarina Rangnitt na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Baraza la Waislamu BAKWATA Mkoa wa Tanga Shk Hassan Kabeke
Balozi wa Swedeni nchini Katarina Rangnitt katikati akimsikiliza kwa umakini Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga kulia akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa uzinduzi huo

Sehemu ya wadau walioshiriki uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa YDCP Jijini Tanga
Sehemu ya wanahabari walioshiriki kwenye uzinduzi huo




IMEELEZWA kuwa kuongezeka kwa vitendo vya ukatili pamoja na matukio yauhalifu na ufisadi nchini inatokana na jamii kusahau swala la malezibora hususani katika ngazi ya familia.

Hayo yameelezwa hapo jana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Baraza la Waislamu BAKWATA Mkoa wa Tanga Shk Hassan Kabeke wakati wa uzinduzi wakampeni ya baba bora iliyofadhiliwa na ubalozi wa Swedeni kwa kushirikiana na madhehebu ya dini nchini.

Alisema kuwa shida zote za kimaadili zinazoendelea kulikumba taifa kwa sasa zinatokana na jamii kusahau jukumu lake la malezi na kuachiwa mtu mmoja pekee ambaye ni mwanamke.

“Jamii bado inaendelea kuteseka katika ufisadi na maovu mengine sasa imefika wakati wa baba nae kuhakikisha nachukuwa nafasi yake katika malezi ili kujenga watoto wenye tabia njema”alisema Shk Kabeke.

Kwa upande wake Balozi wa Swedeni nchini Katarina Rangnitt alisema kuwa kampeni hiyo imelenga katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika jamii kuhusu malezi kupitia viongozi wa dini.

“Kupitia maonyesho ya picha naamini watu wataweza kujadili zaidi maanaya kuwa baba bora kwa kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wao kwani inafaida kubwa “alisema Balozi huyo.

Alisema kuwa viongozi wa dini wanaushawishi mkubwa katika maswala hayo na wanaweza kuchukuwa jukumu la pekee katika kufikia na kuendeleza haki za kijinsia kwa wababa katika malezi .
Hata hivyo Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga alisema kuwa wababa wa Tanzania wanafikiri kuwa ubaba ni kutoa mahitaji muhimu pekee wakati kwa uhalisia ni zaidi ya hivyo.

Alisema kuwa kuwa baba bora ni kuhakikisha unakuwa tayari kujitolea nakuwekeza muda wako katika malezi ya watoto na sio kuhusu unachofanya pekee.

Kampeni ya baba imezinduliwa rasmi katika mkoa wa Tanga ambapo itajumuisha maonyesho ya picha ya wababa wa kitanzania na kiswidiinatoa fursa nyingine kwa baba kuonyesha nafasi yao katika malezi ya watoto.

RAIS DK. SHEIN AZINDUA KONGAMANO LA KUMBUKUMBU YA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR

April 05, 2018
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya wakati alipofika kuzindua Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo Bububu Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alipofika kuzindua Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo Bububu Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapungia mkono waalikwa alipofika kuzindua Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu Wilaya ya Mmagharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,(kushoto) Mkuu wa Mkoa Mjini Mahgaribi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mohamed Aboud Mohammed (wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) na Mkuu wa Zanzibar,wakisimama wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu.

Viongozi walioshiriki katika Uzinduzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu.


Baadhi ya Vijana walioshiriki katika Uzinduzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu ambalo limezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)

Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo Bububu Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza jambo wakati akizindua kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo Bububu Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Picha na Ikulu

LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 1 MWAKA HUU

April 05, 2018



Timu 28 zinatarajia kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL))msimu wa 2017/18 inayotarajia kuanza Mei 1,2018 mpaka Mei 16,2018 kwenye vituo vinne.

Vituo vitakavyotumika ni Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro.

Makundi ya RCL yatakuwa na timu saba kila kundi yakipangwa kwa kufuata Jiografia ya kikanda katika soka.

Mwisho wa kuwasilisha jina la Bingwa wa Mkoa ilikua Machi 30, 2018 ambapo mikoa yote 26 iliweza kutimiza ndani ya muda huo uliowekwa na TFF.

Mikoa iliyothibitisha mabingwa wao wa RCL watakaocheza ligi hiyo msimu huu :

1. Dar Es salaam (Karume Market, Ungindoni FC, Temeke Squard)

2. Pwani (Stand FC)

3. Morogoro (Moro Kids)

4. Dodoma (Gwassa Sports Club)

5. Singida (Stand Dortmund)

6. Tabora (Tabora Football Club)

7. Kigoma (Red Stars FC)

8. Geita ( Gipco FC)

9. Kagera (Kamunyange FC)

10. Mwanza (Fathom Sports Club)

11. Mara (Nyamongo Sports Club)

12. Shinyanga (Zimamoto FC)

13. Simiyu (Ambassador FC)

14. Arusha (Bishoo Durning Sports)

15. Manyara (Usalama Sports Club)

16. Kilimanjaro (Uzunguni FC)

17. Tanga (Sahare All Stars)

18. Lindi (Majimaji Rangers)

19. Mtwara (Mwena FC)

20. Ruvuma (Black Belt)

21. Njombe (Kipagalo FC)

22. Songwe (Migombani FC)

23. Mbeya (Tukuyu Stars)

24. Iringa (Iringa United)

25. Rukwa (Laela FC

26. Katavi (Watu FC)

27.Manyara ()Usalama FC)

Mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Tabora kuna malalamiko ya vilabu kupinga mabingwa wa mikoa, malalamiko ambayo TFF inaendelea kuyafanyia kazi.



Kundi A (GEITA)

Geita, Kagera, Mara, Mwanza,Shinyanga, Simiyu, Dar 2



Kundi B (RUKWA)

Rukwa,Katavi, Kigoma, Tabora, Ruvuma, Songwe, Mbeya



Kundi C (SINGIDA)

Singida,Dodoma,Iringa, Njombe, Dar 3, Lindi, Mtwara



Kundi D (KILIMANJARO)

Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Manyara, Pwani, Morogoro, Dar 1
MAANDALIZI YA UZINDUZI WA UKUTA KUZUNGUKA MIGODI YA TANZANITE MEREARNI YAKAMILIKA

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA UKUTA KUZUNGUKA MIGODI YA TANZANITE MEREARNI YAKAMILIKA

April 05, 2018

Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla ya kikao cha majumuisho kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akipokelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla ya kikao cha majumuisho kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florence Turuka wakati wakikagua maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (wapili kutoka kushoto) akikagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kufanyika tarehe 6 Aprili 2018.



Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (wapili kutoka kushoto) akikagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kufanyika tarehe 6 Aprili 2018.

\

Sehemu ya Majukwaa yatakayotumika wakati wa uzinduzi wa ukuta unaouzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa tarehe 6 Aprili 2018 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.



Mafundi wakiwa katika hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.



Mmoja wa mafundi akiendelea na kazi ya kuandaa eneo litakapowekwa jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.



Sehemu ya geti la kuingia katika eneo la mgodi wa Tanzanite kama inavyoonekana katika picha.



Kanali Mtaula akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa ukuta wa kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara kwa viongozi mbalimbali akiwemo Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Florence Turuka na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Saimon Msanjila, unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.

Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexandar Mnyeti unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.


( Picha zote na Maelezo , Manyara
MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI

MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI

April 05, 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma.

……………..

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi kuwaweka ndani madereva wanaosababisha ajali kutokana na mwendo kasi na baadaye kupelekwa Mahakamani.

Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu muongozo wa Mbunge wa Ulanga Morogoro Mhe. Goodluck Mlinga, juu ya chanzo cha ajali ya basi la City Boy kutoka Karagwe Mkoani Bukoba kuelekea Dar es Salaam ambalo liligongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga usiku wa Aprili 04 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 12.

“Hatuwezi kuacha watu wanapotea kwa ajili ya uzembe wa mtu mmoja na kuleta hasara na vilio vikubwa kwa Watanzania,” alisema Dkt. Mwigulu.

Amesema, ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasabishwa na mwendokasi na sio tatizo la miundombinu ambapo katika ajali zilizoripotiwa ajali 1500 zilisababishwa na mwendo kasi na ajali 89 zimetokana na miundombinu.

Aidha Dkt. Mwigulu amesema, Tanzania ni moja ya nchi zenye barabara bora hivyo ajali nyingi zinazotokea husababishwa na uzembe wa madereva pamoja na mwendokasi.

Wakati huohuo bungeni hapo, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali imeweka utaratibu mashuleni wa kuwawezesha watoto wa kike kuripoti matukio ya udhalilishaji na pia imeanzisha klabu mbalimbali za kuwajenge uwezo na ujasiri wa kuweza kuripoti matukio ya udhalilishaji.

Hata hivyo Prof. Ndalichako amewataka watoto kutokuwa na uwoga wowote kwa sababu Serikali yao inawalinda, hivyo pale wanapofanyiwa vitendo kinyume na matakwa ya Serikali watoe taarifa ili Serikali ichukue hatua stahiki kwa wale wote wanao wadhalilisha na kusababisha watoto wasisome kwa amani.
WADAIWA SUGU WA MADENI YA “COMMODITY ORT SUPPORT (CIS) WATAKIWA KULIPA MADENI YAO NDANI YA SIKU 30

WADAIWA SUGU WA MADENI YA “COMMODITY ORT SUPPORT (CIS) WATAKIWA KULIPA MADENI YAO NDANI YA SIKU 30

April 05, 2018





TANGAZO KWA WADAIWA SUGU WA MADENI YA “COMMODITY IMPORT SUPPORT (CIS)

Katika miaka ya 1980 hadi 2000 Wahisani walitoa fedha za kigeni kwa Serikali ya Tanzania kwa mpango maalum uliofahamika kama “Commodity Import Support (CIS)” kwa lengo la kuipa Serikali uwezo wa kuimarisha uchumi kwa kuzipatia Taasisi, Makampuni, Viwanda na wafanyabiashara uwezo wa kuagiza bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi, kwa kuwa wakati ule nchi ilikuwa na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni.

Fedha za msaada za CIS zilitolewa kama mkopo wenye masharti nafuu kwa wanufaika, ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba katika kipindi cha miezi 18. Kwa mujibu wa sheria ya CIS {The Commodity Import Support Regulation Act, CAP 261 R.E. 2002 (S. 8 (1) (b)}, mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asilimia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania inapoikopesha Serikali (discount rate) katika kipindi husika. Zaidi ya makampuni 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huu. Pamoja na juhudi kubwa iliyofanywa na Serikali ya kuwataka wakopaji wote kurejesha mkopo huo, ikiwa ni pamoja na tangazo la tarehe 30 Desemba, 2015, bado urejeshaji wa mikopo hiyo umekuwa sio wa kuridhisha.

Ili kuhakikisha wadaiwa wote wanalipa mikopo yao, Serikali imeunda Kikosi Kazi ambacho kinajukumu la kufuatilia na kukusanya madeni toka kwa wadaiwa wote ili fedha hizo ziweze kutumika kwa miradi ya maendeleo. Serikali inawataka wadaiwa wote kulipa madeni hayo ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili. Kwa wote ambao hawatarejesha mikopo hiyo katika kipindi cha siku 30, majina yao yatatangazwa katika vyombo vya habari na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Kikosi Kazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam, chumba Na. 352, Simu Na. +255 739 40 30 25.

“FEDHA ZA UPANUZI WA VITUO VYA AFYA ZIFANYE ZAIDI YA KAZI ILIYOTARAJIWA”, RC GALLAWA.

April 05, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na mafundi wanaojenga katika kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na baadhi ya watendaji na wananchi wa kijiji cha Iyula waliojitokeza katika eneo la ujenzi katika kituo cha Afya cha Iyula Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.

Grace Gwamagobe-Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu fedha zilizotolewa na serikali mkoani humo kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.

Gallawa ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi alipokagua maendeleo ya upanuzi wa vituo vya afya vya Isansa kilichopokea milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula Kilichopokea milioni 400, kwa ajili ya ujenzi wa maabara, nyumba ya daktari, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.

“Fedha hizi lazima zifanye kazi iliyopangwa vizuri na pia tuongeze kazi nyingine ya ziada kutokana na kuwa tumepata nguvu ya wananchi lakini pia mafundi wetu hawa tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo ya kwetu kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza kazi nyingine”, amesema Gallawa.

Ameongeza kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza bado ana Imani kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.

Gallawa amesema kukamilika upanuzi wa vituo hivyo vya afya kutavifanya vituo hivyo vivutie na hata mgonjwa akifika apate matumaini ya kupona na sio kukatishwa tamaa na hali mbovu ya mazingira.

“Tiba ya kwanza ya mgonjwa akifika kituo cha afya akute mazingira yanavutia na sio majengo mabovu na uchafu hivyo vitamfanya akate tamaa ya kupata matibabu sahihi, tukimaliza ujenzi wa hayo majengo tutahakikisha tunapaka rangi paa za majengo yote zifanane ili vituo vyetu vya afya vivutie”, amefafanua Gallawa.

Aidha Gallawa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Lauteri Kanoni kuhakikisha anaweka mfumo wa maji safi katika vituo hivyo hasa mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili vituo vikikamilika maji yawepo kwa ajili ya matumizi.

Naye Mkazi wa kijiji cha Isansa Wilaya ya Mbozi Bi Stela Mkeya ameonyeshwa kufurahishwa na upanuzi wa kituo cha Afya Isansa huku akieleza baadhi ya kero walizokuwa wakizipata awali.

“Tunaishukuru sana serikali ya Magufuli kwakweli wametusaidia, tulikuwa tunapata shida kufuata huduma za upasuaji wa akina mama wajawazito huko hospitali ya Wilaya iliyopo Vwawa lakini pia hapa kwenye kituo cha afya mzazi akijifungua hata mazingira ya kwenda kujisafisha vizuri kama vile mabafu yakiwa hayatoshi kabisa”, ameeleza Bi Mkeya.

Kwa upande wao mafundi waliokabidhiwa kazi ya upanuzi wa vituo hivyo vya Afya wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na haraka huku wakimuomba Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa awasaidie upatikanaji wa taa ili waweze kufanya kazi mchana na usiku naye Mkuu wa Mkoa amekubaliana na mapendekezo hayo.

MWALIMU RUFIJI ASHINDA PASAKA MZUKA JACKPOT YA MILIONI 260

April 05, 2018


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar wakati wa kumtambulisha mshindi Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga (Kulia) na kumpongeza kwa ushindi mkubwa wa kujishindia kiasi cha Shiling Milion 260. Kushoto ni Mkaguzi kutoka michezo ya Bahati Nasibu Bakari Maggid.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 260 kwa mshindi wa Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga .

Mshindi wa Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msengi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutambulishwa na kushukuru kwa kupata fedha hizo na kuwataka watanzania waamini kuwa mchezo huo unatenda haki.

Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini leo umetangaza na kumtambulisha kwa wana habari mtanzania aliyebahatika kushinda milioni 260 kwenye Pasaka Mzuka Jackpot ambayo ilionyeshwa mubashara kupitia ITV, Clouds TV na TV 1 jumapili ya Pasaka.

Edward Msengi (56), ambaye anatokea Rufiji, Pwani ndiye aliyebahatika kuondoka na kitita cha shilingi milioni 260 ambayo ni jackpot kubwa kuwahi kutolewa kwa mshindi mmoja katika nchi hii.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alimtambulisha mshindi na kumpongeza kwa ushindi huo mkubwa. “ Sisi Tatu Mzuka tunayo furaha kiasi kwamba tumeamua kumleta mshindi Dar es salaam ili kushiriki pamoja nanyi katika tukio hili kubwa” . Msengi ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Singida na baba wa watoto wanne alikuwepo kudhihirisha furaha yake na kuhadithia safari yake aliyopitia mpaka kushinda kitita kikubwa cha milioni 260.

“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama ningeweza kupata fursa kubwa kama hii. Ninategemea kujenga nyumba nzuri kwa ajili ya familia yangu na kuwekeza katika biashara pamoja na kuhakikisha kwamba watoto wangu wote wapo katika shule nzuri” alisema Bwana Msengi

Mbali ya tukio hilo adhim,Maganga aliufahamisha umma juu ya ujio wa kampeni ya mwezi April ijulikanayo kama Mzuka FULL CHARGE.

“Maisha ni kusaidiana ndio maana unaposhinda Tatu Mzuka na kuwa ‘FULLCHARGE’; tunakupa fursa ya kumbusti mtu mwingine ambaye utamchagua. Shinda milioni 6 kila saa na upate nafasi ya kuingia kwenye jackpot ya milioni 10 kila siku na milioni 60 jumapili hii ili umbusti yoyote unayemtaka”

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

JUMUIYA YA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA MKOA WA DAR ES SALAAM, YAADHIMISHA KWA KISHINDO MIAKA 63 YA KUANZISHWA KWA UMOJA HUO. KOMREDI MPOGOLO ANOGESHA KONGAMANO LA MAADHIMISHO HAYO, KATIKA UKUMBI WA MWALIMU NYERERE, LEO.

April 05, 2018




Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) Cheti cha Skurani kutoka Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo, wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 63 ya Umoja wa Wazazi Tanzania, lililoandaliwa na Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, leo


MWANZO⤋



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akishuka katika gari lake baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, kuadhimisha miaka 63 ya kuzaliwa Umoja wa Wazazi Tanzania.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akikaribishwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa wa Mikutan wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akisalimiana na Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akisindikizwa na viongozi kwenda ukumbini baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe, na kutoka kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa huo Lugano Mwafongo na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Kate Kamba



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akipata maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha baada ya kuwasili katika chumba cha Wageni maarufu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.



Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo (kushoto) akiwa na Katibu wa CCM mkoa huo Saad Kusilawe wakati wa mazungumzo hayo.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwaunga mkono wajumbe waliokuwa wakimshangilia baada ya kuwasili ukumbini kwenye Kongamano la miaka 63 ya kuzaliwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoandaiwa na Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa dar es Salaam Frank Kamugisha.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwa na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, tayari kushiriki kongamano hilo



Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Mwinyimkuu Sangaraza akifungua pazia la kongamano hilo kwa kufanya utambulisho



"Jamani sare maalum ya sherehe hizi ilichelewa kidooogo, lakini ninayo imeshafika hii hapa" akasema Sangaraza na kuwaacha wajumbe na mgeni rasmi wakicheka



Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala akisalimia baada ya kutambulishwa



Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam wakisalimia baada ya ktambulishwa. Kutoka Kushoto ni Katibu wa Uchumi na Fedha habib Nasser, Mwafongo na Kamugisha



Wazee wa Jumuiya ya Umoja wa wazazi mkoa wa Dar es Salaam (mstari wa mbele) wakiwa kwenye kongamano hilo



Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo akizungumza kwenye kongamano hilo.



Wajumbe wakimshangilia Mwanfongo wakati akifanya utambulisho



Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Jumiya ya Umoja huo Mzee Mkali akisalimia baada ya kutambulishwa



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha akitoa nafasi ya kufanywa dua na maombi kabla ya kongamano kuanza rasmi



Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akiomba dua kabla ya kongamano kuanza



Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akiomba dua kabla ya kongamano kuanza



Wajumbe wakipokea dua ya Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) kabla ya kongamano kuanza



Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira wa Jumiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Wilson Tobola akisoma maombi kabla ya kongamano hilo kuanza



Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo akisoma taarifa ya maadhimisho ya miaka 63 ya Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania wakati wa Kongamano hilo



Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo akimkabdhi taarifa hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo baada ya kuisoma



Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Beatrice Mandia akizungumzia maadili wakati wa kongamano hilo



Katibu wa Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Habib Nasser akitangaza Wajumbe wa Baraza la Uchumi na fedha kwenye kongamano hilo



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana mkoa wa Dar es Salaam akisalimia



Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam ndugu Busolo akizungumza kwenye kongamano hilo



Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Mkali akizungumza kwenye kongamano hilo



Vijana wa Vyombo vya Habari vya CCM Jumanne Gude wa Gazeti la Uhuru na mwenzake kutoka Uhuru FM wakiwa makini wakati wakichukua taarifa kwenye kongamano hilo



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate kamba akizungumza katika kongamano hilo



Mwenyekiti wa Jumuiya wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza kwenye kongamano hilo



Baadhi ya wajumbe ukumbini



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akizungumza na wajumbe wakati wa kongamano hilo



Baadhi ya wajumbe ukumbini



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) Cheti cha Skurani kutoka Jumuiya ya Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo, wakati wa Kongamano hilo.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) Cheti cha pongezi kutoka Jumuiya ya Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kongamano hilo



Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akifurahia baada ya kupewa Cheti cha Skurani kutoka Jumuiya ya Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Doto Msawa Cheti cha Skurani kutoka Jumuiya ya Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali, anayekabidhiwa ni katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali, Anayekabidhiwa ni Ndugu Busoro



Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam akimpongeza Busoro



Frank Nkinda (kulia) ambaye ni Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwa ukumbini



Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akizungumza kutoa neno la shukurani mwishoni mwa kongamano hilo


PICHA ZA PAMOJA⇩













Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiagana na wajumbe baada ya kongamano hilo



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiagana na Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) mwishoni mwa kongamano hilo.



Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe (kushoto) akiondoka ukumbini mwishoni mwa kongamano hilo la Maadhimisho ya miaka 63 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Wazazi Tanzania, lilioandaliwa na Jumuiya ya Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO -- Best regards Bashir Nkoromo Blogger & Photojournalist UHURU PUBLICATIONS LTD Dar es Salaam, TANZANIA Cell: +255 712 498008, +255 789 498008, BLOG: theNkoromo Blog Email: nkoromo@gmail.com