DIWANI WA CUF TANGA AJISALIMISHA CCM KWENYE MKUTANO WA HADHARA JIJINI TANGA.

September 02, 2014
Diwani wa Chama cha Wananchi (CUF) kata ya Marungu jijini Tanga,Bakari Mambea aliyejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano mkoani Tanga wa pili kutoka kushoto akiwa anaongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdallah Bulembo wa pili kulia akila kiapo cha utii kujiunga na viongozi wa CUF waliojiunga na chama hicho kulia ksuhoto kwake ni Mwenyekiti wa CUF mtaa wa makoko jijini Tanga Abubakari Nguli naye alijiunga na chama hicho,wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Gustav Mubba,
MAMBEA AKISALIMIANA NA WANACHAMA WA CCM MARA BAADA YA KUWASILI UWANJANI.

KAMBI ZA VIJANA VINAWAPA UJASIRI WA KUWEZA KUJITAMBUA NA KUJITEGEMEA-MAKANGE

September 02, 2014
MWANDISHI WETU,HANDENI.
MWENYEKITI wa Jumiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdi Makange amesema kuwa kambi za vijana zinazofanywa kupitia umoja huo mkoani hapa ni jambo jema kwa sababu linawajengea ujasiri wa kuweza kujitambua na kujitegemea katika maisha yao kwa sasa na baaade.

Aliyasema hayo wakati alipotembelea kambi la Vijana wa Jumuiya hiyo wilayani Handeni linaloendelea katika shule za sekondari Kideleko pamoja na kuzungumza na wanakambi hao ikiwemo kuwataka kuwa kudumisha amani na utulivu kwa kipindi chote cha kambi hilo.

Alisema kuwa kambi hiyo inawaandaa vijana kwa vitu vitatu muhimu ambayo kwanza ni kuwa wazalendo na nchi yao pamoja na kuwaandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani hivyo.

Akizungumzia suala la makundi, Makange aliwataka vijana hao kuachana nayo kwa sababu hayana mashiko zaidi ya kusambaratisha umoja wao hivyo badala yake waungane kwa pamoja na kulilinda chama hicho na kukitetea ili kiweze kuendelea kuwatumikia wananchi.

Alisema kuwa endapo wakizingatia kupitia kambi hiyo litaweza kuwainua kimaisha pamoja na kuwajenga kiukakamavu jambo ambalo linawapa uzalendo ambao utawawezesha kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa jamii wanazoishi.

  “Vijana ni askari shupavu hivyo ni hatari sana askari kuwa na
makundi miongoni mwenu hakikisheni mnalipiga vita suala hilo kwa
sababu sio zuri kwenu “Alisema Makange

CHADEMA TANGA YASEMA KUWA ALIYEKUWA KATIBU WA WILAYA ALIYEJIUZULU HAKUWA KATIBU WAO

September 02, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Tanga kimesema Khalid Rashid hakuwa katibu wake wa Wilaya ya Tanga kamaalivyoeleza wakati  akitangaza kujiunga na chama kipya cha ACT-Tanzania  bali alishafukuzwa kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zilizokuwa zikimkabili.

Hali kadhailika wamesema kuwa majina  yaliyotangazwa na Khalid kujiuzulu pamoja naye wakidai ni wajumbe wa kamati ya utendaji hayakuwamo kwenye safu ya uongozi wa Chadema Wilaya ya Tanga bali ni ulaghai kwa wananchi na viongozi wa chama kipya alichoamua kujiunga.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga,Jonathan Bahweja  alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa kujibu taarifa ya katibu huyo na wajumbe wa kamati ya utendaji chadema waliyoitoa hivi karibuni.


Alisema kuwa Rashidi hakuwa tena mwanachama wala katibu wa Chadema Wilaya ya Tanga na hata hao aliowatangaza kwamba walikuwa wajumbe wa kamati ya utendaji majina yao hayamo kwa sababu nafasi zao zilianza kujazwa kutokana na kutokuwepo kwao.

Alisema Chadema mkoa imefurahishwa sana na hatua ya Khalid
kutangaza kujiunga na chama kingine kwa sababu katika kipindi cha miaka  zaidi ya 10 aliyokuwa akiongoza kabla ya kufukuzwa hakuweza kupata hata diwani mmja .

“Chadema Tanga wamefurahi sana alikuwa mzigo,fikiria katika kipindi chake cha uongozi kwa miaka zaidi ya 10,Chadema Tanga haina mbunge wala diwani anaondoka akiwa mtupu”alisema Bahweja

Katibu  huyo alisema hata hivyo Chadema haina muda wa kufanya
malumbano na mtu ambaye ameonyesha utovu wa nidhamu  bali kinajipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kinapata viti vingi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na wabunge na madiwani mwakani
.

SHIME:MGAMBO IPO TAYARI KWA LIGI KUU TANZANIA BARA

September 02, 2014
KOCHA Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga, Bakari Shime amesema kikosi cha timu hiyo kipo imara na kimekamilika vilivyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu hapa nchini.
Shime alitoa kauli hiyo wakati akiongea na TANGA RAHA BLOG mara baada ya kumalizika mchezo wao maalumu wa kujaribu matumizi ya mfumo wa kieletronici kati yao na African Sports ambapo timu hizo ziitoka suluhu pacha ya kutokufungana, uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa.
Alisema kuwa wao wataendelea na maandalizi ya kawaida kujiandaa na mechi yao ya Kagera Sugar ikiwa ni kufungua pazia la michuano hiyo mikubwa hapa nchini na kuhaidia kufanya vizuri kwa sababu ya kikosi hicho kuimarika kila siku.
Katika hatua nyengine, Kocha Shime alisema uongozi wa timu hiyo umeingia mkataba wa miezi sita na aliyekuwa mlinda Coastal Union, Said Lubawa kuichezea kwenye msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumzia sababu za wao kutokucheza mechi za majaribio,alisema kuwa mechi za aina hiyo wakati mwengine zinaweza zikawa hazina faida kwa timu kutokana na kuwa timu inaweza kucheza mechi hiyo lakini ikifika kwenye ligi kuu ikafanya vibaya.

SAMATTA, KAZIMOTO ULIMWEMGU WATUA DAR KUJIUNGA NA STARS, KIKOSI KUONDOKA DAR IJUMAA, MECHI JUMAPILI BUJUMBURA

September 02, 2014
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
NYOTA wa Tanzania wanaocheza nje, Mbwana Ally Samatta, Thomas Emmanuel Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto Mwitula wote wamewasili kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi Jumapili wiki hii.
Taifa Stars itacheza na Int’hamba Murugamba mjini Bujumbura Septemba 7 katika mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kikosi cha Stars kinaanza mazoezi leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 
Mbwana Samatta kushoto na Thomas Ulimwengu kulia wakiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry. Vijana wamekuja kulitumikia taifa

Mwesigwa amesema kwamba kikosi kitaondoka Ijumaa Dar es Salaam na kurejea Jumatatu baada ya mchezo huo. “Timu itaondoka hapa Septemba 5, Saa 11:10 alfajiri kwa ndege ya Kenya na kurejea  Septemba 8 saa Saa 1:00 usiku,”amesema.
Wakati Samatta na Ulimwengu, wote wanatokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kazimoto anatokea Al Markhiya ya Qatar.
Kikosi kinaanza mazoezi leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kikosi kamili alichoteua kocha Mholanzi, Mart Nooij kwa ajili ya mchezo huo ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Luizio (ZESCO, Zambia).

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA AMANI NA USALAMA WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA JIJNI NAIROBI

September 02, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi leo kujiunga na viongozi wengine wanaounda Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tioshio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla.
Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi katika mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kuzungumzia masuala ya tioshio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiteta jambo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi katika mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla.
Nyimbo za AU na Kenya zikipigwa kabla ya mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi.

AMERICAN SENATORS VISIT SERENGETI NATIONAL PARK

September 02, 2014

 Director General of TANAPA Mr. Allan Kijazi (right) welcomes the Chairperson of the US Senate Committee on Agriculture, Nutrition and Forestry and Michigan Senator Ms. Debbie Stabenow during the arrival of the US Senators delegation at Serengeti National Park.
 Chief Park Warden for Serengeti National Park Mr. William Mwakilema (right) was also there to welcome the US Senators at Serengeti National Park.
 US Senators heading to the vehicles ready for their game drive at Serengeti National Park.
 Supporting staff of the US Senates delegation busy taking pictures.
Lions in a relaxing positions enjoying the fiesta at Serengeti National Park.
 Zebras were also there to give US Senators maximum satisfaction of the beauty of Serengeti.
This giraffe could not afford to miss out this important visit by US Senators.
 *****
Five American Senators have started a two days visit in Serengeti National Park as part of the official program in the country.

The delegation led by the Senator of Michigan Ms. Debbie Stabenow who is also the Chairperson of the US Senate Committee on Agriculture, Nutrition and Forestry will have an opportunity to witness firsthand the vital role of conservation and good natural resources management in promoting sustainable economic development.

The US Senate delegation will also specifically demonstrate the challenges of combating the Wildlife Trafficking Crisis and methods for mitigation at the local, regional, national and the international level.

While in Serengeti, the delegation will visit sites of local conservation projects, view elephants and rhinos in their natural habitats, meet with leaders on the front lines in the war on poaching, and visit community projects that are working to preserve their natural resources, including threatened species. 

They will also learn about human-wildlife conflict and other issues of importance to local people.

Other Senators in the delegation includes Ms. Cantwell (Washington); Ms. Amy Klobuchar (Minnesota); Ms. Heidi Heitkamp (North Dakota) and Ms. Maize Hirono (Hawaii).

YANGA TUNAWASUBIRI MOROGORO KUWAPA KICHAPO: MTIBWA SUGER

September 02, 2014


N a Fadharkidev Blog
KOCHA wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime,amesema kikosi chake kimejiandaa kuitoa nishai Yanga katika mchezo wa ufunguzi utakaochezwa Septemba 20 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mexime aliyewahi kufundishwa na kocha wa Yanga Mbrazili Marcio Maximo wakati huo akiwa kocha wa ‘Taifa Stars,alisema namuheshimu kocha huyo lakini hatokubali kuona timu yake ikipoteza mchezo huo wa ufunguzi tena mbele ya mashabiki wao.

“Hatukuwa na matokeo mazuri sana msimu uliopita lakini kwa sasa tumejipanga kuhakikisha tunarekebisha kasoro zutu ndiyo maana tumefanya usajili mzuri ambao ninaimani tutapata matokeo ya ushindi kuanzia mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Yanga,”alisema Mexime.

Yanga ambayo itaanzia ugenini dhidi ya Wakata miwa hao wa Manungu wanabidi kujipanga kwani hawana matokeo mazuri katika uwanja huo wa Jamuhuri katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita zaidi ya kuambulia kipigo na sare.
NISHATI NA MADINI WAIMARISHA MKAKATI WA UTUNZAJI MAZINGIRA

NISHATI NA MADINI WAIMARISHA MKAKATI WA UTUNZAJI MAZINGIRA

September 02, 2014
day 2 - pic 1Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Emmanuel Shija akiwasilisha mada kuhusu ‘Uchimbaji mdogo wa Madini na Mazingira’ wakati wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa. Semina hiyo ya siku nne inafanyika jijini Mwanza (Septemba 1-4, 2014) na imeandaliwa na Kitengo cha Mazingira cha Wizara husika.

day 2 - pic 2Katibu Mtendaji wa TAREA (Tanzania Renewable Energy Association) Tawi la Kanda ya Ziwa, Bw. Jacob Ruhonyora akizungumzia uzoefu wake kuhusu faida za matumizi ya nishati jadidifu,kwa Wajumbe wa semina ya mafunzo ya mambo ya mazingira inayoendelea jijini Mwanza kuanzia Septemba 1, 2014. Semina hiyo ya siku nne imeandaliwa na Kitengo cha Mazingira cha Wizara ya Nshati na Madini.
day 2 - pic 3Afisa Misitu Mkuu kutoka Kitengo cha Mazingira – Wizara ya Nishati na Madini (Kulia), Theodory Silinge akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kuhimiza jamii kutumia nishati mbadala wakati wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika jijini Mwanza, Septemba 1 – 4, 2014day 2 - pic 4Afisa Sheria kutoka Wizara ya Nishati na Madini Renatus Damian, akiwasilisha mada kuhusu masuala ya sheria katika utunzaji mazingira wakati wa semina kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika jijini Mwanza Septemba 1 – 4, 2014.
day 2 - pic 5Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nassor Abdullatif (Kushoto), akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kufanya Tathmini ya Mazingira (Environmental Impact Assessment – EIA) kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi wowote katika siku ya pili ya semina kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika jijini Mwanza Septemba 1 – 4, 2014.

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA MARAIS WA VISIWA VYA COMORO NA SEYCHELS

September 02, 2014

 Rais wa Serikali ya Visiwa vya Comoro Ikililou Dhoinine akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia.
 Rais wa Serikali ya Visiwa vya Comoro Ikililou Dhoinine akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Seychels James Michel  walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana   na Rais wa Seychels James Michel  baada ya mazungumzo walipokutana kwa   jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia.

Wajumbe wa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa wakiwa katika ukumbi  wa jengo la Apia wakati michango mbali mbali ikitolea jana na Vingozi wa Nchi zilizoshiriki mkutano huo
 Wajumbe wa  Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa na Maafisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini michango inayotolewa katika mkutano huo unaoendelea huko Nchini Samoa katika ukumbi wa jengo mkutano huo.
 Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka nchi mbali mbali zilizoshiriki Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa  wakichukua taarifa zilizotolewa na michango kiatika mkutano huo unaoendelea katika jengo ya Ukumbi wa Apia nchini Samoa.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Bibi Fatma Fereji akiwa mwenyekiti katika sehemu moja ya Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa unaoendelea katika jengo ya Ukumbi wa Apia nchini Samoa,(kulia) Kaimu Sekretary (UN)  Bibi Erner Herity na (kushoto)Marrio Barthelemy  Mkurugenzi wa Uchumi na Mambo ya Kijamii. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.