WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA RASMI LEO MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR ES SALAAM.

WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA RASMI LEO MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR ES SALAAM.

September 19, 2014

image[1] 
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa nasaha fupi katika hafla fupi ya kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza ambao wamestaafu rasmi Utumishi wa Umma tangu Julai 1, 2014. Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 19, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
image_1[1] 
Wastaafu wa Jeshi la Magereza(katika picha) wakiwa na familia zao wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa nasaha fupi kwa Wastaafu hao ambao wamestaafu Utumishi wa Umma tangu Julai 1, 2014.
image_2[1] 
Kwaya ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza inayoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza ikitumbuiza kwenye hafla hiyo ya kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo imefanyika leo mchana Septemba 19, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam.
image_3[1] 
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishangilia Wimbo Maalum uliotumbuizwa na kwaya ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika hafla fupi ya kuwaaga Maafisa na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza ambao wamestaafu Utumishi wao kwa mujibu wa Sheria tangu Julai 1, 2014.
image_4[1] 
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) akikabidhi zawadi kwa Sajin Taji wa Jeshi la Magereza, Kessy Ngwengwe(kushoto) ambaye alikuwa ni Dreva wa Magari ya Viongozi Makao Makuu ya Jeshi Magereza. Askari huyo amestaafu Utumishi wake wa Umma tangu Julai 1, 2014.
photo[1] 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wastaafu wa Jeshi la Magereza(waliosimama mstari wa nyuma) kwenye hafla fupi ya kuwaaga Wastaafu hao ambao amestaafu Utumishi wao wa Umma tangu Julai 1, 2014(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
WIZARA YA AFYA YASHINDWA KUTIMIZA AHADI YAKE HOSPITALI TEULE YA TUMBI KIBAHA

WIZARA YA AFYA YASHINDWA KUTIMIZA AHADI YAKE HOSPITALI TEULE YA TUMBI KIBAHA

September 19, 2014



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka wakati alipowasili mjini Kibaha kuendelea na ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Katibu mkuu pia anahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuimarisha chama, Katika msafara huo Kinana anaogozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. Kero kubwa iliyojitokeza katika ziara hiyo ni pale Mkurugenzi wa huduma za Afya katika hospitali ya Tumbi Dr. Peter Dattan aliposema Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii iliahidi kununua vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo(ICU) Lakini ahadi hiyo haijatekelezwa yapata miaka mitatu sasa, Pamoja na kwamba hospitali ya Tumbi Kibaha inapokea majeruhi wengi na wanahitaji tiba maalum kutokana na majeraha mbalimbali yanayosababishwa na majeruhi wa  na ajali, Hospitali ya teule ya Tumbi inapokea asilimia 80% ya majeruhi wa ajali. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBAHA) 2 
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka akitoa maelezo ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha kwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha. 4 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika eneo ambali ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha inajegwa mjini Kibaha 6 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akipanda mti katika jengo la ofisi mpya ya CCM wilaya ya Kibaha inayojengwa. 7 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapongeza watoto wa chipukizi baada ya kuimba ngonjera yao mbele yake. 8 
Baadhi ya vijana wa Kambi ya vijana ya UVCCM ya wilaya ya Kibaha wakiimba nyimbo kumkaribisha Katibu mkuu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea kambi yao iliyopo Boko Timiza mjini Kibaha. 11 
 Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka wakishiriki katika shughuli za usafishaji wa shamba la vijana wa Kibaha mjini lililopo Boko Timiza. 13 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Dr. Peter Dattan Mkurugenzi wa Shughuliza Afya katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. 16 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutokwa kwa  Dr. Peter Dattan Mkurugenzi wa Shughuliza Afya katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha wakati alipotembelea chumba cha wagonjwa mahututi ICU katika hospitali hiyo. 17 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa  Dr. Brayson Kiwele  daktari bingwa wa mifupa  katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha alipotembelea chumba cha upasuaji. 18 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF mara baada ya kutembelea katika hospitali teule ya Tumbi. 19 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu katika ukuta wa tanki la mradi wa maji wa mtaa wa  Muheza mjini Kibaha.  20 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa mtaa wa Muheza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi huo, aliyesimama juu ni Grace Lyimo Mhandisi wa maji wa wilaya ya Kibaha. 21 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiakiwa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwinshehe Mlao. 22 
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza kushoto akiwa  na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Pwani  katikati ni Imani Madega Mlezi wa CCM mkoa wa Pwani.

23 
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka wakionyesha vyeti vyao baada ya kutambuliwa na uongozi wa CCM mkoa wa Pwani kwa mchango wao wanaoutoa kwa CCM Pwani
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI WA MAFUNZO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI WA MAFUNZO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

September 19, 2014

01 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kama ishala ya kuzindua rasmi mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Kazi, na Ajira, Gaudensia Kabaka (kushoto) ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Shukuru Kawambwa
4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa kuzindua rasmi mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.
5 
Baadhi washiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Charles Gwambassa, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali. Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.03 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Mwajuma Massoud, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali  Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.04Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Tumpe Samwely, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.05Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi  wa VETA na washiriki na wadau waliohudhuria uzinduzi huo. 06 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo katika Chuo cha VETA na wakufunzi wao baada ya uzinduzi huo.07 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wawakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani ILO  waliohudhuria uzinduzi huo. 08 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Kazi, na Ajira, Gaudensia Kabaka, wakati akiondoka katika Hoteli ya Kunduchi Beach baada ya uzinduzi huo wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo.
WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WATAALAM WA UTAFITI WA HALI YA UMASIKINI KATIKA KAYA TANZANIA.

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WATAALAM WA UTAFITI WA HALI YA UMASIKINI KATIKA KAYA TANZANIA.

September 19, 2014

Picha na 1 
Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba akifungua mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15.Picha na 2 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwakaribisha washiriki wa mafunzo ya wiki 3 ya utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15 mkoani Morogoro.
Picha na 3Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumzia  umuhimu wa matumizi ya takwimu sahihi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya nchini mwaka 2014/15.
Picha no 4 
Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15 mkoani Morogoro.
Picha na 5Washiriki wa mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya nchini mwaka 2014/15 yanayofanyika mkoani Morogoro wakifuatilia masuala mbalimbali .

RAIS KIKWETE AWASILI WASHINGTON DC KWA MIKUTANO MBALIMBALI PAMOJA NA HAFLA YA USIKU WA JAKAYA

September 19, 2014


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa La Guardia jijini Washington DC tayari kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali na pia katika hafla ya “USIKU WA JAKAYA”  leo jioni

 Rais Kikwete akilakiwa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kuwasili hoteli aliyofikia

 Karibu Washington DC Mheshimiwa

 Rais akiendelea kusalimia na na wafanyakazi wa ubalozini

 Mapokezi yakiendelea

 Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Lucas Mkama wa Vijimambo Blog

Karibu sana Mzee…

MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMAJARO (KINAPA).

September 19, 2014

 Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 wametembelea hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) na kujifunza mambo mengi kuhusiana na hifadhi hiyo ya mlima kilamanjaro. Pichani ni warembo hao wakipiga picha na mdau mkubwa wa masuala ya urembo mkoani Kilimajaro, Athena Mawalla wa mgahawa wa Meku's Bistro wakati warembo hao walipomtembelea wakiwa njiani kwenda KINAPA.
 Warembo wakiwa katika gari njiani kuelekea KINAPA. 
 Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico (kulia) akitoa maelekezo baada ya kufika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimajaro.
 Warembo wakipanda kuelekea geti kuu la kupandia Mlima Kilimanjaro.
 Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.
 Eliud Bemba ambaye anaongoza timu ya utayarishaji Vipindi maalum vya warembo hao kutoka True Vision akichapa picha na walimbwende.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Erastus Lufungulo akitoa maelezo ya mlima huo kwa warembo wa Miss Tanzania.