Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Simba,
Zdravok Logarusic, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata
ili washinde katika mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo unaotarajiwa
kupigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Logarusic alisema timu yote inahitaji ushindi katika mechi yao hiyo,
hivyo jambo kubwa ni kuona vijana wake wanakuwa makini zaidi uwanjani.
“Tumepoteza pointi muhimu
katika mechi iliyopita kwasababu ya wachezaji kutotumia ipasavyo nafasi za wazi
wanazozipata, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limetugharimu.
“Naamini wakati huu
wachezaji wote wanafahamu jambo gani muhimu wanapaswa kufanya uwanjani kwa ajili
ya kuwapatia maatokeo mazuri, maana mpira ni mchezo wa makosa,” alisema.