SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA ZAMBIA.

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA ZAMBIA.

April 25, 2017
A 2
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kaunda suti nyeusi katikati)akipiga picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Mhe. Douglas Syakalima, ambae ni Mwenyekiti wa Kamati na Kiongozi wa Msafara/Ujumbe huo katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
A 3
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia)akimkabidhi kitabu chenye Sheria Mbali mbali za Bunge Mhe. Douglas Syakalima (wa pili kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu na Kiongozi wa Msafara wa kutoka Bunge hilo, Wabunge hao wamekuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigala King.
IMGL6982
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
A 4
Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati)akizungumza  katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, Wabunge hao walikuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu.
V
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Prof. Norman Sigala King akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR

RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR

April 25, 2017
A
Baadhi ya Walimu na viongozi wa michezo katika maskuli waliohudhuria katika hafla ya Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza Zanzibar.
A 1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein katikati akimkabidhi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma Jezi pamoja na Mipira kwa ajili ya mashindano ya maskuli vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.
A 2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein katikati akimkabidhi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma Viatu vya mpira wa Miguu  kwa ajili ya mashindano ya maskuli vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.
A 3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein katikati akimkabidhi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma Kikombe cha kushindaniwa katika mashindano ya maskuli vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza.
A 4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein akitowa hotuba katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI SIMBACHAWENE AZINDUA TAWI LA DCB MKOA WA DODOMA LEO

April 25, 2017
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB) ameipongeza benki ya DCB kwa hatua kubwa waliyofikia ya  kwa kuwa miongoni mwa benki zilizoanzisha huduma zinazoendana na teknolojia ya kisasa kama ilivyo kwa huduma za kibenki kwa njia ya mawakala (DCB Jirani) na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi (DCB Pesa).

Simbachawene amesema kufunguliwa kwa tawi hili zitasogeza huduma za kibenki karibu na wafanyabishara na wakazi wa mji wa Dodoma na haya ndiyo maendeleo tunayotaka katika sekta ya kibenki ili huduma za benki zipatikane kwa urahisi zaidi kwa wananchi na nina hakika wananchi wengi watapata huduma bora kupitia tawi hili. 
Hivyo nawaasa wafanyabiashara, wafanyakazi na wakazi wote wa mkoani Dodoma watumie fursa hii kwa kufungua akaunti mbalimbali za DCB kupitia tawi hili, ni imani yangu kwamba huduma zitakozotolewa na tawi hili zitakuwa bora na zenye kumjali mteja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa ametoa shukrani za dhati kwa Mhe. George Simbachawene, Waziri wa TAMISEMI kwa kukubali kuwa Mgeni rasmi katika hafla hii ikiwa ni mara yako ya pili kukubali wito kuwa mgeni rasmi. Mara ya kwanza ilikuwa ni kuzindua rasmi tawi la Benjamini Mkapa lililopo maeneo ya Samora karibu na ofisi za Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkwawa amesema kwa upande wa Dodoma wamefanikiwa kupata mawakala 38 ambao muda si mrefu wataanza kutoa huduma za DCB mitaa ya Dodoma karibu zaidi na wananchi. Mbali na hapa Dodoma, pia wana mpango wa kupeleka huduma za DCB mikoa mingine kupitia DCB Jirani kama vile mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kahama, Mtwara, Arusha, Iringa na Mbeya lengo ni kuwa na mawakala 1,500 nchi nzima kufikia Disemba mwaka huu. 

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka  ametoa wito kwa wakazi wote wa Dodoma na vitongoji jirani wazipokee huduma za DCB na wawe mstari wa mbele kutumia huduma za benki tawini hapo ili kukuza tawi hili na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia wananchi wengi zaidi katika suala zima la kupiga vita umasikini. 
Prof Msambichaka ameongezea na kusema wana imani wengi watanufaika na benki hii kwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba mara kwa mara, kuimarisha usalama wa fedha zenu na kujenga uwezo wa kupanua biashara kwa kutegemea. Huduma hizi zina lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na kuongeza amana za benki ambazo ndio uti wa mgongo wa benki zote duniani.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB) akizundua tawi la Benki ya DCB mkoa wa Dodoma akishuhudiwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania John Malecela(Kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka .

WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO

April 25, 2017
              Na. Immaculate Makilika- MAELEZO - DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.

“Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama

Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo.

“Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana

Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.

Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.

 Waziri Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri  leo Mjini Dodoma.
 Baadhi ya wananchi wakifuatilia maonesho ya maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu Serikali ilipohamia Dodoma.
 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.

BIA YA CASTLE LITE YAZINDUA PROMOSHENI YA “CASTLI LITE UNLOCKS” IKIMTAJA MWANAMZIKI FUTURE ATAKAYEFANYA ONYESHO TANZANIA!

April 25, 2017

Dar Es Salaam –  Usiku wa tarehe 20 Aprili katika Club ya Next Door ndani ya Masaki, Dar es Salaam, Castle Lite ilizindua promosheni ya  'Castle Lite  Unlocks kwa mara ya kwanza Tanzania, na hivyo kuiweka  nchi katika msisimko wa aina yake. Chumba kilikuwa kimejaa hamasa wakati Castle Lite ikimzindua Mfalme wa Muziki Kimataifa-FUTURE.
Uzinduzi huo ulishereheshwa na malkia mpya wa muziki wa pop na mtangazaji maarufu wa televisheni, Mini Mars, tangazo hilo lilibainisha kwamba Rapa ambaye ni mshindi wa tuzo ya “Turn On The Lights” atakuwa nyota katika  onesho la Julai 22, 2017 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, ambapo upatikanaji wa tiketi  utatangazwa katika hatua nyingine zitakayofuata.
Castle Lite pia imetangaza kwamba mwanamuziki Diamond Platnumz atakuwa mshiriki mwenza katika tamasha hilo la Extra Cold Unlocks. Diamond Platnumz ni  msanii wa kwanza Afrika Mashariki kusaini mkataba na kampuni ya kurekodi muziki ya Universal Music na hivyo  kuwa mwanamuziki rasmi wa kimataifa.
 “Ninawaahidi Watanzania burudani ya kipekee”, alisema Diamond Platinumz alipokuwa akizungumza kuhusu tamasha hilo.
Likiwa linawashirikisha wasanii wengine  maarufu wa Kitanzania ambao watatangazwa katika hatua zitazofuata kuelekea katika tamasha hilo,
“Kampeni ya 'Castle Lite Unlocks' imekuwa kwenye harakati za maandalizi kwa miaka michache sasa, ambapo Castle Lite imebadili mfumo wa kawaida uliozoeleka kwa kuwaletea wasanii wa ngazi ya juu kimataifa ili kuburudisha nchini mbalimbali Afrika na kwa mara ya kwanza burudani inaletwa katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki jijini Dar es salaam alisema Mkurugenzi wa Masoko wa Afrika Mashariki, Thomas Kamphius.
"Tunaelewa kwamba wateja wetu sio kila mara wanapata fursa ya kuona baadhi ya matukio haya makubwa, hivyo tunataka kuwaletea fursa hii na kuendelea kuwaletea burudani za namna hii kwa miaka ijayo.Kamphius aliongeza.
Fuatilia matangazo mbalimbali katika vyombo mbalimbali vya habari , ikiwepo Radio, TV, mitandao ya kijamii na Magazeti ili kupata muendelezo wa matukio kutoka sasa hadi siku ya tamasha lenyewe Julai 22. Kwa hivi sasa chukua Castle Lite yako soma maelekezo jinsi ya kushiriki ili kupata fursa ya kushinda nafasi ya kuwa sehemu ya sehemu ya Burudani ya'Castle Lite Extra Cold Unlocks' ndani ya Dar es Salaam.