KIJIJI CHA NANJILINJI A CHATOA RUZUKU KWA WA MAMA WAJAWAZITO

January 09, 2016
Na. Ahmad Mmow, Kilwa-LINDI.
Uhifadhi wa msitu katika kijiji cha Nanjirinji A, wilayani Kilwa mkoani Lindi, umeendelea kuwanufaisha wananchi wakazi wa kijiji hicho baada ya kuanza kuwapatia ruzuku akina mama wajawazito wanaoishi katika kijiji hicho.
Kilwa
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Jafari Nyambate, mwanzoni mwa wiki hii alipozungumza na Lindiyetu.com mjini Kilwa masoko. 

Nyambate alisema baada ya kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii kwa kutumia fedha zilizotokana na mauzo ya mazao ya msitu waliohifadhi, unaofahamika kwa jina la Mbumbila, Kijiji kimeanza kuwapa ruzuku ya shilingi 30,000 akina mama wajawazito wakazi wa kijiji hicho.

Ikiwa ni mchango wa maandalizi ya gharama za matibabu wakati wakujifungua.
"Fedha hizo zinatolewa kwa mama ambaye mimba yake imefikisha umri wa miezi tisa, muda ambao anatarajia kujifungua ili aweze kufanya maandalizi ikiwamo kununua vifaa vitakavyotumika wakati huo,"alisema Nyambate.

Alibainisha kuwa huo nimwendelezo wa huduma mbalimbali za jamii zilizotekelezwa kutokana na mapato ya msitu huo. Ambapo baada ya kufanikiwa mpango huo,wanajipanga kuanza kutoa ruzuku kwa wazee wasiojiweza.

Mwenyekiti huyo aliitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kutokana na mapato ya msitu huo kuwa ni vyumba vi 3 vya madarasa ya shule ya msingi, visima vifupi 7 vya maji, soko, vyoo vya kudumu vya shule ya msingi vyenye matundu 6.

Aliitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na nyumba moja ya mwalimu, madawati 26, bomba la maji la shule na viti 100 vinavyotumika wakati wa mikutano mikuu ya kijiji.

Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, mwenyekiti huyo alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Ikiwamo uvamizi unaofanywa na wakulima, hasa wa zao la ufuta ambao wanalazimisha kuendesha shughuli za kilimo ndani ya msitu waliouhifadhi.
"Lakini pia wapo wanaopasua mbao kwa njia haramu, nao wanatusumbua sana ila tunakabiliana nao kwa kufanya doria za mara kwa mara, hasa baada ya kamati ya maliasili kuwezeshwa pikipiki tatu zinazotumika kwa doria," aliongeza kusema.

Uvunaji katika msitu huo wenye hekta 61724, ulianza rasmi mwaka 2012.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MHE. MWIJAGE ATEMBELEA TBL

January 09, 2016

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akisalimiana na viongozi wa TBL alipowasili kwenye kiwanda cha TBL kwa ziara ya kikazi Dar es Salaam Januari 8 2016. Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin.
Waziri wa viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akisalimiana na Emma Urio alipowasili kiwanda cha TBL Dar es Salaam Januari 8 kwa ziara. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin na viongozi waandamizi wa kampuni hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akiongozwa na Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin (kushoto) wakati wa ziara hiyo TBL
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya viwanda wa wizara hiyo, Obadiah Nyagiro.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya viwanda wa wizara hiyo, Obadiah Nyagiro.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akiongozwa na Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin (kushoto) wakati wa ziara hiyo TBL.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akisalimiana na mwendesha mitambo wa kampuni ya TBL, Mecky Mlay kabla ya kupata maelezo kwa kuhusu utendaji wake wa kazi alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akifurahia jambo na mwendesha mitambo wa kampuni ya TBL, Mecky Mlay alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. Kulia (kwake) ni Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kulia) akipata maelezo kwa mwendesha mitambo wa kampuni ya TBL, Mecky Mlay alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. Kulia (kwake) ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin na Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akifuahia jambo aliowasili kwenye mitambo ya uzalishaji wa bidhaa za TBL.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kushoto) akipata maelezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa TBL alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin na Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin, alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin, alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kushoto) akitembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. Pamoja naye ni Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akitoka kuangalia uzalishaji wa kiwanda hicho wakti wa ziara hiyo. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin (kushoto), Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin pamoja na Mkurugenzi wa Jumla wa Mahusiano wa TBL, Georgia Mutagahywa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin (kushoto) pia Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akidadisi jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin (kushoto) na viongozi waandamizi wa TBL wakati wa ziara hiyo. Kutoka (kulia) ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Afrika Mashariki, Gavin van Wijk, Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin na Mkurugenzi wa Maendeleo ya viwanda wa wizara hiyo, Obadiah Nyagiro.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiwa katika akiwa pamoja na wenyeji akihitimisha zaira yake.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin wakati wa ziara yake kiwandani hapo Januari 8, 2016. Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Afrika Mashariki, Gavin van Wijk.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin wakati wa ziara yake kiwandani hapo Januari 8, 2016.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin wakati wa ziara yake kiwandani hapo Januari 8, 2016.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin (kulia kwake) pamoja na viongozi waandamizi wa TBL baada ya kumaliza ziara yake kiwandani hapo Januari 8, 2016.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin.
Waziri wa viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiagana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Afrika Mashariki, Gavin van Wijk.
Waziri wa viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akiagana na Mkurugenzi wa Jumla wa Mahusiano wa TBL, Georgia Mutagahywa. Kulia pia Mkurugenzi wa Maendeleo ya viwanda wa wizara hiyo, Obadiah Nyagiro akiagana na viongozi wa TBL.

TAJATI YAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA VIWANDANI JIJINI MBEYA NA KUSHUHUDIA MAGOFU NA MITAMBO ILIYOTELEKEZWA

January 09, 2016

Baadhi ya mitambo iliyotelekezwa kwenye Kiwanda cha kutengenezea Zana za Kilimo ZZK

Mitambo ambayo ilikuwa ikitumika kutengenezea Zana za Kilimo katika kiwanda cha ZZK Iyunga jijini Mbeya ikiwa imetelekezwa

Niranjan Bandi, aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa shughuli zinazoendelea katika kiwanda cha ZZK  chini ya kampuni ya CMG akiwapa maelezo waandishi wa habari.

Waandishi wakitoka katika kiwanda cha ZZK huku wakijiuliza maswali mbali mbali kutokana na walichokikuta ndani ya kiwanda hicho

Baadhi ya waandishi wakichungulia ndani ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha kutengeneza sabuni HISOAP Kushuhudia kama kuna kilichosalia.

Huu ndiyo muonekano wa ndani ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha kutengenezea sabuni HISOAP kukiwa hakuna kitu licha ya kuwepo Mlinzi

Muonekano wa Jengo la kiwanda cha HISOAP lililotelekezwa ili hali serikali ya awamu ya tano ikisisitiza kuwa serikali ya Viwanda

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) katika kutekeleza majukumu yake kimefanya ziara katika viwanda vine vilivyopo Iyunga jijini Mbeya na kushuhudia baadhi vikiwa vimetelekezwa.
Waandishi hao  15 kutoka vyombo mbali mbali ambao ni wanachama wa TAJATI, walifanya ziara hiyo iliyoanzia katika majengo yaliyokuwa ya Kiwanda cha kutengenezea sabuni kilichokuwa kikijulikana kwa jina la HISOAP kilichopo Iyunga jijini Mbeya na kukutana na majengo hayo yakiwa yametelekezwa.
Mbali na kutelekezwa kwa majengo hayo,pamoja na  kuwepo kwa mlinzi ambaye alikiri kulinda majengo ambayo ndani yake hajui kilichomo kwa kupitia matundu ya mlangoni,wanahabari hao walishuhudia ndani kukiwa hakuna hata mtambo mmoja ulichosalia na na matanki makubwa yanayoendelea kuoza nje.
“Mimi nalinda hapa kwa maagizo ya bosi wangu lakini huko ndani hakuna shughulli yoyote inayofanyika kwani hata hizo mboga zilizolimwa ni mali ya walinzi wenzetu ndiyo wamelima,sijui humo ndani kama kuna mitambo sijawahi kuona milango ikifunguliwa hata mwenye funguo simjui” alisema Mlinzi ambaye alitaka jina lake lihifadhiwe kwa usalama wake.
Aidha katika ziara hiyo timu ya waandishi ilifika katika majengo ya kilichokuwa kiwanda cha serikali, Kiwanda cha kutengenezea zana za kilimo maarufu kwa jina la ZZK ambapo timu hiyo ilipokelewa na raia mmoja wa kigeni mwenye asili ya kiasia,  Niranjan Bandi, aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa shughuli zinazoendelea hapo chini ya kampuni ya CMG.
Katika maelezo yake kwa waandishi wa habari Bandi alisema ndani ya kiwanda hicho kuna shughuli za kutengeneza vipuri vya magari, uunganishaji wa matrekta madogo ya kilimo(powertiller ) kutoka China na kwamba zana za kilimo wameshindwa kutengeneza kutokana uchakavu wa mitambo iliyopo na imepitwa na teknolojia.
Aliongeza kuwa ifikapo januari 15 mwaka huu wanatarajia kuanza kutengeneza mabati baada ya kupata mtambo kutoka China ambao hivi sasa unafanyiwa marekebisho kabla ya kuanza kazi sambamba na uanzishwaji wa kiwanda cha kuzalisha bia cha Serengeti.
Wakati mwekezaji huyo akijieleza na kuonyesha mashaka makubwa ya uzalishaji kuwa ni changa la macho,Waandishi wa habari  walishuhudia mitambo iliyokuwa ya kutengenezea zana za kilimo ikiwa imetekelezwa bila kufanya kazi ndani ya majengo hayo ambapo Mkurugenzi huyo alisema hawana uwezo wa kuiendesha.
Baada ya kukamilisha mahojiano na Mkurugenzi huyo waandishi hao walielekea moja kwa moja katika kiwanda cha Malumalu cha Marmo Granito ambapo walitembelea mitambo ya kuchonga na kukata mawe na bidhaa mbali mbali zinazotokana na  miamba ya asili.
Mkurugenzi wa Marmo,Salim Jessa alisema tangu walipoanza uwekezaji katika Mkoa wa Mbeya wameanza kupata masoko nje ya nchi ikiwemo India,Italia na kutafuta masoko mengine nchini  China ambako watakuwa wakiuza malighafi zilizoongezwa thamani kwa ajili ya matumizi mengine.
Alisema changamoto kubwa ni ushindani wa soko baada ya kampuni zingine kujitokeza na kuanza kutengeneza bidhaa zinazotokana na mawe ya asili kama wao sambamba na uingizaji wa bidhaa zilizochakachuliwa kutoka nje kwa lengo la kuharibu soko.
Ziara hiyo ya TAJATI ilihitimishwa katika kiwanda cha Bia cha TBL ambapo waandishi walitembezwa kiwandani hapo na kisha kupata muda wa kuuliza maswali kutoka kwa wahusika.
Akizungumza na wanachama hao, Meneja wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari alisema licha ya mafanikio waliyoyapata katika uzalishaji wanakabiliwa na changamoto kubwa ambazo ni miundombinu mibovu, gharama kubwa za maji na umeme sambamba na mlundikano wa vinywaji kutoka nje ya nchi vinavyoharibu bei ya vinywaji vinavyozalishwa nchini.
Jemedari alisema bia nyingi zinaingizwa nchini kutoka nje zinauzwa bei ya chini hivyo kupelekea wateja wengi kukimbilia na kuua soko la vinywaji vya ndani.

Na Mbeya yetu
TFF YAWASHUKURU WATANZANIA

TFF YAWASHUKURU WATANZANIA

January 09, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewashukuru watanzania wote, wapenzi, na wadau wa mpira wa miguu Tanzania waliojitokeza usiku saa 8 uwanja wa ndege wa JK Nyerere kumpokea mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani Mbwana Samatta.
Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK Nyerere, Samatta alipokelewa na viongozi wa serikali, TFF, familia yake wakiwemo baba na mama yake mzazi na watanzania wengi walijitokeza kumlaki mchezaji huyo.
Mara baada ya mapokezi ya uwanja wa ndege, TFF ilimpeleka moja kwa moja kupumzika katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta jijini Dar es salaam, ambapo imemlipia gharama ya kukaa kwa siku mbili.
Akiwa hoteli ya Serena, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda alitoa salamu za pongezi kwa niaba ya Serikali, kisha mchezaji alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari.
Kwa kuwa Jumanne, Januari 12 ni Sikukuu ya Mapinduzi, na Janauri 13 ni fainali ya kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar, siku ya Alhamisi Januari 14 TFF imeandaa dua maalumu ya kumpongeza Samatta itakayongozwa na viongozi wa dini mbalimbali katika uwanja wa Karume kuanzia saa 11 jioni.
Hata hivyo ratiba zingine za kumpongeza Mbwana Samatta zinazoweza kuandaliwa na wadau wengine zinaweza kuendelea ilimradi TFF ijulishwe mapema kwa ajili ya kuratibu uwepo wa mchezaji mwenyewe.

"TUTAKUWA MAMIZI GRAND RESORT JIJINI MWANZA WIKENDI HII"

January 09, 2016
Binagi Media Group tunaungana na Wapenzi wa burudani Jijini Mwanza leo Jumamosi ya Januari 09,2015 na kesho Jumapili ya Januari ya 10,2015 ili kufurahi pamoja katika Kiota cha Burudani cha Mamiz Grand Resort Kilichopo Mkolani ikiwa ni baada ya shughuli nzito za juma zima. 

Ni Mamiz Grand Resort pekee itakayotuwezesha kufurahia pamoja tukiwa na ndugu, jamaa na marafiki huku tukipata huduma bora kama vile Chakula safi, vinywaji vya kila aina, vyumba bora vya kulala vilivyonakshiwa  kiafrika bila kusahau michezo mbalimbali ya watoto pamoja na Muziki wa Live.

Fika wikendi hii Mamiz Grand Resort ili ujionea utofauti wa burudani.
 Kumbuka pia kutembelea Mamiz Gate Way Mkolani.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi 0767 024 094
Kampuni ya Tigo yawakutanisha wamiliki wa Mitandao ya Jamii

Kampuni ya Tigo yawakutanisha wamiliki wa Mitandao ya Jamii

January 09, 2016
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Tigo kwa kuwakutanisha baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Tigo kwa kuwakutanisha baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es SalaamBaadhi ya wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) wakiwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika 'Facebook' ya kampuni hiyo. Tigo ilitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaofuatilia ukurasa wao (Facebook page). Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) wakiwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika 'Facebook' ya kampuni hiyo. Tigo ilitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaofuatilia ukurasa wao (Facebook page)Msanii maarufu wa dance nchini, Christian Bella akiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika ukurasa wa 'Facebook' wa kampuni hiyo. Msanii maarufu wa dansi nchini, Christian Bella akiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika ukurasa wa 'Facebook' wa kampuni hiyoMsanii maarufu wa Dance nchini, Christian Bella wa Bandi ya Malaika kulia akicheza na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika 'Facebook' ya kampuni hiyo.
Msanii maarufu wa dansi nchini, Christian Bella (kulia) wa Bandi ya Malaika kulia akicheza na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika 'Facebook' ya kampuni hiyo.Baadhi ya wanamitandao ya jamii wakisakata rumba na msanii maarufu wa Dance nchini, Christian Bella (wa tatu kulia) toka Bandi ya Malaika alipokuwa akiwaburudisha wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanamitandao ya jamii wakisakata rumba na msanii maarufu wa dansi nchini, Christian Bella (wa tatu kulia) toka Bandi ya Malaika alipokuwa akiwaburudisha wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanamitandao ya jamii wakisakata rumba na msanii maarufu wa Dance nchini, Christian Bella (wa pili kulia)  wa Bandi ya Malaika alipokuwa akiwaburudisha wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanamitandao ya jamii wakisakata rumba na msanii maarufu wa dansi nchini, Christian Bella (wa pili kulia) wa Bandi ya Malaika alipokuwa akiwaburudisha wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es Salaam"...TWANGA PHOTOOO..." Baadhi ya wanamitandao ya jamii wakiji-selfie na Msanii maarufu wa Dance nchini, Christian Bella wa Bandi ya Malaika mara baada ya kutoa burudani. "...TWANGA PHOTOOO..." Baadhi ya wanamitandao ya jamii wakiji-selfie na Msanii maarufu wa dansi nchini, Christian Bella wa Bandi ya Malaika mara baada ya kutoa burudani.Mshereheshaji wa hafla hiyo, Taji Liundi (kulia) akimkaribisha Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi kutoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Tigo kwa kuwakutanisha baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner). Mshereheshaji wa hafla hiyo, Taji Liundi (kulia) akimkaribisha Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi kutoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Tigo kwa kuwakutanisha baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner).Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi (kulia) wakibadilishana mawazo na mmoja wa maofisa kutoka kampuni ya Tigo, Shavkat Berdiev katika hafla hiyo. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maofisa kutoka kampuni ya Tigo, Shavkat Berdiev katika hafla hiyo.[/caption] ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com