ULINZI WAIMARISHWA NYUMBANI KWA Dk. MAGUFULI, UKAWA NA MGOMBEA WAKE

July 13, 2015
 
Ni Jumatatu nyingine tena na inawezekana uchambuzi wa magazeti leo Julai 13 umekupita. Nimekusogezea stori zote za magazeti kupitia @Clouds.Fm zikiwa na baadhi ya stori hizi kubwa.
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ateuliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM na ameahidi kutokukiangusha Chama hicho, huku akimteua Samia Suluhu Hassan kama mgombea mwenza. 
Ulinzi wa nyumbani kwa Dk. John Magufuli umeimarishwa baada ya kutangazwa kuwa Mgombea Urais kupitia chama cha CCM, Viongozi wa Vyama vya upinzani UKAWAwasema hawatishwi na John Magufuli na wamejipanga kumtangaza rasmi mgombea wao wa Urais kesho.
MGOMBEA URAIS ZANZIBAR DKT SHEIN APOKELEWA KWA KISHINDO

MGOMBEA URAIS ZANZIBAR DKT SHEIN APOKELEWA KWA KISHINDO

July 13, 2015

sn1
Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
sn2
Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akivalishwa Shada la maua mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo.
sn3
Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanahabari  mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo.
sn4
Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya Wanachama waliojitokeza kumlaki barabarani mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

BALOZI LIBERATA MULAMULA AWAAGA TAMCO RASMI, ASEMA UMOJA NA MSHIKAMANO WAO NI MFANO WA KUIGWA NA JUMUIYA ZINGINE

July 13, 2015

Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani, 
Mhe. Liberata Mulamula leo jioni siku ya Jumapili July 12, 2014 alijumuika na wanajumuiya ya Kiislam ya DMV (TAMCO) katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na jumuiya hiyo na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.
 
Katika hotuba yake. Mhe. Liberata Mulamula  aliwakuwakumbusha alipokuja kwa mara ya kwanza kulitumikia Taifa kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani , Jumuiya hiyo ndio iliyomkaribisha kwa mara ya kwanza hapa DMV na leo nimerudi tena kuagana nanyi rasmi. Mhe. Liberata Mulamula aliwashukuru TAMCO kwa ushirikiano na mshikamano wao na kuzitaka Jumuiya zingine za Watanzania ziige mfano wao kwani TAMCO ni jumiya ya Kiislam iliyoimara, isiyotetereka na yenye uongozi makini. Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliushukuru uongozi wa TAMCO kwa kumkaribisha aje azungumze na Watanzania wanajumuiya ya TAMCO na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.
 
Uongozi wa TAMCO ulimuzawadia Mhe. Balozi Liberata Mulamula zawadi na yeye kutoa mchango wake wa mwaka kwa jumuiya hiyo inayo wakubali Watanzania wote bila kubagua rangi, kabila wala dini.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Watanzania DMV
(TAMCO)Ustadh Ally Mohamed akimlaki Mhe. Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulaula mara tu
alipowasili kwenye ukumbi wa park iliyopo Silver Spring, Maryland
nchini Marekani alipokuja yeye Mhe. Balozi akiambatana na mumewe Eng.
George Mulamula (hayupo pichani) na mwanae Alvin Mulamula (kulia)
kujumuika na wanajumuiya hao katika futari ya pamoja na kutumia futari
hiyo kuwaaga rasmi. Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo
Blog.

 Mtunza fedha msaidizi wa TAMCO. Bi. Asha Hariz(kushotao)
akiongozana na Mhe. Liberata Mulamula kuelekea ukumbini siku ya
Jumapili July 12, 2015 siku Mhe. Balozi alipopata mwaliko wa Jumuiya
hiyo wa kufuturu pamoja na kuwaaga rasmi.

Mwenyekiti wa TAMCO ustadh Ally Mohamed akiongea machache na baadae
kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea na
wanajumuiya.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Wanajumuiya wa TAMCO na
kuwaaga rasmi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akikabidhi mchango wake wa TAMCO wa
mwaka kwa mtunza fedha msaidizi ustadh Shamis Abdullah.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha
msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha
msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.

Picha ya pamoja

TAMASHA LA NCHI ZA JAHAZI 2015 KUFANYIKA NGOME KONGWE ZANZIBAR KUANZIA JULAI 18 HADI 26

July 13, 2015


 Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo (kulia), akizungumza katika mkutano na wadau wa filamu na wanahabari Dar es Salaam leo jioni kuhusu tamasha la nchi za jahazi litakalofanyika kuanzia Julai 18 hadi 26 mwaka huu Ngome Kongwe mjini Zanzibar.Kutoka kushoto ni Meneja wa Tamasha, Daniel Nyalusy na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando (kushoto), akizungumza kuhusu tamasha hilo kubwa la jahazi. Kulia ni  Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo.
 Meza Kuu. Kutoka kushoto ni Mratibu John Mchaina 'Simple', Mratibu Rehema Jonas, Mjumbe wa Bodi, Mahabobo Champs, Daniel Nyalusy, Ofisa Mtendaji Mkuu, Martin Mhando na Mjumbe wa Bodi, Fatma Allo.
 Baadhi ya wasanii watakaotoa burudani siku hiyo ya tamasha.
 Wanamuziki na  wasanii wa filamu  wakiwa kwenye mkutano huo wa kutambulisha tamasha hilo.
 Mtayalishaji wa muziki, Cadrake Touch (kushoto), Msanii wa filamu Mzee Chilo na mwanamuziki Elias Barnaba wakiwa kwenye mkutano huo.

Wanahabari na wadau wa filamu wakiwa kwenye mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

DK.SHUKURU KAWAMBWA APATA MPINZANI JIMBO LA BAGAMOYO

July 13, 2015

 Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew 
Juma Salum Yangwe.
 Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew Juma Salum Yangwe (katikati), akizungumza na makada na wanahabari wakati akitangaza nia mjini Bagamoyo mkoani Pwani Pwani jana. Kushoto ni Meneja wa Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe na Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga.
Meneja wa  Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga(kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mzee Abdallah Ngumbe akizungumza katika mkutano huo na wakati akimpa ushauri mbalimbali mtangaza nia huyo.
 Profesa Sameheni Kejeli akizungumza katika mkutano huo.
 Mzee Hussein Lugome akizungumza katika mkutano huo.
 Mama mzazi wa mtangania huyo, Mary Yungwe akiwasalimia makada wa CCM katika mkutano huo.
 Mtangaza nia huyo akipongezwa na vijana baada ya mkutano huo.
 Pongezi zikiendelea.
 Mkutano ukiendelea.
 
 Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Mtangazania huyo akiwa na wadau wake.
 
Na Dotto Mwaibale
 
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa amepata mpinzani baada ya kijana mdogo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Yungwe kutangaza nia ya ubunge katika jimbo hilo.
 
Akizungumza na makada wa CCM na waaandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana, Yungwe alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ili kusukuma maendeleo ya jimbo hilo ambayo yamekwama kwa muda mrefu.
 
“Wanaccm wenzangu na wazee wangu nimeamua kugombea nafasi hii ili niwatumikie kwani Bagamoyo naelewa vizuri na nitaendelea kuwa wilayani hapa ili tushirikiane katika mambo mbalimbali ya nmaendeleo” alisema Yungwe.
 
Yungwe alisema mambo atakayoyapa kipaumbele ni matatu, uchumi, Afya na Mawasiliano na kuwa hata penda aitwe mbunge bali aitwe mratibu na kuwa atakuwa na ofisi yake ya ubunge katika wilaya hiyo kwa lengo la kuwa jirani na wananchi zaidi.
 
Alisema maeneo mengine atakayoyafanyia kazi kwa kushirikiana na wananchi ni pamoja na kuinua uchumi wa jimbo hilo kupitia uvuvi, kuweka mipango mizuri ya kukusanya fedha kupitia viwanja vya michezo, utalii na mapato yatokanayo na uwekezaji na ujenzi wa soko la kisasa.
 
Alisema pia atashughulikia migogoro ya ardhi katika maeneo yote ya jimbo hilo yakiwemo ya Zinga na Pande ambayo inapunguza kasi ya maendeleo ya wananchi katika jimbo hilo.
 
Yungwe alisema kauli mbiu yake ni “Fikiri Tofauti, Badilika kwa Maendeleo Endelevu ya Bagamoyo.
 
Jimbo la Bagamoyo katika kpindi cha miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa lilikuwa likiongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

GGM Kili Challenge takes 38 Climbers to Uhuru Peak in the Fight Against HIV/AIDS

July 13, 2015

  A team of 38 Heroes who reached Uhuru Peak arrived safely at the foot of Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo, addressing the media (not in picture) joined by Michael Lomo (right) and Susan Elias (left) from Moyo wa Huruma, an orphanage centre that has benefited from the Kili Challenge basket of funds who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania. This is the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has raised about TZS 1.2B funds this year to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo, addressing the media (not in picture) at the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho, addressing the media (not in picture) at the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 13 year old Susan Elias, from Moyo wa Huruma Orphanage centre in Geita reached Uhuru Peak thus receiving her certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 Kili Challenge Ambassador from South Africa's Rugby team Mr. Krynauw Otto reached Uhuru Peak thus receiving his certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 13 year old Michael Lomo, from Moyo wa Huruma Orphanage centre in Geita reached Uhuru Peak thus receiving him certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 The Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho celebrating the 39 Heroes from 7 different countries that is Tanzania, Mali, Egypt, Indonesia, United States, Guinea and South Africa at Mweka Gate in Moshi, that decided to undertake Kili Challenge for a good cause to demonstrate their solidarity with the rest of Tanzania and the World in responding to the challenge of HIV/AIDS.
 Celebrating the 39 Heroes from 7 different countries that is Tanzania, Mali, Egypt, Indonesia, United States, Guinea and South Africa at Mweka Gate in Moshi, that decided to undertake Kili Challenge for a good cause to demonstrate their solidarity with the rest of Tanzania and the World in responding to the challenge of HIV/AIDS.
Some of the celebrated 39 Heroes from 7 different countries that is Tanzania, Mali, Egypt, Indonesia, United States, Guinea and South Africa at Mweka Gate in Moshi, that decided to undertake Kili Challenge for a good cause to demonstrate their solidarity with the rest of Tanzania and the World in responding to the challenge of HIV/AIDS.

BREAKING NEWZZZ......MAJAMBAZI YATIKISA KATIKATI YA JIJI LA DAR LEO MCHANA, YATIWA NGUVUNI NA JESHI LA POLISI

July 13, 2015


 Picha ya 1-2 ni mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi akiwa mikononi mwa polisi baada ya kutiwa mbaroni Mnara wa Saa maeneo ya Stesheni Dar es Salaam leo mchana kwa madai ya kupora kiasi kikubwa cha fedha. Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wanne.

 Kijana mwingine anayedaiwa kuwa ni jambazi akiwa amekamatwa.
 Watuhumiwa hao wanne wa  ujambazi  wakiwa ndani ya Noah kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi. Kulia ni askari Polisi.
 Askari kanzu (katikati), ndiye anadaiwa kuwadhibiti majambazi hayo kabla ya kujificha chini ya uvungu wa taxi zinazoegeshwa jirani na Mnara wa Saa katika makutano ya barabara ya Uhuru, Samora na Nkruma.
 Gari lenye namba T 976 BKK walilokuwa wakitumia majambazi hayo liondolewa eneo la tukio kupelekwa kituo kikuu cha polisi.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio.
 Askari Polisi wakilipekua gari walilokuwa wakitumia watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi.
 Upekuzi ukiendelea.
Maofisa wa polisi wakiteta jambo eneo la tukio baada ya kuwakamata majambazi hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)