WAFANYAKAZI WA MGODI WA BULYANHULU WAFANYA SHEREHE KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2018 'SIKUKUU YA FAMILIA'

January 06, 2018

Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga pamoja na familia zao wamesherehekea Sikukuu ya Familia ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’ kwa ajili ya kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018.

WANANCHI WA GAIRO WAFURAHIA UJENZI WA BARABARA YA LAMI

January 06, 2018
Mkuu wa Wilaya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (aliyevaa kiti jekundu la drafti) akimuonyesha Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby madhara ya miundombinu kwa mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani humo.
Mbunge wa Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby, akielezea hali ya barabara kwasasa na jinsi ilivyokuwa zamani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Agnes Mkandya akifafanua jambo.
Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro, Kilian akielezea jambo mbele ya viongozi wa wilaya ya Gairo walifika kutembelea barabara hiyo kujionea eneo lililoadhiriwa na mvua..
Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania (TARURA), Gairo Bw. Simon akielezea jambo wakati wa ziara hiyo. Pembeni kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe na (wa kwanza kulia) ni Mbunge wa Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby wakiwa na viongozi wengine.
--- Na Mwandishi Wetu.
Wananchi wa Wilaya ya Gairo wametoa shukrani zao za pekee kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuwawezesha kupata barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 3.5.
Hayo yamezungumzwa na Kata ya Magoweko mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa ziara ya viongozi wa wilaya ya Gairo walipofanya ukaguzi wa barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo hatua za mwisho kumalizika.
"Wana Gairo tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwani barabara ya lami ni muujiza hatukuwahi kuota kama itatokea," walisema wakazi hao.
Viongozi hao ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe, Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby, Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Bw. Shabani Sajilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Meneja TARURA. Bw. Simon, Wajumbe KUU (W) nk walifanya ziara hiyo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea Wilayani.
Aidha dhumuni rasmi la ukaguzi huo ilikuwa ni kuhakikisha ujenzi huo unaisha kwa wakati ambapo barabara inatakiwa kukabidhiwa Januari mwaka huu.
Barabara hiyo ni matokeo ya ahadi ya aliyekuwa Waziri wa Ujenzi ambaye kwa sasa ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Gairo miaka mitatu iliyopita  kwenye mkutano wa hadhara ambao Mgeni Rasmi alikuwa rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
-- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

WAZIRI UMMY AKABIDHI MIFUKO 200 YA SARUJI KWA SHULE YA SEKONDARI MAWENI.

January 06, 2018
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akichimba msingi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwenye shule ya sekondari ya Maweni Jijini Tanga wakati alipokwenda kushiriki msaragambo na kukabidhi mifuko 200 kwa ajili ya kusaidia ujenzi huo
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akichimba mtaro huo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Sekondari Maweni Jijini Tanga leo Ambapo WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga
 alipokwenda kushiriki msaragambo na kukabidhi mifuko 200 kwa ajili ya kusaidia ujenzi huo
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akichimba msingi wa ujenzi wa vyumba vitatu kwenye shule ya sekondari ya Maweni Jijini Tanga wakati alipokwenda kushiriki msaragambo na kukabidhi mifuko 200 kwa ajili ya kusaidia ujenzi huo
Sehemu ya mifuko ya Saruji iliyotolewa na   WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga
  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga katikati akipokea cheti cha kutambua mchango wake kusaidia maendeleo ya Jiji la Tanga kutoka kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj  Mustapha Selebosi kushoto ni Diwani wa Kata ya Maweni,Joseph Calvas
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj  Mustapha Selebosi kulia akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wao katika kuinua sekta ya elimu kwenye Kata ya Maweni Diwani wa Kata hiyo kushoto  Joseph Calvas
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj  Mustapha Selebosi katika akimshukuru  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kulia kwa kusapoti elimu katika Jijini hilo baada ya kupokea mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Sekondari Maweni
Afisa Elimuy Sekondari Jiji la Tanga,Lusajo Gwakisa akizungumza na waandishi wa habari ambapo walimshukuru WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kulia kwa kusapoti elimu katika Jijini hilo baada ya kupokea mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Sekondari Maweni

 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akisaini kitabu cha wageni katika shule ya Sekondari Maweni Jijini Tanga katikati  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj  Mustapha Selebosi kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Ramadhani Posi
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akiteta jambo na  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Ramadhani Posi
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akipiga picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Maweni Jijini Tanga
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga katikati akiteta jambo na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Maweni Zawadi Ponera kulia
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akitembelea maeneo mbalimbali katika shule hiyo kushoto ni diwani wa Kata ya Maweni,Joseph Calvas na kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Zawadi Ponera

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akimsikiliza kwa umakini Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaji Mustapha Selebosi kulia ni Kaimu Mhandisi wa Jiji la Tanga Mussa Mkomola (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU PAMOJA NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

January 06, 2018
Picha namba 1-6. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akisali pamoja na watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi pamoja na wafanyakazi wengine wa Taasisi hiyo mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wapishi wanaofanya kazi ndani ya Hospitali ya Muhimbili wakati akitoka kuona wagonjwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Kaka wa Profesa Anna Tibaijuka ajulikanye kwa jina la Richard Kajumulo ambaye amelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na manesi wanaohudumia wagonjwa katika Wodi ya ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na manesi wanaohudumia wagonjwa katika Wodi ya ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mzee Hamadi Lila aliyekuwa akilia kwa furaha mara baada ya kumuona Rais alipofika katika wodi ya Sewahaji.-PICHA NA IKULU