MBUNGE RITTA KABATI KUSAIDIA UJENZI WA OFISI TATU ZA CHAMA CHA MAPINDUZI MANISPAA YA IRINGA

February 24, 2017
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akimkabidhi mifuko ya saruji kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama katika kata ya Ruaha kwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa katika eneo la uwanja wa kujenga ofisi ya kata ya Ruaha
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akibadilishana mawazo na katibu wa ccm manispaa ya Iringa Nuru Ngereja
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa hama hicho wa kata ya ruaha
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akipokelewa na wanachama wa mtaa wa kigamboni mkoani Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameanza kusaidia Ujenzi wa ofisi za Matawi ya CCM katika kata mbali mbali za Jimbo la Iringa mjini kama sehemu ya majukumu yake ya kukijenga chama hicho ambacho kilipoteza kiti cha ubunge na halmashauri kuchukuliwa na wapinzani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za Tawi Kigamboni na Ruaha ,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya kutekeleza ilani na maadhimio ya miaka arobaini ya chama cha mapinduzi.
“Nakipenda chama changu ndio maana napigana sana kuhakikisha chama cha mapinduzi mkaoni mhapa iringa kinarudi mahala pake na kuhakikisha kinaaminika kwa wananchi na wanachama wa  manispaa ya Iringa”.alisema Kabati 

Hata hivyo Kabati alisema kuwa ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili kuona ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ama sita kila tawi linakuwa na ofisi yake ya tawi na aliwataka wanachama wa CCM kushikamana na kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pamoja na kujihusisha na shughuli nyingine za kijamii

"Haiwezakani chama kikubwa kama hiki kukosa ofisi za matawi wakati tunamaeneo mengi ya kujenga ofisi nitakikisha tunashirikiana na wanachama na wananchi wengine kujenga hizo ofisi ili kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli ambaye anapambana kuhakikisha cha mapinduzi kinakuwa chama cha wananchi wa chini na sio matajiri pekee yao".alisema Kabati

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza aliwataka wanachama kuwa kusahau yaliyopita na kuanza kujenga chama upya.
“Tulipoteza halmashauri ya Iringa na jimbo hivyo inabidi tukae chini na tujipange upya kukijenga chama maana tunajua kwa kujenga ofisi za matawi zitatusaidia kurudisha hadhi na hali ya chama hapa manispaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wote bila kuchagua chama”.alisema Kiponza 

Kiponza alimshukuru mbunge wa viti maalumu Ritta kabati kwa mchango anaoutoa kwa kuleta maendeleo katika manispaa ya Iringa hasa ukiangalia ujenzi wa majengo mbalimbali ya shule,taasisi za kidini,taasisi za kijamii hapa kujenga majengo ya chama.

Lakini Kiponza alimtaka mbunge Kabati kuwasaidia wananchi wanaodhurumiwa na kunyang’anywa mali zao katika manispaa ya Iringa.

“Hapa kigamboni kunawananchi wanapigwa na viongozi wa mtaa kwa kuwa wapo CCM tu na wamenyang’anywa kituo cha kuchotea maji ambacho kilikuwa mradi wa chama cha mapinduzi hivyo lazima upambane kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na mali za chama zinarudi kwenye chama”.alisema Kiponza

 Naye Katibu wa CCM manispaa ya Iringa Nuru Ngeleja alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha ofisi zote za chama zinajengwa na zinakuwa katika ubora unaotakiwa kutokana na ukubwa wa chama cha mapinduzi(CCM) na kuahidi kuwa wataendelea kumuunga mkoano Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr John Pombe Magufuri.

“Sisi tunafanyakazi ya kumsaidia mwenyekiti wetu wa chama ambaye ni Rais wetu kwa kufanya kazi na kuisimamia serikali kufanya kazi kwa uhakika na kuwafaikia na kuwatumikia wananchi waliowaweka madarakani mpaka sasa”. Alisema Ngereja

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akutana na Rais wa Ivory Coast Mheshimiwa Alassane Ouattara jijini Abidjan

February 24, 2017
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 23Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Ivory Coast, Mhe. Alassane Ouattara katika Ikulu yake jijini Abidjan.. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Waziri wa Fedha na Waziri wa Elimu.
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Ouattara wamezungumzia hali ya elimu bara la Afrika na Ivory Coast kwa ujumla na haja ya kufanya mageuzi makubwa katika elimu ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea.
Rais Mstaafu Kikwete amempongeza Rais Outtara kwa jitihada kubwa anayoifanya kuinua elimu nchini mwake. Kwa mujibu wa utafiti wa Kamisheni, Ivory Coast iko katika nafasi nzuri ya kufikia viwango vya juu vya ubora wa elimu vya nchi zilizoendelea iwapo itaongeza juhudi ya kufanya mageuzi kulingana na mapendekezo ya Kamisheni hiyo.
Rais Outtara amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini mwake. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
Akiwa jijini Abidjan, Rais Mstaafu ametembelewa na viongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika na Watoto  wa Watanzania hao ambao walitaka kujua kuhusu masuala ya uongozi na maisha baada ya kustaafu. 
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa na Rais Alassane Ouatara wa Ivory Coast jijini Abidjan katika Ikulu ya nchi hiyo.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi ripoti ya 'Kizazi cha Elimu' Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazungumzo na Rais Alassane Ouattara. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Daniel Kablan Duncan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Rais Alassane Ouattara baada ya mazungumzo yao   Ikulu ya Ivory Coast.

 Rais MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia mazungumzo na baadhi ya watoto wa Watanzania waishio Ivory Coast waliomtembelea hotelini kwake Abidjan
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasainia autograph  watoto waliomtembelea hotelini kwake  jijini Abidjan

MAFUNZO YA UKAKAMAVU KIDATO CHA KWANZA JITEGEMEE JKT SEKONDARY YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

February 24, 2017
 Mgeni rasmi wa kufunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Jitegemee Sekondari Mgulani JKT, Meja Haule (katikati), akiwa na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga, Msanifu wa Shule, Meja Rehema Wanjara, , Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila na Makamu Mkuu wa Shule Taaluma, Ema Mosha.

REA III kuja na umeme mwingi

February 24, 2017


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa, utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA)utakuja na umeme mwingi kutokana na kujengwa kwa njia za kusafirisha umeme wenye msongo mkubwa.

Profesa Muhongo aliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa REA Awamu ya Pili , katika Wilaya za Rorya na Butiama mkoa wa Mara ambapo pia alieleza mipango ya Serikali katika utekelezaji wa REA awamu ya Tatu.

Prof. Muhongo aliongeza kuwa, REA III itajikita katika kuyafikia maeneo yaliyorukwa katika awamu ya I na ya pili, kuyafikia maeneo ambayo hayajafikiwa kabisa na nishati hiyo, vilevile awamu hiyo itajikita katika matumizi ya nishati jadidifu hususan katika maeneo yote ya visiwani.

Vilevile, alisema kuwa, lengo la Serikali kupeleka umeme mwingi na wa uhakika katika maeneo ya vijiji ni kuchochea mapinduzi ya viwanda vidogo vidogo na hivyo kuwataka wananchi kuachana na siasa badala yake wajikite katika shughuli za kiuchumi ili kuchochea maendeleo ya kijamii na Taifa kwa ujumla.

" Wananchi tunatakiwa kuachana na siasa badala yake tujikite katika shughuli za kiuchumi. Tuzungumzie uchumi na maendeleo. Umeme ndio kichocheo kikuu cha uchumi na ndiyo maana Serikali inatekeleza mradi wa REA ili kufikia azma hiyo," amesisitiza Prof. Muhongo.

Pia, Prof. Muhongo alisisitiza suala la fidia katika utekelezaji wa REA awamu ya tatu na kueleza kuwa, serikali haitatoa fidia kwa wananchi watakaotoa maeneo yao ili kupitisha nguzo za umeme na kueleza kuwa, wanaotaka fidia wachague kati ya fidia au kupelekewa nishati hiyo. REa Awamu ya Tatu inatarajia kutekelezwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi Hamis Komba alimweleza Profesa Muhongo kuwa, Shirika hilo limeridhia kutoa sehemu ya eneo lake katika mgodi wa Buhemba linalotumiwa na wachimbaji wadogo ili waweze kulitumia kwa shughuli za uchimbaji madini .

Mhandisi Komba amesema kuwa, eneo hilo linaendelea kupimwa ili kujua ukubwa wake na kuongeza kuwa shughuli ya kuligawa kwa vikundi 13 vilivyojiandikisha litafanywa siku ya jumatatu tarehe 27 Februari, 2017, baada ya ukubwa wa eneo husika kujulikana.

Kutokana na kutoa eneo hilo ambalo lilikuwa linamilikiwa na STAMICO, Mhandisi Komba amewataka wachimbaji watakaopewa eneo husika kufanya shughuli za uchimbaji unaozingatia usalama, Sheria na taratibu za uchimbaji madini.

Profesa Muhongo alitembelea Wilaya za Rorya na Butiama katika Kata za Mirwa, Tai na Muriaza tarehe 23 Februari,2017
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiongea jambo wakati akiwaeleza wananchi na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Nyamagongo Wilaya ya Rorya kuhusu utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya III. Shule hiyo ni miongoni mwa maeneo ambayo yatafikiwa katika mradi wa REA awamu ya Tatu. Wengine wanaofuatilia ni Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos Maganga, (katikati) Meneja wa TANESCO Wilaya ya Rorya, Sospeter Kswahili (wa kwanza kulia). Wengine ni Mtaalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini Mhandisi Emmanuel Yesaya na Mkandarasi wa Kampuni ya Angelica International.
Afisa Uhusiano na Huduma za Jamii kwa Wateja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), James Vesso, akitoa elimu kuhusu Kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa Kijiji cha Muriaza Kata ya Muriaza Wilaya ya Butiama wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini kijijini hapo. Kifaa hicho hakihitaji mtandao wa umeme katika nyumba.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos Maganga, akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini wananchi wa Nyamagongo ambapo Waziri na wataalam wa REA na TANESCO wameeleza kuhusu utekelezaji wa REa Awamu ya Pili na ya Tatu. Wengine ni Mameneja wa TANESCO, Wilaya ya Rorya na Mkoa wa Mara, na Wataalam kutoka REA na TANESCO.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha na viongozi wa Mkoa, wakimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kukagua miradi ya REA awamu ya II na kueleza mipango ya Serikali kuhusu utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu.