WAZIRI NYALANDU MGENI RASMI MAONYESHO YA UTALII MKOANI TANGA KUANZIA YATAKAYOANZA KESHO

January 19, 2015
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonyesho ya utalii ya kwanza mkoani Tanga yatayaoanza Januari 20 mpaka 24 mwaka huu kwenye viwanja vya Mwakidila mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa Habari,Mwenyekiti wa Wafanyabiashara mkoa wa Tanga(TCCIA) Paul Bwoki alisema kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi na waziri Januari 22 na kufungwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga.Said Magalula.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Tanga (TCCIA) Paul Bwoki akizungumza na waandishi wa habari juzi kuhusu maonyesho ya utalii yatayaoanza kufanyika mkoani Tanga kuanzia Januari
20-24 mwaka huu kwenye viwanja vya mwakidila jijini Tanga kushoto kwake ni Katibu Tawala Msaidizi Mazingira Mkoa wa Tanga,Hassani Kayombo kulia ni Afisa Biashara wa Jiji la Tanga Lucy Marandu
Alisema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo yanaendelea vizuri ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya utalii mkoani hapa ikiwemo wanyama kama vile Simba, Chui, Mamba, Ngamia, Fisi na wengine wakubwa watakaokuwa kwenye mabanda maalumu.

Aidha alisema kuwa pamoja na kuwepo wanyama hao lakini watatumia fursa hiyo kuweza kutangaza vivutio vikubwa vilivyopo mkoani hapa ikiwemo mapango ya amboni, mbunga za wanyama zilizopo mkoani Tanga na vivutio vya asili.

Alisema kuwa lengo kubwa ni kutangaza fursa za utalii zilizopo mkoani hapa ikiwemo milima ya Usambara.

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea maonyesho hayo, Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Lucy Marandu alisema kuwa wamejipanga vizuri ikiwemo kuhamasisha wasafirishaji kujipanga kwa sababu maonyesho hayo yatashirikisha wadau wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa tayari jiji hilo limeshatoa eneo ambalo kutafanyika
maonyesho hayo ambapo maandalizi yake yanaendelea vizuri ikiwemo kuandaa sehemu za vivutio vya utalii vinavyopatikana mkoani hapa.

Kwa upande wake, Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi mkoani hapa, Aisha Kisoki alisema maonyesho hayo yatawasaidia kuutangaza  mkoa wa Tanga kwenye nyanya za utalii na vivutio vyake jambo ambalo litachangia kuinua uchumi