MHE. BALOZI WILSON MASILINGI AWA MGENI RASMI FUTARI YA PAMOJA DMV

June 18, 2017
Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta (kushoto) akimlaki Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi siku ya Jumamosi June 17, 2017 siku Mhe. Balozi alipokua mgeni rasmi kwenye futari ya pamoja inayoandaliwa na Jumuiya ya Waislam DMV (TAMCO) Silver Spring, Maryland.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akipokewa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam DMV (TAMCO) ustaadh Ally Mohamed mara tu alipowasili na kujumuika na wanajumuiya hao waislam wa DMV na marafiki zao katika futari ya pamoja iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring, Maryland.
mwenyekiti wa TAMCO ustaadh Ally Mohamed akimwongoza Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi ndani ya ukumbi.
Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta, mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi na The Maryland House of Delegates Legislative District 41 Baltimore City Mhe. Bilal Ali ambaye nae alialikwa na Jumuiya hiyo kwenye futari ya pamoja DMV.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi na The Maryland House of Delegates Legislative District 41 Baltimore City Mhe. Bilal Ali wakiongozwa na  mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo kwenye futari ya pamoja iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring, Maryland.
 Kutoka kushoto ni Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico mama Marystela Masilingi, Balozi Liberata Mulamula, Zawadi Sakapala na dada Jasmine wakipata futari.
 Picha ya pamoja
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

 Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja
Picha ya pamoja,

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA SIASA NA UONGOZI KWA KINA MAMA WA UWT

June 18, 2017
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi” akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum  Wanawake (CCM)  (MNEC) Bi. Khadija Hassan Aboud pamoja  na  viongozi  mbali mbali wa UWT Mkoa wa Mjini  Zanzibar mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mjini CCM uliopo Amani Unguja
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi” akiwahutubia  mamia  ya wanachama na viongozi  wa UWT Mkoa wa Mjini  Unguja, mara baada ya kufungua mafunzo ya Wanawake na Uongozi katika siasa huko  Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mjini CCM uliopo Amani Unguja
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini, Waridi Juma Othman akizungumza  na viongozi na wanachama  hao kabla ya kumkaribisha mgeni  rasmi afungue  mafunzo hayo  Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mjini CCM uliopo Amani Unguja.
 Mbunge wa Viti Maalum  Wanawake (CCM)  (MNEC) Khadija Hassan Aboud akitoa maneno ya shukrani kwa mgeni rasmi  Dkt. Abdulla Juma Saadalla “ Mabodi”  kabla ya kuanza mafunzo hayo.
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini, Waridi Juma Othman akizungumza  na viongozi na wanachama  hao kabla ya kumkaribisha mgeni  rasmi afungue  mafunzo hayo  Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mjini CCM uliopo Amani Unguja.
  Mkufunzi  wa Mafunzo  hayo  Emiley Nelson Fwambo  akizungumza na washiriki wa mafunzo  ya Wanawake  na Uongozi  katika siasa.
baadhi ya Viongozi na wanachama wa UWT walioudhuria katika mafunzo hayo wakifuatilia kwa umakini nasaha za mgeni rasmi  Dkt. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”  wakati  akizungumza mara baada ya kufungua  mafunzo hayo.( PICHA NA AFISI KUU ZANZIBAR).

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO DKT. TITO MWINUKA AWAHAKIKISHIA WATANZANIA MRADI WA UMEME WA GESI ASILIA WA KINYEREZI II UNAENDELEA KWA KASI

June 18, 2017
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini, (TANESCO), limewahakikishia watanzania kuwa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika kama ilivyopangwa.
Hakikisho hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240 za umeme.
“Niwahakikishie watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi II utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.” Alisema Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
Dkt. Mwinuka alifuatana na wakurugenzi watendaji wasaidizi, Mhandisi Abdallah O. Ikwasa, (anayeshughulikia Uzalishaji), Mhandisi Khalidi James, (anayeshughulikia uwekezaji miradi) na Mhandisi Kahitwa Bishaija (anayeshughulikia Usambazaji).
Dkt. Mwinuka alisema watanzania wanahitaji umeme ulio wa uhakika na kwamba Serikali kupitia TANESCO imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa watanzania na hivyo kuchangia pato la taifa.

“Kama mjuavyo serikali imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha Shirika linatekeleza miradi hii na tayari shilingi Bilioni 110 zimetolewa na serikali katika kutekeleza mradi huu wa Kinyerezi II.” Alifafanua Dkt. Mwinuka.

Awali Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephens S.A.Manda, alisema, wataanza kuingiza umeme kwenye gridi ya taifa kila mwezi kuanzia Desemba mwaka huu 2017 ambapo Megawati 30 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa.

“Tuna mashine 8 ambazo zitafua umeme huo kwa hiyo kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, tutaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na tutafanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kwani tunaelewa kuwa serikali ambayo imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda, tunaona umeme ni hitajio muhimu kwa hivyo kila tutakapokamilisha mtambo mmoja tunaingiza umeme kwenye gridi ya taifa hatutasubiri kuwasha mitambo yote minane.” Alisema Mhandisi Manda.
Mhandisi Manda alisema, mradi mzima ambao umeanza kutekelezwa rasmi Machi 3, 2016, utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 344,059,746.00 kati ya hizo asilimia 15 zimetolewa na serikali.

“ Kufikia leo Juni 17, 2017, asilimia 63 ya ujenzi wa mitambo imekamilika, na tunahakika ya kukamilisha ujenzi wa jumla kwa vile tayari mitambo yote inayohitajika imeshalipiwa na mingine iko njiani inaletwa nchini.” Alifafanua na kuongeza mitambo yote iliyoagizwa na TANESCO imo kwenye makontena 900 na tayari makontena 400 na ushee yamekwishawasili na baadhi ya mitambo imefungwa na tunatarajia mashine zingine kwenye hayo makontena yaliyosalia zitawasili nchini wakati wowote. Alisema.

Akizungumzia kuhusu makontena 20 yaliyokuwa yamezuiliwa na TRA bandarini, Mhandisi Manda alisema, taarifa hizo hazina msingi wowote kwani kiasi hicho cha makontena 20 ni sehemu ya makontena 900 na tayari TANESCO imeshalipa fedha hizo za kodi na mizigo hiyo imefika site.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Mwinuka ;pia alitembelea mradi wa umeme wa upanuzi wa Kinyerezi II ambako nako ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake. 


Mradi huo ambao unasimamiwa na Mhandisi Simon Jilima, utawezesha ongezeko la megawati 35 na hivyo Kinyerezin I ambayo inatoa Megawati 150 itakuwa na uwezo wa kutoa Megawati 185 za umeme.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na  Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi   Simon Jilima,(kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere, wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.




 Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda
 Meneja wa mradi wa upanuzi Kinyerezi IMhandisi Simon Jilima

ZIFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM

June 18, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Umaarufu wa Dar es Salaam kwenye shughuli za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu kuvizingatia vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa kuviona tu lakini bila ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana na wageni huja wakitokea nchi mbalimbali kujifunza.
 
Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi eneo la Oyster Bay, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba unaweza kujifunza na kufurahia mambo mengi pindi utakapotembelea maeneo yafuatayo.

Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni. Makumbusho haya awali yalifunguliwa mwaka 1940 kama kumbukumbu ya Mfalme George wa tano ambapo kihistoria huwarudisha watanzania nyuma walipotokea. Makumbusho haya huonyesha mabaki muhimu ya binadamu wa kale yaliyogunduliwa na Dkt. Leakey aliyoyachimbua kwenye bonde la Olduvai. Wageni wanaweza kujifunza urithi wa kitamaduni kutoka kwa makabila mbalimbali Tanzania pamoja na athari za biashara ya utumwa kipindi cha utawala wa kikoloni. Baadhi ya vitu vingine vinavyopatikana katika makumbusho haya yaliyopo mtaa wa Shaaban Roberts ni zana za jadi, desturi, mapambo na vyombo vya muziki.  
 
Kijiji cha Makumbusho. Takribani maili 6 kutokea katikati ya jiji, kuna kiji cha makumbusho ambacho kimehifadhi tamaduni za makabila zaidi ya 120 yanayopatikana Tanzania. Wageni wanaweza kuzunguka kwenye vibanda kadhaa vya nyasi vinavyopatikana pale kwenye ukbwa wa takribani hekari 15 na kujionea ufundi wa kijadi katika kuchora, ufumaji na uchongaji. Kijiji hiki kinachopatikana eneo la Kijitonyama, barabara ya Bagamoyo pia huwa na ngoma na michezo ya jadi pamoja shughuli nyingize za kitamaduni.

Sanamu la Askari. Likiwa limetengenezwa kwa shaba sanamu hili ya Askari huonyesha askari akiwa amevalia vazi rasmi lililotumika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia huku ncha ya mbele ya bunduki (kama kisu) ikiwa imeelekezwa karibu na bandari iliyopo jirani. Sanamu hili huonyesha kama kumbukumbu ya majeshi ya waafrika walioshiriki kupigana kwenye vita ya Kwanza ya Dunia na linapatikana mtaa wa Azikiwe na Samora.
 
Boma la Kale. Likiwa limejengwa mnamo mwaka 1866 mpaka 1867 na Majid Bin Said, Sultani wa Zanzibar, Boma hili la kale ni jengo lenye umri zaidi ambalo linapatikana kwa sasa jijini Dar es Salaam. Jengo hili lilitumika kuwakarabisha wageni wa Sultani ambaye alikuwa na kasri lake pembeni yake. Vitu vya kuvutia kwenye jengo hili lililopo mtaa wa barabara ya Sokoine ni namna lilivyojengwa kwa ndani vikiwemo mlango wa mbao kutokea Zanzibar na kuta zilizojengwa kutokana na matumbawe.

TIGO YAFUTURISISHA WATOTO YATIMA MIKOA YA MWANZA NA MBEYA

June 18, 2017
Mwanafunzi wa darasa la nne wa  Islamic Yatima Foundation Fadhira  Hamidu, akipokea msaada wa chakula kwa niaba ya wengine,  kutoka kwa Meneja Mauzo Mkoa wa Mwanza  wa Kampuni ya Tigo Kassim Aziz Kassim, wakati wa hafla ya makabidhiano eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.Msaada wa Sh 3.5 Milion ulipokelewa
 Mwanafunzi wa darasa la saba wa  Islamic Yatima Foundation Zahor Hamoud, akipokea msaada wa chakula kwa niaba ya wengine, kutoka kwa Meneja Mauzo Mkoa wa Mwanza  wa Kampuni ya Tigo Kassim Aziz Kassim, wakati wa hafla ya makabidhiano eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.Msaada wa Sh 3.5 Milion ulipokelewa
Wanafunzi wa Islamic Yatima Foundation, wakipata futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Tigo eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.
Wanafunzi wa Islamic Yatima Foundation, wakipata futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Tigo eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.
Meneja wa  Kampuni ya Tigo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ladislaus  Karlo (kushoto) akimkabidhi sehemu ya zawadi kutoka kampuni hiyo kwa Mhasibu wa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Nuru, kilicho Uyole Jijini Mbeya,Semu Mwansasu, (kulia) kabla ya wafanyakazi wa Tigo Mbeya kushiriki pamoja na watoto hao kwenye futari iliyoandaliwa na Tigo ofisi ya Mbeya.
Meneja wa  Kampuni ya Tigo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ladislaus  Karlo  akikabidhi sehemu ya zawadi kutoka kampuni hiyo kwa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Nuru, kilicho Uyole Jijini Mbeya,Semu Mwansasu, (kulia) kabla ya wafanyakazi wa Tigo Mbeya kushiriki pamoja na watoto hao kwenye futari iliyoandaliwa na Tigo ofisi ya Mbeya.