MTWARA ICHUNGUZWE SABABU ZA KUFELI KIDATO CHA PILI-MAJALIWA

MTWARA ICHUNGUZWE SABABU ZA KUFELI KIDATO CHA PILI-MAJALIWA

January 17, 2017
 MAJALIWA CU ELIMU MTWARA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi Wazara wa Elimu Sayansi na Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili kutoka mkoani humo.
Pia ameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Januari 17, 2017) wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Kwa mujibu wa matokeo hayo kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa, Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka  huku ya Tanga ikiwa ni Nywelo.
“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara wakafuatilie kwa kina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” amesisitiza.
Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia Waziri Mkuu amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo mabaya na sasa inafanya vizuri na wahakikishe shule za mikoa hiyo hazishuki na badala yake ziendelee kupata matokeo mazuri zaidi.
Awali, akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato cha pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa ukiongozwa na mkoa wa Geita.
Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JANUARI 17, 2017.
Mwenyekiti wa NEC awataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uchaguzi

Mwenyekiti wa NEC awataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uchaguzi

January 17, 2017

AQO
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na Msimamizi wa Uchgauzi wa Jimbo la MorogoroMjiniBw. John Mgalula wakati alipotembelea na kufuatilia mwenendo wa uchgauzi wa Kata ya Kiwanja cha Ndege katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, inayotarajia kufanya Uchaguzi Mdogo tarehe 22 Januarimwaka 2017.Picha na Hussein Makame-NEC-Morogoro.
……………..
Hussein Makame, NEC- Morogoro
Mwenyekitiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage amewatakawasimamizi wa Uchaguzi mdogounaotarajiwakufanyikaJumapili hii kuwa wahakikishewanazingatiaSheria, Kanuni na Taratibu ili kuepushakubatilishwa kwa Uchaguzi.
Jaji (R) Kaijage aliasema hayo baada ya kupokea taarifa ya mwenendowa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Kiwanja cha Ndegeiliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mogoro kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la MorogoroMjini.
Alisemakutozingatiwakwataratibu za Kisheria za Uchaguzi kunawezakusababishakubatilishwa kwa Uchaguzi mzima na hatimayekuisababishiaSerikalihasarakubwa, hivyo amemkumbushaMsimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha wanafuataSheria.
“Kwa kuwa miongozo yote mnayoya Sheria, KanuninaTaratibuza Uchaguzi, hakikishenimnatekelezakilawajibu wa Kisheria katika zoezi hilikwa sababu kutozingatiwakwataratibu za Kisheriakunawezakusababisha Uchaguzi ukabatilishwa” alisemaJaji (R) Kaijage.
Akitoa taarifa ya mwenendowa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Kiwanja cha Ndege,Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la MorogoroMjini, Bw. John Mgalula, alisemamaandalizi ya Uchaguzi yanakwendavizuri na wanakamilishaujenzi wa baadhi ya vituo vya kupigiakura.
Alisemakamati za maadilizimeshaundana hadi wiki iliyopitazilikuwahazijapokeamalalamikoyoyoteingawajuziJumatatuwalitarajiakukutananawawakilishi wa vyama vya CHADEMA, CUF na CCM ili kuwakumbusha kuzingatia maadili ya Uchaguzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi waHuduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel KawishealimkumbushaMsimamiziwa Uchaguzi kuwafahamisha mapema watendaji wa vituo kuhusumalipo ya poshoya kazi yao ili kuepushasintofahamu.
Alisemawakati wa semina kwa wasimamizi wa vituo na makaraniwaongozaji ni vyema Msimamizi wa Uchaguzi akawatangazia watendaji hao kuhusu malipo ya posho kwani inawezakusababishavurugu na uharibifu wa vifaaiwapohawataridhika na malipo husika.
NayeMkuuwa Kanda ya Kati ya Uchaguzi wa Tume, Bi.SaadaKangetaalimsisitizaMsimamiziwa Uchaguzi kuwakumbushawasimamizi wa vituo au wasaidizi wao watumiemamlakamliyopewavizuri kwa sababu baadhi yao wanazitumiavibaya.
“Kuna wakatiinatokea baadhi ya wasimamiziwanapopewamamlaka ya kusimamiakituoanajionaanamamlaka ya kumuoneamtukwa sababu waligombana.Hivyowakumbusheniwatumiemamlakawaliyopewavizuri kwanikilamamlakainaSheria na Sheriazipo na zinatakiwakufuatwa” alisema Bi. Kangeta.
Alimkumbushamsimamiziwa Uchaguzi kuwatangaziawapigakurakuhakikimajina yao kwenye Daftari la Wapiga kuralililobandikwa kwenye vituo vya kupigiakura kwani kutofanya hivyo kunawezakusababishausumbufu siku ya kupigakura.

DKT. SHEIN, MZEE MWINYI WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MAMBO YA NJE KATIKA TAMASHA LA TATU LA BIASHARA ZANZIBAR

January 17, 2017


Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein akimsikiliza Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Othman Maalim Othman (kulia), wakati akitoa maelezo kuhusu majukumu ya Wizara hiyo kwa . Mwingine ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Amina Salum Ali. 
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein akipatiwa maelezo ya namna ya wajasiriamali wa Tanzania watakavyoweza kufaidika kwa kutumia soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka kwa Bi. Vivian Rutaihwa, Afisa Biashara kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Naibu Waziri (OR) wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Khamisi Juma Mwalim anbaye aliwahi kuwa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje akisaini Kitabu cha wageni katika Banda la Wizara hiyo. 
Rais mstaafu wa Awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipatiwa maelezo ya namna ya wajasiriamali wa Tanzania watakavyoweza kufaidika kwa kutumia soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka kwa Bi. Vivian Rutaihwa, Afisa Biashara kutoka Wizara hiyo.
Alhaji Ali Hassan Mwinyi akisaini Kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Silima Haji Kombo, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar naye alitembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje. 
Diwani wa Kata ya Magomeni huko Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa Bw. Tahir Bakari, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. 
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Amina Salum Ali akitoa hotuba ya kufunga Tamsaha la Tatu la Biashara ambalo ni sehemu ya shamrashamra ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi. 
Mhe. Waziri akikabidhi vyeti kwa baadhi ya washiriki waTamsaha la Tatu la Biashara. 

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA BODI YA MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA

January 17, 2017



Mhe Charles Mwijage akimkabidhi vitendea kazi Mhandisi Christopher Chiza Mwenyekiti mpya wa bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania baada ya uzinduzi wa bodi hiyo


Mhe Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji asisitiza mageuzi ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu yanayolenga katika kujenga viwanda na kupunguza biashara ya kuuza malighafi na ilenge kwenye kuhamasisha biashara za kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani. 

Hayo aliyasema kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendelo ya Biashara Tanzania (TanTrade) uliofanyika tarehe 16 Januari, 2017 katika ofisi za TanTrade zilizopo kwenye kiwanja cha Mwl J.K Nyerere barabara ya Kilwa. 

Mhe Mwijage amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ni kuhamasisha shughuli za biashara Tanzania na wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ni wizara ambayo matumaini mengi ya watanzania yameangalia huko hivyo watu wanategemea matumaini makubwa sana. 

Akaendelea kwa kusema kuwa kwa mwaka 2017 kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (DITF) yawe ya tofauti kwa watakaokuja kuonyesha bidhaa zao kutoka nchi za nje, waoneshaji hao waje na mashine za viwanda vidogo ili watanzania watakaokuja kuona na kununua mashine hizo ziweze kusaidia kuongeza thamani za bidhaa zao ili kasi ya kuuza malighafi nje ya nchi ipungue bali bidhaa za viwandani ziweze kuongezewa thamani ili kuweza kuuza nje ya nchi. 

Mhe Mwijage aliendelea kuiambia Bodi ya Wakurugenzi iliyoteuliwa kuwa kazi zote ambazo zilisimama zifanyiwe kazi mapema ili kueza kukamilisha maamuzi yote usiku na mchana akaongeza kwa kusema kuwa maamuzi ambayo hayakufanyika ni mabaya mno na gharama zake ni kubwa afadhali maamuzi ambayo yamefanyika ila mabaya hivyo asingependa kufanya maamuzi ya bodi bila bodi kumshauri ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. 

Akaongeza kwa kusema kuwa tunapoelekea kwenye uchumi wa viwanda Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yapaswa kwenda kuwafundisha watanzania ili waelewe kile wanachopaswa kwenda kukiuza nchi za nje na kuwashawishi wale wanaokuja kuonesha bidhaa zao nchini waje kuonesha vitu gani kwetu vyenye tija. Natamani maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es salaam (DITF) kuwe na viwanda vidogovidogo vingi, tuwashawishi wanaokuja kuonesha kwa kutumia teknolojia zao ila yatupasa kufanyaTantrade kutumia mwenyekiti wao wafanye survey kwa kuhusisha wataalam kama teknolojia zao zinakidhi haja ya mazingira ya nchi yetu na matakwa ya wananchi.

Mhe Mwijahe akatoa maagizo kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuulizia ofisi zote za serikali na za watu binafsi ni maonesho gani yaliyopo mwaka 2017 sababu kisheria maonesho yote Tanzania yanasimamiwa na tantrade hata wanaokwenda nje ya nchi kwenye maonesho mbalimbali wapate Baraka za TanTrade kwa kutambulika hivyo asionekane asionekane mtu anaenda bila kupata kibali kupitia TanTrade na pia kuhakikisha taasisi hiyo haitawanyi rasilimali zilizopo bali ikazane kuongeza trade volume za bidhaa za viwanda ziende kwa wingi nje ya nchi. 

Nae mhe Mhandisi Christopher Chiza Mwenyekiti wa bodi mpya ya wakurugenzi kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) alisema kuwa nguzo kubwa atakayotumia katika kutekeleza majukumu ni sheria iliyoanzisha mamlaka ya kuendeleza Biashara Tanzania ya mwaka 2009 na sheria zingine za nchi. 

Akaendelea kusema kuwa kwa uchache majukumu ambayo atakayosimamia ni pamoja na kusimamia na kujiridhisha kwamba mali za mamlaka zinazohamishika na zisizohamishika zinatunzwa na zinatumika vzuri kwa manufaa ya Umma, Kuelekeza mamlaka kubuni na kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha na kwa fedha zote zitatumika kwa manufaa ya umma, kusaidia mamlaka kubuni na kubaini fursa za biashara na kuziunganisha fursa hizo na wadau mbalimbali ili zijulikane ndani na nje ya nchi kuwawezesha wadau wengine wazichangamkie. Hivyo kama taasisi ya muungano ambayo sehemu kubwa inawagusa makundi mbalimbali ya wazalishaji hawana budi kupanua wigo wa huduma hizo ilikuwafikia kwa ukaribu. 


Mnamo Desemba 17, 2016 Mhe Dkt John Magufuli Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na kumteua Mhandisi Christopher Kajolo Chiza kuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo na kufuatiwa uteuzi wa wajumbe wa bodi hiyo uliofanywa na Mhe Charles Mwijage Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji.

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA UTOAJI WA TAARIFA KWA UMMA

January 17, 2017


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na  baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass(kushoto) akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa IPP Media upande wa Televisheni wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  alipotembelea Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza mara baada ya kuwasili katika kampuni ya IPP media kwa ajili ziara yake ya kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya Kampuni hiyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipata maelekezo kutoka kwa mmoja ya wafanyakazi wa Ipp Media kuhusuana na ufanyaji kazi wa vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.


ZINGATIA HAYA ILI KUREJESHA ARI YA KUFANYA KAZI BAADA YA LIKIZO

ZINGATIA HAYA ILI KUREJESHA ARI YA KUFANYA KAZI BAADA YA LIKIZO

January 17, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

IWAPO unazitambua vizuri barabara za jiji la Dar es Salaam, basi utagundua kwamba kuna tofauti kubwa kwenye msongamano wa magari ukilinganisha na kipindi cha sikukuu. Hali hiyo imetokana na idadi kubwa ya watu kurejea jijini kuendelea na shughuli za kazi, ambapo wengi walikuwa kwenye likizo na mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Mwezi Januari ni mgumu sana miongoni mwa watu wengi wanaorudi maofisini kutokana na uchovu uliotokana na mapumziko ya kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka. Hivyo huwawia ugumu wengi wao kuendana na mazingira ya kazi ambayo huyaona ni mapya kutokana na kulewa starehe za mapumziko.

Zifuatazo ni mbinu chache ambazo Jumia Travel (www.travel.jumia.com) inakushauri kuzifuata ili kuhakikisha unarudisha mawazo na ari yako kazini kama ilivyokuwa awali.

Tegesha ‘kengele kwenye saa’ ya kukuamsha mapema asubuhi

Najua kwamba kipindi cha mapumziko watu huamka muda wanaoutaka bila ya wasiwasi wa kuwahi ofisini. Kutokana na sababu hiyo huwa hakuna haja ya kutegesha kengele kwenye saa ya kukuamsha asubuhi, basi kama ulifanya hivyo sasa huna budi kuirudisha ili uweze kuwahi shughuli zako.

Anza kwa kumalizia ‘viporo’ ulivyovibakisha

Sio watu wote wanaoenda likizo wanakuwa wamemaliza kazi zao za ofisini, kwani huwa haziishi hata hivyo. Kwa hiyo, pindi unaporudi ofisini kitu cha kwanza ni kuhakikisha kwamba unamalizia viporo vya kazi vyote ulivyoviacha ili kuuanza mwaka na majukumu mapya. 

Ulizia kwa wafanyakazi wenzako kazi zilizofanyika wakati wewe hukuwepo

Haimaanishi wewe ukiwa mapumzikoni kwamba kazi haziendelei ofisini. Ni muhimu kuulizia kazi zilizofanyika wakati wewe haupo ili uende sawa na wenzako au kufahamu yapi ni majukumu yako.

Fanya mazoezi ili kuweka mwili na akili yako katika hali nzuri

Mazoezi ni tiba kubwa sana kwa afya ya mwili na akili, hii itakufanya urudi katika hali yako ya kawaida ili kufanya kazi kama kawaida. Unaweza kufanya mazoezi asubuhi au baada ya kumaliza shughuli zako jioni pindi unaporudi nyumbani. Mazoezi yanaweza kufanyika katika vituo maalumu vilivyowekwa au kwa kukimbia au kutembea pembezoni mwa barabara.
  
Jifanyie tathimini kwa uliyoyatimiza mwaka uliopita

Kipindi unachotoka mapumzikoni kinafaa kutumika kwa kufanya tathimini juu ya yale uliyoyatimiza mwaka uliopita. Kwa kufanya hivyo utajua kama ulifanikisha malengo uliyojiwekea au kutoyatimiza ili kuweka mikakati thabiti kwa mwaka huu unaoanza.

Omba ushauri 
Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kwa uwezo na utaalamu tulionao katika kukabiliana na mabadiliko katika miili yetu. Hivyo tunashauriwa kuomba msaada kutoka kwa wakuu wetu wa kazi kutokana na uzoefu walionao, kwa sababu wao pia walipitia na wanaifahamu hali hiyo. Lakini pia kuwaona wataalamu wa afya kwa ajili ya ushauri zaidi ni muhimu.

Zipo mbinu kadhaa za kukabiliana na hali ya uchovu au kutokujisikia kufanya kazi baada ya kurudi kutoka mapumzikoni. Jumia Travel (www.travel.jumia.com) inakushauri kuzifuatilia hizo chache kwani zitakusaidia sana ili usiharibu kazi kwani ndio msingi wa maisha na Taifa lolote katika kuleta maendeleo. 

WAZIRI MKUU AONGOZA KUZINDUA DUKA LA BOHARI YA DAWA (MSD), MPANDA, MKOANI KATAVI

January 17, 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Dawa la Bohari ya Dawa (MSD), Mpanda mkoani Katavi. Kutoka shoto mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa  Katavi, Peter Mselemu, Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali mstaafu Raphael Muhuga. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.


Jiwe la Msingi.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu wakifurahi wakiwa ndani ya duka hilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa MSD.
Mwonekano wa duka hilo la MSD, mkoani Katavi.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema utaratibu wa MSD wa kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji litaboresha upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama za kununua dawa kutoka nje ya nchi.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la dawa la MSD,  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, ambalo linaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka 7 ya dawa nchini.

Waziri Mkuu pia amesema kwa mwaka huu wa fedha shilingi Bilioni 251 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba ili kupunguza changamoto za uhaba wa dawa na kueleza kuwa shabaha ya serikali ni kufikia asilimia 95-100 ya upatikanaji wa dawa hadi itakapofika mwezi Juni, 2017.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa duka hilo wataliendesha kwa mwaka mmoja tu,na kisha kulikabidhi kwa Halmashauri ili iliendeshe na kuongeza mapatao yao.

Kwa upande wa upatikanaji wa dawa, Bwanakunu amesema kuwa kwa sasa fedha sio tatizo,na dawa zinaendelea kuagizwa kulingana na mahitaji. 

TIGO YAZINDUA TWENDE APP KUSAIDIA HUDUMA YA USAFIRI WA TEKSI NCHINI TANZANIA

January 17, 2017


 Mkuu wa Zana za Kidijitali wa Kampuni ya Simu ya Tigo,  Tawonga Mpore (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuzindua Twende APP kwa ajili ya kusaidia huduma ya usafiri wa teksi nchini. Kulia ni Mkuu wa Utawala na Fedha wa DTBi ambao ni wawezeshaji wa mradi huo, Mramba Makange na Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu wa Costech,  Dk.Digushilu Mafunda.
Ofisa Mtendaji na Muasisi wa Twende App, Justin Kashaigili, akielezea jinsi ya kutumia mfumo huo kupitia simu ya mkononi.

 Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu wa Costech,  Dk.Digushilu Mafunda (katikati), akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassan Mshinda.
 Wadau mbalimbali na waandishi wa habari wakiwa 
kwenye uzinduzi huo.
 Wapiga picha wakichukua tukio hilo.
Uzinduzi ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imezindua huduma mpya ya kidijitali inayoitwa Twende App ambayo ni suluhisho la kuita teksi na hivyo kuwapatia wateja wake huduma sahihi na  wanayoimudu ya usafiri wa teksi nchini Tanzania.

Kwa kuunganishwa moja kwa moja na madereva wa teksi, huduma hiyo inawawezesha watumiaji kufurahia kiwango cha chini kuliko ambavyo wangetumia njia nyingine mbadala za mitaani. Twende App itakuwa na mawasiliano ya madereva teksi, bajaj na boda boda ambao wamehalalishwa na vyama husika vya madereva.

Akitangaza huduma hiyo mpya katika mkutano wa wanahabari jijini Dar es Salaam leo asubuhi , Mkuu wa Zana za Kidijitali wa Tigo Tawonga Mpore  alisema, “Huduma hii ni kielelezo cha Tigo kujikita katika mageuzi ya mtindo wa maisha ya kidijitali kwa kutoa suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wateja wake. Tunaamini kwamba Twende App itatoa huduma nzuri kwa abiria kwa kuwaunganisha na madereva ambapo watapata huduma bora zilizo na gharama nafuu na zenye ufanisi wa hali ya juu.”

Mpore aliongeza: “Tunaamini kwa kutoa njia mbadala kwa usafiri uliopo wa teksi,  tunaweza kusaidia kuboresha  usafiri kwa ujumla nchini Tanzania. Tunafahamu msongamano wa vyombo vya usafiri  uliopo jijini kwa sasa; hivyo tunalenga kuwa sehemu ya suluhisho katika kutatua adha hiyo. 

Kimsingi tunaamini  kupunguza usumbufu  katika barabara za jijini  na kupunguza athari za kimazingira zinazotokana na  msongamano wa magari  ikiwa ni sehemu ya kukua kwa uchumi.”
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  Dk. Hassan Mshinda ambaye alisema: “Napenda kumshukuru mbia wetu Tigo ambaye kila mara  amekuwa mstari wa mbele  katika kuhakikisha wajasiriamali  wetu vijana katika teknolojia ya kisasa wanapata msaada muhimu katika kufikia malengo yao na kwa huduma  hii naamini itawapatia fursa mpya zenye manufaa  kwa madereva kote jijini.”

Akizungumza  wakati wa uzinduzi, Ofisa Mtendaji na muasisi wa Twende App, Justin Kashaigili alisema: “Nimesukumwa na kasi ya maendeleo ya miundo mbinu  na nguvu ya ujasiriamali hapa nchini. Ninategemea kuwapatia wakaazi wa jiji la Dar es Salaam chaguo wanalolimudu, rahisi na linalofaa kwa ajili ya  usafiri  salama.”

Akielezea jinsi ya kujiunga na huduma hiyo, Kashaigili alisema, “abiria analotakiwa kufanya ni kupakua Twende App katika simu yake  ambayo itamuunganisha na dereva moja kwa moja  badala ya kuhangaika kwenda mwenyewe kufuata  sehemu ilipo teksi. Huduma hii pia inatumia muda sahihi wa taarifa za dereva, mfumo hai wa satelaiti unaowezesha ramani  ya kufahamu sehemu alipo abiria  na kumuunganisha abiria mwenyewe na dereva aliyepo karibu na wakati huo huo kumwezesha dereva kutoa majibu.”

Twende App  hivi sasa  inatoa mbadala sahihi wa malipo  kupitia Tigo Pesa kwa namba binafsi za Tigo Pesa kwa madereva na inapatikana  katika mfumo wa Android na hivi karibuni itapatikana kwa watumiaji wa simu zilizo na mfumo wa iOs.



MAMLAKA YA BANDARI YASHAURIWA KUFANYA TARATIBU ZA KURASIMISHA BANDARI BUBU NCHINI

January 17, 2017

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (kulia) akielekea katika Gati namba moja la Bandari ya Tanga kuangalia shughuli mbalimbali zinazoendelea bandarini hapo. Penmbeni yake ni Mhandisi wa Bandari hiyo Bw. Saleh Sapi.

Na Adili Mhina, Tanga.
Mamlaka ya Bandari nchini imeshauriwa kuangalia taratibu za kurasimisha bandari bubu ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kuhakikisha bidhaa zinazopitishwa katika maeneo hayo zinakubalika kisheria. 

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati  timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilipofanya ziara katika Bandari ya Tanga kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tahmnini ya shughuli zinazotekelezwa bandarini hapo. 

Mwanri alieleza umuhimu wa kurasimisha bandari bubu baada ya kupata taarifa kuwa katika Mkoa wa Tanga pekee kuna bandari bubu takriban 42 ambazo zinaendesha shughuli mbalimbali bila  ya usimamizi wa Mamlaka ya Bandari. 
Mhandisi wa Bandari ya Tanga Bw. Saleh Sapi (mwenye t-shirt) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (koti jekundu) juu ya kina cha maji katika bandari hiyo. Upande wa kulia ni Bw. Jordan Matonya na Bi Anna Kimwela, wachumi kutoka Tume ya Mipango. Upande wa kushoto (mwenye miwani ya jua) ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Bibi Moshi Mtambalike.

RITA KABATI: WAPINZANI HAWATASHINDA UCHAGUZI MDOGO WA KATA YA IGOMBAVANU NA IKWEA

January 17, 2017
 
Mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati akimpigia kampeni mgombea udiwani wa kata ya Igombavanu na kuwataka wapinzani kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
 Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo
 Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga kura kumpigia kura nyingi diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe diwani wa kata ya Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo
Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho 

Na Fredy Mgunda,Iringa

MBUNGE wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati amewataka wapinzani kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
 
Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Makongomi mbunge Kabati aliwaambia wananchi kuwa jimbo la Mufindi kaskazini na wilaya ya Mufindi kwa ujumla ni ngome ya chama cha mapinduzi (CCM) hivyo wapinzani wasipoteze muda wa kupiga kampeni kwa kuwa hawawezi kushinda chaguzi zote za jimbo hilo.

Kabati alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Mufundi bado wanakipenda chama cha mapinduzi na wanahakika watashinda kutokana na mapokeo mazuri kutoka wapiga kura ambao wanazikubali sera za chama cha mapinduzi na wanaendelea kumuamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mimi nikiangalia naona nyuso za furaha tu hapa na nimepemda kuwa mmetukikishia kushinda uchaguzi huu basi furaha yangu itakuwa siku ile diwani wetu kutoka chama cha mapinduzi anatangazwa kuwa mshindi kwa kura nyingi,nawapenda na naomba mkipe kura nyingi chama cha mapinduzi”.alisema Kabati 

Naye mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga kura kumpigia kura nyingi diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe diwani wa kata ya Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo.

“Jamani nipeni huyu diwani ili tuendelee kufanya maendeleo kwa kuwa mimi mnaniamini basi naomba mpeni kura nyingi na kuondokana na maneno machafu kutoka kwa wapinzani kwani wapinzani hawana jipya saizi”.alisema Mgimwa 

Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo,alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua Rashidi Mkuvasa kwa kuwa ni kiongozi mzuri na atawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo.

“Tumeona wagombea wengi wakija hapa kupiga kampeni na kuomba kura kwa njia ya matusi na kuhamasisha kutomchagua kiongozi furani pasipo kutaja au kuongelea hata hoja za msingi kwanini wanaomba kura zetu” alisema Mhagama

Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho au kunakili namba za vitambulisho hivyo
.
“Tuwakatae viongozi wa namna hiyo kwa kuwa lengo lao ni kutaka kununua uongozi kwa nguvu ya pesa na kuwa wao sio chaguo la wanachi hivyo wananchi msithubutu kufanya hivyo mtapoteza haki yenu ya msingi na hamtampata kiongozi atakaye waletea maendeleo”.alisema Mkuvasa

Aidha wananchi wa kata ya Igombavanu katika jimbo la Mufindi Kaskazini wamempongeza mgombea udiwani wa kata kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Rashidi Mkuvasa kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuwapa matumaini kuwa atakuwa kiongozi mzuri na kuwaletea maendeleo katika kata hiyo.