KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENT YAIPIGA TAFU JUKWAA LA WAHARIRI MILIONI 14

April 05, 2017



KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement Tanga, kimesema moja ya faida yake imekuwa ikiipeleka katika masuala ya kijamii yakiwemo, Afya, Mazingira na Elimu.
Akizungumza mara baada ya Wahariri (Jukwaa la Wahariri TEF)  kumaliza  ziara ya kutembelea kiwanda cha Saruji kujionea shughuli ambazo zinafanywa, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart, alisema moja ya faida huipeleka kwa wananchi.
Alisema wamekuwa wakisaidia madawati, mifuko ya saruji na majengo pamoja na vyoo kwa shule ambazo zimekuwa zikihitaji msaada.
Akikabidhi shilingi milioni 14 kwa Jukwaa hilo, Swart alisema pesa hizo zinaweza kuwasaidia katika majukumu  yao mbalimbali ukiwemo mkutano mkuu ambao utafanyika kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deudas Balile, alisema amefurahishwa na uzalishaji wa Saruji pamoja na mipango kabambe kiwandani hapo.
Akizungumzia msaada huo, Balile alisema utasaidia katika masuala mbalimbali ya Jukwaa hilo ikiwa na pamoja na  mkutano mkuu wa Moshi kesho na kutoa shukurani na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano kama huo.



 Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri wa Habari (TEF), Deudatus Balile (kulia) , akipokea mfano wa hundi wa shilingi milioni 14 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji kiwanda cha Saruji cha Tanga  Simba Cement, Renhardt Swart, kusaidia jukwaa hilo katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.



Afisa Mawasiliano na Masoko kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga , Hellen Maleko, (kulia) akiwakabidhi hundi yenye mfano wa shilingi milioni 14 Wahariri wa Jukwaa la vyombo vya habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo ikiwa ni msaada katika mambo yao mbalimbali ukiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.

MISA-TAN YAWANOA WANAHABARI KANDA YA KASKAZINI JUU YA SHERIA MPYA YA HUDUMA ZA HABARI.

April 05, 2017
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Ltd,Jesse Kwayu akiwaongoza washiriki wa warsha inayotolewa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) juu ya changamoto zilizopo katika sheria mpya ya Huduma za Habari.
Baadhi ya Wanahabari kutoka mikoa ya Tanga,Arusha ,Manyara na Kilimanjaro wakishiriki katika warsha hiyo inayofanyika katika Hoteli ya Impala jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Luninga cha ITV mkoa wa Manyara,Charles Masanyika akichangia jambo wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi mkoa wa Manyara ,Joseph Lyimo akichangia jambo katika warha hiyo.
Wakili Msomi na Mwanahabari mwandamizi James Marenga akiwapitisha washiriki wa warsha hiyo katika vifungu mbalimbali vya sheria ya Huduma ya Habari.
Baadhi ya Washiriki.
Afisa Habari na Utafiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN) Sengiyumva Gasirigwa
Baadhi ya wanahabari wanaoshiriki warsha hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

TANZANITE ONE KUJENGA UPYA SHULE YENYE MADARASA MANNE NA WANAFUNZI 1126 

April 05, 2017
Mkurugenzi  mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma pamoja na viongozi wa serikali na wajumbe  wa kamati ya shule ya Songambele  akikagua madarasa ambayo hayatumiki  kutokana na nyufa baada ya shule kukumbwa na mafuriko na kutangaza kujenga madarasa  saba.




Mkurugenzi mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma akizungumza katika mkutano na wazazi wa shule ya msingi Songambele  ambayo ina uhaba wa madarasa na kutangaza kujenga madarasa  saba Mwaka huu ili kupunguza tabu waipatayo wanafunzi hao kwa kukoisa vyumba vya madarasa.

ANDREA NGOBOLE; PMT
Siku tatu baada ya kuripotiwa shule ya msingi Songambele iliyopo Mererani wilaya ya Simanjiro, yenye wanafunzi 1126 kusoma katika madarasa manne,Kampuni ya Tanzanite One imetangaza kujenga madarasa saba ili kuondoa uhaba wa madarasa katika shule hiyo.

Mkurugenzi  mwenza wa kampuni ya Tanzanite One,Faisal Shabhai amesema,baada ya kuona kwenye vyombo vya habari shida ya madarasa katika shule hiyo,wameamua kujitokeza kujenga shule hiyo.

Shabhai  alisema,Tanzanite one kama mwekezaji Katika migodi ya Tanzanite wanawajibu wa kusaidia masuala ya kijamii hasa kwa kuwa wananufaika na madini ya Tanzanite.

"Tunajua tunawajibu wa kusaidia jamii hivyo tutajenga madarasa  saba katika shule hii"alisema

Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro,Zuwena Omar  alishukuru kampuni Tanzanite One kwa msaada waliotoa kujenga madarasa hayo.

Omar alitoa wito kwa wawekezaji wengine waliopo Mererani kusaidia maendeleo ya Mererani.

Mwalimu  Mkuu shule hiyo.Mwanahamisi Mussa alisema wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa madarasa, matundu 40 ya vyoo,Nyumba za walimu na ofisi kwani wanafanyakazi chini ya miti.

MAKAMU WA RAIS ALIPOWAKARIBISHA SERENGETI BOYS NYUMBANI KWAKE  

April 05, 2017
1 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys  jijini Dar es Salaam alipowaalika  nyumbani kwake na kupata nao chakula cha jioni kabla ya vijana hao kuondoka Tanzania..kuelekea katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon, Serengeti Boys wanaondoka  Aprili 5 kuelekea Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya michuano hiyo.
3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe akizungumza na kuwatakia vijana hao ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon.
6
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys.
7 8 9 10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon.

Picha zote na Philemon Solomon-www.mtazamonews.com

Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Yakabidhi Vifaa Kwa Uongozi wa Timu ya PBZ Kuweza Kushiriki Vizuri Katika Michuano ya Mei Mosi 2017

April 05, 2017
 
Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Mussa Mvita, akimkabidhi Seti ya Jezi Nahodha wa Timu ya PBZ Ndg Hassan Maulid, kwa ajili ya kuweza kushiriki vizuri katika michuano ya Kombe la Mei Mosi linalojumuisha Timu za Wafanyakazi wa Serikali na Mashirika ya Umma yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, wakishuhudia Viongozi wa Timu ya PBZ, hafla hio ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya michezo yamefanyika katika Ofisi ya Benki hiyo Darajani Zanzibar. 
Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Mussa Mvita,mwenye kati akimkabidhi Seti ya Jezi Nahodha wa Timu ya PBZ Ndg Hassan Maulid na kulia Katibu wa Timu ya PBZ Ali Mwinyijuma.






Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Akabidhi Vifaa Kwa Kituo Cha Afya Bogowa Wilaya ya Mkoani Kijiji cha Mganyageni Pemba

April 05, 2017
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wac Wilaya ya Mkoani Mhe Hemed Suleiman alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa kwa ajili ya kukabidhi Vifaa kwa ajili ya Chuma cha Wazazi katikac Kituo hicho cha Afya  katika Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya Mkoani Pemba wakati alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa kukabidhi vifaa vya afya katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Balozi wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr. Mbwana Shoka, akitowa maelezo wakati wakitembelea Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr. Mbwana Shoka akitowa maelezo wakati wa ziara ya Mke wa Rais wa Zanzibar kutembelea kituo hicho na kukabidhi vifaa vya Afya kwa Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Harusi Siad Suleiman wakati wa hafla hiyo, wakiwa katika viwanja vya Kituo hicho Bogowa Mkanyageni Pemba.
Mfanyakazi wa Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba Mwanahawa Mohammed Abdallah akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi na wananchi wa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.  
Mganga Mkuu wa Kanda ya Pemba Dr Mbwana Shoka akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya chumba cha wazazi kwa Kituo hicho cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba. 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pembe Mhe. Omar Khamis akizungumza wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein. wakati wa kukabidgi vifaa vya Afya kwa Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Pemba Wilaya ya Mkoani.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Balozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis wakati wa hafla hiyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya afya kwa Chumba cha Wazazi katika Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakifuatilia hafla hio ya kukabidhi vifaa vya afya kwa ajili ya chumba cha Wazazi katika Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said Suleiman akizungumza kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Wananchi wa Jimbo la Mkanyageni wakati wa kukabidhi Vifaa vya Afya kwa ajili ya Chumba cha Wazazi katika Kituo hicho.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya Afya katika Kituo cha Bogowa Mkanyageni kwa ajili ya Wazazi wanaofika katika Kituo hicho kuja kujifungua.
Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na wananchi hao na kutowa nasaha zake kabla ya kukabidhi vifaa vya afya kwa chumba cha wazazi katika kituo cha Afya Bogowa Mkanygeni Pemba.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashuka kwa Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashine ya kupimia Sukari katika Kituo hicho kwa  Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mashine ya kupimia presha wazazi katika kituo hicho kwa Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi pempasi kwa ajili ya watoto wanaozaliwa katika kituo hicho akipkea Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Muuguzi Mkuu wa Afya na Jamii wa Kituo cha Afya Bogowa Bi. Moza Mohammed Ali, akitowa shukrani kwa msaada huo kwa kituo hicho. kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Bogowa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.

Viongozi wa meza kuu wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi vifaa vya afya katika kituo cha afya bogowa mkanyageni Wilaya Mkoani Pemba.
Imetayarishwa na Othman Maulid  
Zanzinews.Blog .com