MAJALIWA AKUTANA NA RAIS WA MAKAMPUNI YA CCECC NA UJUMBE WAKE

MAJALIWA AKUTANA NA RAIS WA MAKAMPUNI YA CCECC NA UJUMBE WAKE

April 08, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Makampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) , Bw. Zhao Dianlong wakati alipozungumza na ujumbe wa Makampuni hayo kutoka Tanzania, Afrika Mashariki na China, ofisini kwake mjini Dodoma Aprili 8, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na ujumbe kutoka Makampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kutoka Tanzania, Afrika Mashariki na China, ofisini kwake mjini Dodoma Aprili 8, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Rais wa Makampuni ya CCECC, Bw. Zhao Dianlong na kulia kwa Waziri Mkuu ni Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
MAUAJI YA KIMBARI SI JAMBO LA KUFIKIRIKA – DKT KOLIMBA

MAUAJI YA KIMBARI SI JAMBO LA KUFIKIRIKA – DKT KOLIMBA

April 08, 2018


wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzani Kolimba wa pili kushoto waliokaa baada ya kufungua semina ya wabunge kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, uhalifu uawa kivita na ubaguzi dhidi ya binadamu



wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzani Kolimba wa pili kushoto waliokaa baada ya kufungua semina ya wabunge kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, uhalifu uawa kivita na ubaguzi dhidi ya binadamu



wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzani Kolimba wa pili kushoto waliokaa baada ya kufungua semina ya wabunge kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, uhalifu uawa kivita na ubaguzi dhidi ya binadamu


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzani Kolimba akisalimiana na Mbunge Ally Saleh baada ya kufungua semina ya wabunge kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, uhalifu uawa kivita na ubaguzi dhidi ya binadamu



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku akizungumza katika semina ya Wabunge kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, uhalifu uawa kivita na ubaguzi dhidi ya binadamu

…………..

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan Kolimba amesema Suala la Mauaji ya Kimbari sio jambo la kufikirika kwani limeshatokea katika nchi za ukanda wa Maziwa Makuu na ndio maana Serikali katika nchi hizo zimekuwa zikiandaa mikakati mbalimbali ili kuhakikisha tukio hilo linakuwa historia..

Dkt. Kolimba amesema hayo alipokuwa akifungua semina ya Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Katiba na Sheria na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambapo alimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.

“Mauaji ya kimbari sio jambo la kufikirika, limeshawahi tokea katika nchi zetu, ndio maana kumekuwa na mikakati mbalimbali ili kuhakikisha mauaji kama hayo yanakuwa historia, tunataka mauaji haya yawe historia kwa nchi zetu na yasije jirudia tena,” alisema mhe. Kolimba

Alisema kwamba nchi za maziwa makuu kwa sasa zinatakiwa kuongelea maendeleo na mashirikiano na sio vita au ubaguzi wa aina yoyote ile.

Alisema viongozi wanatakiwa kujua kuwa wameshilikilia hatma za watanzania mikononi mwao na hivyo hawana budi kuweka mbele utu, uzalendo na utaifa dhidi ya tashwishi za kisiasa kwa mustakabali mzuri wa wananchi.

Mhe. Kolimba alitumia nafasi hiyo kuipongeza Tanzania na Kamati ya Kitaifa ya mauaji ya Kimbari kwa kuwa ni moja ya nchi zilizotajwa na Umoja wa Mataifa kuwa zinafanya vizuri katika eneo hilo.

Kikao hicho kinachifanyika mjini Dodoma kinalenga kuwapitisha Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hizo juu ya Mkataba wa Kuzuia mauaji ya kimbari kwa nchi za Maziwa Makuu wa mwaka 2006 ili kuwapatia uelewa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na ubaguzi dhidi ya binadamu.

Tanzania pamoja na nchi nyingine 12 za Maziwa Makuu walitia saini kuridhia utekelezaji wa mkataba huo. Nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi, Congo DRC, Sudani Kusini, Sudani,Zambia,Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Congo.

Semina hiyo ya wabunge imeandaliwa na Kamati ya Kitaifa ya kuzuia mauaji ya Kimbari nchini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia mauaji ya kimbari ya New York Marekani.

BENKI YA UBA YAENDELEZA UJIRANI MWEMA KUPITIA MICHEZO

April 08, 2018



Mlinda mlango wa Timu ya Wafanyakazi wa Benki ya United Bank of Africa (UBA) Tanzania akiwa langoni wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya taasisi mbalimbali kutoka Uganda zilizopo nchini. Mchezo huo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.


Vijana wakiwa uwanjani wakimenyana.


Mchezo ukiendelea.


Picha ya pamoja.



Kikosi cha Timu ya Wafanyakazi wa Benki ya United Bank of Africa (UBA) Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja. Wafanyakazi hao wamecheza mechi ya kirafiki na timu ya taasisi mbalimbali kutoka Uganda zilizopo nchini. Uganda ilishinda kwa mabao 2 dhidi ya UBA (Tanzania) 0. Mechi hiyo ilichezwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindini Mikocheni Dar es salaam jana&n

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAGERA (KCU) CHAFAFANUA KUHUSU MALIPO YA AWALI YA KAHAWA YA WAKULIMA

April 08, 2018


Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Mwingine ni Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg John kanjagaile. Picha Zote Na Mathias Canal, WK



Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo (Kilimo 4).

Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila ametoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd kama ilivyojadiliwa kwenye Mkutano wao Mkuu tarehe 27/03/2018.


Amebainisha hayo wakati akizingumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mjini Dodoma na kusema kuwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera si Kampuni ya kununua kahawa bali ni ushirika wa wakulima wadogo wadogo wenye lengo la kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kuhudumia zao la kahawa na kuliwasilisha sokoni kwa utaratibu wenye tija endelevu na kisha kugawana mapato baada ya kufanya mauzo.

Alisema bei halisi ya mkulima kwa upande wa Ushirika inapatikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika ambapo wakulima hulipwa malipo ya mwisho kwa kadri ya bei ya kuuzia iliyopatikana sokoni na hesabu ya mwisho kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu.

Hivyo kwa vile mchakato wa mauzo huchukua si chini ya kipindi cha mwezi mmoja tangu mkulima awasilishe kahawa yake kwenye ushirika hadi malipo ya mwisho kufanyika, basi ili kumuondolea mkulima adha ya kusubiri malipo yake yote baada ya mauzo wakati anahitaji kujikimu na kukidhi mahitaji yake muhimu, wakulima wenyewe kwa utashi wao kupitia Mkutano Mkuu, wanajadili malipo ya awali atakayotanguliziwa mkulima wakati anasubiri malipo ya mwisho.


Niyegila alibainisha kuwa mnamo tarehe 27/03/2018, Chama Kikuu cha Kagera kilifanya Mkutano wake Mkuu ambao pamoja na mambo mengine wanachama walijadili malipo ya awali ya mkulima (Advance Payments). Katika makisio hayo, Menejimenti na Bodi ya KCU (1990) Ltd walipendekeza malipo ya awali yawe ni TZS 1,000 kwa kilo moja ya kahawa ya maganda.

Alisema kuwa baada ya mjadala, wanachama waliagiza kupitiwa upya kwa makisio hasa katika upande wa malipo ya awali na kuangalia namna ya kupandisha kiwango cha malipo ya awali. Aliongeza kuwa Kiwango kipya pendekezwa kitawasilishwa kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kwa ajili ya kuidhinishwa.

Alisisitiza kuwa kile kilichojadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama si tangazo la bei bali ni malipo ya awali kwa mkulima ambapo Kwa mujibu wa sheria, bei elekezi ya zao la kahawa inatolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa utaratibu wa ushirika, bei halisi itajulikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika sokoni na si vinginevyo.

Niyegila aliongeza kuwa kwa utaratibu wa sasa wa Serikali, kahawa yote itakusanywa kupitia kwenye Vyama vya Ushirika na kupelekwa sokoni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani.

Kwa mantiki hiyo, hakuna mkulima yeyote atakayeruhusiwa kuuza kahawa nje ya mfumo wa ushirika

AGAPE YAENDESHA WARSHA KWA WAWAKILISHI WA VIJANA NA WATU WAZIMA KUKUTANA NA WAIDHINISHA NDOA KISHAPU

April 08, 2018



Mkurugenzi wa shirika la AGAPE,John Myola akizungumza katika warsha kwa warsha kwa wawakilishi wa vikundi vya vijana na watu wazima wanaoshiriki katika mapambano dhidi ya mila na desturi kandamizi wilayani Kishapu


Shirika la AGAPE Aids Control Programme limeendesha warsha kwa wawakilishi wa vikundi vya vijana na watu wazima watakaokutana na waidhinisha ndoa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ili kukabiliana na mila na desturi kandamizi zinazochangia ndoa na mimba za utotoni.

Warsha hiyo ya siku moja imefanyika leo Ijumaa Aprili 6,2018 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni vijana,wazee maarufu,viongozi wa kimila,viongozi wa dini,wanasheria,viongozi wa dini ,idara ya afya na maafisa kutoka Shirika la AGAPE.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo,Meneja Mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi Peter Amani alisema warsha hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa na shirika la AGAPE kwa kushirikiana na shirika la Save The Children kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

“Lengo la warsha hii ni kuwajengea uwezo wawakilishi wa vijana na watu wazima kuhusu madhara ya mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa mimba na ndoa za utotoni ambapo wawakilishi hawa watakwenda kutoa elimu hii kwa wathibitisha ndoa katika jamii”,alisema Amani.

Alisema shirika hilo linatekeleza mradi huo katika kata 12 za halmashauri ya wilaya ya Kishapu na katika warsha hiyo,washiriki wametoka katika kata sita ambazo ni Lagana,Mwamashele,Itilima,Mwakipoya,Masanga na Mwamalasa.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa shirika la AGAPE,John Myola alisema watoto wameendelea kukosa haki zao kutokana na baadhi ya watumishi katika vyombo vya dola ikiwemo mahakama kuendekeza rushwa na kukwepesha sheria kulinda wahalifu hasa wale wanaowapa mimba na kuozesha watoto.

Nao viongozi wa dini Sheikh Adam Njiku na Mchungaji Lucas Mwigulu waliiasa jamii kupeleka shule watoto na kutowabagua watoto wa kike.

Aidha waliomba sheria za nchi ziseme dhahiri kuwa umri halisi wa kuolewa ni kuanzia miaka 18 badala ya kuchanganya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto kuolewa akiwa na umri kuanzia 14/15 kwa ridhaa ya wazazi.

Naye mzee wa mila, Suzana Mbalu alisema ndoa na mimba za utotoni zinachangiwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii hivyo kuwataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao ambao wanakumbwa na na utandawazi na kuiga maisha ya mataifa mengine duniani.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI





Meneja Mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi Peter Amani kutoka shirika la AGAPE akielezea malengo ya warsha kwa wawakilishi wa vikundi vya vijana na watu wazima watakaokutana na waidhinisha ndoa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.





Washiriki wa warsha hiyo wakiandika dondoo muhimu...





Meneja Mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi Peter Amani akielezea kuhusu madhara ya mila na desturi kandamizi kwa watoto.





Mkurugenzi wa shirika la AGAPE,John Myola akiwahamasisha washiriki wa warsha hiyo kutumia elimu waliyopewa kuielimisha jamii kuhusu madhara ya mila na desturi kandamizi na kuhakikisha watoto wanapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao.





Sheikh Adam Njiku kutoka Bakwata Kishapu akielezea kuhusu taratibu za uthibitishaji/uidhinishaji wa ndoa katika dini ya Kiislamu. Sheikh Njiku aliiasa jamii kupeleka watoto wa kike shule kwani wanawake ni wasaidizi wakubwa katika familia na jamii kwa ujumla





Mchungaji Lucas kutoka kanisa la KKKT Kishapu akielezea kuhusu taratibu za uthibitishaji/uidhinishaji wa ndoa katika dini ya Kikristo. Aidha aliwataka wazazi kutoozesha watoto kwa kuwalazimisha huku akisisitiza nguzo kuu katika ndoa ni upendo na utii.





Mzee wa mila, Suzana Mbalu akielezea kuhusu taratibu za uthibitishaji/uidhinishaji wa ndoa kimila ambapo alisema hakuna mila inayoruhusu mtoto aolewe chini ya miaka 18 isipokuwa jamii imebadilika kutokana na utandawazi unaosababisha jamii kuiga maisha ya mataifa mengine.





Wakili wa AGAPE, Ellen Lucas akielezea matakwa ya kisheria juu ya ndoa na mimba kwa watoto kwa sheria za Tanzania.





Mzee Jabai Tema akichangia hoja ukumbini



Kijana Sarah Mwanamboka akichangia hoja katika warsha hiyo.



Mzee wa mila, Suzana Mbalu akisikiliza hoja kwa umakini



Afisa Mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi Sophia Rwazo kutoka shirika la AGAPE akiwasisitiza washiriki wa warsha hiyo kutumia elimu waliyopata kuelimisha wathibitisha ndoa katika jamii watambue madhara ya mila na desturi kwa watoto.


Kaimu Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Neema Mwaifuge akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo.


Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

GAUDENTIA KABAKA: WANAWAKE MSIONE FAHARI KUITWA 'DUME JIKE', BALI KUWENI WENYE MSIMAMO IMARA NA JASIRI KATIKA KUPIGANIA MAENDELEO

April 08, 2018



Mwenyekiti ya Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka akizungumza na Waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Suwata Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Bara Eva Kihwelo (Picha na Bashir Nkoromo).


NA BASHIR NKOROMO

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka amewataka Wanawake kote nchini wasione fahari kuitwa 'Dume-Jike' bali wawe wanawake wenye msimamo imara na jasiri kwa maendeleo yao na ya nchi kwa jumla.


Gaudentia ameto mwito huo, wakati akiwasilisha salaam maalum za pole kwa ndugu jamaa, marafiki na hasa wanawake wote hapa nchini na duniani kote kufuatia kifo cha Winnie Mandela aliyemwelezea kuwa alikuwa amwanamke shupavu katika kupigania haki na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.


"Tazama Winnie Mandela alikuwa mpambanaji hata kabla ya kuwa mke wa Rais Nelson Mandela, kwa hiyo tukiangalia historia yake tunabaini kuwa hakuhitaji msukumo wa nguvu za mwanaume katika kuonyesha ushupavu wake", alisema.


Alisema Winnie Mandela aliyefariki dunia Aprili 2, mwaka huu, aliendelea kuonyesha ushupavu wake katika kupambana na udhalimu na ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini hata wakati Mandela akiwa gerezani


"Winnie atakumbukwa na Watanzania na dunia nzima kwa ujasiri wake pia atakumbukuwa kwa umaarufu alioupata hata akiwa bado mwanafunzi, msichana kabla ya kuolewa. Alichukia kuona Mwafrika anabaguliwa, anatengwa asifike kwenye maeneo walipokuwa weupe. Kwa hiyo umaarufu wa Winnie haukutokana tu kwa kuwa ni mke wa Rais yaani “First lady “ lakini umarufu wake ulikuwa wa kwake mwenyewe. Alijitambua, akajiamini, akatimiza wajibu wake kama Binadamu, kama Mwafrika, baadaye kama Mke, Mama, Mwanasiasa na Kiongozi" alisema Gaundetia


"Wanawake wa Tanzania hasa wanasiasa tuna mengi ya kujivunia na kujifunza kutoka kwa mwana mama huyu mtoto wa Afrika. Tumejifunza kuishi sisi wenyewe na sio kutegemea tufanyiwe, tupendelewe ndipo tuonekane tunaweza.


Tunatambua uwezo tulionao wanawake lakini pia tuwe wastahimilivu tunapokumbana na magumu tupambane hadi mwisho. Kama Winnie Madikizela Mandela aliweza kutetea Waafrika wenzake hata baada ya mume wake kufungwa; kwa sababu hiyo kwa nini sisi wengine tusiweze kujitokeza waziwazi na kuiunga Serikali na Rais wetu Dk. John Magufuli katika juhudi zake za kupiga vita ufisadi, wizi wa mali ya umma, kutowajibika", Alisema Gaudentia.


"Wanawake wa Tanzania na wa Afrika nzima tunapomlilia Winnie Mandela kwa nini tusiige ujasiri wake kwa kukemea bila woga tabia mbaya kama mahusiano ya jinsia moja, ubakaji na utumiaji dawa ya kulevya, katika jamii yetu. Wanawake wa Tanzania tumapomlilia Winnie Mandela kwanini tusijitokeze waziwazi kupinga mfumo dume unaoendelea kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini kwetu na kusababisha kina mama kutojiamini", alisema.


Alisema, kama Winnie Mandela alivyotimiza wajibu wake katika harakati za Waafrika kuing’oa Serikali dhalimu ya kibaguzi nchini Afrika kwa nafasi yake kama mwanamama, na wanawake wa Tanzania kila mmoja kwa nafasi yake wanaweza kuwa chachu ya kuleta mabadiliko ya kweli hapa nchini.


"Tunafahamu kuna wanawake wa nchi yetu ambao wameonyesha ujasiri kama huo wa Winnie Mandela wakiiwakilisha nchi yetu Kimataifa. Sisi UWT tunajiandaa kuwatambua hivi karibuni, nia yetu ni kutambua michango yao wakiwa wanafanya kazi nje ya nchi yetu na hivyo wametuleta sifa wanawake wa Tanzania, lakini pia kuwatia moyo wengine watimize wajibu wao, Alisema Gaudentia.", alisema Gaudentia.


Akizungumzia mrejesho wa ziara aliyoifanya hivi karibuni aliwapongeza wanawake wanaowajibika ipasavyo Mijini na Vijijini hapa nchini akisema yeye na timu yake walitembelea Mikoa na Wilaya zote za Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini na kubaini kuwa wanawake ni wajasiriamali wazuri, ni wakopaji na walipaji wazuri na kuzitaka Halmashauri kuwapa mikopo wanawake hao ili wapanue shughuli zao za ujasiriamali na kwamba hicho ndicho kilio chao kikubwa, akihimiza halmashauri hizo kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani.


"Tunapenda ifahamike kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mwelekeo wa Sera zake kwa Mwaka 2010 - 2020 na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015-2020 kwa pamoja zimeweka msisitizo wa kuyawezesha makundi Maalum ikiwemo Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu na katika kutekeleza maelekezo CCM, Serikali imeshatoa Maelekezo kwa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Wilaya na Miji Midogo kutenga asilimia kumi za makusanyo yao ya ndani kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu Alisema Gaudentia na kungeza;


"Tunapenda kuwakumbusha wale wote wenye dhamana katika Mamlaka hizi kwamba ni Maelekezo ya CCM kutoa bila kukosa fedha hizi ili kuwawezesha wananchi katika makundi haya muhimu. Kuanzia sasa UWT itafuatilia kwa ukaribu suala hili na hatutasita kupendekeza kwa Mamlaka za uteuzi kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa wale wote wanaosuasua au kutenga kutoa fedha hizi ili kujihakikishia kuwa wanawake hawa wachapakazi wapate mahali pa kupata mikopo kwa bei nafuu kwa maana ya riba nafuu".


"Tunawaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii watimize wajibu wao wa kutembelea vikundi vya wakina mama ili kuwapatia elimu ya kujisajili, Kuendesha shughuli zao, Kupata mikopo ya Halmashauri, Kupata mikopo kutoka benki kwa wale watakaoweza. Tunawapongeza Wakurugenzi na Maafisa wa Maendeleo ya Jamii ambao tulikuta wanatimiza wajibu wao kikamilifu, kwa mfano, Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Chunya ambayo inaongozwa na Wanawake (Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Afisa Maendeleo ya Jamii) ndiyo Halmashauri ya mfano kwa kutenga asilimia kwa wanawake, pia Halmashauri ya Njombe (V) inaongozwa na Mwanamke na ina fanya vizuri ikifuatiwa na Halmashauri ya Mufindi", alisema Daudentia.


Kuhusu Maadili, Gadentia alisema UWT wataendelea kukemea maadili yaliyoporomoka kwa vijana wa kike na wa kiume jambo ambalo ni hatari kwa kizazi kijacho na kuhumiza wazazi na walimu kukemea uvunjaji wa Maadili na hasa mimba za utotoni.


"UWT inashauri kwenye maeneo tunakoishi ambako kuna Kamati mbalimbali kama vile polisi jamii na nyingine, Jamii iongeze Kamati ya za Maadili zitakazosimamia maadili kwa vijana wa kike na wa kiume kwa kila Kata, ambazo zitakuwa na wajumbe wafuatao, Viongozi wa Dini zote, Madiwani wa Kata na Viti Maalum, Wazee na watu wazima wanaoishi ndani ya Kata hizo, Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata. Kamati hizo zisimamie kikamilifu zoezi hilo na viongozi waliotajwa hapo juu na ikibidi watakaokiuka wachukuliwe hatua za kinidhamu kama wahalifu wengine", alisema Gaudentia


Alisema, baada ya kukamilisha ziara hiyo UWT iliandaa Mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja Viongozi na Watendaji wa UWT wa ngazi ya Wilaya na Mikoa hiyo ya Nyanda za Juu Kusini. Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 26 – 27/03/2018 katika Mkoa wa Mbeya na kwamba ziara na mafunzo haya yataendelea kufanyika katika Mikoa yote. -- Best regards Bashir Nkoromo Blogger & Photojournalist UHURU PUBLICATIONS LTD Dar es Salaam, TANZANIA Cell: +255 712 498008, +255 789 498008, BLOG: theNkoromo Blog Email: nkoromo@gmail.com

NFRA YAJIPANGA UZINDUZI WA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA APRILI 21, 2018

April 08, 2018


Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma, Leo 6 Aprili 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-NFRA

Wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma wakifatilia kwa umakini kikao cha kazi kilichoongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba, Leo 6 Aprili 2018.

Kutoka kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Fredy Mbonde, Afisa Ugavi NFRA Magreth Salia Kavishe, na Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA wakifatilia kwa umakini kikao cha kazi kilichofanyika katika Ofisi za NFRA Mtaa wa Kizota Mjini Dodoma, Leo 6 Aprili 2018

Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA na Mratibu wa Mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula, akiwasilisha maelezo mafupi ya namna mradi utakavyotekelezwa wakati wa kikao kazi cha wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA, Leo 6 Aprili 2018

Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma, Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa maendeleo na Bishara wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Mikalu Mapunda (Kshoto), Leo 6 Aprili 2018.


Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula katika dhifa itakayofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula zilizopo Mtaa wa Kizota Mjini Dodoma.


Hayo yamebainishwa leo 6 Aprili 2018 na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma.


Bi Zikankuba ameeleza kuwa Mradi huo utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 55, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni sehemu ya kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Aidha, amesisitiza kuwa mikataba ya ujenzi ilianza kufanya kazi tarehe 9 Disemba 2017 huku akisema Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za Kandarasi kutoka Poland ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o) ambapo msimamizi wa utekelezaji wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


Alisema Mradi utahusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala ya kisasa pamoja na ukarabati wa ofisi na kutekelezwa katika maeneo nane ambayo ni Arusha (Babati), Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Mpanda.


Baada ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa 250,000 MT zaidi (vihenge vya kisasa 190,000MT na maghala 60,000 MT) jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.


Alisema kupatikana kwa Mradi huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.


Hifadhi ya Chakula inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani 500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 1992 Wakala ulipoanzishwa.


Pia, technologia ya vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi chakula kwa muda mrefu Zaidi, itasaidia kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa.

Katika kikao kazi hicho Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba amewasihi wafanyakazi wote wa NFRA kufanya kazi kwa ushirikiano na kutambua kuwa nidhamu na bidii yao itakuwa chachu ya mafanikio zaidi katika kuimarisha utendaji wa NFRA.