TANZANIA NA CUBA KUENDELEZA USHIRIKIANO

TANZANIA NA CUBA KUENDELEZA USHIRIKIANO

October 03, 2016
mao1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakati alipokutana naye Ikuu leo kwa mazungumzo ambapo wamezungumzia  jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.(PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
mao2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan  na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  viongozi wa Tanzania na Cuba.
mao3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha ya mnyama Chui anayepatikana  katika mbuga za wanyama za Tanzania Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa.
mao4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa  Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa , Kulia ni Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
……………………………………………………………………………………
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali ya  Tanzania na Cuba zimeahidi kuendeleza ushirikiano  uliopo, ambao umeasisiwa na viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania pamoja na Fidel Castro  Rais  mstaafu wa Cuba.
Akizungumza na waandishi wa habari,  Ikulu leo jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu, amesema kuwa  Makamu wa Rais wa Cuba,  Mhe. Salvador Valdes Mesa ameitikia mwaliko huo wa kuja nchini kwa vile nchi  hizo mbili zimekua na ushirikiano na mahusiano mazuri kwa muda mrefu.
“Ziara hii ni moja ya jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili ili kuhakikisha mahusiano yaliyopo yanaimarika zaidi” alisema Makamu wa Rais
Katika ziara  hiyo ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini, mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo masuala ya Afya, Elimu, Michezo, na Utamaduni, ambapo katika sekta ya afya nchi ya Cuba  imepiga hatua na kuahidi  kushirikiana na Tanzania  ili kujenga kiwanda cha kisasa  cha kutengeneza madawa ya binadamu.
Aliongeza kuwa Tanzania imeomba Serikali ya |Cuba kuendelea kusaidia sekta hiyo kwa kufundisha wataalamu wa afya, ambapo tayari madaktari 24 kutoka Cuba wako nchini kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma  za kitabibu na mafunzo katika mikoa mbalimbali  ya Tanzania Bara na Visiwani.
Masuala mengine yaliyojadiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya elimu, biashara, utalii na uwekezaji.
Ambapo pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu amesisitiza nia ya Serikali ya Tanzania kudumisha ushirikiano huo ikiwa ni pamoja kupongeza jitihada za kuboresha uhusiano wa Cuba na Marekani.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais  wa Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa nchi yake na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania.
“Tumeamua kuendelea kuboresha mahusiano yetu na Tanzania kwa kuongeza ushirikiano wetu katika sekta nyingine ambazo hatukuwa tunashirikiana hapo awali kama vile sekta ya utalii” alisema Makamu wa Rais wa Cuba
Aidha, Mhe. Mesa ameiomba Tanzania kuendelea kuiunga mkono Cuba katika masuala ya kimataifa ili kuendeleza ushirikiano na kukuza uchumi kwa nchi zote mbili.
Makamu wa Rais wa Cuba aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya siku tatu  ambapo alipata fursa ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli .
Rais Kabila awasili nchini apokewa na Mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli

Rais Kabila awasili nchini apokewa na Mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli

October 03, 2016

jos1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JNIA.
jos2 jos3 jos4 jos5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake.
jos6 jos7 jos8
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
jos9 jos11
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati kikundi cha ngoma za asili kilipokuwa kinatumbuiza uwanjani hapo. PICHA NA IKULU
Wasafirishaji wa mizigo mikoani wapewa semina kuhusu elimu ya mlipa Kodi

Wasafirishaji wa mizigo mikoani wapewa semina kuhusu elimu ya mlipa Kodi

October 03, 2016
gar1
Muelimishaji kutoka Kitengo cha Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Gabriel Mwangosi akielezea jambo wakati wa semina na wanachama wa Chama cha Wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI) leo Jijini Dar es Salaam.
gar2
Muelimishaji kutoka Kitengo cha Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bibi. Valentina Baltazar fafanua jambo wakati wa semina na wanachama wa Chama cha Wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI) leo Jijini Dar es Salaam.
gar3
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI), ambaye pia ni mwakilishi wa Kampuni ya Bob Transpoter, Bw. Ally Luwago akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu elimu ya mlipa Kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
gar4
Muelimishaji kutoka Kitengo cha Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Gabriel Mwangosi akionyesha nakala ya namba ya mlipa kodi (TIN) iliyofanyiwa maboresho wakati  wa semina na wanachama wa Chama cha Wasafirishaji wa mizigo mikoani (UWAMI) leo Jijini Dar es Salaam.
gar6
Mmoja wa wanachama wa chama cha usafirishaji mizigo mikoani (UWAMI) aliyefahamika kwa jina moja la David, akichangia mada wakati wa semina kuhusu elimu ya mlipa Kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: MAELEZO
PROF. MBARAWA AITAKA TTCL KUTAFUTA WATEJA

PROF. MBARAWA AITAKA TTCL KUTAFUTA WATEJA

October 03, 2016
ry1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akiangalia taarifa zinazoingia katika mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
ry2
Msimamizi wa masuala ya TEHAMA Bw. John Chorai (kulia), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), namna kifaa cha kurekodia malipo kinavyofanya kazi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
ry3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akikagua moja ya kifaa cha kuhifadhi Kumbukumbu katika kituo Mahiri cha Internet Data Centre cha Taifa kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
ry4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa watumishi wa kituo Mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo.
ry5
Mwakilishi wa Kibiashara kutoka Ubalozi wa Uingereza anayesimamia nchi ya Tanzania na Kenya Bw. Lord Hollick (wa pili kulia) akifafanua jambo  kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) wakati alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia masuala ya kuboresha miundombinu nchini. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Bi Sarah Cookie.
………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kutafuta wateja wa kuhifadhi kumbukumbu zao kwenye Kituo mahiri cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Center), jijini Dar es Salaam
Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo kuwa mbunifu na kuanza kufuata wateja ana kwa ana na si kusubiri wateja hao kumfuata ofisini kwake.
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo lililopo eneo la Kijitonyama ambapo ameelezea umuhimu wa kufanya jitihada za haraka kutafuta wateja hao kwa lengo la kuongeza kipato cha Taifa.
“Natoa wiki mbili kwa Mkurugenzi wa Masoko kuhakikisha analeta wateja wa kuhifadhi kumbukumbu zao katika kituo hiki, ikishindikana atupishe tutafute watu wanaofaa katika taaluma hiyo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema kuwa Kituo hicho kimeimarishwa kiusalama kwani kimeunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo wateja wataweza kuchukua taarifa zao kwa  uharaka zaidi.
Ameongeza kuwa masuala yote yanayohusu makubaliano ya kibiashara katika kituo hicho yawekwe kwa njia ya maandishi ili kuweza kuweka kumbukumbu sahihi na ufatiliaji inapohitajika.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Peter Mwasalyanda amemuahidi Waziri Mbarawa kutekeleza yale yote aliyoyaagiza yafanyike ili kuboresha huduma katika kituo hicho.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekutana na Mwakilishi wa Kibiashara kutoka ubalozi wa Uingereza anayesimamia nchi ya Tanzania na Kenya Bw. Lord Hollick na kuzungumzia masuala mbalimbali ya kuboresha miundombinu nchini.
Kituo mahiri cha Internet Data Centre ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na asilimia 75 zimetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za Serikali hivyo ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji.

UPELELEZI KINONDONI KUISHA NDANI YA SIKU SITINI

October 03, 2016
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu yamefadhiliwa na Tasisi ya Hanns Sidel. Picha na Tamimu adam- Jeshi la Polisi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe( katikati) akiimba wimbo wa maadili wa ofisa wa Polisi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mafunzo ya upelelezi yanayofanyika katika chuo cha polisi kidatu. Mafunzo hayo kwa askari 100 yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe) akiingia katika ofisi ya mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kuzindua mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100. Mafunzo hayo ya upelezi yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe) akisalimiana na wakufunzi wa chuo cha polisi kidatu alipokwenda kuzindua mafunzo ya upelelezi.Mafunzo hayo ya upelezi yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel. (picha na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi)

Na. Tamimu Adam - Jeshi la Polisi

Mkuu wa mkoa wa Morogoro mhe. Dkt Kebwe Stevin kabwe amesema Jeshi la polisi Tanzania ni kioo kwa majeshi ya polisi yalipo Afrika mashariki na hata afrika kwa ujumla kutokana na umahili wake wa kutoa mafunzo mbalimbali ya uaskari kwa baadhi ya nchi zilizopo afrika mashariki .

Dkt Kebwe aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi miwili ya upelelezi katika chuo cha Polisi kidatu yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel kwa askari polisi 100 waliotoka katika mkoa wa kipolisi kinondoni ambalo wamechaguliwa kwa ajili ya kutekeleza kwa weledi mpango wa kuborewsha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa huo wa kipolisi.

“Huwezi kwenda kujifunza katika nchi ambayo haifanyi vizuri, na ndioo maana nchi za jirani huja Tanzania kwa ajili ya kujifunza namna Jeshi la Polisi Tanzania linavyo weza kuimarisha usalama wa raia na mali zao” alisema Dkt Kebwe.

Aliwataka askari hao wanafunzi wa upelelezi kujifunza kwa makini ili kuboresha umahiri walionao katika kufanikisha upelelezi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kivitendo katika mkoa wa kinondoni kama eneo la mfano na hatimaye maboresho hayo yaweze kuenea na kutekelezwa katika mikoa yote nchini hivyo kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Kwa upande wake mkuu wa kitendo cha kusimamia mapango huo wa kuboresha usalama wa jamii kutoka makao makuu ya Polisi Naibu kamishina wa Polisi ( DCP)Godluck Mongi alisema mafunzo hayo ya upelelezi yataleta mafanikio makubwa katika mkoa huo wa kinondoni kwa kuharakisha upelelezi wa kesi na hakuna kesi itakayocheleweshwa chini ya siku sitini kwa maana hiyo ndani ya siku sitini upelelezi wa kesi inatakiwa iwe imeisha.

Aliongeza kuwa lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2019  askari wote upelelezi wawe wamepata mafunzo hayo ili waweze kuandana na kasi inayotakiwa katika mpango huo wa maboresho ya usalama wa jamii. 

Naye mwakilishi wa taasisi inayofadhili mafunzo hayo, Bw. Ombeni mhina lisema kwamba, ufadhili wa mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100 kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni ni sehemu ya mpango wa Taasisi ya Hanns Seidel kuunga mkono jitihata za jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia na mali zao kupitia mpango wa kuboresha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni.

Aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi sitini ambazo jumla ya miradi 100 inaendelea kutekelezwa ikiwa na lengo la kukuza demokrasia, amani na maendeleo duniani kote.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kamishina Msaidizi wa Polisi ( ACP) Andrea Mwang’onda aliwataka wanafunzi wanapata mafunzo hayo ya upelelezi kuzingatia kile wanachofundishwa na kufuta maadili yote ya uaskari wakati wote watakapokuwa katika mafunzo hayo.

MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI AMKABIDHI MHE. JAJI MKUU BENDERA YA TAIFA NA YA AFRIKA MASHARIKI.

October 03, 2016

Mpicha Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kabla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa na Ile ya Afdrika Mashariki leo katika Ofisi ya Jaji Mkuu jijini Dar es salaam.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akifurahia Zawadi ya Tai ya Bendera ya Taifa aliyopewa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akimwonyesha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kitabu cha Sheria kuhusu matumizi ya Vielelezo vya Taifa kabla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kabla ya kukabidhiwa  Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  ofisini kwake leo jijini Dar salaam. 

Na Mary Gwera, MAHAKAMA
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amezitaka Wizara, Halmashauri na Taasisi nyingine za Serikali kutumia vielelezo vya Taifa kama bendera na nembo ya taifa katika ofisi zao ili kuenzi tunu na vielelezo vya Taifa.

Aliyasema hayo ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea rasmi bendera ya Taifa na Afrika Mashariki kutoka kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo.

Alisema kuwa  vielelezo hivi vya taifa vinalindwa kisheria kwa hiyo inabidi vipate heshima yake kwa kuwa vinawakilisha taifa.

“Sheria pia inavitambua vielelezo hivi hivyo ni muhimu vikapewa heshima yake, kwani hata mtu akichezea vitu hivi anaweza kufungwa kwa mujibu ya sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Aliongeza pia Mahakama ya Tanzania pia iko katika mchakato wa kupata bendera yake kama ilivyo kwa Taasisi nyingine kama Bunge, pamoja na nembo yake ili ziweze kutumika katika Mahakam azote nchini.

Awali; akiongea na Jaji Mkuu pamoja na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano hayo, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo pia alizitaka Taasisi za Serikali kutopuuzia umuhimu wa matumizi wa vielelezo vya Taifa.

Alisema kuwa baadhi ya Ofisi nyeti za Serikali hazina bendera na vielelezo vingine muhimu ambavyo vinaiwakilisha Taifa na kusisitiza matumizi yake ili kuenzi tunu za Taifa.

“Ofisi nyingi za Serikali zinatumia bendera zilizochakaa na nyingine hazina kabisa, vitu hivi ni muhimu kwa taifa hivyo ni vyema kuvienzi na kuvithamini pamoja na kuvitunza,” alisema Bw. Chibogoyo.

MAKAMU WA RAIS WA CUBA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

October 03, 2016

7
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzanai Mhe.Samia Suluhu Hassan (kulia), akiwa na mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu  hapa Nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini.
Makamunwa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia moja ya kikundi kilichokuwa kinatumbuiza kwa matarumbeta mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchin
…………………………………………………………

     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa amewasili jioni hii katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa atafanya ziara ya kikazi ya siku Tatu hapa nchini na lengo la ziara hiyo ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya, utamaduni,michezo,kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.
 Tarehe 3/09/2016 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba atakutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa pia atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu na baada ya mazungumzo hayo ya faradha viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo MBILI.
Nchi nyingine ambazo Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba anazitembelea ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo- DRC-,Botwana na Zimbabwe.

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CUBA, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

October 03, 2016

1kin1
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Makamu wa Rais wa Cuba,Salvador Valdes Mesa kabla ya kuanza mazungumzo yao leo katika hotel ya Hyatt, Kilimajaro Kempiski jijini Dar es Salaam, leo.Kulia ni Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka
2kin
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa , leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Bashir Nkoromo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Makamu wa Rais wa Cuba,Salvador Valdes Mesa kabla ya kuanza mazungumzo yao leo katika hotel ya Hyatt, Kilimajaro Kempiski jijini Dar es Salaam, leo.Kulia ni Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka na Katibu wa SUKI Dk. Pindi Chana
 Msemji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Makamu wa Rais wa Cuba,Salvador Valdes Mesa kabla ya kuanza mazungumzo baina ya  Makamu huyo wa Rais wa Cuba na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) leo katika hotel ya Hyatt, Kilimajaro Kempiski jijini Dar es Salaam, leo
  Katibu wa NEC SUKI, Dk, Pindi Chana akisalimiana na Makamu wa Rais wa Cuba,Salvador Valdes Mesa kabla ya kuanza mazungumzo baina ya  Makamu huyo wa Rais wa Cuba na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo katika hotel ya Hyatt, Kilimajaro Kempiski jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia ukumbini na Makamu wa Rais wa Cuba,Salvador Valdes Mesa kwa ajili ya mazungumzo yao leo katika hotel ya Hyatt, Kilimajaro Kempiski jijini Dar es Salaam, leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa , leo jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbea wake katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa, baada ya mazungumzo leo jijini Dar es Salaam. 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika akimshukuru Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa, baada ya mazungumzo yao, leo jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Jorge Luis Lopez,baada ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Nchi hiyo leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Spika wa Bunge Job Nugai ambaye baadaye alikutana na kuwa na mazungumzo na Makamu huyowa Rais wa Cuba
 Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Spika wa Bunge Job Ndugai aliyekuwa akisubiri kuzungumza na Makamu huyo wa Rais wa Cuba
 Kaibu wa NEC-SUKI, Dk Pindi Chana akisalimiana na Spika wa Bunge Job Ndugai aliykuwa akisubiri kuzungumzana  na Makamu huyo wa Rais wa Cuba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Augustine Mahiga wakati akiondoka hotelini baada ya mazungumzoyake na Makamu wa Rais wa Cuba leo. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka