MKUTANO WA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAWAKUTANISHA WADAU JIJINI MWANZA.

March 22, 2017
Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa, akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika Jijini Mwanza.

Judith Ferdinand, BMG
Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka  nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.

Elimu hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 2010 bila vikwazo  pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za ujenzi.

Dkt. Mwakyusa amesema, wameona watumie utaratibu wa kuelimisha Maofisa wa Jeshi la Polisi na ofisi ya DPP,ili waelewe sheria hiyo na waweze kutoa msaada wa haraka pale unapohitajika.

Pia amesema,Bodi imesajili wataalamu 1442  lakini wamaotenda kazi ni wacheche kutokana na wengine kuwa walimu vyuoni, hivyo wameona jeshi la Polisi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pale ujenzi unapoanza  kama umefuata taratibu za kiserikali kwa kufatilia stika na vibao vinavyobandika kama ilivyo kwa bima na leseni kwa dereva.
Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea.

Kwa upande wake  Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani ambaye ndiye  mgeni rasmi amesema, jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Bodi hiyo, katika usimamizi wa sheria pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa mtu yoyote atakayeenda kinyume na maelezo ya Sheria namba 4 ya mwaka 2010.

Aidha ameiomba, Bodi hiyo kutoa ushirikiano hasa pale ushahidi unapotakiwa kwa muda muafaka,kwani kila fani ina  wataalamu wake.

"Ikumbukwe kila fani inawataalamu wake, hivyo ushirikiano wenu katika kutoa taarifa za kitaalamu utasaidia sana wataalamu wa jeshi la Polisi kuchukua hatua syahiki kwa wakati na wepesi," alisema Marijani.

Naye DPP Mganga amesema, siyo wapelelezi wote wana taaluma ya uhandisi, hivyo kujua chanzo  cha jengo kubomoka mpaka wapate ushirikiano kutoka kwa wahandisi.

Kadhalika amesema,mtu yoyote atakayefanya kosa katika ujenzi na kuwepo kwa ushahidi atafikishwa mahakamani.
Displaying Pix.JPG 

KAMATI YA KUDUMU YA KATIBA NA SHERIA YA BUNGE YATOA USHAURI WA KUTATUA CHANGAMOTO KATIKA TUME YA HAKI ZA BINADAMU

March 22, 2017

Aliyevaa Shirt jeupe, Mwenyekiti wa kamati ya kudumu  ya Katiba na Sheria ya Bunge, Mhe. Joseph Mhagama, akimsikiliza  Mhe. Ally Seif Ungano (Mb.) wa Kibiti Mkoani Pwani, anayezungumza kushoto kwake, wakati wa ziara ya kamati hiyo kisiwani Pemba, wengine katika Picha ni wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo na maofisa wa serikali zote mbili waliokuwepo katika ziara hiyo.

Pichani kulia ni Mhe. Saum Sakala, Mbunge viti Maalum (CUF) kutoka katika mkoa wa Tanga, akimuonyesha Mhe. Twahir Awesu Mbunge wa Mkoani Pemba (CUF) sehemu ya kipande cha barabara ya Chanjamjawiri, kaskazini Pemba, kilichojengwa chini ya Mradi wa  MIVARF, ambacho kamati ya Bunge ya Katiba na sheria Imependekeza mradi kuongeza muda ili kukifanyia maboresho ikiwa ni pamoja na kujenga daraja ili kuhepuka kujaa maji hadsa katika kipindi cha Mvua.

Picha inaonyesha karavati lililowekwa katika moja ya Barabara ya Chanjamjawiri katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, lililojengwa na mradi wa MIVARF, moja wa mradi wa muungano wenye lengo la kuboresha miundombinu na kuinua maisha ya wakazi wa Unguja na Pemba.
Picha ya pamoja imepigwa katika uwanja wa ndege kisiwani Pemba, ikionyesha wabunge wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria na Baadhi ya watendaji na watumishi wa Serikali ya SMT na SMZ. (Habari na Picha Zote na Evelyn Mkokoi wa OMR)


Evelyn Mkokoi-Pemba

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeona kuna kila sababu ya kumshauri Waziri mwenye dhamana ya katiba na sheria Mhe.Harrison Mwakyembe kutatua changamoto zinazoikabili tume ya haki za binadamu kwa  kuboresha Ofisi zote za tume hiyo  nchini  hususan Ofisi za Pemba na Lindi ili ziweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. 

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe.Joseph Mhagama (Mb.) Mabada Songea, alisema hayo wakati akifanya majumuisho ya Ziara ya kamati hiyo kisiwani Pemba.

Baada ya Kupokea taarifa ya Mtendaji Mkuu wa tume hiyo Nchini Bi. Mary Massey, Mhe. Mhagama alisema Ofisi hizo zinakabiliwa na changamoto ya rasilimali watu, fedha, vitendea kazi  pamoja samani  hivyo kufanya utendaji wa Tume hiyo kisiwani humo kuwa mgumu.  

Pia àlishauri tume hiyo kujengewa uwezo katika eneo LA utawala bora kama serikali ya awamu ya tano inavyosisitiza.

Awali mbunge wa Bukene Tabora, Mhe. Suleiman Zedi alisema ufinyu wa bajeti katika tume hiyo unazuia utekelezaji wa mambo mazuri yaliyokusudiwana serikali, ikiwemo elimu kwa umma kuhusu ukiukwaji wa misingi ya haki za Binadamu na utawala bora.

Pamoja na hayo  imeelezwa kuwa, ufinyu wa bajeti iliyotengwa Pemba kwa mwaka huu wa fedha unaenda kuisha, umepekelekea Ofisi Hizo kwa upande wa Pemba kupata kiasi cha sh. 100,000 kwa mwezi , na wakati mwingine kutopatikana kabisa unasababisha tume kutotekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na pia kushindwa kusogeza huduma zake karibu zaidi kwa wananchi. 

Aidha, ufinyu huo wa Budget umesababisha upungufu mkubwa wa watumishi kwani tume hiyo imeshindwa kuwalipa watumishi kutoka Dar es Salaam na kuwahamisha kwenda kwenye matawi ikiwemo tawi LA Pemba ambalo Lina mfanyakazi mmoja.

Kamati ya kudumu ya katiba na Sheria ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, imetembelea maeneo ya Mashirikiano ya Muungano ya Tume ya Haki za Binadanu na Mradi wa MIVARF kisiwani Pemba, ikiwa na lengo la kuona namna maeneo hayo yanavyofanya kazi kisiwani humo katika kuimarisha Muungano.



WAZIRI MKUU AHAMASISHA WAWEKEZAJI KUJA NCHINI

WAZIRI MKUU AHAMASISHA WAWEKEZAJI KUJA NCHINI

March 22, 2017
NHULU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika samaki aina ya jodari na kuwakaribisha viongozi wa kiwanda hicho kuja nchini kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya samaki.
Amesema Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji na pia ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya samaki, ambayo ni bahari, mito na maziwa ambayo aina mbalimbali za samaki.

Waziri Mkuu amesema hayo jana jioni (Jumanne, Machi 21,2017) wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha Mer des Mascareignes kilichoko  jijini Port Louis nchini Mauritius.

“Tanzania kuna fursa nyingi za uwekezaji hasa kutokana na mazingira yake. Mnaweza kuja kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki tuna bahari, mito na maziwa yenye samaki wa aina mbalimbali,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda ili kuongeza tija kwa Taifa na kwa wananchi kiujumla hivyo wanahitaji wawekezaji waliotayari kuja kuwekeza nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed alisema Tanzania inahitaji wawekezaji watakaowekeza kwenye uvuvi wa kina kirefu na ujenzi wa viwanda vya samaki.
Dkt. Khalid alisema lengo la uwekezaji huo ni kukuza uchumi wa Taifa pamoja kupanua soko la ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake.

Naye Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Patrick Hill alisema wamefurahi na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia fursa na uwekezaji na kwamba wako tayari kushirikiana na Serikali.

Alisema kampuni yao inajishughulisha na usindikaji wa samaki aina moja tu ya jodari na wananunua kutoka kwa makampuni makubwa ya uvuvi huku wateja wao wakubwa wakiwa ni bara la Ulaya.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda kingine cha  Chantier Naval Del`Ocean Indien Limited (CNOI) ambacho kinatengeneza na kukarabati meli , boti na pantoni na kujionea uwezo mkubwa walionao, ambapo Watanzania wanaweza kuja kujifunza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, MACHI 22, 2017.
MAKACHERO SARPCCO WAJADILI UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA.

MAKACHERO SARPCCO WAJADILI UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA.

March 22, 2017


CCO
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki akisaluti kwa wimbo wa taifa kabla ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabili uhalifu unaovuka mipaka. Kushoto ni Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai DCI, Robert Boaz. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
CCO 2
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahmani Kaniki akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabiliana uhalifu unaovuka mipaka. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
CCO 3
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahmani Kaniki akionyesha zawadi kutoka kwa Mkuu wa Interpol kanda ya kusini (kulia) baada ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabiliana uhalifu unaovuka mipaka. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
……………
 
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Wakuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai kusini mwa Afrika wametakiwa kuongeza ushirikiano katika kubadilishana taarifa za wahalifu na uhalifu unaovuka mipaka ili kuufanya ukanda wa kusini mwa Afrika kuwa salama.
 
Wito huo umetolewa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki mjini Bagamoyo alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Upelelezi wa Polisi kutoka Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika sambamba na kamati za ufundi za SARPCCO kwa lengo la kupanga mikakati ya kupambana na uhalifu na wahalifu.
 
Kaniki alisema ili kuwabaini wahalifu kwa urahisi ni vyema ushirikiano wa kubadilishana taarifa ukafanyika kwa haraka hasa kwa kuimarisha teknolojia ya habari na mawasiliano na mafunzo kwa maafisa wa Polisi ili kuwajengea uwezo wa kubaini mapema viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.
Aidha aliziomba Serikali za nchi wanachama kuendelea kutenga bajeti zinazokidhi mahitaji ya majeshi ya Polisi ili kuyawezesha kufanya kazi kwa ufanisi ambapo pia aliyataka majeshi hayo kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha zinazotengwa kwa lengo la kuimarisha mifumo ya kuzuia na kupambana na uhalifu.
 
Kwa upande wake Mkurungezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Robert Boaz alisema umoja huo utaendelea kuandaa oparesheni za pamoja katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka unaohusisha wizi wa magari, dawa za kulevya, biashara haramu ya usafirsishaji wa binadamu, uharamia, pamoja na ujangili.
Boaz alibainisha kuwa mkutano huo utajadili kwa kina utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa Wakuu wa Polisi uliofanyika mwezi Septemba mkoani Arusha pamoja na kuweka mikakati endelevu ya kukabiliana na uhalifu.
 
Naye Mkuu wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) Kanda ya Kusini Bw. Mubita Nawa alisema umoja huo umepata mafanikio makubwa kutokana na oparesheni mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mara kwa mara katika kukabiliana na uhalifu ambapo amesema biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu bado ni changamoto kwa nchi wanachama.
 
Shirikisho la Wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) lipo chini ya Uenyekiti wa Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania ambapo hivi sasa umoja huo unaundwa na nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesotho, Mauritius, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Shelisheli.
WAZIRI NAPE APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA TUKIO LILILOTOKEA CLOUDS MEDIA.

WAZIRI NAPE APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA TUKIO LILILOTOKEA CLOUDS MEDIA.

March 22, 2017
NOKO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Hassan Abbass.
NOKO 1
 Katibu wa Kamati ya Kuchunguza Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.
NOKO 2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati hiyo Deodatus Balile.
NOKO 3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa sakata hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass leo Jijini Dar es Salaam.
NOKO 4
 Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha Televisheni cha Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye ushahidi wa CCTV uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi leo Jijini Dar es Salaam.
NOKO 5
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia makabidhiano ya ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea taarifa ya kina kuhusu chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media akiwa na walinzi wenye silaha Machi 17, 2017.
Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas  ameishukuru Kamati kwa utulivu wao na kuifanya kazi hiyo kwa utaalamu na umakini mkubwa huku jamii ikitaka matokeo kwa haraka.
Aidha Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uamuzi na maelekezo.
“Nimeipokea ripoti na ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa wakubwa zangu wao ndo wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.
Kamati aliyoiunda Mhe Waziri ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni Bw.Deodatus Balile kutoka Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi Nengida Johanes wa Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Hassan Abbas  .

Tigo watoa simu 1,200 zenye thamani ya 113m/- kwa ajili ya zoezi la usajili wa vyeti vya kuzaliwa vya watoto chini ya miaka mitano mjini Geita

March 22, 2017
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya akihutubia wakazi wa Geita mara baada ya uzinduzi wa mradi wa mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano katika mikoa ya Geita na Shinyanga  ambapo kampuni ya simu za mkononi Tigo wametoa simu aina ya smartphone 1,200 zenye thamani ya Tshs. 133 zitakazo saidia kufanya usajili mikoani humo. Hafla iliyofanyika mkoani Geita jana. 




Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Harrison Mwakyembe akimkabidhi mtoto Agnes cheti cha kuzaliwa mara baada ya uzinduzi wa mradi wa mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano katika mikoa ya Geita na Shinyanga  ambapo kampuni ya simu za mkononi Tigo wametoa simu aina ya smartphone 1,200 zenye thamani ya Tshs. 133 zitakazo saidia kufanya usajili mikoani humo. Hafla iliyofanyika mkoani Geita jana. 



Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Harrison Mwakyembe akizindua  mradi wa mpango wa usajili wa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano katika mikoa ya Geita na Shinyanga ambapo kampuni ya simu za mkononi Tigo wametoa simu aina ya smartphone 1,200 zenye thamani ya Tshs. 133 kwa ajili ya kusajili vyeti vya kuzaliwa.Hafla iliyofanyika mkoani Geita jana. 

Baadhi y wakina mama na watoto wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kujiandikisha.


Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali na  wafanyakazi wa tigo,Unicef na RITA mara baada ya uzinduzi wa mradi wa mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano katika mikoa ya Geita na Shinyanga  ambapo kampuni ya simu za mkononi Tigo wametoa simu aina ya smartphone 1,200 zenye thamani ya Tshs. 133 zitakazo saidia kufanya usajili mikoani humo. Hafla iliyofanyika mkoani Geita jana. 
WILAYA YA BAGAMOYO KUNUFAIKA NA VISIMA VIREFU 17

WILAYA YA BAGAMOYO KUNUFAIKA NA VISIMA VIREFU 17

March 22, 2017
BGO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (kushoto) akiwa katika kikao cha majumuisho na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Maggid Mwanga mara baada ya kukamilisha ziara katika Wilaya hiyo.
BGO 1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) akiongea na Bi. Tatu Rajab mmoja wa wafanyakazi katika Kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Sea Salt. Waziri Makamba alifanya ziara kiwandani hapo kuangalia changamoto za mazingira.
BGO 2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah mara baada ya kutembelea kijiji cha Buyuni na kuongea na wananchi.
……………..
Na Lulu Mussa
Saadani – Pwani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake Ofisi yake imeandaa mradi utaonufaisha shule za msingi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Akiwa Wilayani Bagamoyo Waziri Makamba amesema kuwa, moja ya changamoto kubwa ya Wilaya ya Bagamoyo ni ukame unaotokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, uliopelekea kupanda kwa kina cha bahari na kusababisha visima vilivyochimbwa pembeni mwa miji na fukwe za bahari kufukiwa na maji na chumvi.
“Ofisi ya Makamu ya Rais imeamua kuisadia Wilaya ya Bagamoyo kuchimba visima kumi na saba (17) virefu kwenye maeneo ambayo yameathirika na kupanda kwa kina cha maji na maeneo yenye ukame mkubwa” Makamba alisisitiza.
Takribani kila kisima kitagharimu kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini na Ofisi ya Makamu wa Rais pia itaandaa mfumo wa kuvuna maji katika shule tano mradi utakao gharimu takribani Milioni mia moja sabini.
Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kiwanda cha Sea Salt kilichopo Saadani, Wilaya ya Bagamoyo kuona namna kiwanda kinavyofanya kazi kwa kuzingatia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
Waziri Makamba ambaye amewasili Mkoani Tanga kujionea hali ya mazingira na changamoto za uhifadhi pia ametembelea Wilaya ya Pangani na kukagua mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Pangani.
Waziri Makamba, amemtaka mkandarasi anayejenga ukuta wa mto Pangani kampuni ya ( DEZO CIVIL CONSTRUCTION L.TD ) kukamilisha ujenzi wa ukuta kwa kipindi cha muda wa miezi kumi, kama mkataba unavyoonyesha na kuzingatia ubora. Ujenzi huo wa  sehemu ya ufukwe wa kaskazini ambao una urefu wa mita 950 ambazo kati yake mita 550 zipo katika ujenzi wa awali utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 2.4
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zainab Abdalah amemuomba Waziri Makamba kutuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu kwa fukwe pekee iliyoko katika maeneo ya Tanga DECO ambayo imeathirika kwa kiasi kikubwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi na haipo katika bajeti kwa mwaka huu wa fedha.
Ziara ya kikazi wa Waziri Makamba leo imeingia siku ya pili na ametembelea Kijiji cha Buyuni ambapo pia alifanya mazungumzo na wakazi wa eneo hilo.

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI MKATABA WA MIAKA MITATU WA MASUALA YA UTAMADUNI

March 22, 2017
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia) wakibadilishana mkataba wa makubaliano utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya nchi hizo wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena ijini Dar es Salaam leo.

JUKWAA LA WAHARIRI LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MAKONDA

March 22, 2017
 Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena (katikati) akizungumza katika mkutano ana waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu tamko la vyombo vya habari la kususia kuandika habari za matukio ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ijumaa iliyopita alivamia kituo cha Clouds Media usiku akiwa na askari waliokuwa na bunduki. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Dar Press Club, Shadrack Sagati na Mjumbe wa TEF, Lillian Timbuka.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0754264203
 Meena ambaye alisoma  tamko la pamoja la TEF, Dare sSalaam Press Club na Umoja wa Vilabu vya Habari nchini akijibu moja ya maswali ya wanahabari
 Wanahabari wakiwa kazini
 Meena akifafanua jambo

 Meena akisisitiza kuwa mwandishi yeyote atakayekiuka tamko hilo kwa kwende kwenye matukio ya RC Makonda, litakalompata TEF haitahusika kwa lolote.

MKUU WA MKOA WA TANGA, MARTIN SHIGELLA AWAPIGA MSASA MAKATIBU TAWALA

March 22, 2017
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, amesema Utafiti mpya wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi kwa kutumia mfumo wa (CD4T-cell count) utasaidia kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
Amesema Utafiti huo utaangazia pia kuwepo kwa Viashria vya Usugu wa dawa, kiwango cha maambukizo ya Kaswende na homa ya Ini kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.
Amesema Tafiti tatu zilizotangulia zimekuwa zikiwahusiha wananchi wenye umri wa miaka 15 hadi 49 tofauti na utafiti wa mwaka 2016/ 2017 ambao ni wa  kipekee ambapo kwa mara ya kwanza wananchi wa rika zote katika kaya zilizochaguliwa watahusihwa.
Kwa upande wake, Meneja Takwimu Mkoa wa Tanga, Tonny Mwanjoto, aliwataka Makatibu Tawala kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi shuleni kutokomeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Alisema kufanya hivyo itasaidia  juhudi za Serikali kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua ikiwa na pamoja na kuyatokomeza moja kwa moja.

BOMOA BOMOA KANDO YA RELI YALIKUMBA ENEO LA KURASINI DAR

March 22, 2017

 Katapila likibomoa majengo ya Baa ya Pentagon  katika oparesheni ya bomoa bomoa nyumba zote zilizojengwa katika hifadhi ya Reli ya Kati eneo la Mivinjeni, Kurasini Dar es Salaam. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0754264203
 Makontena ya biashara yakiwa yamefumuliwa na katapila
 Baa ya Pentagoni ikiwa imebomolewa 
 Katapila likiendelea na kazi ya bomoa bomoa

 Baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwa na vibanda vya biashara pamoja na wananchi wakishuhudia ubomoaji huyo
 Askari wakilinda doria wakati wa ubomoaji
Wataalamu wakipima mita 20 kutka kwenye reli ili nyumba na mabanda yaliyo ndani ya hifadhi ya reli zibomlewe kupisha ujenzi wa reli ya kisasa.

PICH ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0754264203