Abiria
waliokwama na treni Dodoma wakusubiri mabasi kwa ajili ya usafiri
wa kuelekea mikoa ya Morogoro, Dar es saalam na Kigoma baada ya abiria
hao kukodishiwa mabasi na shirika la Reli kutokana na kushindwa
kuendelea na safari baada ya njia ya Reli kukumbwa na mafuriko katika
eneo la Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Hapa abiria
hao wakiendelea kusota katika Kituo cha Treni mjini Dodoma.
Abiria hao wakiwa katika kituo hicho hawajui la kufanya kutokana na kukosa chakula katika
stesheni ya reli mkoani Dodoma walipotangaziwa kuanza kusafirishwa kwa mabasi
lakini mpaka kufikia leo jioni zaidi ya abiria 900 kati ya 1600 walikuwa bado
hawapatiwa usafiri huo.
Mfanyakazi wa shirika Reli kituo cha Dodoma akiandika tangazo katika
ubao wa matangazo lililowataka abiria waliokuwa wanaelekea mikoa ya kanda ya ziwa
kurudishiwa nauli zao kutokana na usafiri wa treni kusitishwa kwa muda
usiojulikana.
Askari wa kuzuia Ghasia (FFU) wakiangalia usalama kwa abiria wa treni
waliokwama kutokana na treni kushindwa kuendelea na
safari tangu juzi mara baada ya kufika kituo cha reli mkoani Dodoma kutokana
na maji ya mvua iliofunika reli wilayani Mpwapwa.
Na John Banda, Dodoma
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limelazimika kuwasafirisha abiria
waliokwama katika kituo cha Treni cha Dodoma kwa mabasi, kwa siku mbili
katika Stesheni mkoani Dodoma waliokuwa wanasafiri kwa Treni kutoka
mikoa ya Kanda ya Ziwa, kutokana na kushindikana kwa ukarabati
unaoendelea kufanyika mpaka sasa ambao umeonekana kushindikana kutokana
na wingi wa maji yaliyopo kwenye eneo hilo la Gulwe na Godegode
lililopo Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Stesheni hii Masta wa Kituo
cha Reli Dodoma, Zakaria Kilombele alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya
ukarabati huo unaoendela kwa hivi sasa kwenye njia hiyo ya relishirika
limeamua kuwasafisha abiria hao waliokwama kwa kutumia mabasi.