WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA MKOANI SIMIYU

March 06, 2016

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua jengo la matibabu ya wazee baada ya kulizindua kwenye hospitali ya Wilaya ya Meatu iliyopo Mwanhuzi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na watumishi wa serikali katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Metu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu kuhutubia Mkutano wa hadhara Machi 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu kuhutubia Mkutano wa hadhara Machi 5, 2016.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Erasto Mbwilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Stendi mjini Mwanhuzi. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali  katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa  
Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha  taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu.

Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya mishahara. 

Akitolea mfano wa kada ya ualimu, Waziri Mkuu alisema ajira za walimu zilikuwa zinaanzia Idara ya Utumishi wa Walimu  (TSD)  lakini anapaswa aende kuripoti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  (DED) ambaye ni mwajiri wake chini ya TAMISEMI. "Hii ilileta ugumu wa malipo ya kupanda madaraja, uhamisho ama likizo kwa sababu mwajiri anakuwa hajatenga hizo fedha."

"Sasa hivi tuna Tume ya Utumishi wa Walimu  (TSC) ambayo iko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Kwa hiyo ni rahisi wao kukaa pamoja na kuamua tuwapandishe daraja walimu 10 na wote hao wakalipwa bula bila kuchelewa," alisema.

Alisema mfumo huo umeanza kutumika tangu mwaka 2012 na ulianza kwa ajira mpya za wakimu na hadi sasa umethibitisha kuwa inawezekana kumlipa mtumishi mshahara wake hata kama ameajiriwa ndani ya mwezi huohuo.

"Kama mtumishi anaripoti kwenye kituo kipya hata iwe wilaya ya wapi ili mradi amefika na barua zake zote na ziko sahihi mtu huyu ataingiziwa taarifa zake na wakati huohuo taarifa zitaonekanaOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na pia zitapokelewa kwa maafisa wanaoshughikia mishahara kule HAZINA."


Alisema changamoto pekee waliyokutana nayo wakati mfumo huo umeanza ilikuwa ni kutoingizwa taarifa za wale ambao wameripoti baada ya tarehe 10 ya mwezi husika. "Hii ni kwa sababu matayarisho ya mishahara yanakuwa yameshaanza. Kwa hiyo wengi walishauriwa kuripoti kati ya tarehe 25 hadi tarehe 9 ya mwezi uliofuata na wote hawa hawakupata matatizo ya kucheleweshewa mshahara," alisema.

Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema  Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya. "Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara  na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua hiyo hiyo " alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelazimika kukatisha ziara ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa imalizike kesho kutokana na msiba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo alipangiwa kuitembelea leo.
Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. 

Atasafirishwa kwenda Muleba  kwa mazishi.

Akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya kumuombea marehemu Kagenzi iliyofanyika nyumbani kwake Maswa mjini, Waziri Mkuu alisema ameshtushwa na msiba huo uliotokea ghafla na kwamba Taifa limempoteza mtumishi mahiri ambaye bado Taifa lilikuwa likimtegemea.

"Nimeshtushwa sana na taarifa za msiba huu. Nimeambiwa hadi juzi usiku alikuwa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hii kuandika taarifa ya ziara ya wilaya hii. Kwa niaba ya Serikali, ninawapa pole sana wafiwa na Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi," alisema.


"Nimelazimika kukatisha ziara ya mkoa huu kwa sababu huyu ni mtumishi mwenzetu.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWAHUTUBIA WANAWAKE KWENYE MAADHIMISHI YA KIMATAIFA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWAHUTUBIA WANAWAKE KWENYE MAADHIMISHI YA KIMATAIFA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

March 06, 2016

WN1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TRUMARK Agnes Mgonge alipowasili katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.
WN2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja Viongozi wa Kampuni ya TRUMARK iliyoandaa sherehe ya maadhimisho ya siku ya Ki,ataifa ya Wanawake Duniani alipowasili katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni  March 05,2016 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho hayo.
WN3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidha katika maonesho ya Vikundi vya Wajasiriamali wa Vikoba kutoka katika taasisi mbalimbali  kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016. kulia Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangala.
WN4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidha katika maonesho ya Vikundi vya Wajasiriamali wa Vikoba kutoka katika taasisi mbalimbali  kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016. kulia Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangala.
WN5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidha katika maonesho ya Vikundi vya Wajasiriamali wa Vikoba kutoka katika taasisi mbalimbali  kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016. kulia Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangala.
WN6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidha katika maonesho ya Vikundi vya Wajasiriamali wa Vikoba kutoka katika taasisi mbalimbali  kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016. kulia Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangala.
WN7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtunza msanii wa kikundi cha Barnaba Bibi Patrisha Hilary alipokua akiimba nyimbo ya kusifu siku ya Wanawake Duniani  kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016.
WN8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana March 05,2016.
WN11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja Viongozi wa Kampuni ya TRUMARK iliyoandaa sherehe ya maadhimisho ya siku ya Ki,ataifa ya Wanawake Duniani alipowasili katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni  March 05,2016 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho hayo.
WN12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuzungumza na Wajasiriamali wa Vikundi vya Vikoba kutoka katika taasisi mbalimbali baada ya kuwahutubia kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016 (Picha na OMR)

MFANYABIASHARA WA UTALII ARUSHA ATOA MISAADA YA KIJAMII HOSPITALI MKOA WA ARUSHA LEO.

March 06, 2016

 
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet .c.Mfuko akizima mshumaa alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyofanyikia katika hospitali ya mt.Meru jijini Arusha jana
 Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet .C.Mfuko akikata keki alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa iliyo fanyika katika hospitali ya mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimlisha keki mkurugenzi mwenzake, ambae ni (mme wake) ndugu Kim Godwin Fute,alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyo fanyika katika hospitali ya mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimkabidhi shuka mganga mkuu mfawidhi wa hospital ya mt.Meru dr.Jackline Urio alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.
 Picha ya pamoja ya marafiki wa Violet ilipigwa.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimuombea mgonjwa Frida Shayo alipotembelea hospitali ya mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana. 
Mkurugenzi Viola Mfuko anamlisha keki Habibya Fadhili alipotembelea hospital ya mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.
********************
Katika kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani machi nane baadhi ya wanawake jijini Arusha wanaadhimisha siku hiyo kwa matukio mbalimbali ambapo mwanamke mjasiriamali wa jijini humo Violet Mfuko amejitolea kujenga sehemu ya kusubiria na kufanyia ibada katika mochwari ya hospitali ya mkoa wa Arusha ya mountmeru pamoja na mashimo nane ya vyoo katika sehemu hiyo.
 
Akiwa ameongozana na wakina mama wengine walianzia kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika wodi ya wanawake na watoto ambapo Viola anasema baada ya kutembelea sehemu ya mochwari katika hospitali  hiyo aligundua changamoto hiyo ambayo ilimgusa na kuamua kujitolea kuanza ujenzi wa jengo hilo kuanzia jumatatu machi 7 ambalo litagharimu kiasi cha shilingi milioni 50.
 
Alisema ameamua kujikita katika kusaidia jamii badala ya kutumia fedha zake katika mambo ambayo hayana faida kwa jamii na kysisitiza kuwa baada ya kupewa ramani na uongozi wa hospitali ataanza ujenzi jumatatu machi 7 mwaka huu.
 
Alisema baada ya kujionea adha wsnayoipata wafiwa kukosa sehemu ya kusubiria miili ya marehemu na vyoo vinavyotumika kuwa ndani ya mochwari aliguswa na suala hilo na kuamua kujenga vyo na sehemu hiyo.
 
“Tayari nimeshapokea ramani nitaanza ujenzi jumatatu nawaomba wana Arusha mnipe ushirikiano tuweze kumsaidia rais magufuli yeye alianza na muhimbili sisi tumeamua kumsaidia hospitali yetu ya mkoa”alisema Violet.
 
Viola ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Viola car hire yenye makao makuu yake jijini Arusha anatumia siku yake ya kuzaliwa kutoa msaada katika hospitali hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa mji wa Arusha kuanza kuisadia serikali kuboresha sekta ya afya kwa kuwa sekta hiyo inachangamoto nyingi.
 
“Mimi nikiwa ni mwanamke ninajua changamoto nyingi zinazotukaabili kina mama na watoto  ambapo naamini ukimsaidia mama na mtoto umegusa jamii nzima”alisema Violet
 
Hata hivyo baadhi ya wajasiriamali wengine wa jijini humo wanaunga mkono jitihada za mwanamama huyo  ambapo daktari Edmund Matafu anajitolea mashine mbili za hewa safi kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya muda yaani njiti.
 
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya mountmeru Jackline Uriyo amemshukuru Violet na Dakta Matafu kwa  msaada wao ambao amesema umefika  wakati mwafaka.
 
“Kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya mountmeru tunatoa shukrani za dhati kwa Viola na dakta Matafu tunawaomba waendelee na moyo huo lakini tunatoa wito kwa watu wengine wenye mapenzi mema kuisaidia hospitali ya mkoa kwani inalabiliw na changamoto nyingi”alisema Uriyo
 
Mbali na msaada huo Viola pia ametoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka mia mbili,sabuni,mchele,juisi soda mablanketi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.
Mama Janeth Magufuli awataka wadau kujitokeza kusaidia wazee na watu wasiojiweza.

Mama Janeth Magufuli awataka wadau kujitokeza kusaidia wazee na watu wasiojiweza.

March 06, 2016


net1

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini Mwanza kushiriki zoezi la utoaji wa msaada wa vifaa mbalimbali kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
net2
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali, Chama pomaja na Wananchi walifika kumpokea alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
net3
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali, Chama pomaja na Wananchi walifika kumpokea alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
net5
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiangalia burudani ya ngoma alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
net6
Baadhi ya misaada iliyotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
net7
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shada la maua alipowasili kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
net12
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa heshima na kuwasalimia wananchi walifika kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei.
net13
Baadhi ya sehemu ya wazee wakiimba kwa furaha wakati hafla ya utoaji wa Msaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
net14
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mwajuma Nyiruka akiongea na wananchi waliojitokeza katika hafla ya utoaji wa Msaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza na kumshuruku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa kushiriki katika hafla hiyo.
net15
Afisa Mfawidhi na Mlezi wa Kituo kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza kilicho chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii Bw. Michael Bundala akiongea na wananchi na kushukuru wadau waliotoa msaada katika kituo hicho.
net16
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akiongea na wazee wa kituo kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza, wananchi waliohudhuria hafla ya utoaji wa Msaada katika kituo hicho na kumshukuru Mama Janeth Magufuli kwa kuwakumbusha juu ya utoaji msaada na kuwajali wazee na watu wasiojiweza na kumahidi kuandaa sera mpya ya kusaidia watu wenye mahitaji.
net17
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma na wazee wa  Kituo kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
net18
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akimkaribisha Mama Janeth Magufuli kuongea na Wazee na pia kuwahakikishia wazee kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia katika ahadi zake hasa katika kuhakikisha wazee wanapata huduma bila usumbufu.
net19
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika Kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali na kuyashukuru mashirika, Taasisi za serikali pamoja na sekta binafsi kwa kutoa misaada hiyo ikiwemo Mchele, Unga, Maharage, Mafuta ya kupikia, mashine za kufulia pamoja na solar panel pia akatoa rai kwa wadau wengine kujitolea kusaidia wazee na watu wasiojiweza.
net20
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kumaliza kuongea na wazee
net21
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kumaliza kuongea na wazee
net22
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akishiriki katika kukabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo CRDB, PPF na Makampuni binafsi  kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
net23
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akishiriki katika kukabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo CRDB, PPF na Makampuni binafsi  kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
net24 net25
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee katika kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
net25
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na watoto wakati wa hafla ya utoaji wa Misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza Bukumbi Mkoani Mwanza