RAIS MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JESHI LA ULINZI TANZANIA 165

February 19, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa hafla ya utoaji wa Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi la Ulinzi waliohitimu Chuo cha Mafunzo kwa Maofisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha, iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akitoa Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi la Ulinzi Tanzania waliohitimu Chuo cha Mafunzo kwa Maofisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22. Katika wahitimu wa jumla walikuwa 180 ambapo 15 ni kutoka nchi jirani za Uganda(2), Burundi(5), Rwanda(3) na Kenya(5).
Maofisa wapya wa Jeshi la Ulinzi Tanzania wakivalishana vyeo mara baada ya kupewa Kamisheni na Rais John Pombe Magufuli katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi mmoja wa Afisa wa Jeshi la Ulinzi  Tanzania wakati wa hafla ya kutoa Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi la hilo waliohitimu Chuo cha Mafunzo kwa Maofisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22. Katika wahitimu wa jumla walikuwa 180 ambapo 15 ni kutoka nchi jirani za Uganda(2), Burundi(5), Rwanda(3) na Kenya(5).
Mkuu wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli (TMA)  Meja Jenerali Paul Massao akitoa historia fupi ya Kozi ya kwa Maofisa wa Jeshi waliotpewa Kamisheni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Maofisa wapya wa Jeshi la Ulinzi Tanznia mara baada ya kumalizika kwa zoezi la utoaji wa Kamisheni kwa Maofisa ha oleo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Kwanza Jenerali Mstaafu Merisho Sarakikya, Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22. Picha zote na:  Frank Shija & Eliphace Marwa - MAELEZO

DC MUHEZA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA UBWARI KUJIONEA ZOEZI LA UPASUAJI MACHO KWA WANANCHI WANAONA MATATIZO YA JICHO LA MTOTO.

February 19, 2017
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akiingia kwenye kituo cha Afya Cha Ubwari leo wakati alipokwenda kuangalia zoezi la upasuaji wa macho kwa wakazi wa wilaya hiyo wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya mtoto wa Jicho iliyoendeshwa na Taasisi ya Medewell Charitable Health Centre kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo,Mathew Mganga na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Luiza Mlelwa.

 Baadhi ya wazee waliofanyiwa upasuaji wakisubiri zoezi la kupatiwa dawa na miwani
 Baadhi ya wananchi waliofanyiwa upasuaji wakisubiri zoezi la kupatiwa dawa na miwani
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa akizungumza wakati wa zoezi hilo la upasuaji
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa zoezi la upasuaji huo.
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee waliojitokeza kupatiwa huduma za upasuaji wa macho waliokuwa na matatizo ya mtoto wa Jicho


 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akimkabidhi msaada wa vyakula mbalimbali mwakilishi wa wazee waliofanyiwa upasuaji wa macho ili viweze kuwasaidia baada ya kumalizika upasuaji huo watakapokwenda majumbani mwao wanaoshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa ,Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo,Mathew Mganga wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza
Desderia Haule
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa akipongezwa na mwakilishi wa wazee hao mara baada ya Mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo wa pili kulia kuwakabidhi vyakula vitakavyowasaidia watakapotoka kwenye matibabu hayo na kurejea makwao

SHAKA AZINDUA MAFUNZO YA UJASIRIA MALI KWA MAKATIBU NA WENYEVITI UWT KATA 18 MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

February 19, 2017
 Mwenyekiti wa UWT wa Uwt Mkoa wa Kaskazini akimkaribisha Mgeni Rasmi katika Ufunguaji  wa Semina ya Mafunzo ya Ujasiliamali Shaka Hamdu Shaka Kaimu Katibu Uvccm Taifa
 Kaimu Katibu UVCCM  Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika kufungua Semina hiyo ya mafunzo ya Ujasilia mali kwa Makatibu na Wenyeviti wa UWT kata18 Mkoani Kaskazini Unguja Alisema”Lazima tuhamasishane kwani  dhana hii ya Tanzania ya viwanda haihitaji mamilioni ya pesa tunaweza kuanzisha viwanda vidogo  vidogo  na vijana wakapata ajira, kukamilika kwa mafunzo haya  na tija yake ikaonekana ndani ya jamii naamini tutakuwa tumepunguza malalamiko ya vijana na wakinamama,  jukumu kubwa sasa ni kuwasimamia, kuwaendeleza  ili mkikamilisha
mafunzo haya  malengo yaweze kufikiwa , na pia tunataka  mkawe kielezo kizuri  cha uhalisi wa jambo hili katika maeneo yenu, hata hizi million moja  nilizowachangia naelekeza zikanunuliwe malighafi ili kuongeza
 uzalishaji na kuimarisha mfuko wenu muda huu mkiendelea na mafunzo”

Mbunge wa viti  Maalum na mfadhili Mkuu wa mafunzo hayo Mhe  Malembeka akimkabidhi moja ya Bidhaa  iliyo tengenezwa  katika Mafunzo hayo aina ya batiki kaimu katibu mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka katika ufunguaji wa semina ya mafunzo ya  Ujasiria mali kwa makatibu na wenyeviti UWT kata 18 Mkoani Kaskazini Unguja.
Baadhi ya Washiriki wa Semina hiyo
Kaimu Katibu  Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akionyeshwa aina mbali mbali za Batiki zilizo tengenezwa na Washiriki wa Semina ya mafunzo ya ujasiliamali kwa maklatibu na wenyeviti UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mbunge wa viti  Maalum na mfadhili Mkuu wa mafunzo hayo Mhe  Malembeka wa kwanza kushoto akimuonesha na kumfafanulia Ndg:Kaimu Katibu Mkuu namna kemikali zinazo baki mara baada ya utengenezaji wa batiki
 
(picha zote na Fahadi Siraji)
RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA NYUMBANI KWAKE UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA NYUMBANI KWAKE UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM

February 19, 2017

MSU1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu.
MSU2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
MSU3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
MSU4
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake Upanga kwa ajili ya  kumjulia hali.
MSU5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
UKO NA MPENZI.....? NAFASI NDIO HII

UKO NA MPENZI.....? NAFASI NDIO HII

February 19, 2017
Hookup 255 ni reality TV Show inayo kukutanisha wewe na mtu ambaye haujawahi kukutananae ila mnaendana kitabia, upendo, malengo na end of the day mnaweza kuwa wapenzi forever. https://www.youtube.com/watch?v=fA1U61XSMN0 Nafasi ni yako msichana wa Kitanzania mwenye umri wa 18- 34 unaweza kutuma picha na namba yako inbox kwenye acount zetu Instagram na Facebook page ili uingizwe kwenye list ya washiriki wa kipindi chetu kizuri. Kutakuwa na mchujo coz tunahitaji watu walio Serious kuhusu kupata mpenzi mwenye vigezo vinavyo stahili. Endapo utapita kwenye mchujo wetu utapatiwa form ya kujaza, utakapo irudisha form utalipia Tsh: 2000/= tu. Huenda zari ikakudondokea wewe mdada kukutana na Hookup 254 ya Kenya na mambo yakawa Bam bam.

Usajili wa Tigo Kili Half Marathon 2017 jijini Dar Es Salaam

February 19, 2017


 Katibu wa Kawe jogging Social and sport Club,  Seif Muhere akipokea tiketi za Kili marathon kutoka kwa Mwakilishi wa Tigo,  Viola Mboya kwa ajili ya ushiriki wa mashindano Tigo Kili Half Marathon 21Km, yanayotarajiwa kufanyika jumapili ijayo Tarehe 26 Februari  mkoani Kilimanjaro. Usajili huo ulifanyika jana Jumamosi Mlimani city jijini Dar es Salaam kwa kujisajili kwa kulipia kwa kutumia Tigopesa na zoezi  linaendlea leo siku ya jumapili.



Usajili unaendelea Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Wananchi mbalimbali wakiendelea na Usajili wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwenye banda la Tigo jijini Dar es Salaam jana tayari kwa mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 26 mwezi huu, Usajili huo ulifanyika kwa kutumia huduma ya Tigopesa,Zoezi la usajili linaendelea leo pia.



Wananchi mbalimbali wakiendelea na Usajili wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwenye banda la Tigo Mlimani city  jijini Dar es Salaam jana tayari kwa mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 26 mwezi huu Mkoani Kilimanjaro , Usajili huo ulifanyika kwa kutumia huduma ya Tigopesa.


KIPINDUPINDU CHAPIGA HODI JIJINI DAR ES SALAAM CHAUA MTU MMOJA WENGINE 12 WALAZWA HOSPITAL

February 19, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 Na Dotto Mwaibale

WAKATI jiji la Dar es Salaam likiwa katika  mapambano ya kukabiliwa na dawa za kulevya jiji hilo limekumbwa na ugonjwa wa kipindupindu ambapo mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Ramadhan Kiumbo (maarufu kwa jina la Popo) mkazi wa Kibada Kigamboni amefariki kutokana na ugonjwa huo.

RC MTAKA: MFUKO WA BIMA YA AFYA NDIO MTINDO WA KISASA WA HUDUMA KATIKA NCHI ZOTE DUNIANI

February 19, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akihutubia katika Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF/CHF

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda akizungumza katika Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF/CHF Mkoani Simiyu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (kulia) katika Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF/CHF
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya Taifa Ndg Leonard Konga akitoa taarifa ya Maboresho ya huduma kwa wanachama na wadau wa mfuko wa Bima ya afya
Rc Mtaka akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda akisisitiza jambo katika Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF/CHF Mkoani Simiyu
Kaimu Meneja wa Bima ya afya Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Shinyanga Ndg Immanuely Imani akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF Mkoa wa Simiyu
Rc Mtaka akielezea ruksa ya uwekezaji katika mkoa wa Simiyu ikiwa ni pamoja na ruhusa ya kutoa eneo la ardhi bure kwa yeyeote anayetaka kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe Tano Mwera akishauri uongozi wa Bima ya afya Taifa kuweka wazi magonjwa yasiyotibiwa kwa kutumia Bima ya afya huku akitilia mkazo kadhia ya unyanyapaa wanayokumbana nayo watumiaji wa Bima ya afya
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka katika Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF/CHF alipozuru katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Wadau wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF/CHF wakisikiliza kwa makini huku wengine wakipata nafasi ya kuuliza maswali kwenye mjadala katika Mkutano huo

Na Mathias Canal, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amesema kuwa ushirikiano baina ya Ofisi yake,Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na wananchi kwa ujumla utaufanya mkoa huo kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi kujiunga kwenye mfuko wa Bima ya Afya kama ambavyo lengo la Bodi na wizara ya afya limekusudiwa Kwani wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya afya ndio mbinu pekee rahisi na kisasa katika matibabu duniani kote.

RC Mtaka ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF/CHF, Mkutano uliokuwa na madhumuni ya kubaini changamoto zinazowakabili wananchi wanaotumia Mfuko wa Bima ya afya sawia na kutoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Bima ya afya.

Ameeleza kuwa kujiunga na mfuko huo ni muhimu kwa wananchi kwani watapunguza gharama kubwa wakati wa matibabu kwa wale ambao hawajajiunga kwani wanapaswa kutambua kuwa ugonjwa hauna Siku rasmi ya kuingia mwilini unawakumba watu wakati wowote pasina kubisha hodi.

Katika kufikia dhamira ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ili kuwa na Tanzania ya viwanda Mkuu Huyo wa Mkoa wa Simiyu ameiomba Bodi ya Mfuko huo wa Bima ya afya kuanzisha ofisi za Mkoa kwani watapatiwa eneo la ujenzi pasina kulipia.

Hata hivyo amesema kuwa kwa yeyote anayetaka kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha kutengeneza Dawa na vifaa tiba atapatiwa eneo Bure kwa ajili ya kuanzisha kiwanda hicho.

Awali akitoa taarifa ya Maboresho ya huduma kwa wanachama na wadau wa mfuko wa Bima ya afya Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya Taifa Ndg Leonard Konga amesema kuwa Mfuko wa Bima ya Afya ni Taaisi ya umma iliyoundwa kwa mujibu wa sheria sura Na 395 TL 2002 ambapo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya mabadiliko katika sekta ya afya iliyoanza kutekelezwa kuanzia miaka ya 1990.

Mfuko huo umeanzishwa kwa dhamira ya kutoa Bima ya afya kwa makundi mbalimbali ya wananchi, Kujenga uwezo wa kifedha kwa vituo, Kushirikisha sekta binafsi katika kuharakisha maendeleo ya sekta ya afya.

Konga amesema kuwa mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Bima ya afya yanategemea kila mdau kutimiza wajibu wake kwani mazingira ya kiutendaji ni kusimamia na kutekeleza miongozo na maagizo ya serikali kupitia wizara yenye dhamana ya kusimamia upatikanaji wa huduma za afya.

Amebainisha kuwa lengo mahususi katika utekelezaji wa mpango wa Mfuko wa Bima ya afya ni kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi ngazi ya hospitali ya Mkoa, Kuongeza wigo mpana zaidi kwa watanzania wanaopata huduma za matibabu kupitia Bima ya Afya.

Naye Kaimu Meneja wa wa Bima ya afya Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Shinyanga Ndg Immanuely Imani akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF Mkoa wa Simiyu amezitaja changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na Upungufu wa dawa katika baadhi ya vituo, Ukosefu wa vifaa tiba na ubovu wa majengo, Baadhi ya waajiri kuchelewesha madai, Watoa huduma wachache kuwasilisha madai yenye kutiliwa shaka na mwitikio mdogo wa wananchi kujiunga na NHIF/CHF.

Sambamba na hayo pia ameelezea matarajio ya Mfuko wa Bima ya afya katika Mkoa wa Simiyu kuwa ni pamoja na kuelimisha watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji kwa ajili ya kununulia dawa, kuhimiza watoa huduma kuomba mikopo ya vifaa tiba, ukarabati, dawa na vitendanishi.

Matarajio mengine ni pamoja na kuendelea kuimarisha ukaguzi wa waajiri ili kutoa michango sahihi kwa wakati, Kuimarisha mifumo ya ulipaji madai ili kuzuia malipo ya madai yasiyo halali na kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika kuhamasisha jamii kujiunga na Mfuko wa Bima ya afya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda Amesema kuwa Bodi yake imekusudia kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi sawia na kupinga vikali lugha mbovu zitolewazo na baadhi ya watoa huduma katika sekta ya afya dhidi ya wananchi wanaoenda kupata matibabu katika Zahanati, Vituo vya afya, Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa.

Amesema katika maeneo mengi waliyopita wamebaini kuwa wananchi wengi wametumia fedha zao kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya lakini wanapoenda kuhudumiwa wanakumbana na matusi pasina huduma bora.
Bi Makinda amesema kuwa wanaendelea na utaratibu wa kubaini zahabati, kituo cha afya ama Hospitali zinazokiuka utaratibu Na baada ya kubainika tu watachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Hata hivyo ameeleza jinsi ambavyo mtandao wa matibabu wa serikali ulivyo mzuri kwani unaanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.

Bodi hiyo imeahidi kufungua Ofisi za mikoa mipya ya Njombe, Katavi, Geita huku wakiahidi pia kuanza ujenzi na kufungua ofiai katika Mkoa wa Simiyu baada ya kupewa eneo la ujenzi Bure na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Antony Mtaka.

Ndalichako kumaliza migogoro ya walimu kwa kushirikiana na wizara nyingine

February 19, 2017

  Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akiendesha mjadala wa kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili wa wadau wa elimu kutoka nchi 13 uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conventional Centre (JNICC) jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige)
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, iliyona makazi yake nchini Marekani akielezea kuhusu mradi wa XPRIZE unahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao ukilenga watoto wa miaka 5-12 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akielezea jitihada zitakazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu kuelekea utekelezaji wa SDG4 kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Elimu, Rasilimali Watu na Tafiti za Kisayansi wa Mauritius, Leela Dookon Luchoomon (kushoto) akieleza mipango ya serikali yake katika kuboresha elimu wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank.
 Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles akizungumza kwa niaba ya nchi wahisani wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Djibouti, Mh. Moustapha Mohamed Mahamoud akiwasilisha mapendekezo ya serikali yake katika kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Waziri wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh. Nansubuga Rosemary Seninde (kulia) akitoa mapendekezo ya serikali yake katika kuboresha elimu kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mh. Mhandisi Stella Manyanya (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo wakiandika mapendekezo muhimu yaliyokuwa yakiwasilisha kwenye mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Sehemu ya mawazi wa elimu kutoka Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia, Comoro na Djibouti walioshiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
  Sehemu ya wadau wa sekta ya elimu kutoka nchi 13 walioshiriki kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na wadau wa sekta ya elimu wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) walioshiriki kufanikisha mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo (kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.


Na Zainul Mzige
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wizara yake itashirikiana na wizara nyingine nchini kuhakikisha kwamba migogoro ya walimu inamalizwa ili kufanikisha utoaji wa elimu kuwa bora na jumuishi.
Kauli hiyo aliitoa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika siku ya pili ya kuhitimisha kwa mkutano ulioshirikisha nchi 13 za Afrika Mashariki kujadili lengo la nne la elimu kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs)
Alisema kwamba migogoro ya walimu inayogusa mishahara, marupurupu pamoja na mazingira bora ya kazi linagusa pia Wizara za TAMISEMI na UTUMISHI na kusema kwamba wao kama wasimamizi wa elimu watakachoweza kufanya ni kuzungumza na wenzao kuhakikisha kwamba migogoro hiyo inafutwa ili utoaji wa elimu uendane na mipango ya kitaifa na kidunia ya lengo la maendeleo 2030.
Pamoja na kujibu swali hilo Prof Ndalichako alizungumzia  kwamba walimu walikuwa ni ajenda muhimu  na humo walikubaliana kwamba mwalimu ni kila kitu katika utoaji wa elimu na kuwa hawawezi kufanikiwa katika elimu bora na jumishi bila kuwa na walimu wenye umahiri, wanaowezeshwa kufanya hivyo.
Kutokana na ukweli huo wamejipanga kuhakikisha kwamba walimu wanapata mafunzo bora na kuwakutanisha kubadilishana uzoefu.
Alisema kila nchi itakuwa na mpango mkakati wake na kuonesha viashiria kwamba vinatekelezwa kwa namna gani. Mwisho wa siku mwaka 2030 mataifa yote yanapaswa kuhakikisha kwamba agenda namba 4 ya maendeleo endelevu ya elimu imetekelezwa.
Alisema katika mkutano huo wa siku mbili wa mawaziri wa elimu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank wamebainisha kwamba mikakati ya pamoja ni lazima ichukuliwe ili kufanikisha elimu jumuishi yenye usawa na ubora kwa watu wote huku ikitoa fursa ya elimu kwa wakati wote.
Alisema kwamba mkutano ulitambua kwamba elimu haina mwisho, elimu inataka kuwa na mfumo wa kuwa na maendeleo ya kujifunza kwani mambo hayasimami kutokana na kubadilika kwa teknolojia, hivyo elimu inayotolewa haina budi kujazia nafasi hiyo kwa kuwapa uhuru watu kujisogeza zaidi.
Alisema nchi hizo 13 zimekubaliana kwa pamoja kufikia malengo endelevu 2030 kama yalivyosainiwa na kila nchi mwaka 2015 kwa kuweka mikakati ili mataifa hayo yaweze kufikia malengo yanayotakiwa.
Aidha alisema kama walikubaliana kwanza kuimarisha elimu ya awali kwa lengo la kuweka msingi wa kujifunzia, kwani ipo methali inayoaminika kwamba samaki mkunje angali mbichi na taifa likitaka watoto wasome ni lazima kuwaanzia wadogo.

Aidha  mataifa hayo yamekubaliana upimaji wa wanafunzi kufanyika kwa ajili ya kujifunza, ukilenga kutumia matokeo kuandaa mafunzo kwa wanafunzi. Upimaji uoneshe eneo la ambalo walimu watalazimika kufanya kazi ya ziada ili wanafunzi wao waelewe.
Mfumo wa sasa wa kupima umelenga kujua watoto wangapi wamefaulu na wangapi wamefeli.
Ndalichako alisema ni vyema upimaji huo kutumika kuimarisha mafunzo ya walimu.
Jambo la tatu ambalo walikubaliana ni kuhakikisha kwamba mtoto wa kike anasoma na wale wenye mazingira hatarishi pia; na bila kujali kujali mazingira yao nchi zinatakiwa kuweka mikakati ya  elimu iliyobora kwa wote.
"Suala muhimu katika elimu ni kupanga mipango sahihi. Takwimu sahihi ni changamoto kutokana na ukweli kuwa takwimu hazipatikani kwa wakati au hazina usahihi au hazifanyiwi uchambuzi katika kufanya maamuzi vizuri, " alisema Prof Ndalichako.
Pia mataifa hayo yakiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia, Comoro na Djibouti yamesisitiza haja ya kuimarisha elimu nje ya mfumo rasmi na kwa kuwa kuna mfumo wa elimu wa kujiendeleza wa wakati wote mfano wa uhasibu.
Alisema inafaa kuimarisha mifumo ya elimu nje ya mfumo rasmi bila kusahau elimu ya watu wazima. Pia wametaka watoto wanaolikoroga kwa sababu moja au nyingine na kujikuta hawapati masomo ni vyema wakarudishwa shuleni kuendelea na masomo hivyo ipo haja ya kutengeneza mfumo wa kupata elimu kwa staili hiyo.

"Katika hili tumekubaliana watoto walionje ya shule wanarudi shuleni au wanatengeneza mfumo wa kupata elimu" alisema na kuongeza kuwa pia ilionekana ipo haja ya kuimarisha elimu na ufundi stadi ili elimu hiyo imwezeshe kujiajiri, kujijenga na kuwa na ujuzi kuendana na soko la ajira.
Aidha alisema kwamba  kunatakiwa kuanzishwa kwa kampeni maalumu ya kufichua wasichana wasiopelekwa shule ili kuwepo mwenedelezo wa kila mtu kuingia shule.
WAKATI huo huo serikali ya Uganda imesema itaongeza nguvu katika shule za awali kuimarisha msingi wa utoaji elimu kwa watu wake.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh. Nansubuga Rosemary Seninde wakati akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki kuhusiana na lengo namba 4 la elimu kati ya malengo 17 ya dunia.
Alisema serikali yake imejikita katika kuhakikisha kwamba waganda wanapata elimu nzuri na yenye ushindani ikihakikisha ujuzi na uzoefu katika ujuzi.
Aklisema nchi yake haiwezi kumpa mtu digrii mpaka awe amefanya “intern” na hilo linasaidia sana kujenga uzoefu wa kile alichosomea.
Alisema ingawa kuna tatizo la bajeti, mipango ni muhimu kuhakikisha kwamba taifa linatoka katika changamoto za utoaji wa elimu bora.

Alisema badala ya kusubiri sera, watendaji wanatakiwa kuangalia maeneo ya kuanzia na kisha kutengenezea taratibu za kubadilishwa kwa sera ili iendane na kasi inayotakiwa.
-- Zainul A. Mzige, Managing Director, Mzige Media Limited, www.thebeauty.co.tz +255714940992.