KESI ZA DAWA ZA KULEVYA, ULAWITI ZATAJWA KUSHAMIRI TANGA

January 26, 2023
WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi Jijini Tanga wakiwa mmoja ya mabanda yaliyopo katika eneo la Urithi kunakofanyika maadhimisho ya wiki ya Sheria kimkoa 
Wanafunzi kutoka shule za Msingi Jijini Tanga wakipata elimu kwenye Banda la Jeshi la Zimamoto na 
Uokoaji Tanga 

Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga Lucky Titus Kaguo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za Sekondari na Msingi za Jijini
Tanga waliotembelea Banda lao kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa.
Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga Lucky Titus Kaguo akitoa elimu 
AFISA Uchunguzi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Khadija Luwongo akitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda lao
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Humphrey Paja akipatiwa elimu na Afisa  Uchunguzi wa Takukuru Frank Mapunda   kuhusu namna wanavyofanya shughuli zao kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya rushwa wakati alipotembelea banda lao

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Mkoa wa Tanga (TLS) Tumaini Bakari akitoa elimu kwa wanafunzi wa chuo cha Utalii cha Masai kilichopo Jijini Tanga kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa wanapokumbana na vitendo vya ukatili
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) mkoa wa Tanga Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo


Na Oscar Assenga,TANGA

OFISI ya Taifa Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga imesema kwamba kesi zinazopokelewa kwa wingi mkoani humo ni za biashara ya dawa za kulevya,ukatili wa kijinsia ikiwemo ulawiti na ubakaji.

Hayo yalisemwa leo na Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga Lucky Titus Kaguo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za Sekondari na Msingi za Jijini Tanga waliotembelea Banda lao kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa.

Banda hilo lipo kwenye viwanja vya Urithi Jijini humo ambako kunaendelea maonyesho ya wiki ya Sheria Tanzania huku akieleza mkakati ambao wameupanga kuweza kukabiliana na vitendo hivyo.

Alisema mkakati wa kwanza ni kwamba wanakusudia kuandaa mpango wa kutoa elimu kwa wananchi na wanafunzi juu ya athari ya vitendo hivyo ili kuweza kuibadilisha jamii iondokana navyo.

“Kwa mkoa huu tunapata shida kwenye makosa ya jinai aina mbili madawa ya kulevya na unyanyasaji wa kijinsia ubakaji na ulawiti makosa ambayo yameshamiri sana kwa mkoa wa Tanga “Alisema

Aidha alisema kutokana na uwepo wa hali hiyo wanaandaa mpango wa kuzunguka kwenye shule za msingi na sekondari ikiwemo kukutana na wanafunzi ikiwemo wananchi kuwaeleza iumuhimu wa kutoa taarifa za unyanyasaji unapotokea na wanapoona watu wanauza dawa na wanapata marejesho chanya suala hilo na bado linaendelea kufanyiwa kazi

Hata hivyo alisema kwamba wameshiriki kwenye maonyesho hayo ya wiki ya sheria kutoa elimu kwa wanafunzi na wananchi kwa kutatua matatizo yao na kuwaleta wananchi kuhusu ofisi hizo na kueleza majukumu yao na kutatua matatizo yao.

Alisema pia kuwaeleza ofisi hizo na umuhimu wake katika mashauri wanayopalekwa na wananchi huku wakieleza jitihada za serikali katika kutatua mashauri yake kwa nia ya usuluhihi badala ya njia ya mahakama

Mwisho.