TANZANIA NA IRAN ZIMESAINI MAKUBALIANO YA KUONDOA UTOZAJI KODI MARA MBILI

January 19, 2024

 Na. Scola Malinga, WF, Dar es Salaam


Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Iran zimesani makubaliano ya majadiliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili baada ya kufanyika kwa majadiliano ya kina kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yamesaniwa Jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, kwa upande wa Tanzania na Mkurugenzi wa Sheria na Mikataba ya Kodi wa Irani, Dkt. Hossein Abdollah

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Bw. Mhoja alisema kuwa makubaliano hayo yanahusu misingi ya utozaji kodi ya mapato katika shughuli zinazofanywa na raia, kampuni na taasisi za nchi mojawapo kwenye nchi hizo.

“Makubaliano hayo yanaweka misingi ya ushirikiano katika usimamizi wa kodi kati ya mamlaka za usimamizi wa kodi za nchi hizi mbili kupitia ubadilishanaji wa taarifa za kikodi na kusaidiana kwenye masuala ya kodi”, alisema Bw. Mhoja

Alisema kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo kulianza na majadiliano yaliyofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 18 Januari 2024, jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa yalikuwa ya duru ya tatu kutokana na kushindwa kufikia maridhiano katika duru mbili zilizotangulia.

Bw. Mhoja alieleza kuwa, Tanzania na Iran zina ushirikiano wa kihistoria katika masuala mbalimbli ya kiuchumi hivyo kukamilika kwa majadiliano na kusainiwa kwa makubaliano hayo kutaimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kwa kufungua fursa mpya za ajira, biashara na uwekezaji.

Kufuatia kukamilika kwa majadiliano hayo, inasubiriwa kukamilika kwa taratibu za ndani za kisheria kwa kila nchi kuwezesha Mkataba kuridhiwa na kusainiwa ili kuanza kutekelezwa.

Majadiliano hayo yameshuhudiwa na Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Hossein Alvandi Behine na Mkurugenzi wa Idara ya Nchi za Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima.

Aidha wajumbe wa pande zote mbili wamezipongeza Timu za Wataalam kutoka nchi hizo kwa kuendesha majadiliano hayo kwa weledi na kuzingatia maslahi ya kila nchi na hatimaye kuweza kufikia maridhiano.

Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja na Mkurugenzi wa Sheria na Mikataba ya Kodi wa Irani, Dkt. Hossein Abdollah, wakisaini mkataba wa makubaliano ya majadiliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili baada ya kufanyika kwa majadiliano ya kina kati ya nchi hizo mbili, jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja na Mkurugenzi wa Sheria na Mikataba ya Kodi wa Irani, Dkt. Hossein Abdollah, wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya majadiliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili baada ya kufanyika kwa majadiliano ya kina kati ya nchi hizo mbili, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Nchi za Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima na Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Hossein Alvandi Behine wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya majadiliano ya kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili kati ya nchi hizo mbili, jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja na Mkurugenzi wa Sheria na Mikataba ya Kodi wa Irani, Dkt. Hossein Abdollah, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa pande hizo mbili baada ya kusainiwa makubaliano ya majadiliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili kati ya nchi hizo mbili, jijini Dar es Salaam.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

WIZARA YA FEDHA YAANZA KUTOA ELIMU YA FEDHA KUPITIA SANAA

January 19, 2024

 Na. Peter Haule, WF, Morogoro


Wizara ya Fedha kupitia Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji Elimu ya Uraia (TACCI) wamefanikiwa kuwafikishia elimu ya Fedha baadhi ya wakazi wa Morogoro kwa njia ya Sanaa ikiwa ni mwanzo wa mkakati wa kufikisha elimu hiyo nchi zima ili kutekeleza Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kwaka 2021/2022 hadi 2029/2030.

Akizungumza baada ya elimu hiyo iliyotolewa mtaa wa Malikula Chamwino, mkoani Morogoro, Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, alisema kuwa elimu kwa njia ya Sanaa mkoani Morogoro ni mwanzo wa matukio kama hayo yatakayofanyika nchi nzima hususan maeneo ya vijijini kwa kuwa njia hiyo imeonesha mafanikio makubwa.

“Lengo kubwa ni kufika vijijini ambako kuna uelewa mdogo wa masuala ya elimu ya Fedha na tutajitahidi kuchagua maeneo mahususi ambayo yameainishwa kwenye utafiti wa FISCOPE wa mwaka 2023 ambao unaonesha ujumuishwaji mdogo wa masuala ya fedha unaochangiwa na uelewa mdogo”, alieleza Bw. Kimaro.

Kwa upande wake Mtaalamu wa masuala ya Vikundi vya Kijamii vinavyotoa Huduma Ndogo za Fedha, Bw. Joseph Msumule, alisema kuwa muitikio wa wananchi kujitokeza kwa wingi kusikiliza elimu ya fedha kumechangiwa na Sanaa ya maigizo na ngoma iliyofanywa kwa weledi mkubwa ikilenga elimu ya fedha kwa njia rahisi.

Alisema maigizo hayo yalilenga kuweka akiba, uwekezaji, mifuko ya hifadhi ya jamii, usimamizi binafsi wa masuala ya fedha na namna ya kusajili vikundi ili kuepusha wananchi kudhulumiwa na kukopa maeneo ambayo hayajaainishwa katika Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha.

Kwa upande wao wananchi wa mtaa wa Chamwino Morogoro, wameipongeza Wizara kwa kuwapelekea elimu ya fedha kwa njia ya sanaa kwa kuwa inawarahisishia kuelewa na wapo tayari kuanza kuifanyia kazi kwa kuwashinikiza viongozi wa vikundi vya Kijamii vya Huduma ndogo za Fedha (CMG) kujisajili kwa mujibu wa Sheria.

Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha unalengo la kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2025 asilimia 80 ya wananchi wawe na uelewa wa kutosha wa elimu ya fedha.

Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akielezea umuhimu wa usajili wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha, wakati wa kutoa elimu ya fedha kwa vitendo kwa njia ya sanaa katika Mtaa wa Malikula Chamwino mkoani Morogoro.

Mtaalamu wa masuala ya fedha wa Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyanza, akifafanua kuhusu kuwatumia wahamasishaji wa elimu ya fedha waliosajiliwa ili kuwa na elimu sahihi, wakati wa kutoa elimu ya fedha kwa vitendo kwa njia ya sanaa katika Mtaa wa Malikula Chamwino mkoani Morogoro.

Mtaalamu wa masuala ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Joseph Msumule (katikati) na Debora Mlimba kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), wakitoa zawadi ya mfuko kwa Bw. Sijali Omar Mogela, mkazi wa mtaa wa Malikula Chamwino mkoani Morogoro, baada ya kujibu kwa ufasaha maswali yaliyotokana na elimu ya fedha iliyotolewa na wasanii kutoka TACCI.

Mtaalamu wa masuala ya huduma ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Joseph Msumule (katikati) na Debora Mlimba kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), wakitoa zawadi ya mfuko kwa Bi. Hadija Haji, mkazi wa mtaa wa Malikula Chamwino mkoani Morogoro, baada ya kujibu maswali yaliyotokana na elimu ya fedha iliyotolewa na wasanii kutoka TACCI.

Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), wakitoa elimu ya fedha kwa njia ya sanaa kwa wakazi wa mtaa wa Malikula Chamwino mkoani Morogoro.

Wakazi wa mtaa wa Malikula Chamwino mkoani Morogoro, wakifuatilia igizo kuhusu namna ya kusajili vikundi vya kijamii vya huduma ndogo ya fedha, kutoka kikundi cha Sanaa cha Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) (hawapo pichani)

Kikundi cha Ngomma kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) kikitumbuiza kabla ya kuanza kutoa elimu ya Fedha kwa Wakazi wa mtaa wa Malikula Chamwino mkoani Morogoro.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)

WAZIRI UMMY :MAGONJWA YA ZAMANI IKIWEMO SHINIKIZO LA DAMU YAONGEZEKA KWA VIJANA

January 19, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


MAGONJWA maarufu ya zamani kwa wazee sasa yanaongezeka kwa vijana ambapo hivi karibuni, utafiti umeonyesha ongezeko la uwiano wa vijana wenye shinikizo la damu lililoongezeka kutoka 0.2% hadi 25.1% katika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti ongezeko za aina 5 za kisukari aina ya kwanza miongoni mwa watoto na vijana kati ya mwaka 2011 na 2021.

Ameyasema hayo leo Januari 19, 2024 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Amesema kuwa wakati maendeleo makubwa yamepatikana, dhahiri katika kupunguza matokeo duni ya lishe kama vile kudumaa kutoka 34.7% katika 2014 hadi 31.8% mwaka 2018, anemia kati ya wanawake wa umri wa uzazi imepungua kutoka 44.8% katika 2015 hadi 28.8% kwa mwaka 2018 pamoja na kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU, hata hivyo baadhi ya maeneo ya vijana kama vile afya ya akili bado yanahitaji juhudi zaidi.

Aidha amesema kuwa tunahitaji ushahidi zaidi wa kisayansi ambao unaweza kuchangia kuimarisha utendaji wa sekta yetu ya afya na ushirikiano ulioonyeshwa hapa kwamba kuhusisha wanasayansi mbalimbali na wataalam wa afya ya umma wa ndani na nje ya Tanzania ambao ni mfano wa kuigwa.

"Nimefurahi kuona Taasisi zetu za Serikali kama Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Jamii Muhimbili, Chuo Kikuu cha Dodoma, Halmashauri mbalimbali za Mikoa na Wilaya, Taasisi ya Afya ya Ifakara, Taasisi ya MDH pamoja na ZAPHA+ kutoka Zanzibar zikiwa sehemu ya kazi hii". Ameeleza Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesisitiza juu ya umuhimu wa kuendeleza ajenda ya afya miongoni mwa vijana ili kuboresha afya na ustawi wao kwa ujumla, kuinua kizazi cha afya na watu wenye kinga kali, uwezo wa kufikiri kwa umakini na wenye ubora kitaaluma ambayo itachangia maendeleo ya taifa letu.

"Ninatoa wito kwa kila mmoja wetu, watunga sera, watafiti, watoa huduma za afya, wazazi, wanajamii na vijana kuibebaa ajenda hii. Mafanikio haya hayawezi kupatikana bila kushirikiana na washirika wa ndani na wa kimataifa na wafadhili". Amesema

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Africa Academy for Public Health (AAPH) Bi.Mary Sando amesema kuwa jukumu muhimu katika kuitisha Mtandao wa ARISE unaojumuisha taasisi wanachama 21 kutoka nchi tisa (Botswana, Burkina Faso, Ethiopia, Ghana, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania na Uganda) za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo umekuwepo kwa miaka mingi kutokana na ushirikiano wa ndani na kimataifa na umesaidia kupitisha ruzuku,maombi, na usambazaji na tafsiri ya matokeo ya kisayansi yenye athari katika programu zinazoweza kutekelezeka.

Aidha amesema azma yao katika mkutano huo ni kusudi endelevu la kuziba pengo la utafiti kwa kupitia njia Shirikishi ya mafunzo,kwa lengo la kujenga uwezo na tafsiri ya maarifa.

"AAPH imeendelea kudumisha mashirikiano na vyombo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa Kushirikiana na Wizara ya Afya,Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Taasisi za ndani na nje ya nchi kama vile MUHAS, UDOM na HIGH, pamoja na shirika letu dada la MDH, ambapo tunawasaidia katika shughuli za utafiti na kuhakikisha ubora wa data ili kufahamisha ufanyaji maamuzi"Bi.Mary Sando Amesema.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akizungumza katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhiwa tuzo maalumu ya kutambua mchango anaoutoa kwenye sekta ya afya kwa kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Africa Academy for Public Health (AAPH) Bi.Mary Sando katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza jambo na mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, Bw. Mark Elliott katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

 Mtendaji wa Taasisi ya Africa Academy for Public Health (AAPH) Bi.Mary Sando akizungumza katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle akizungumza katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.







Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa katika Mkutano wa 5 wa Kisayansi wa “ARISE Network” wenye lengo la kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kwa vitendo na Sera zinazoweza kutekelezwa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao umefanyika leo Januari 19,2024 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

CRDB YAPANDA MITI 500 SIMANJIRO

January 19, 2024



Na Mwandishi wetu, Simanjiro



BENKI ya CRDB katika kuadhimisha wiki ya jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania, imepanda miti 500 Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwa lengo la kutunza mazingira na kurejesha uoto wa asili.


Mwenyekiti wa jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania, sheikh Alhad Mussa Salum amefanya uzinduzi huo wa kitaifa kwa kupanda miti kwenye zahanati ya kijiji cha Nakweni, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara.


Sheikh Alhad ambaye pia ni balozi wa kampeni ya mazingira kwenye ofisi ya Makamu wa Rais amesema uzinduzi huo ni wa kitaifa na kilele chake kitafanyika Machi 6 mwaka 2024 jijini Mbeya.


Sheikh Alhad amewapongeza CRDB kwa kutoa miche hiyo 500 ambayo itakuwa imetunza mazingira ya eneo hilo la Nakweni na kuwanufaisha watu wanaozunguka eneo hilo.


Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera, amewataka wakazi wa kijiji cha Nakweni kuitunza miti hiyo kwa kutoachia mifugo kuzagaa na kuiharibu.


"Hili ni tukio la kitaifa kwa kukusanya viongozi wakubwa kuja kupanda miti hivyo tujitahidi kuitunza miti hii na kuwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadaye, kwa kunufaika na kivuli na matunda," amesema DC Serera.


Meneja wa CRDB, kanda ya kaskazini, Cosmas Sadat amesema wameungana na jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania kwa kuadhimisha siku hiyo ndiyo sabuni wakatoa miche 500 ili kuwaunga mkono.


"Benki ya CRDB ni mdau mkubwa wa maendeleo mbalimbali nchini katika sekta ya elimu, afya, mazingira na mengine, ndiyo maana tukachangia miche hiyo 500 ya matunda na vivuli ambayo itakuwa manufaa ya wakazi wa Nakweni kata ya Shambarai," amesema Sadat.


Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, amewashukuru jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania kwa kuadhimisha siku hiyo wilayani Simanjiro kwani wamewapa heshima kubwa mno.


"Tunawashukuru mno CRDB kwa kutoa miti hiyo 500 nasi tunaahidi kuitunza na kuongeza miche mingine kwa lengo la kuwashukuru na kuwaunga mkono kwenye jambo hili la kitaifa," amesema Ole Sendeka.


Diwani wa kata ya Shambarai, Julius Lendauwo Mamasita, amesema upandaji wa miti hiyo kwenye zahanati hiyo utawanufaisha jamii ya eneo hilo hasa wanawake wajawazito kwani watapata eneo zuri la kupumzikia.


"Jamii ilikuwa inatembea umbali mrefu wa kilomita 35 hadi mji mdogo wa Mirerani kufuata huduma za afya, tunawashukuru CRDB kwa kutoa miti hiyo ambayo itakuwa faida kwetu miaka ijayo," amesema Mamasita.




NAPE AITAKA BODI PDPC KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA MUJIBU WA SHERIA NA SI MATAKWA AU UTASHI WA WATU.

January 19, 2024


Na Janeth Raphael MichuziTv- Dodoma.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye ameitaka Bodi ya Tume ya PDPC kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa na si kwa Matakwa na Utashi wa watu fulani.

Waziri Nape ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma katika Uzinduzi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)

Na kuongeza kuwa anatamani kuona time hii Inakuwa huru na kutoingiliwa kwa namna yeyote kwani Sheri na miongozo ipo wazi.

"Natamani tume muhakikishe, tume inaanza kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria,kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa. Kama kuna tume tunataka iwe huru kutekeleza majukumu yake hii tume nataka iwe huru mlinde hilo,tusiingilie na nyie msikubali kuingiliwa mlindwe na Sheria tumezitunga,ziko kanuni kama kuna shida mahali ni Bora turekebishe Sheria na kanuni,lakini msiendeshwe kwa Matakwa na Utashi wa watu tuendeshe kwa mujibu wa sheria".

Aidha Waziri Nape amewataka viongozi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuilinda Imani ya Raisi juu yao kwa kuwekwa katika nafasi kwa kutekeleza majukumu yao kwa tija,ufanisi na uzalendo na asitokee mtu yeyote kuupuuza Imani hiyo

"Mmepewa Kazi ya kutujengea msingi ambao wengi watakapokuja watajenga katika msingi ambao mmeujenga nyie,kwahiyo jukumu lenu ni kubwa Raisi amekuwa na Imani na nyie na sisi tuna Imani na nyie pia, kwahiyo Raisi kuwa na Imani na nyie maana yake kwa niaba ya Watanzania Raisi amewaamini, hii Imani kubwa ambayo kama viongozi wa tume mnapaswa kulinda na kusimamia majikumu ya Tume kwa tija, ufanisi na uzalendo kama nilivyosema Raisi amefanya kwa niaba ya Watanzania kuwaamini nyie, hivyo asitokee mtu akaipuuza Imani hii"

Pia amaelezea namna Tume hii ilivyo kuwa na nafasi kubwa ya kulinda Heshima,Haki na Utu wa mtu kwa taarifa zao zinavyotumika katika njia inayozingatia Haki.

"Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Ina jukumu kubwa la kulinda Heshima, Haki na Utu wa watu kwa kuhakikisha taarifa zao binafsi zinatumika kwa njia inayozingatia Haki, Heshima na Utu wao,tunataka taarifa za watu katika Nchi yetu, Watanzania,Wageni na wote watakaokuja katika Nchi hii wawe na hakika kuwa taarifa zinatumika katika njia inayozingatia Haki Heshima na Utu wa mtu,Tunatamani Nchi hii Iheshimike Duniani kwa kuheshimu Haki ya taarifa za watu, Heshima ya taarifa za watu ili watu wakimbilie Taifa letu na kuona ni sehemu sahihi".

Pia Waziri amesema si vibaya kwa Bodi kujifunza kwa Nchi ambazo zilianza na mfumo huu ili kuona wapi zilipofanikiwa na penye mapungufu tuone namna ya kufanya maboresho.

" Wapo waliotangulia hivyo mnaweza kujifunza kutoka kwao wamefanyaje vizuri,wamekosea wapi sisi tuone namna tunavyoweza kuboresha. Ni matumaini yangu baada ya muda mfupi watu waje Tanzania kujifunza namna Bora ya kulinda Utu na Heshima za watu"

Naye Katibu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla ametumia nafasi hii kutoa Rai kwa Bodi hii kuhakikisha wanatekeleza majuku ya msingi kama yalivyoainishwa katika Sheria na kanuni zake.

"Mheshimiwa Waziri kwa kuwa kikao hiki mahsusi kwako kwa kutoa maelekezo,nitumie nafasi hii kutoa Rai kwa Bodi kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya msingi kama yalivyoainishwa kwenye sheria,kanuni na miongozo uliotolewa na Msajili wa Hazina pamoja na ahadi zako ulizotoa kwenye Hotuba ya Bunge ya mwaka 2023/2024".

Awali akitoa taarifa fupi ya PDPC,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hii ACP Emmanuel Mkilia amesema Bodi imepata matokeo kwa asilimia 90 ndani ya siku 100 kwa Mambo iliyokuwa imejiwekea ikiwemo kujenga uwezo wa Taasisi na pia kujenga uwezo kwa Watumishi wao.

"Matokea yetu ambayo tumeyafanya katika hizi siku 100 tulifanikiwa kwa kiwango cha asilimia 90 kwa Mambo Yale ambayo tulijipangia kufanya huku tukiwa tunajipima,kujenga uwezo wa Taasisi na kujenga uwezo wa Staff pia".

Tume ilianza kutekeleza majukumu yake Rasmi tarehe 1 May 2023 ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi namba 11 ya mwaka 2022.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizindua Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Adadi Mohammed na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mohammed Khamis Abdulla.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizindua Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Adadi Mohammed na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mohammed Khamis Abdulla.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma leo Januari 19, 2024.

SHIRIKA LA GIZ LATOA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA HOSPITALI YA KOROGWE MJI

January 19, 2024

Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe kulia akikabidhi vifaa vya Tehama wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Mark Tanda akifuatiwa na Mratibu wa GIZ Apolinary Primus 


Sehemu ya Vifaa hivyo











Na Oscar Assenga, KOROGWE.

Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) limetoa msaada wa vifaa vya tehama katika Hospitali ya Mji wa Korogwe ya Manundu na kuweka miundombinu ya Intaneti,Ufugaji wa Mfumo wa kieletroniki ambao ni mfumo wa taarifa za usimamizi wa Hospitali za Serikali ya Tanzania (GoTHOMIS) pamoja na kufanya mafunzo endelevu kwa watumishi.

 Ambapo hadi sasa zaidi ya wafanyakazi 150 katika hospitali ya Korogwe tayari wamefundishwa jinsi ya kutumia mfumo wa GoTHOMIS ambapo uwekezaji wake wa awali umegharimu Milioni 200,000,000 uliofanywa na GIZ hadi sasa na msaada zaidi ya kuifundi umepangwa ili kuhakikisha lengo linafikiwa ifikapo mwaka 2025.

 Akizungumza wvakati wa makabidhiano rasmi ya vifaa vya Tehama, Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe amesema kuwa mpango huo unalenga kubadilisha taratibu za kiutawala na kiafya katika hospitali hii kwa kuondoa matumizi ya kumbukumbu za karatasi, kuboresha uhifadhi na upatikanaji wa takwimu za wagonjwa, kuongeza hospitali ufanisi na kupunguza makosa katika takwimu.

Alisema kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani ambao ni wafadhili wao lakini pia wameshirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya pamoja na  Ofisi ya Rais Tamisemi wamekuwa wadau kwa mkoa wa Tanga kwa miaka tisa kwa awamu ya miaka mitatu mitatu.

Msoffe alisema kuwa mara nying wamekuwa kwenye awamu uliyoanza mwaka 2023 na itakwenda mpaka 2026 kwa mkoa wa Tanga na wana jumla ya Hospoitali 18 wanazozisaidia lakini katika eneo la Tehama pamoja na kwamba huyko nyumba wamefanya kazi na Hospitali nne kwenye eneo hilo lakioni watawasapoto kuweka miunbdombi na kuwafanya mafunzo watumishi waweze kuutumia.

 “Kwanini tupo Korogwe kuhakikisha sisi kama wadau na Serikali ikiwemo Hospitali wanaweza kufanya juhudi za kipekee kuona ni gharama gani zinahitajika ili kuitoa Hospitali ya wilaya kutoka kwenye matumiz ya mifumo ya katarasi na kwenda katika asilimia 100 ya matumizi ya Kiletroniki”Alisema

 Alisema katika mafanikio yatakayopatikana katika hospitali ya Korogwe, yatatumiwa na serikali ya Tanzania kuongeza mageuzi haya ya kidijitali kwa hospitali nyingine chini Tanzania.

“GIZ inaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya kisera na kutoa msaada wa kitaalamu katika kuboresha huduma za afya chini Tanzania”Alisema.

Alisema maboresho hayo yanayoendelea katika mifumo ya kidigitali na hasa mfumo wa GOTHOMIS ambao ni moja ya mifano tosha ya dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kusaidia vituo vya afya kuboresha huduma za afya kupitia teknolojia ya kidijitali.

 Hatua hiyo ni moja ya mambo ya msingi ya kuongeza ufanisi Hospitali ya Mji wa Korogwe inatangaza kwa fahari uamuzi wake wa kuachana na mifumo inayotumia makaratasi kabisa. Hospitali hiyo inakumbatia manufaa ya teknolojia katika kuimarisha huduma za afya na kurahisisha shughuli mbali mbali.

 Uamuzi huo umekuja baada ya ongozi na wafanyakazi kutambua changamoto zinazoendelea kukabili mfumo wetu wa huduma za afya zikiwemo uhaba wa watumishi, kazi kubwa inayowakabili watumishi kwa kujaza karatasi nyingi, takwim duni lakini pia muda mrefu ambao wagonjwa hukaa hospitalini kupata huduma.

Kwa hiyo hospitali ya Korogwe imejitolea kutumia maendeleo ya kidijitali ili kutoa huduma ya hali ya juu kwa wateja wake. Kuachana na matumizi ya makaratasi na kuharnia mifumo ya kidigitali ni tatua muhim katika kufikia lengo hili.

 Deutsche Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH kupitia mpango wake wa afya wa Kuboresha Huduma ya Afya Tanzania (ICP) ni mshirika wa muda mrefu na wamekuwa wakisaidia mkoa wa Tanga na haswa hospitali ya Korogwe kutekeleza afua za afya za kidijitali ambazo zinalenga kuongeza fanisi na ubora wa huduma za afya.

Awali akizungumza Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mji wa Korogwe Dkt Heri Kilwale alisema kuwa kubadilika kutoka matumizi ya karatasi na kutumia mifumo ya kidijitali itawasaidia watoa huduma za afya kuweza kupata taarifa za mgonjwa kwa wakati na salama.

Alisema pia kutapunguza muda ambao wafanyakazi hutumia kufanya kazi za kujaza makaratasi mengi na hivyo wataalamu wa afya wataelekeza zaidi muda katika kutoa huduma kwa wagonjwa na hivyo kupelekea kuongezeka kwa ubora wa huduma zinazotolewa.

Korogwe ni miongoni mwa hospitali chache ambazo zimeanza kutumia toleo jipya la GoTHOMIS na kva msaada wa mara kwa mara kutoka kwa serikali, ongozi wa hospitali na washirika wa maendeleo, inatarajiwa kuwa hospitali ya Korogwe itafanikiwa katika dhamira yake ya mabadiliko kutoka matumizi ya karatasi Kwenda katika mifumo ya huduma za kidijitali na kwamba. Serikali itapanua msaada huo kwa hospitali zingine baada ya hapo.

RAIS SAMIA ATETA NA VIONGOZI WA CCM UNGUJA

RAIS SAMIA ATETA NA VIONGOZI WA CCM UNGUJA

January 19, 2024







Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amezungumza na viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa mikoa mitatu ya Unguja kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara yake kichama.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja Januari 18, 2024.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa mikoa mitatu ya Unguja kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara yake kichama uliofanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 18 Januari, 2024.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mikoa mitatu ya Unguja wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani), wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake kichama uliofanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 18 Januari, 2024.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mikoa mitatu ya Unguja wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani), wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake kichama uliofanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 18 Januari, 2024.

WATEKAJI WATATU WA WATOTO GEITA WADAI MILIONI 4 KUWAACHIA

January 19, 2024


 Watu watatu wanashikiriwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma za kuteka watoto maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa lengo la kujipatia kipato.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP .Safia Jongo amesema kumezuka wimbi kubwa la utekaji watoto Mkoani humo ambapo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao huku chanzo kikitajwa ni kutaka kujipatia Fedha.

“Lakini pia limeibuka wimbi la wizi wa watoto Geita vyanzo ikiwa ni kipato tuna tukio ambalo limetokea mbogwe Mtoto wa Miaka 4 Ametekwa waliomteka wakadai Milioni 4 lakini ndani ya siku tatu Jeshi la polisi tumepambana na tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu ambao walishirikiana kumteka huyo mtoto, ” ACP. Jongo.

Aidha ACP. Jongo amewatahadharisha wazazi na walezi kuhakikisha wanawalea watoto na kuwajengea mazingira Mazuri ya kimalezi ili kukabiliana na wimbi hilo ambalo limeibuka ndani ya Mkoa wa Geita huku akitoa tahadhali na kuwaonya waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi kuwa washirika wakubwa wa Matukio hayo.

ACP. Jongo amesema Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wananchi katika kupunguza wimbi la Mauwaji ndani ya Mkoa wa Geita ambalo limekuwa likichangiwa na Imani za Kishirikina .


Chanzo :Milladayo