WAZIRI UMMY MGENI RASMI MATEMBEZI YA KILOMITA 5 JIJINI TANGA

February 28, 2023




Na Mwandishi Wetu,Tanga


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  mazoezi ya viungo na matembezi ya umbali wa kilomita tano (5km) yenye kauli mbiu " Tembea na JKCI - Linda Afya ya Moyo Wako" yatafanyika Machi 11 mwaka huu yatakayoanzia kwenye viwanja vya NIMR Bombo Hospitali.


Matembezi hayo yameandaliwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya JKCI 


Akizungumza kuhusu matembezi hayo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Zakaria alisema maandalizi yamekamilika.


Dkt Naima alisema  matembezi hayo yataanza saa 12:30 asubuhi hadi saa 2:30 asubuhi yatakayokwenda sambamba na ufungaji wa kambi upimaji.


Alisema matembezi hayo yataanzia kwenye viwanja vya NIMR Bombo Hospitali kupitia Mkonge Hotel, Raskazone Polisi hadi Nyinda Classic kuelekea Ukuta wa Mbolea (GBP), Masai Utalii College, Lulu Image,Tanga International School, Splended, Tanesco, Toyota Mataa na kumalizikia Bombo Hospitali Viwanja vya Mapokezi.


Hata hivyo Dkt Naima alivitaka vilabu vya mazoezi viweze kushiriki nao pamoja katika ufanyaji wa mazoezi ili kulinda Afya ya Moyo sambamba na kupunguza athari zinazotokana na  magonjwa yasiyo ambukiza kwa jamii.


Mwisho


SHULE YA SEKONDARI COASTAL YA JIJINI TANGA KUANZA KUNUFAIKA NA MKONGE

February 28, 2023

 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akizungumza wakati wa maafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga yaliyofanyika kwenye Hotel ya CBA Jijini Tanga

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George



Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George




Na Oscar Assenga,Tanga.

Shule ya Sekondari Coastal ya jijini Tanga,itaanza kunufaika na uwekezaji wa sekta ya mkonge baada ya Bodi ya Mkonge Tanzani (TSB) kuahidi kuiingiza katika majaribio ya klabu za vijana watakaoendelezwa.

Pia shule hiyo imeahidiwa kupewa ekari 100 kwa ajili ya kilimo cha mkonge ikiwa ni sehemu ya kuiongezea kipato .

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mko n ge nchini,Saad Kambona alitoa ahadi hiyo wakati wa mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita walioanza mtihani ya kitaifa.

Alisema bodi hiyo imeandaa programu maalumu itakayowawezesha vijana kujiinua kiuchumi kuptia kilimo cha mkonge na bidhaa zitoakanazo na zao hilo.

Alisema kama inavyofahamika Bodi ya Mkonge ni taasisi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ni kama imekufa sasa imeshafungua rasmi ofisi katika jengo lake na kuwezesha kuinua sekta ya mkonge kwa ujumla wake.

“Lakini tunategemea tunapokwenda mbele vijana wengi sana kutoka kwenye shule za Tanga ndiyo wahusike kwenye mpango mzima wa kuleta mapinduzi kwenye zao la mkonge kwani sasa hivi tunapozungumzia mkonge tunazungumzia bidhaa moja tu ya nyuzi za mkonge zitengeneze vikapu, makapeti, magunia, kamba na bidhaa nyingine zitokanazo na zao hilo ,lakini kuna bidhaa nyingti zinahitajika kama sukari,mbolea mvinyo na hata vyakula vya kunenepesha mifugo” alisema Kambona

Mkuu wa shule hiyo,Joseph Gaspar alisema ilianza rasmi mwaka 2000 na kwamba kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikitoa ufaulu wa daraja la kwanza A na pili kwa wanafunzi wote wa kidato cha sita wote katik a mitihani ya kitaifa ya mchepuo wa sayansi.

“Hadi sasa shule hii imetimiza miaka 22 lakini kwa kipindi cha miaka miatatu mfululizo i mekuwa ikitoa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza na la pili katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha sita...tunatarajia mitihani hii ufaulu utakuwa wajuu zaidi”alisema Gasper.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George alisema kuwa miongoni mwa mambo yanayotiliwa mkazo ni masomo ya sayansi wakiamini kuwa jukumu lao ni kupata wataalamu watakaoiendeleza nchi katika sekta ya uhandisi,udaktari na utafiti mbalimbali ikiwamo sekta ya kilimo na ufugaji.