SABA WANUSUFIKA KIFO WAWILI WAJERUHIWA BAADA YA CARRY WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA

October 08, 2017
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba akikagua gari hiyo jioni hii
Watu saba wamenusufika kifo huku wawili  wakijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo baada ya gari ndogo waliokuwa wamepanda aina ya Carry kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ya Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda walieleza kuwa gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya reli wakati lijaribu kusimama ndipo lilipofeli breki na kuiparamia treni hiyo.

Ajali hiyo ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini  Tanga iliacha mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa ikitokea eneo la kwaminchi.

Akithibitisha kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati ikipita katika eneo hilo.

Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo kuwa ni T.343 DCQ  iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuingia  kwenye stesheni ya Tanga.

Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo walifikishwa  kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa gari hilo alitokomea kusikojulikana.

Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo,Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha reli wanakaa mita 50.

Awali akizungumza mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo,Said Kiruwasha alisema wakati wakiwa kwenye eneo hilo wakailiona gari hilo moshi likitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ndipo gari hilo lilipokuwa likipita ndipo ilipofeli breki baada ya kusikia honi ya treni hiyo.

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA MAMA HAPPYFANIA KOMBA KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM LE

October 08, 2017

 Marehemu Happyfania Komba enzi za uhai wake. Happyfania Komba alifariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa usingizini na mazishi yake yatafanyika kesho Tunduru mkoani Ruvuma.

NHIF YATOA HUDUMA ZA UPIMAJI KWENYE BONANZA LA MICHEZO JIJINI TANGA LEO

October 08, 2017
 Afisa Mdhibiti wa Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Dkt Lawi Kupaza akiangalia taarifa za moja ya wakazi wa Jiji la Tanga ambao walijitokeza kupima uzito,sukari na presha wakati wa bonanza la michezo ambalo limefanyika leo kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
 Daktari wa NHIF kushoto akimpima presha Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati wa bonanza la michezo
Afisa Mdhibiti Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dkt Lawi Kupaza akichukua maelezo ya Ofisa wa Polisi kutoka Ofisi ya RCO,Saidi Mwagara wakati wa bonanza hilo
Afisa Madai wa NHIF mkoani Tanga,Marry Daniel katikati aliyevaa tisheti ya njano akifuatilia taarifa wakati wa wananchi walipojitokeza kwenye banda lao kwenye bonanza la michezo ambalo lilifanyika viwanja wa shule ya Sekondari Popatlaly kupima afya 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akiwa kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kuangalia zoezi la upimaji wa afya kwa wanamichezo 150 waliweza kupima afya ambapo kati yao

waliokuwa na uzito mkubwa 65,waliokutwa na sukari juu wanne,waliokuwa na Presse sita na wasiokuwa na matatizo 75
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akiwaongoza askari wa Jeshi hilo kuwavuta kamba Bandari Tanga wakati wa Bonanza hilo leo
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akiwaongoza askari wa Jeshi hilo kuwavuta kamba Bandari Tanga wakati wa Bonanza hilo leo

PSPF YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE KWENYE KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

October 08, 2017
 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwatumikia wateja, (wanachama) wa Mfuko.
Bw. Mayingu ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku tuzo na zawadi wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyoanza Oktoba 2 na kumalizika Oktoba 6, 2017.
Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwanzo wa wiki ya mwezi Oktoba kila mwaka, hulenga kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao wa kuwahudumia wateja kwa kuzingatia weledi wa utoaji huduma bora kwa mteja.
"Wakati nikiwa Iringa nimepokea pongezi nyingi za Wanachama wetu, wakiwapongeza nyinyi wafanyakazi kwa kuwahudumia vizuri, hongereni sana na niwaombe muendele kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwani huo ndio wajibu wetu." Alisema Bw. Mayingu katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 6, 2017 kwenye ukumbi wa makao makuu ya PSPF, Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. 
Bw. Mayingu aliwapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo kote nchini, kwa kazi nzuri na kuwaeleza kuwa kitendo cha wafanyakazi na maafisa wa Mfuko huo kutoka maofisini na kuwafata wateja, (wanachama) majumbani kwao ili kuzungumza nao na kuwahudumia kimesifiwa sana.
"Kaimu Mkurugenzi Mkuu, alifuatana na baadhi yenu kwenda kule Kipunguni B. na kukutana na mwanachama wetu, Bw. Kassim Mafanya, ambaye alikipongeza kitedo kile na kusema hakutegemea maishani mwake yeye kama mstaafu angetembelewa nyumbani kwake na PSPF, hili ni jambo jema." Alibainisha Bw. Mayingu.
Wafanyakazi waliopata tuzo ni Elizabeth Shayo, kutoka kitengo cha Huduma Kwa Wateja, Makao Makuu, ambaye kupitia teknolojia, (mifumo), ni wateja wenyewe ndio waliompendekeza kutokana na maoni yaliyopokelewa lakini idadi ya watu aliowahudumia.
Mwingine ni Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), ambaye naye alitunukiwa tuzo na kupewa zawadi kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wateja bila kuchoka.
Tuzo hizo pia zimekwenda kwa walezi wa mikoa wa PSPF, kampuni mshirika ya Ardhi Plan Limited na pia makampuni washirika yaliyoshirikiana na PSPF kwenye wiki ya huduma kwa wateja, ambayo ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mabenki ya CRDB, NMB, TPB na Mwalimu Commercial Bank (MCB).
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.
 Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Elizabeth Shayo.
  Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Bi.Valley Malinga
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akiwa na maafisa waandamizi wa Mfuko huo.
 Baadhi ya wafanyakzi wa PSPF
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017


Meneja wa Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na AfIsa Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. January Buretta, wakihakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwenye hafla hiyo

Baadhi ya wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo

Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.


Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.


Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.

Dk.Hamisi Kigwangalla: “Tuzidi kuombeana dua tu, sintowaangusha Watanzania”

October 08, 2017
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka watanzania kuendelea kumuombea dua pamoja na ushirikiano katika majukumu yake mpya.
“Nimepokea salamu nyingi za pongezi na shukrani kwa Mungu aliye juu. Sintoweza kumjibu kila mtu, uungwana ni kutambua pongezi zenu na dua tele mlizotuombea, nawashukuru sana ndugu zangu. Tuzidi kuombeana dua tu.
Tuna kazi ngumu ya kukimbia kukidhi matarajio ya kiongozi wetu Mkuu aliyetuamini na matarajio ya wananchi wenzetu. Binafsi nawaahidi nyote kuwa sintowaangusha! Ahsanteni sana ndugu zangu, natarajia ushirikiano wenu wa kila hali.” Alieleza Dk. Hamisi Kigwangalla.
Awali taarifa za kuteuliwa kwake katika wizara nyingine, alizipata kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kwa njia ya simu  wakati akiwa kwenye majukumu ya  ziara ya kuboresha mfumo wa afya, akiwa Wilayani Nachingwea, Kata ya Kilimalondo umbali wa zaidi ya kilometa 100, kutoka Makao makuu ya Wilaya hiyo ya Nachingwea, aliweza kusitisha ziara yake hiyo ambayo alitakiwa kuendelea katika Vijiji na Wilaya nyingine ya Liwale.

 
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi. 
Dk.Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa kituo cha Afya Kilimalondo wakati wa ziara hiyo
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vipya vya chumba cha upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi. Kituo hicho kilifungiwa kisifanye upasuaje mpaka kitakapokidhi vigezo, hata hivyo Dk.Kigwangalla alitoa miezi mitatu kiwe kimefanyiwa marekebisho na kianze kazi mara moja
Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi akimpatia taarifa Dk. Kigwangalla juu ya uteuzi wake mpya hivyo kusitisha shughuli zote zilizokuwa zimepangwa kuendelea katika wilaya hiyo.
 
 Dk.Kigwangalla akiagana na viongozi wa Wilaya ya Nachingwea  baada ya kusimamisha ziara yake kufuatia uteuzi mpya. Baada ya kupata taarifa hiyo kila kitu ilibidi kisimame hapo hapo. Namba za NW AMJW ilibidi ziondolewe na safari ya kutoka huko ianze.

MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA KUUTANGAZA UTALII WA TZ ZIARA YA THAILAND

October 08, 2017
 Mratibu wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Resorce Afrika Limited, Idrissa Songoro akizungumza kuhusu maandalizi ya ziara ya mafunzo ya Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA),nchi Thailand inayotarajia kuanza katilati ya mwezi ujao Novemba mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Adam Ngamange na Mwenyeikiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kisui . Kisui.UJUMBE wa Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) unaokwenda ziara ya mafunzo nchini Thailand, umejiandaa pia  kwenda kuutangaza utalii wa Tanzania.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Richard Mwaikenda

Akizungumza mjini Dar es Salaam wakati wa kikao cha maandalizi na baadhi ya Wana Mkikita watakaokwenda Thailand, Mtaribu wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Resorce Afrika Limited, Idrissa Songoro amesema kuwa maandalizi ya ziara hiyo kwa upande wa Thailand kwa asilimia kubwa yako tayari.

Amesema kuwa ziara hiyo ya wiki moja Wanamkikita watanufaika kwa mambo mengi, ambapo licha ya kutangaza vivutia mbalimbali vya utalii pia wataonesha utamaduni wa mapishi ya kila aina ya vyakula vya asili vya kitanzania.

Amesema Wanamkikita ambao miongoni mwao ni Wakulima, Wafanyabiashara na Wajasiriamali watapata wasaa wa kubadilishana mawazo na wenzao wa Thailand kwa lengo la kukuza ushirikiano katika masuala ya kibiashara,kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa.

Songoro amewaasa Wanamkikita kufanya maandalizi  ya uhakika ili wakienda Thailand wanufaike na ziara hiyo na kuwa na mrejesho mzuri watakaporejea nyumbani.

"Kitabia Wathailand wanafanana na Watanzania, kwani ni wakalimu, wapole, waungwana lakini pia ni wachapakazi na wako makini sana katika kila jambo wanalolifanya,"amesema Songoro.

Amesema kuwa Ujumbe huo utapata pia fursa ya kutembelea eneo la viwanda, mashamba ya wakulima pamoja na eneo la utafiti wa kilimo la Chiang Mai na Mji Mkuu wa Bangkok.

"Wathailand wana elimu mkubwa katika nyanja ya uhifadhi wa vyakula na kuviongezea thamani pamoja na kutangaza logo za kibiashara,. Pia wana mbegu za mazao mbalimbali zinazotoa mazao mengi kwa hekali, kwa mfano unaweza kuzalisha kabeji tani 25 kwa heka moja,"amesema Songoro.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kisui S. Kisui  aliwaasa Wanamkikita kuichangamkia ziara hiyo kwani watakaokwenda watanufaika kwa kupata fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo masuala ya kilimo cha kisasa na biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Adam Ngamange alielezea jinsi Mkikita ilivyopanga kuwaandaa wanajachama watakao kwenda huko kwa kuwapiga msasa kwa kutumia vikao na semina mbalimbali ili wawe na uelewa kwa kujua mambo mbalimbali watakayokwenda kufanya katika ziara hiyo muhimu.

Aliimpongeza Songoro kwa jitihada zake kwa kujitolea kwa moyo mkunjufu kuratibu ziara hiyo itakayokuwa na makubwa kwa Mkikita, Wanachama na Tanzania kwa ujumla.



 Songoro na viongozi wa Mkikita wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanamkikita wanaotarajia kwenda Thailand kwa ziara ya wiki moja.
 Dk. Kisui akielezea jinsi Mkikita ulivyojipanga kwa ziara hiyo, itakayowanufaisha wanachama kwa kukutana ana kwa anakwa mazungmzo  na wafanyabiashara na wakulima wa Thailand pamoja na kuingia nao mikataba mbalimbali. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Ngamange akifafanua jambo kwa wajumbe
 Ngamange akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mkikita wakati wa kikao hicho 

RAIS MAGUFULI AMEKATA KIU

October 08, 2017


Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kufanya mabadiliko madogo mapya kwenye Baraza jipya la Mawaziri alilolitanga Jumamosi Oktoba 7, 2017 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika Baraza hilo jipya limeongezeka Wizara mbili mpya ambazo ni Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetenganishwa na kuwa Wizara ya Kilimo na  Wizara ya Mifugo na Uvuvi; na Wizara ya Nishati na Madini imetenganishwa na kuwa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini kufanya Wizara kuwa 21 toka 19 za awali.

Pia kuna ongezeko la Mawaziri 2 na Manaibu Waziri 5. Baadhi ya wapya walioongezeka ni Mhe. Abdallah Ulega, Mhe. Kangi Lugola, Mhe. Faustine Ndugulile, Mhe. Mary Mwanjelwa, Mhe. Juliana Shonza, Mhe. Kakunda n.k

Mabadiliko haya mapya madogo yamekuja wakati ambao Wizara mbalimbali zikiwa hazina Mawaziri na Manaibu Waziri na hivyo kuja kuzipa mapengo yaliyokuwa yakisababisha kusua sua kiutendaji. Baadhi ya Wizara hizo ni Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Nishati na Madini.

Ukamilifu huu uliotokana na mabadiliko haya madogo umepeleka injini ya kuongoza nchi kukamilika na kuwa mpya na Watanzania tunatarajia maboresho makubwa ya utendaji kazi ya utekelezaji ilani ya uchaguzi kwa kasi ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo nchini.

Naendelea kumpongeza Rais Magufuli kwa kuteua Baraza lililokata kiu ya uteuzi kwa kuhakikisha kila kanda inapata uwakilishi, kuchanganya wakongwe na wapya, kuchanganya dini zote lakini Kubwa nina imani Baraza limejaa Watu weledi, wasomi wanaoendana na  nafasi walizopewa.

Katika mabadiliko haya Rais Magufuli ameendelea kuonyesha yeye ni kipenzi na Vijana kwa kuteua vijana wengi kwenye Baraza hili jipya la Mawaziri. Baadhi ya vijana waliopata fursa ya kuaminiwa ni Juliana Shonza, Abdallah Ulega, Dk. Faustine Ndugulile, Anthony Mavunde, Dk. Hamis Kigwangallah, Hamad Masauni, Mwigulu Nchemba, Mhe. Jafo, January Makamba na wengineo.

Vijana hawa wote walioteuliwa ni Watu weredi, makini na sahihi kabisa waliokuja kwa wakati sahihi. Kiukweli wametosha kabisa katika nafasi zao na watunze heshima ya asilimia 60 ya Vijana Watanzania na heshima ya Rais Magufuli aliyewaamini na kuwateua.

Rai yangu kwa Wateuliwa wote kwenda kufanya kazi kweli kweli ya kumsaidia Rais Magufuli kutekeleza ilani ya uchaguzi, kumsaidia kutimiza lengo la kuifanya nchi yetu kuwa Tanzania ya Viwanda yenye kufikia malengo ya uchumi wa kati na kwenda kutatua kero na shida za Watanzania.

Kama ambavyo Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli alivyowaamini, hata nami nikiwa sehemu ya Watanzania nina imani Kubwa na Baraza hili jipya la Mawaziri. Wakafanye Kazi kweli kweli.

Hakika kimya kingi kina mshindo mkuu. Hongera sana Rais Dk. Magufuli kwa kusuka Baraza la Mawaziri linaloendelea kuleta imani na amani kwa Watanzania la Hapa kazi Tu!

Mungu Mbariki Rais Dk. Magufuli
Mungu Ibariki Tanzania.

IMETOLEWA NA:

Emmanuel J. Shilatu
0767488622

MAHAFALI YA KWANZA YA DARASA LA SABA NA PRE - UNIT SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA YAFANA

October 08, 2017

Jana Jumamosi Oktoba 7,2017 kumefanyika mahafali ya kwanza ya Darasa la Saba katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
Mbali na kufanyika kwa mahafali hayo ya darasa la saba pia kumefanyika mahafali ya sita ya darasa la awali (Pre Unit) sambamba na uzinduzi wa Bendera na Wimbo wa shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wazazi na wadau mbalimbali wa elimu alikuwa Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis Salum maarufu “Salum Mbuzi”.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic alisema shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ilianzishwa Julai mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi 12 na kwamba mwaka huu ndiyo mara yao ya kwanza kufanya mahafali wakiwa na wahitimu 35.
“Tulianza na wanafunzi 12 katika chumba cha gereji huko Mwasele,leo shule ina jumla ya wanafunzi 622,waliohitimu mwaka huu ambao tunawafanyia mahafali ni 35,hii ni hatua nzuri tunamshukuru Mungu na wazazi ambao wamekuwa bega kwa bega nasi kuhakikisha shule hii inafanikiwa”,alieleza Dominic. 
Naye Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita aliipongeza bodi ya shule, walimu,wafanyakazi wa na wazazi kwa ushirikiano walionao katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inatoa elimu bora kwa wanafunzi. 
Katika hatua nyingine Mwita alisema ili kuinua kiwango cha elimu,wameanzisha ujenzi wa shule ya sekondari na wanafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanapata usajili ili shule ianze kupokea wanafunzi kuanzia mwaka 2018. 
Aidha aliwaomba wazazi na wadau wa elimu kuendelea kutoa ushirikiano katika kukamilisha ujenzi unaoendelea wa jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” . 
Akitoa hotuba yake,mgeni rasmi Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products aliipongeza shule hiyo kuendelea kutoa elimu bora na kuwa na mazingira bora ya kujifunzia hali inayosababisha watoto wakue vyema kiakili,kimwili na kimaadili. 
“Msingi mzuri wa elimu kwa mtoto ni kuanzia shule ya msingi hivyo nawasihi wazazi kupeleka shule,serikali yetu inapigania viwanda,viwanda hivi vinahitaji rasilimali watu,lazima tuwapatie elimu hawa watoto wetu ili maarifa wanayopata wayatumie katika viwanda hivi”,aliongeza. 
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye Mahafali hayo ametusogezea picha za matukio yaliyojiri…Tazama hapa chini
Hapa ni katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya Darasa la Saba na mahafali ya sita ya darasa la awali (Pre Unit) yaliyofanyika leo Jumamosi Oktoba 7,2017
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza katika mahafali hayo
Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Wazazi na walezi wakiwa katika mahafali hayo
MC Kifagio akikoleza neno kwa Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita
Mgeni rasmi bwana Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis Salum maarufu “Salum Mbuzi” akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi akizungumza
Muonekano wa eneo la mahafali
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Little Treasures Tilulindwa Sulus akizungumza katika mahafali hayo. 
Mwalimu mkuu wa shule hiyo,Paul Kiondo akizungumza wakati wa mahafali hayo