STARTIMES YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTAMBULISHA CHANELI MPYA

October 05, 2016
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania,  Carter Luoh (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Bw. Gaspa Ngowi. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Gaspa Ngowi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Gaspa Ngowi akizungumza na wateja walipotembelea kitengo cha huduma kwa wateja wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
 Meneja wa Ufundi wa StarTimes Tanzania, Yusuph Baracha (kushoto) akiwaelekeza wateja walipotembelea chumba cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana kupitia king’amuzi cha kampuni hiyo  wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
 Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Kitengo cha Huduma kwa Wateja wakiwahudumia wateja kupitia njia ya simu. Wateja wa StarTimes pamoja na waandishi wa habari walipata fursa ya kutembelea kitengo hicho pamoja na cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana kupitia king’amuzi cha kampuni hiyo  wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Lif


Na Dotto Mwaibale

KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayosherehekewa duniani kote na makampuni na taasisi mbalimbali katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba, StarTimes wamewaletea wateja wake chaneli mpya ambazo zitanogesha zaidi burudani.

Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh amebainisha kuwa wanafanya jitihada za kutosha kuhakikisha mkoa yote nchini inafikiwa na huduma zake.

“StarTimes inajivunia kuwa kinara katika huduma za matangazo ya dijitali nchini ikiwa na wateja zaidi ya milioni moja nchi nzima. Mpaka hivi sasa tumekwishaifikia mikoa takribani 17 ambapo hivi karibuni tumezindua huduma zetu mkoani Kigoma na tukiwa mbioni kuzindua na Mtwara pia. 

Mbali na mikoa hiyo lengo kuu ni kuhakikisha kuwa nchi nzima inafikiwa na huduma zetu ambapo tutahakikisha tunasambaza maduka na ofisi zetu. Zote hizi ni jitihada za dhati ambazo kampuni iliahidi katika kuhakikisha kila nyumba ya mtanzania inafikiwa na huduma za matangazo ya dijitali. Hivyo basi tumekuwa tukijitahidi kukamilisha dhamira hiyo huduma na bidhaa zetu zinapatikana kwa bei nafuu ambayo hata mtanzania wa kipato cha chini anaweza kumudu.” Alisema Luoh

“StarTimes inajivunia kuwa na watoa huduma takribani 300 ambao wapo tayari kuwahudumia wateja muda wote kupitia nambari 0764 700 800. Mbali na watoa huduma hao pia kupitia ofisi zetu na za mawakala wetu wateja pia wanahudumiwa katika ubora ule ule katika mikoa yote tunayopatikana. Pia tunayohuduma ya baada ya mauzo ambapo tunao mafundi waliotapakaa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kuwafuata wateja walipo. Hii yote inadhihirisha na kwa namna gani tunavyowajali wateja wetu.” Alihitimisha Mkurugenzi huyo wa Uendeshaji

Naye kwa upande wake Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo  Gaspa Ngowi ameongezea kuwa ndani ya mwezi huu wamewaletea wateja wao chaneli mpya ambazo ni ST Bollywood, ST Bolyywood Africa na FOX Life huku nyinginezo zikiwa njiani kuja rasmi.

“Wiki hii ni maalumu kwa wateja wetu hususani katika kuonyesha kuthamini mchango wao katika kuunga mkono huduma zetu. StarTimes inapenda kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kuleta chaneli mpya katika ving’amuzi vyake ambazo ni ST Bollywood, ST Bolyywood Africa ambazo zinaonyesha filamu kali na mpya za kihindi huku kukiwa na chaguo kwa mtazamaji kuchagua lugha anayoipenda ikiwemo Kiswahili; na FOX Life ambayo yenyewe inaonyesha filamu na mfululizo wa tamthiliya za runinga.” Alisema  Ngowi

Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja wa StarTimes alihitimisha kwa kusema kuwa, “Mbali  na chaneli mpya pia tumewaletea bidhaa za runinga na projekta ambazo ndani yake kuna ving’amuzi ambapo wanaweza kutazama chaneli na vipindi mbalimbali. Hivyo basi wateja wakae mkao wa kula ili kujipatia bidhaa hizi ziliunganishwa na mfumo wa dijitali moja kwa moja.”

Katika kusherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja, StarTimes imeadhimisha kwa kuwakaribisha wateja kutembelea ofisi zake ili kujionea jinsi wanavyoendesha shughuli zao.

Wateja hao walipata pia fursa ya kutembelea kitengo cha huduma kwa wateja ambapo waliweza kuonana na kuzungumza moja kwa moja na watoa huduma hao, pamoja na chumba cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana ndani ya king’amuzi cha kampuni hiyo.


Click here to Reply, Reply to all, or Forward 15.32 GB (102%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 23 minutes ago Details People (4) Dotto Mwaibale Show details

BENKI YA DCB YAZINDUA UTARATIBU MPYA KWA WATEJA WAKE WA KUTOA MAONI KWA KUTUMIA MASHINE YA HAPPY OR NOT.

October 05, 2016

                Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENKI ya DCB imezindua utaratibu mpya kwa wateja wake wa kutoa maoni kwa kutumia mashine ya Happy or not katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu- DCB, Samwel Dyamo amesema kuwa huduma hii mpya itasaidia kupata taarifa kwa mapema zaidi kwani zitakuwa ni kwa njia ya mtandao na zitatoa mrejesho kwa kampuni ili kuzidi kuboresha zaidi.

Dyamo amesema, kwa sasa wateja wetu watatumia mashine hiyi badala ya kutumia boksi la maoni kwani ni njia rahisi sana kuweza kuwafikia wao kwa mapema kwanj mrejesho utakuja haraka zaidi na mapema.

Kwa pamoja benki ya DCB waliweza kukata keki na kusherehekea na wateja wao huku baadhi wakisifia huduma nzuri zinazotolewa na wanapata mikopo kwa njia rahisi sana na kwa riba nafuu.

Fatma Simba, amesifia huduma za benki ya DCB na kusema kuwa wanatoa mikopo kwa urahisi sana ndani ya siku tatu kuanzia kima cha 50,000.

Wiki ya huduma kwa mteja inaadhimishwa dunia nzima kwa makampuni mbalimbali na taasisi, ambapo Benki ya DCB wamekuja na kauli mbiu ya Wewe ni mhimili wetu, tupo kwa ajili yako. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu DCB, Samwel Dyamo akizindua kwa kubonyeza kutufe katika mashine ya Happy or Not jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo.       
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mind Source, Abubakar Faraji akielezea namna ya kuitumia mashine ya Happy or Not kwa wateja wa Benki ya DCB leo Jijini Dar es salaam kwenye wiki ya Huduma kwa Mteja.
 Wateja na wafanyakazi wa DCB Benki wakiwa wanashuhudia kukata kwa keki sambamba na wateja hao kukata keki.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Mikakati na Uhakiki wa beki ya DCB, Samwel Dyamo akizungumza na wateja wao katika wiki ya Huduma kwa Mteja leo Jijini Dar es salaam.  
 Wafanyakazi wa Benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Kitengo cha Mikakati na Ubunifu Samwel Dyamo katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja tawi la Magomeni. 
Tawi la Benjamin mkapa wakisheherekea wiki ya huduma kwa wateja pamoja na wateja wao. Sambamba  Meneja wa tawi hilo Badru Lashku.

RAIS DKT MAGUFULI AMWANDALIA DHIFA YA TAIFA RAIS JOSEPH KABILA WA DRC, IKULU, DAR ES SALAAM

October 05, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu alikomwandalia dhifa ya Kitaifa kwaheshima yake
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu alikomwandalia dhifa ya Kitaifa kwa heshima yake

 Rais Joseph Kabila akimwamkia Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima yake
 Rais Joseph Kabila akimwamkia Mama Sitti Mwinyi, Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi,  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima yake

 Rais Joseph Kabila akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima yake

  Rais Joseph Kabila akisalimiana na  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima yake
  Sehemu ya waliohudhuria dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima ya Rais Joseph Kabila wa DRC
 Sehemu ya waliohudhuria dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima ya Rais Joseph Kabila wa DRC. Kutoka kushoto ni rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi
 Sehemu ya wageni waalikwa katika dhifa hiyo akiwemo Prof Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Suzan Kolimba na Mawaziri kutoka DRC
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa mambo ya Nje wa DRC Mhe. Raymond Tshibanda 
 Wakuu wa vyombo vya ulinzi wa Tanzania na DRC
 Sehemu ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi
 Cecilia Kabila (kulia), mdogo wake Rais Joseph Kabila wa DRC alikuwepo
 Wadau waalikwa 
Waalikwa
 Meza kuu ikiwa na Rais Dkt Magufuli na mgeni wake Rais Joseph kabila na Makamu wa rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli
 Rais Dkt Magufuli akiwa meza kuu na mgeni wake Rais Joseph kabila na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Wafanyabishara maarufu nchini Saidi Salim Bakhressa (kushoto) na Mohamed Dewji
  Wafanyabishara maarufu nchini Saidi Salim Bakhressa (kushoto) na Mohamed Dewji wakiwa na wenzao wa DRC na Tanzania
 Msanii mkongwe Zahir Ally Zorro alikuwepo kutoa burudani
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
 Mabalozi wa nchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Wadau mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Mkarimani mahiri Dkt. Mussa Lulandala akiwa kazini
 Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuhutubia
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisimua wasikilizaji wa hotuba yake
 Mama Janeth Magufuli akigonganisha glasi na Rais Joseph Kabila wa DRC baada ya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Glasi zikigongwanishwa baada ya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Meza kuu ikisimama wakati wimbo wa Taifa wa DRC ukipibgwa baada ya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Waalikwa wote walisimama wakati wa wimbo wa Taifa wa DRC ukipigwa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia
 Wote walisimama wakati wa wimbo wa Taifa wa DRC ukipigwa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akihutubia
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akiendelea kuhutubia
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akimtakia heri mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akigonganisha glasi kumtakia heri mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akigonganisha glasi na Mama Janeth Magufuli kumtakia heri yeye na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila akigonganisha glasi na makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam
  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Rais Dkt Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli wakati wa dhifa ya Taifa iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu jijini Dar es salaam
 Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa 
 Cecilia Kabila na wageni waalikwa wakisimama wakati wa wimbo wa Taifa
 Waalikwa wote walisimama wakati wa wimbo wa Taifa wa Tanzania  ukipigwa baada ya Rais Joseph Kabila wa DRC kuhutubia
 Waalikwa wote walisimama wakati wa wimbo wa Taifa wa Tanzania  ukipigwa baada ya Rais Joseph Kabila wa DRC kuhutubia
 Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bw. Gerson Msigwa akiendesha shughuli kwa weledi
 Mwanamuziki Christian Bella akitumbuiza kwenye dhifa hiyo
 Mwanamuziki Christian Bella akitumbuiza kwenye dhifa hiyo
 Mwanamuziki Christian Bella akitumbuiza kwenye dhifa hiyo
 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa "Nani kama Mama" kwenye dhifa hiyo
 Mama Janeth Magufuli akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa "Nani kama Mama" kwenye dhifa hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa "Nani kama Mama" kwenye dhifa hiyo
Mama Salma Kikweteb akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa "Nani kama Mama" kwenye dhifa hiyo