WAZIRI NAPE AWAKARIBISHA WASANII BUNGENI DODOMA LEO

May 13, 2016
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa na wasanii mbalimbali pamoja na blogger nje ya bunge baada ya kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Msanii Wema Sepetu akiwa na baadhi ya wasanii wengine bungeni

 Nape akiwa na baadhi ya wasanii nje ya Bunge
 Nape akisalimiana na wasanii
 Wema Sepetu akiwa na Martha Mlata



Wema akiwa na mmoja wa marafiki zake bungeni Dodoma
Mchekeshaji Masanja wa kikundi cha Ze Comedy akiwa bungeni wakati wa Bajeti hiyo

RAIS DKT. MAGUFULI AONDOKA KAMPALA KUREJEA NCHINI TANZANIA.

May 13, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kikundi cha ngoma za asili cha Entebe nchini Uganda wakati akiondoka kurejea nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga katika uwanja wa ndege wa Entebe wakati akiondoka kurejea nyumbani Tanzania.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na baadhi ya  viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Viongozi wakuu wanchi mbalimbali siku walipowasili Kampala nchini Uganda.
Waandishi mbalimbali wa Habari kutoa nchi tofauti wakiwa na shauku ya kupata picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni zilizofanyika kwenyeuwanja wa Uhuru wa  Kololo, Kampala nchini Uganda. Katika Picha hiyo Rais Dkt. Magufuli alikuwa akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Picha na IKULU.

BLOGGERS WATINGA BUNGENI KWA MWALIKO WA WAZIRI NAPE

May 13, 2016

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (aliyevaa tai) akiwa katika picha  ya pamoja na wamiliki wa Blogs  (Bloggers) aliowaalika wakati wa kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Annastazia  Wambura. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Baadhi ya Bloggers wakiwa bungeni wakati wa Bajeti ya wizara hiyo
 Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ akisoma taarifa ya maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo.
 Baadhi ya Bloggers wakisikiliza mwenendo wa bunge. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Wamiliki wa Bloggers Tanzania (TBN).
 Nape akiwa na Bloggers pamoja na wasanii bungeni Dodoma
 Nape akiwa na Bloggers
 Nape akisalimiana na Blogger Salum Mwinyimkuu
Mmiliki wa Blog ya Fullshangwe, John Bukuku (kushoto) na Mmiliki wa Matukio360 Blog Salum Mwinyimkuu wakiwa na mwandishi wa habari wa Raia Tanzania, Sharifa Malira

WHO NA JUMUIA YA ALYAMIN WATOA VIFAA VYA KUCHUNGUZIA MAJI NA MAJI YA KUNYWA KATIKA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU ZANZIBAR.

May 13, 2016

 MWAKILISHI wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Andemichael Ghirmay, akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipofika ofisini kwake  kukabidhi Vifaa vya kuchunguzia Maji.
 MWAKISHI wa WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo moja ya Vifaa vya kuchunguzia Maji katika  hafla ilioyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
 MTAALAMU wa Maji wa  WHO Michael Habtu, akikifanyia majaribio kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia kwa furaha.
 MTAALAMU wa Maji kutoka WHO Michael Habtu, akiwaonesha matokeo ya Maji alioyapima kwa kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia, wakwanza (kulia ) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili na Mwakilishi wa WHO Dkt. Andemichael Ghirmay
 SHEHENA ya Msaada wa Maji ya kunywa uliotolewa na Jumuia ya Alyamin kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu Zanzibar.
MWENYEKITI wa Jumuia ya Alyamin Dkt. Omar Swaleh akimkabidhi Waziri  wa  Afya Mahmoud Thabit Kombo Msaada wa Maji  na vidonge vya kutibu maji ya kunywa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu, (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili. 
 
PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA UWASILISHWAJI WA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO BUNGENI MJINI DODOMA.

May 13, 2016

 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Zamaradi Kawawa wakiwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajli ya kusikiliza Bajeti ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 13 Mei, 2016.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 13 Mei, 2016.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Profesa Elisante Ole-Gabriel (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (katikati) pamoja na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti
ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016 Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma leo 13 Mei,
2016.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Profesa Elisante Ole-Gabriel (katikati), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bi. Zawadi Msalla (kushoto) pamoja na Katibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Bi, Anna Nkinda wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016 Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wake, Mhe. Anastazia
Wambura wakijadiliana mara baada ya kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma leo 13 Mei, 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Kundi
la Wasanii na Bloggers Bungeni mjini Dodoma 13 Mei, 2016.
 
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, DODOMA)

MWENGE WA UHURU WAINGIA MKOA WA MJINI MAGHARIBI BAADA YA KUMALIZA MBIO ZAKE MKOA WA KASKAZINI

May 13, 2016

 Gari la kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2016 likikata viunga vya Kihinani
Wilaya ya Magharibi A. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
 Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Meja Mstafu. Juma Kasim Tindwa akimkabidhi Mwenge
wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis tayari kwa kukimbizwa katika mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge
wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mwinyiussi Abdalla kwa ajili ya kukimbizwa katika Wilaya yake.
 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mwinyiussi Abdalla akiteta kitu na kiongozi
wa mbio za Mwenge 2016 George Jackson Mbijima wakati wa sherehe za makabidhia
ya Mwenge yaliyofanyika Mfenesini Wilaya ya Magharibi A.
Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 James Sadick Munguji akiongoza
mbio hizo katika mitaa ya Mfenesini,
Wilaya ya Magharibi A.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba KUKABIDHI KOMBE, ZAWADI HADHARANI

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba KUKABIDHI KOMBE, ZAWADI HADHARANI

May 13, 2016

indextt 
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba Madelu kesho Jumamosi Mei 14, 201 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda na Young Africans katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali ya Nchemba ambaye atakabidhi Kombe kwa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/16, wageni wengi maalumu watakaokuwa kwenye mchezo huo ni Mkurugenzi wa Vodacom, Ian Ferrao sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi ya Kuu Tanzania Bara (TBLB).
Mchezo huo utafanyika kwa baraka za TPLB baada ya maombi ya Young Africans kukubaliwa na Ndanda ambao watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaoanza saa 10:00 jioni.
Mara baada ya mchezo huo, Mabingwa Young Africans watapewa Kombe la ubingwa, medali na fedha Sh 81,345,723; Mshindi wa Pili Sh 40,672,861; Mshindi wa Tatu Sh 29,052,044 na Mshindi wa Nne atazawadiwa Sh 23,241,635.
Mcehzaji Bora atapewa Sh 5,742,940 sawa na Mfungaji Bora wa Ligi na Kipa bora wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Vodacom, Bia ya Kilimanjaro, Azam, Startimes na NHIF. Mwamuzi Bora atazawadiwa Sh 8,614,610 saw na Kocha Bora wakati timu yenye nidhamu itavuna Sh 17,228,820.
Young Africans ndiyo iliyoomba kwa Ndanda kadhalika TPLB kuomba ridhaa ya mchezo huo kufanyika Dar es Salaam kwa kuwa inatarajiwa kusafiri kwa ndege Jumapili kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidia ya Sagrada Esperanca ya Angola utakaofanyika ama Mei 17 au 18, mwaka huu.
Barua ya Bodi ya Ligi kwa TFF imesema kwamba Young Africans watatumia mchezo huo ambao Ndanda itakuwa mwenyeji kupokea taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara litakalotolewa na Nchemba ambaye mara nyingi anaonekna uwanjani.
Kanuni ya pili ya Ligi Kuu Bara toleo la 2015/16 imeeleza wazi kuwa, “Katika mazingira maalumu, timu inaweza kucheza mchezo wake wa nyumbani katika uwanja mwingine endapo kuna sababu nzito na za msingi, utambulisho wa uwanja katika mazingira haya pia unawajibika kufanywa katika kipindi cha uthibitisho wa kushiriki ligi au kwa maombi maalumu kwa TPLB,” inasehemu kanuni hiyo. Kwa kuzingatia kanuni hiyo na sababu za yanga ambazo Ndanda na Bodi wameona kuwa ni nzito wamekubaliana kucheza mchezo huo Dar es Salaam.
Tayari Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameipongeza timu ya soka ya Young Africans kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita wa mwaka 2014/2015.
Hii ni mara ya 26 kwa Young Africans ambayo kwa sasa inacheza mashindano ya kuwania kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kutwaa taji hilo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965. Simba inafuatia katika rekodi hiyo baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara 18.
“Nichukue nafasi hii kuipongeza Young Africans kwa ubingwa. Pia nizipongeze timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio,” amesema Rais Malinzi baada ya Young Africans kufikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zilizoshiriki ligi hiyo.

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI LONDON UINGEREZA

May 13, 2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May 12, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.  Kulia ni  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg (kulia) katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.  Wanne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman  na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika katika `Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza   (Minister of State for International  Development) , Justine Greening  katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.   Wapili kushoto ni  Waziri wa Mambo ya Nje , Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda naKimataifa, Augustine Mahiga na watatu kushoto ni Jaji Mkuu, Mohamed Othman.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.