Jumuiya ya Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA Watembelea Kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo

April 22, 2016
 Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo  Juma Rajabu akifafanua jambo kwa wakurungezi wa serikali za mitaa kutoka Uganda , Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji Kanda Group COO – Maxcom Africa Jamson Kassati , Kushoto Mwanzo Mr. Moses Kimaro Kutoka ALAT (jumuiya ya serikali za MItaa Tanzania)  na pembeni yake katikati ni Mwenyekiti wa wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka Uganda Dunstan Balaba ambapo Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania.


Mkuu wa Kitengo cha Biashara Kutoka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari Akifafanua Jambo kwa Wakurugenzi hawa kutoka Uganda, Akielezea Jinsi mfumo wa Ukusanyaji Kodi na tozo mbalimbali ulivyorahisisha upatikanaji wa mapato katika halmashauri mbalimbali na Taasisi za Serikali kwa Ujumla na kuzuia mianya ya upoteaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya halmashauri.
Mwenyekiti  na Msemaji wa Umoja wa wakurugenzi kutoka Uganda  Bwana Dunstan Balaba Akieleza Jambo kwa Hadhara na Kukiri kushangazwa na watanzania Kuweza Kugundua Teknolojia kama hii. Pia Kumwomba Mkurugenzi wa Maxmalipo Afungue Ofisi Uganda Mapema iwezekanavyo.


Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA wakifuatilia Mada Kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya Maxmalipo  Bw. Deogratius Lazari ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo  Juma Rajabu anasema; Safari ya kuuaminisha Umma na Serikali kwamba wazawa wanaweza kubuni mbinu mbalimbali za kusaidia kuboresha makusanyo, inaenda sambamba na ufanisi mzuri uliothibitika katika  kazi mbalimbali ambazo kampuni Imekua ikizifanya, Juma Rajabu ameongeza kwa kuelezea jinsi ambavyo teknolojia imerahisisha ulipajji wa bili mbalimbali Ikiwamo Luku, Kodi za TRA, Ving’amuzi na hata ukusanyaji wa mapato kwenye vivuko.





Mmoja Wa wakurugenzi kutoka Uganda Bibi Lilian Akiuliza Swali kwa Maxmalipo wakati Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii Imeweza kuugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania. 



Jumuiya  ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya MAXCOM Africa  mapema  leo walipokuwa wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii Imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania.


Kawaida;

MATUKIO BUNGENI DODOMA

April 22, 2016
Wabunge wakiingia bungeni mjini Dodoma.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wabunge wakijadiliana jambo ndani bunge
Wabunge wakipata habari kupitia kwenye simu bungeni
Mbunge wa Jimbo la Momba, David Silinde akichangia hoja bungeni
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akichangia hoja
Majadilianao yakiendelea



Wabunge, Prosper Mbene, Dk.Mary Mwanjelwa na Allan Kiula wakiingia bungeni

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akijibu maswali bungeni
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisanga akiuliza swali
Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akijibu maswali
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Huruma ya Dodoma wakitambulishwa bungeni

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE, SOPHIA MJEMA AZINDUA MICHUANO YA UMISETA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

April 22, 2016
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa Michuano ya Shule za Sekondari Nchini (UMESETA), akipiga dana dana wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Shule ya Sekondari ya Azania vilivyotolewa na Kampuni ya Coca Cola. Kulia Ofisa kutoka kampuni ya Coca Cola wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016.
 DC Mjema akisalimiana na mwamuzi wa mchezo kati ya timu ya Sekondari ya Tirav ya Yombo na Makongo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Makongo ilishinda mabao 2-1.
 DC Mjema akiwasalimia wachezaji wa timu ya Tirav.
 DC Mjema akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari.
Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema (kulia), akitoa nasaha zake kwa wachezaji hao kabla ya kuanza kucheza.
DC Mjema hapa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya sekondari ya Tirav na viongozi mbalimbali.
DC Mjema hapa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya sekondari ya Makongo na viongozi mbalimbali.
Hapa akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo huo na viongozi mbalimbali.
Hapa mtanange ukiendelea.
Golikipa wa timu ya Tirav, Abdul Badi akiokoa moja ya hatari katika lango lake.
Wachezaji wa timu ya Makongo wakishangilia baada ya kupata bao lao la kwanza.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema amezindua michuano ya Shule za Sekondari Nchini (UMESETA) katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa yataendelea kuwaibua wachezaji wengi chipukizi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mjema aliishukuru kampuni ya Cocacola kwa kudhamini mashindano hayo huku akiyaomba makampuni na wadau wengine kujitokeza kudhamini michezo mbalimbali.

Mashindano hayo yatashirikisha timu zaidi ya 40 katika mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana wa Shule za Sekondari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini huku ikishirikiana na waandaaji wa michuano ya michezo ya Shule za Sekondari UMISETA katika kuhakikisha wanapata wachezaji wenye elimu kutoka mikoa yote hapa nchini.

Akizungumzia  mashindano hayo  Meneja wa Biashara wa Coca Cola Maurice Njowoka alisema wameamua kuongeza mchezo ili kupanua wigo wa mashindano hayo hapa nchini.

Aidha alisema lengo la kuungana na waandaaji hao, badala ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) pekee ni kutaka kupata wachezaji sahihi, kutoka mikoa yote, na ambao wako katika mashule ya Sekondari.

"Hii itatusaidia kupata wachezaji sahihi wenye elimu na ambao kweli wanasoma shule za sekondari,"alisema Njowoka.
Alisema tofauti na mwaka jana, tuliwatumia TFF pekee jambo ambalo tulipata wachezaji lakini katika mazingira magumu zaidi.

Alisema michuano ya mwaka huu wanaimani watapata wachezaji kiurahisi kwa sababu UMISETA ina rekodi ya wanafuzni wanaosoma katika shule za sekondari.

Njowoka alisema kwa kuanzia jijini Dar es Salaam, wametoa jezi na vifaa kwa shule za Sekondari zilizohudhuria katika mashindano hayo.

Alisema baada ya Dar es Salaam, wanaelekea Mwanza, Mbeya, Arusha na Moshi kwa ajili ya kuzindua rasmi michezo hiyo ambayo shule zinaanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa.

Alisema katika udhamini wao watatumia kinywaji cha Coca Cola kwa upande wa soka, wakati Kikapu watatumia Sprite, lengo ni kufanikisha michuano hiyo safari hii kutokana na kuongeza idadi ya mchezo.



RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WATATU KUTOKA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

April 22, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Vatican alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Rais Dkt. Magufuli mara baada ya kumaliza muda wake ya Ubalozi nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake nchini Francisco Montecillo
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo  Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Algeria hapa nchini Belabed Saada akikabidhi ujumbe uliotoka kwa Rais wa Algeria kuja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Canada alifika Ikulu na ujumbe wake  kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque wapili kutoka kulia pamoja na waakilishi wengine wa Serikali pamoja na Ubalozi wa Canada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA NANE WENYE LENGO LA KUDHIBITI SILAHA HARAMU KWA NCHI WANACHAMA MAZIWA MAKUU

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA NANE WENYE LENGO LA KUDHIBITI SILAHA HARAMU KWA NCHI WANACHAMA MAZIWA MAKUU

April 22, 2016

1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano wa nane kwa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Taasisi inayopambana na tatizo la Silaha Haramu. Mkutano huo wa siku moja unajadili kuhusu kudhibiti matumizi ya Silaha ndogo ndogo katika Nchi za Maziwa Makuu na pembe ya Afrika umefanyika leo April 22,2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Naura Spring Mkoani Arusha. 3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Baadhi ya Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Taasisi inayopambana na tatizo la Silaha Haramu baada ya kufungua Mkutano wa siku moja unajadili kuhusu kudhibiti matumizi ya Silaha ndogo ndogo katika Nchi za Maziwa Makuu na pembe ya Afrika umefanyika leo April 22,2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Naura Spring Mkoani Arusha.
2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Taasisi inayopambana na tatizo la Silaha Haramu baada ya kufungua Mkutano wa siku moja unajadili kuhusu kudhibiti matumizi ya Silaha ndogo ndogo katika Nchi za Maziwa Makuu na pembe ya Afrika umefanyika leo April 22,2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Naura Spring Mkoani Arusha.
(Picha na OMR)
Rais wa Zanzibar Dk.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA ZATUC

Rais wa Zanzibar Dk.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA ZATUC

April 22, 2016

1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar Ukiongozwa na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Castico (wa pili kulia),
2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar Ukiongozwa na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Castico (wa pili kulia),
3i
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) baada ya mazungumzo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar Ukiongozwa na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Castico (wa pili kulia),
[Picha na Ikulu.]

JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOA WA MBEYA KUFANYA KAZI YA UTOAJI HAKI KWA UADILIFU.

April 22, 2016


JAJIMkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika Kanda ya Mbeya. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika kanda hii imelenga kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. 

Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, (katikati) akipata taarifa fupi ya utendaji kazi wa Mahakama Kanda ya Mbeya kutoka kwa Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya (aliyesimama), mara baada ya kuwasili katika kikao kilichohusisha Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye alipata nafasi ya kukagua na kuongea na Watumishi wa ngazi mbalimbali za Mahakama katika mkoa huo.

Katika kikao alichofanya na Watumishi wa Mahakama mkoani humo ikiwa ni pamoja na Wahe. Majaji na Mahakimu, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza mara zote juu ya utendaji kazi kwa kujituma ili kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi ambao ndio wadau muhimu wa Mahakama.
Akiongea na Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Jaji Mkuu alieleza kufurahishwa na kasi ya usikilizaji na umalizwaji wa mashauri katika Mahakama za Mwanzo mkoani humo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza na  Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya alipokutana nao na kuwaasa kuendelea kutenda Haki kwa wakati ili kuweza kupunguza na kumaliza mashauri yanayowasilishwa mahakamani.

Awali; katika taarifa yake kwa Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. Noel Chocha, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, alimtaarifu Mhe. Jaji Mkuu juu ya mkakati waliojiwekea wa kumaliza mashauri ya aina yoyote kwa kipindi kisichozidi miezi sita. 

Aidha Mhe. Jaji Mkuu alitumia ziara hiyo ya kikazi kuwaeleza Watumishi juu ya mikakati ambayo Mahakama imejiwekea katika kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji haki inaboreshwa nchini. 

“Kwa hivi sasa Mahakama ya Tanzania imejiwekea mikakati/vipaumbele ambavyo vinalenga kuboresha huduma ya utoaji haki nchini, na malengo haya inabidi yafanyiwe kazi na kila mmoja wetu kwa maana ya kila Mtumishi na mdau wa Mahakama awajibike katika kufikia malengo yetu ya kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.” Alisema, Mhe. Jaji Mkuu.

Uimarishaji wa ukusanyaji wa takwimu; hili pia ni eneo ambalo limewekwa kama kipaumbele katika maboresho Mahakamani, Mhe. Jaji Mkuu alisema Mahakama pia imejipanga vyema kuhakikisha inakuwa na takwimu sahihi za kesi mbalimbali zilizopo katika Mahakama mbalimbali nchini ili kuangalia ni sehemu ipi inayohitaji nguvu zaidi katika kushughulikia mashauri/kesi za muda mrefu. 

Uboreshaji wa Miundombinu: miundombinu hii ni pamoja na majengo ya Mahakama, vitendea kazi n.k, Mhe. Jaji Mkuu alisema pia katika kuboresha huduma zake Mahakama imejipanga katika kuboresha miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya Mahakama na kukarabati majengo yaliyochakaa. 

“Tatizo kubwa ambalo Mahakama inakabiliana nalo ni uchakavu wa miundombinu yake, kwa hili tuko mbioni kuhakikisha Mahakama inakuwa na miundombinu bora zaidi, tumejipanga kuboresha ikiwa ni pamoja na kujenga Mahakama Kuu katika mikoa yote ambao haina majengo, taratibu zinaendelea na kwa mwaka huu tumepanga kuanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa ya Kigoma na Musoma/Mara.

Uboreshaji wa hali ya Wafanyakazi wa Mahakama; Hili pia ni moja kati ya eneo ambalo limepewa kipaumbele katika maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama; Mhe. Jaji Mkuu aliwaeleza Watumishi wa Mahakama Mbeya kuwa uboreshaji huu unaangalia upatikanaji wa stahili za Watumishi kwa wakati ikiwa ni pamoja na nauli za likizo, madeni mbalimbali, uboreshaji wa mishahara ya watumishi suala ambalo linaendelea kufanyiwa kazi. 

Aidha Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa suala Maadili na nidhamu pia limewekewa kipaumbele, alisema kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Mahakama hawana nidhamu na maadili katika utendaji kazi, hali hii imesababisha kuwa Mahakama nzima kutupiwa lawana juu ya utendaji kazi wake. 

“kuna baadhi ya Watumishi ya watumishi wa Mahakama hawana maadili na nidhamu hali hii inachafua taswira nzima ya Mahakama, lazima tuongeze uadilifu, Watanzania wanataka Watumishi wanaotoa haki, wanaoaminika ili kila mwananchi aridhike,” alisema.
Naibu Msajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya waliokutana na kuzungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania kuhusu utendaji kazi Mahakama kwa Kanda ya Mbeya.

MUOGELEAJI WA TANZANIA HILAL HILAL ATWAA MEDALI YA SHABA DUBAI.

April 22, 2016

 Muogeleaji nyota wa kiume wa Tanzania, Hilal Hilal (wa kwanza kulia) akiwa kwenye jukwaa mara baada ya kupokea medali yake ya Shaba katika mashindano ya Kanda ya Nne ya Cana. 
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinanchoshiriki katika mashindano ya Cana Kanda  ya nne. kutoka kulia ni Amani Doggart, Catherine Mason, Hilal Hilal na Smriti Gokarn.

Na Mwandishi wetu
Muogeleaji wa Tanzania, Hilal Hilal ametwaa medali ya Shaba katika mashindano ya kuogea ya Cana Kanda ya Nne yanayoendelea nchini Mauritius.

Hilal ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa katika mchezo huo, amemaliza katika nafasi ya tatu katika staili ya butterfly kwa kutumia muda wa sekunde 26.70 katika mashindano hayo magumu yaliyoshirikisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudani Kusini na Sudan.

Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na muogeleaji kutoka Zambia,  Ralph Goveia  aliyetumia muda wa 25.11 na kupata medali ya dhahabu huku  Tom Donker wa Zambia pia akimaliza katika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa 25.66 na kupata medali ya fedha.

Hilal pia alishiriki katika mashindano ya mita 50 ya staili ya backstroke na kumaliza katika nafasi ya saba kati ya waogeleaji 13 kwa waogeleaji wenye umri zaidi ya miaka 17.  Hilal alitumia muda wa 29.91 katika mashindano hayo ambapo Mzambia Tom Donker alishinda medali ya dhahabu kwa kutumia muda wa sekunde 27.40.

Mbali ya Hilal, muogeleaji mwingine wa Tanzania Catherine Mason alimaliza  katika nafasi ya nne katika mashindano ya mita 50 butterfly kwa kutumia muda wa 31.89 kwa wasichana wenye umri wa zaidi ya miaka 17. Catherine pia alimaliza katika nafasi ya nne katika mashindano ya mita 50 ya staili ya backstroke kwa kutumia muda wa  34.13.

Pia muogeleaji wa klabu maarufu ya Dar Swim Club (DSC) , Smriti Gokarn alishika nafasi ya 14 kati ya waogeaji 18 katika mashindano ya mita 200 ya backstroke kwa kutumia muda wa 3.21.30.

Muogeleaji huyo pia alishika nafasi ya tisa kwa kumia muda wa 2.31.31 katika mashindano ya freestyle mita 200 na katika mita 50 butterfly alimaliza katika nafasi ya 11 kwa kutumia muda wa 34.28. Pia alimaliza katika nafasi ya 11 katika mita 50 kwa upande wa staili ya backstroke kwa kutumia muda wa 36.43.

Naye Amani Doggart alianza kwa kushika nafasi ya 14 katika staili ya butterfly kwa kutumia muda wa 38.54 na baadaye kumaliza wa Saba katika staili ya backstroke  kwa kutumia muda wa 37.41 katika mashindano ya mita 50.