KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YATEMBELEA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) JIJINI DAR ES SALAAM

August 26, 2016
 Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart,  Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
 Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo na  Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.
 Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.
Mkuu wa Oparesheni wa Chumba cha kuangalia mienendo ya mabasi ya udart yakiwa barabarani, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo unavyofanyakazi.

Na Dotto Mwaibale

Kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa leo asubuhi imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea mradi wa Udart yenye lengo la kujua jinsi mradi huo unavyoendeshwa pamoja na kujua changamoto zake ambapo wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wao Jasson Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba vijijini.

Katika hatua nyingine ya ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha anawaondoa wafanyabiashara katika Miundombinu ya Kampuni ya Mabasi ya mwendo wa haraka (Udart)

Simbachawene alitoa agizo hilo wakati akizungumza na uongozi wa Udart baada ya kufanyika majuisho ya ziara ya kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.

"Namuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwaondoa mara moja wafanyabiashara katika miundombinu ya udart" alisema Simbachawene.

Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa alisema changamoto kubwa iliyopo ni elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart.

Alisema changamoto waliyonayo ni wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart ambapo wamejipanga kuhahikisha kila mwananchi anaipata jambo litakalosaidia kuitunza na kuendelea kupata huduma bora.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza aliutaka uongozi wa udart kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri jijini Dar es Salaam ili kuwapunguzia adha ya usafiri wananchi.

Kamati hiyo ilitembea mradi wa udart katika vituo vikuu vya Kimara mwisho, Moroco makao makuu ya Udart Jangwani, Gerezani na Kivukoni.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA JIJINI NAIROBI

August 26, 2016

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Japan,(JICA) Bw. Hiruchi Kato (kulia kwake) na ujumbe wake , jijini Nairobi Agosti 26, 2016 ambako anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa sita Wa Tokyo International Conference o n Africa Development (TCAD). Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili Nairobi, Kenya kuhudhuria Mkutano wa Mkuu wa Sita wa Wakuu wa Nchi wa TICAD (TICAD VI) utakaofanyika Agosti 27 -28, mwaka huu. Waziri Mkuu anahudhudia mkutano huo kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

Leo asubuhi (Ijumaa, Agosti 26, 2016) Waziri Mkuu amekutana na viongozi wakuu mbalimbali wa makampuni ya kibiashara kutoka Japan ambao wamekuja kuhudhuria mkutano huo.

Waziri Mkuu amekutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Chiyoda Corporation, Bw. Tadashi Izawa ambapo katika mazungumzo yao, pamoja na kuangalia fursa nyingine katika sekta ya gesi Tanzania, kampuni hiyo imekubali kutoa mafunzo ya kujenga uwezo wa wataalamu kwa sekta ya gesi hususan usindikaji wa gesi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi (Liquefied Natural Gas).

Bw. Izawa amemweleza Waziri Mkuu kwamba wamefurahiswa na taarifa za ugunduzi wa gesi ya Helium hapa nchini Tanzania na kwamba kampuni yake ina teknolojia na uzoefu wa muda mrefu katika kutekeleza miradi ya gesi (Gas value Chain Planning and Execution).

“Tunao uzoefu wa muda mrefu, pia tunazo teknolojia za kuendeleza sekta ya gesi ikiwemo Helium kwa mfano ujuzi wa kutenganisha gesi asilia na helium (Separation of Natural Gas and Helium). Tumetekeleza miradi ya namna hii nchini Qatar ambayo kwa sasa ni ya pili kwa uzalishaji wa gesi hiyo duniani ikitanguliwa na Marekani,” amesema.

Amesema mafunzo hayo yatafanyika kuanzia mwakani na yatalenga vijana wasiopungua 10 kutoka Tanzania ambao wamehitimu shahada za uhandisi kwani wameshafanya hivyo kwa vijana wanane kutoka Msumbiji.

Waziri Mkuu alimshukuru Vw. Izawa kwa mpango wao wa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania lakini akamtaka pia waangalie uwezekano wa kuwasaidia vijana wanaotoka maeneo husika yenye gesi ili wapatiwe mafunzo ambayo yatawawezesha kumudu baadhi ya kazi kwenye viwanda vya kusindika gesi.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato na kujadiliana mambo kadhaa yakiwemo ya nishati na miundombinu.

Katika mazungumzo hayo, Bw. Kato alimweleza Waziri Mkuu nia ya shirika hilo kuendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo hapa nchini na hasa katika sekta za afya, maji, kilimo na miundombinu ambazo imekuwa ikijihusisha nazo kwa muda mrefu sasa.

Waziri Mkuu alimshukuru kwa ushiriki wa shirika hilo kwenye miradi ya nishati ya Kinyerezi na akamtaka aendelee kuisaidia Serikali ya Tanzania inainginia kwenye awamu ya tatu ya Kinyerezi (Kinyerezi III).

Katika hatua nyingine, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe alimwoba makamu wa Rais hyo waangalie uwezekano wa kuwekeza kwenye sekta za nishati na miundombinu ya mkoa Dodoma hasa katika kipindi ambacho Serkali imeamua kuhamia huko.


“Tunaomba muangalie sana suala la kuendeleza nishati ya umeme kwani nchi yetu imeamua kuwa nchi ya viwanda. Tutahitaji kuwa na umeme wa kutosha kuendesha viwanda vya usindikaji bidhaa zetu, lakini pia si mbaya mkiangalia suala la kuboresha miundombinu ya barabara na usafirishaji katika mji wa Dodoma,” amesema.
NMB YAWAKUTANISHA WALIMU WA MKOA WA DAR ES SALAAM 'TEACHERS DAY' JIJINI DAR LEO.

NMB YAWAKUTANISHA WALIMU WA MKOA WA DAR ES SALAAM 'TEACHERS DAY' JIJINI DAR LEO.

August 26, 2016


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kulia) wakionesha ujumbe wa maadhimisho mara baada ya kuzindua hafla ya maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kulia) wakionesha ujumbe wa maadhimisho mara baada ya kuzindua hafla ya maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Augustino Mbogela Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Augustino Mbogela Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (mwenye gauni jeusi) ambaye ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa NMB kwenye maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (mwenye gauni jeusi) ambaye ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa NMB kwenye maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akiagana na baadhi ya viongozi wa UWT na NMB mara baada ya kuzindua hafla hiyo ya 'Teachers Day'.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akiagana na baadhi ya viongozi wa UWT na NMB mara baada ya kuzindua hafla hiyo ya 'Teachers Day'.Baadhi ya walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam wakiwa katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Baadhi ya walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam na maofisa wa NMB wakiwa katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.

KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YATEMBELEA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) JIJINI DAR ES SALAAM

August 26, 2016
1
 Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart,  Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
 Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo na  Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.
 Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.
Mkuu wa Oparesheni wa Chumba cha kuangalia mienendo ya mabasi ya udart yakiwa barabarani, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo unavyofanyakazi.
………………………………………………………………..
 
Na Dotto Mwaibale
 
Kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa leo asubuhi imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea mradi wa Udart yenye lengo la kujua jinsi mradi huo unavyoendeshwa pamoja na kujua changamoto zake ambapo wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wao Jasson Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba vijijini.
 
Katika hatua nyingine ya ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha anawaondoa wafanyabiashara katika Miundombinu ya Kampuni ya Mabasi ya mwendo wa haraka (Udart)
 
Simbachawene alitoa agizo hilo wakati akizungumza na uongozi wa Udart baada ya kufanyika majuisho ya ziara ya kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
 
“Namuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwaondoa mara moja wafanyabiashara katika miundombinu ya udart” alisema Simbachawene.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa alisema changamoto kubwa iliyopo ni elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart.
 
Alisema changamoto waliyonayo ni wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart ambapo wamejipanga kuhahikisha kila mwananchi anaipata jambo litakalosaidia kuitunza na kuendelea kupata huduma bora.
 
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza aliutaka uongozi wa udart kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri jijini Dar es Salaam ili kuwapunguzia adha ya usafiri wananchi.
 
Kamati hiyo ilitembea mradi wa udart katika vituo vikuu vya Kimara mwisho, Moroco makao makuu ya Udart Jangwani, Gerezani na Kivukoni.
1

CCM YAOMBOLEZA VIFO VYA POLISI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI, YATOA MSIMAMO WAKE JUU YA MAMBO MBALIMBALI YA KISIASA

August 26, 2016


Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akizungumza na Waandishi wa Habari, kufafanua masuala mbalimbali, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR.

Ifuatayo ni Taarifa rasmi Kama ilivyosomwa na Sendeka wakati wa kikao hicho na waandishi wa Habari

 
Ndugu wanahabari.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa sana taarifa ya kushambuliwa na kuuawa kwa askari wa jeshi la Polisi wakiwa katika kutekeleza majukumu yao ya ulinzi eneo la Mbande, Temeke jijini Dar Es Salaam.

CCM tayari imemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu pamoja na familia za marehemu waliofikwa na umauti katika tukio hilo baya katika historia ya nchi yetu.Tunalaani tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuvipa ushirikiano wa kutosha vyombo vya dola ili kufanikisha wahusika wa tukio hilo kusakwa popote pale na kupatikana ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria haraka.
Mabalozi watembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Mabalozi watembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

August 26, 2016
JK1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania. Kulia ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Edzai Chimonyo. Mabalozi hao wameitembelea taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kitibabu na wamehahidi kuwenda kupatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo badala kwenda nchi nyingine ikiwamo Afrika Kusini kupatiwa huduma za magonjwa ya moyo.
JK2
Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi baada ya kuitembelea taasisi hiyo LEO.
JK3
Profesa Janabi akizungumza na mabalozi katika taasisi hiyo LEO.
JK4
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na mabalozi kwenye taasisi hiyo LEO.
JK5
Mabalozi hao wakiwa katika chumba cha upasuaji.
JK6
Mabalozi hao wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Warsha ya taaluma ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Warsha ya taaluma ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

August 26, 2016
teh2
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Edwin Ngonyani (Mb) akizungumza na wataalamu wa Teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) hawapo pichani wakati akifungua warsha ya   wataalamu wa teknolojia ya habari na Mawasiliano katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.  
teh3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Edwin Ngonyani (Mb) ili kufungua warsha ya  wataalumu wa teknolojia ya habari na Mawasiliano.  
teh4
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Mhandisi Samson Mwela akitoa mada   wakati wa warsha  ya wataalamu wa Teknolojia ya habari na Mawasiliano katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.   
teh5
Baadhi ya washiriki wa warsha ya wataalumu wa teknolojia ya habari na mawasiliano wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Edwin Ngonyani (hayupo pichani) akifungua warsha jijini Dar es salaam.
teh6
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Edwin Ngonyani (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya mawasiliano   na wataalamu wa teknolojia ya habari na Mawasiliano  Jijini DSM.

Lukuvi atembelea eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex Pugu jijini Dar es Salaam

August 26, 2016


Mmoja ya Fundi gereji katika Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam Bw. Mohamed Ali akielezea sababu za wao kuvamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (hayupo pichani).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza kwa makini Afisa Ardhi toka Manispaa ya Ilala Bw. Furaha Mwakapalila akielezea historia ya eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex ambalo kwa sasa limevamiwa na mafundi magari wa kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Afisa Tarafa wa Ukonga Bw. Jeremiah Makorere akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya waziri huyo kubaini migogoro mbalimbali ya ardhi katika eneo la Pugu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha Kisarawe Brick Factory (KIBRICO) wakati wa ziara ya Waziri huyo kubaini migogoro ya ardhi katika eneo la Pugu.
Mwenyekiti ya Kamati ya malalamiko ya wakazi wa Mtaa wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha Kisarawe Brick Factory (KIBRICO) Bw. Deus King΄ung΄alo akisoma risala kwa niaba ya wakazi hao wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya Waziri huyo kubaini migogoro ya ardhi katika eneo la Pugu.

Watanzania washauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili kuutangaza Utamaduni

August 26, 2016

Watanzania wameshauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili katika ulimwengu wa uandishi ili kuutangaza Utamaduni wa nchi.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).

Mkurugenzi amesema kuwa kwa kutumia Lugha ya Kiswahili kutasaidia kuendeleza na kuenzi juhudi za kuenzi na kuendeleza juhudi za watetezi za masuala ya lugha wa masuala ya Lugha na Utamaduni wa mtanzania.

Ameongeza kuwa Serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa imeandaa kanuni za Sheria ya BAKITA ya mwaka 1967 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni ambayo itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili waandishi hapa nchini pamoja na haki zao katika kuendeleza fani mbalimbali za Lugha.

“Katika azma ya kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili tuige mfano wa Rais wetu Mhe.Dkt John Pombe Magufuli wa kutumia Lugha ya kiswahili katika hotuba zake mbalimbali za kitaifa na kimataifa” alisema Bibi. Hajjat Shani.

Kwa upande wake mmoja ya wajumbe wa kamati kuu Bi. Matilda Sendwa katika risala yao kwa mgeni rasmi amesema kuwa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania(UWARIDI) wameamua kutafuta njia ya kurudisha, kutetea, kulinda na kuipandisha heshima yetu kama waandishi na heshima ya kazi zetu zote.

“Tumeamua kutafuta mbinu za kuweza kuhakikisha kuwa heshima ya kazi zetu zinatambuliwa rasmi kiserikali na kijamii kwa ujumla kwa kuanzisha umoja wetu ambao utakuwa na sauti katika kutetea haki za waandishi na kazi zao alisisitiza Bi. Matilda.

Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) umeanzishwa kwa lengo la kuwatetea waandishi wa Riwaya nchini ili waweze kunufaika na kazi zao.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Rais wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Bw. Hussein Tuwa akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Ibrahim Gama akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu Umoja wao wakati wa uzinduzi wa Umoja wa huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akionesha cheti cha usajili wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya kuuzindua umoja huo huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) wakimsikiliza mwakilishi wa mgeni rasmi Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo(hayupo pichani) katika uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamojja na viongozi na wajumbe wa kamati kuu ya Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.

Baadhi ya vitabu vya Riwaya vilivyoandikwa na wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI). (Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)