CCM MANISPAA YA IRINGA YATUMIA ZAIDI YA MILIONI TANO KUTATUA BAADHI YA CHANGAMOTO KATIKA HOSPITAL YA FRELIMO

April 10, 2018




Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo



Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo


Baadhi ya wananchi,makada wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa na viongozi wa chama hicho waliokuwa wameudhulia makabidhiano ya vifaa kati ya uongozi wa hospital na viongozi wa chama hicho manispaa ya Iring


Na Fredy Mgunda,Iringa.


CHAMA cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimetumia zaidi ya shilingi million tano kuanza kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali ya Frelimo iliyopo wilaya ya Iringa kwa kununua mashine mbili za kufulia na televisheni moja aina ya LG nchi 43.

Akizungumza wakati wa kukatibidhi vifaa hivyo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wameamua kuanza kuzitatua kwa awamu na kuangalia vipaumbele stahili

“Tulikuja kwenye ziara hapa na viongozi wangu na tulikutana na viongozi wa hospatali hii wakatueleza changamoto nyingi sana ambazo ni ngumu kutekeleza kwa siku moja hivyo tulitoka na vipaumbele vyetu sisi kama chama ndio maana leo tumenza na hili na tutafuta na jingine” alisema Rube

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mganga mfawidhi wa hospital hiyo, Dr Pilila Zambi alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na changamoto zifuatazo jengo la vipimo na uchunguzi,wodi ya kulaza wagonjwa,wodi ya watoto,wodi ya kulaza wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza,jengo la utakasaji wa vifaa,jengo la kufulia nguo,nyumba za watumishi na ukosefu wa uzio.

Aidha Dr Zambi aliongeza kuwa hospital hiyo inaupungufu wa vifaa tiba ambavyo vimekuwa vikikamisha shughuli za kutoa huduma bora kwa wananchi,vifaa hivyo ni biochemistry machine,hematology machine Viral load analyser,Ultrasound machine na X-ray machine.

“Tukipata pia mashine kama mashine ya utakasaji, mashine ya kufulia na automatic genereta basi hapo tutakuwa tumefanikiwa kutatua changamoto za hospitali na tutatoa huduma bora kwa wananchi wanakuja kupata huduma katika hospital hii” alisema Zambi

Rubeya alisema kuwa kutokana na changamoto hizo ndio maana wameanza na kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000)

“Tuliona tuanze na vifaa hivi vidogo kwasababu inasikitisha kuona kuwa nguo chafu zenye vimelea vya magonjwa mbalimbali vinapitishwa katika ya mji hadi hospital ya Rufaa hivyo tukaamua kutatua kwa hii changamoto, pia wauguzi na madaktari mnatakiwa kujua nini kinaendelea nchi kwetu na nje ya nchi hiyo tukaamua kuwaletea TV hii kwa ajili ya mafunzo mbalimbali” alisema Rubeya

akizungumza kwa niaba ya mstahiki meya diwani wa kata ya mivinjeni Frank Nyalusi amewataka viongozi wote kuleta maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa na kuwashukulu viongozi wa chama cha mapinduzi kwa kuwafungulia njia ya maendeleo.

“Mimi binafsi niwapongezee chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa mliyoifanya hapa kwa kutusaidia kutatua changamoto za hospital hii” alisema Nyalusi

UBUNIFU: MAKEKE KUJA NA VAZI LA UNGO LIJULIKANALO KAMA "LUPAHERO"

April 10, 2018
Jinsi wazo lilivyopatikana.
Katika maandalizi yaonyesho la kwanza kufanywa chini ya MAKEKE INTERNATIONAL lililofahamika kama I AM MAKEKE ndipo wazo hili la lupahero lilipozaliwa. Kwamujibuwa MAKEKE INTERNATIONAL ilimchukua muda mrefu kupata wazo la kufanya katika onyesho hilo licha ya kua na bidhaa nyingi za kubuni nguo mbalimbali ofisini kwake.

Baada ya kuwaza kwa muda mrefu ndani ya ofisi, alitoka nje na kurudi baada ya kutuliza akilila na wakati akirudi aliuona ungo kupitia dirisha uliokua umetundikwa ukutani kama pambo la ofisia mbapo aliamua kuuchukua na kukaa nao huku kichwa kikiendelea kuwaza na kuwazua ni wazo gani ataonyesha kwenye onesho lililokua mbeleyake.

Baada ya kuwaza kwa masaa kadhaa wazo lilimjia na kutaka kutoboa ungo aliokua nao kwakiasi cha kuweza kuvaa shingoni ambapo alifanya hivyo na kupata ladha ya mapambo ya shingoni ya kimasaii la katika mwonekano wa ungo na ndipo alipoanza kufikiria mikato mingine ambayo ungo unaweza kuingia na kudhihirisha ubunifu wa ungo kama vazi.

Baada ya kupata yote hayo Makeke alichukua daftari na kuanza kuchora kila alichokua amekiwaza kwa ufanisi zaidi kufanyia kazi kwa muda aliokua nao hali iliyofanya ubunifu wa ungo kutumika kwamara ya kwanza katikatamasha la I AM MAKEKE mpaka hivisasa.

Mikato ya Lupahero




MAKEKE INTERNATIONAL
imelenga zaidi kujenga dhana ya ushujaa na asili ya kiafrika ili kujenga mazingira ya kuweza kujiamini na kujua kuwa wewe ni bora zaidi kutoka na jinsi ulivyo kama mwafrika na shujaa akiwa katika kila jambo.

Follow us on Facebook @makeke international Instagram@makekeinternational

blog makekeinternational.blogspot.com

On Apr 6, 2018 8:11 PM, "Mr. Lulela" wrote:



LUPAHERO
Baadayauzoefumkubwakatikamatumiziyamapishijikoni, ungoumejizoleaumaarufumkubwabaadayakuingizwarasmikatikatasniayasanaahususanikatikaubunifuwamavazinakupewajina la LUPAHERO naJocktanMakeke.

Maanaya LUPAHERO

Ubunifu huu wa mavazi umepewa jina la LUPAHERO ambalo nimchanganyiko wamajina mawili ambayo ni LUPAPIKE, neno la kinyakyusa lenye maana ya ungo na neno la pilini LUHELO, ambalo ni neno la kihehe lenye maana ya ungo.

Muunganikowamaneno haya mawili yamelenga kuletadhana yaushujaa kutokan ana ladha ya mavazi hayo kuwa na dhima hiyo, huku neno Luhelo likitamkwa herufi zamwisho kama Hero, herufi L ikibadilishwa kuwa R ilikupataneno hero la kingereza lenyemaana ya shujaa nakukamilisha maana halisi yaubunifu huo kuwashujaa wa ungo.

Jinsiwazolilivyopatikana.

Katika maandalizi yaonyesho la kwanza kufanywa chini ya MAKEKE INTERNATIONAL lililofahamika kama I AM MAKEKE ndipo wazo hili la lupahero lilipozaliwa. Kwamujibuwa MAKEKE INTERNATIONAL ilimchukua muda mrefu kupata wazo la kufanya katika onyesho hilo licha ya kua na bidhaa nyingi za kubuni nguo mbalimbali ofisini kwake.

Baada ya kuwaza kwa muda mrefu ndani ya ofisi alitoka nje na kurudi baada ya kutuliza akilila na wakati akirudia aliuona ungo kupitia dirisha uliokua umetundikwa ukutani kamapambo la ofisia mbapo aliamua kuuchukua na kukaa nao huku kichwa kikiendelea kuwaza na kuwazua ni wazo gani ataonyesha kwenye onesho lililokua mbeleyake.

Baada ya kuwaza kwa masaa kadhaa wazo lilimjia na kutaka kutoboa ungo aliokua nao kwakiasi cha kuweza kuvaa shingoni ambapo alifanya hivyo na kupata ladha ya mapambo ya shingoni ya kimasaii la katika mwonekano wa ungo na ndipo alipoanza kufikiria mikato mingine ambayo ungo unaweza kuingia na kudhihirisha ubunifu wa ungo kama vazi.

Baada ya kupata yote hayo Makeke alichukua daftari na kuanza kuchora kilaalichokua amekiwaza kwa ufanisi zaidi kufanyia kazi kwa muda aliokua nao hali iliyofanya ubunifu wa ungo kutumika kwamara ya kwanza katikatamasha la I AM MAKEKE mpaka hivisasa.
Mikato ya Lupahero


MAKEKE INTERNATIONAL
imelenga zaidi kujenga dhana ya ushujaa na asili ya kiafrika ili kujenga mazingira ya kuweza kujiamini na kujua kuwa wewe ni bora zaidi kutoka na jinsi ulivyo kama mwafrika na shuja akiwa katika kila jambo.

Follow us on Facebook @makeke international Instagram@makekeinternational

blog makekeinternational.blogspot.com
TRA YAKUSANYA TRILIONI 11.78 NDANI YA MIEZI 9

TRA YAKUSANYA TRILIONI 11.78 NDANI YA MIEZI 9

April 10, 2018


Mkurungezi Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Akiongea na Wandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kitoa Ufaanuzi juu ya makusanyo ya kodi Kwa kipindi cha meizi Tisa Mwaka wa fedha 2017/2018
………………
Katika kipindi cha miezi tisa Mwaka wa fedha 2017/2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imekusanya jumla ya shilingi Tirion 11.78 ikilinganishwa na shilingi Tirioni 10.86 amabazo zilikusanywa Mwaka wa fedha 2016/2017, Kiasi hiki sawa na ukuaji wa silimia 8.6.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato TRA Bw. Richard Kayombo amesema hayo Leo wakati akizungumza na wandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi kwa kipindi hicho.

Richard Kayombo amongeza kuwa katika mwezi Machi TRA imekusanya jumla ya shilingi Trrioni 1.54 akilinganishwa na makusanyo ya mwezi Machi 2017 Ambapo ilikusanya Shilingi tirioni 1.34 sawa na ukuaji wa asilimia 14.49
Ameongeza na kusema””Katika Kipindi hiki Mamlaka ya Mapato TRA inaendelea na usajili wa walipa kodi wapya ambapo Kwa wiki hii usajili unafanyika mkoani Geita”” alisema Kayombo.
Mkurungezi wa Huduma na Elimu Kwa Mlipa kodi Mamlaka ya Mapato TRA Amewakikishia wananchi kuwa TRA itandele kutoa elimu hii Kwa kila anae stahili kulipakodi Kwa hiyari na kwa wakati na kila Mwenye malalamiko juu ya makadirio amuone meneja wa eneo husika akiwa na vielelezo vyote vinavyotakiwa kwa mlipa kodi

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKABIDHIWA RASIMU YA MWISHO YA SERA YA TAIFA YA MISITU

April 10, 2018

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) akikabidhiwa Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (katikati) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) akizungumza mara baada ya makabidhiano ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( wa pili kushoto) akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kulia) kabla ya makabidhiano ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma
Baadhi ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu iliyokabidhiwa leo na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Kimataifa (FAO) kwa serikali ya Tanzania katika hafla iliyofanyika leo katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.

Baadhi ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu iliyokabidhiwa leo na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Kimataifa (FAO) kwa serikali ya Tanzania katika hafla iliyofanyika leo katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.

( PICHA ZOTE NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)


Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa rasimu ya mwisho ya sera ya Taifa ya Misitu na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kufuatia kukamilika kwa mchakato uliowashirikisha wadau wote muhimu.

Hatua hiyo inafuatia ikiwa ni mwaka mmoja sasa ambapo FAO na wizara ya Maliasili na Utalii ziliposainiana mkataba wa msaada wa Kitaalamu kuisaidia serikali kukamilisha Mapitio ya Sera ya Taifa ya Misitu ambayo ilipitishwa mwaka 1998.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi amesema Tanzania inakabiliwa changamoto katika kuthibiti rasilimali misitu kwa kuwa sera ya misitu inayotumika kwa sasa ni ya zamani hali inayochangia kushindwa kuendana na kasi ya maendeleo sasa.

Ameyasema hayo leo tarehe 10 April, 2018 katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma baina yake, na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero.

Milanzi amesema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka wakati ambapo nchi inakabiliwa na changamoto nyingi za uharaibifu wa misitu.

‘’Tunahitaji sera dhabiti ya kukabiliana na masuala mbalimbali yanayohusu uharibifu wa rasilimali za misitu’’ alisisitiza Milanzi.

Kwa upande wake, Kafeero alisema alisema FAO imepiga hatua kubwa za mafanikio katika kukamilisha mchakato wa kuandaa rasmu hiyo ambayo ni shirikishi.

‘’Tayari FAO imesaidia nchi nyingi kwenye maeneo hayo lengo likiwa kuhakikisha kuwa sera hiyo inatilia maanani masuala ya maendeleleo ya kitaifa na kimataifa.

Aidha, Kafeero alisema misitu ni moja ya maeneo ya majukumu makuu ya FAO kwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu yanayohusiana na matumizi endelevu ya maliasili, uhakika wa chakula na lishe pamoja na maendeleo ya uchumi kwa ujumla.

Wakati huo huo, FAO pamoja na Serikali wanamalizia taratibu za kuandaa mkakati wa kuitekeleza Sera hiyo ili iweze kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa katika misitu nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) akikabidhiwa nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwnza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) hapa nchini, Fred Kafeero (wa pili kushoto) kabla ya makabidhiano ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.

Baadhi ya nakala ya Rasimu ya mwisho ya Sera ya Taifa ya Misitu iliyokabidhiwa leo na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Kimataifa (FAO) kwa serikali ya Tanzania katika hafla iliyofanyika leo katika makao makuu ya ya Wizara mjini Dodoma.

NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUCHEZWA APRILI 20 NA 21

April 10, 2018




NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUCHEZWA APRILI 20 NA 21

Hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inatarajia kuchezwa Aprili 20 na Aprili 21,2018.

Nusu fainali ya Kwanza itachezwa Ijumaa Aprili 20,2018 ikiwakutanisha Stand United ya Shinyanga watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage,Shinyanga saa 10 jioni.

Singida United ya Singida watawakaribisha JKT Tanzania ya Dar es Salaam kwenye nusu fainali ya pili itakayochezwa Uwanja wa namfua Jumamosi Aprili 21,2018 saa 10 jioni.

Washindi kwenye nusu fainali hizo watacheza mchezo wa fainali May 31,2018.

LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE NANE BORA KUENDELEA APRILI 21

Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya Nane bora inatarajia kuendelea Jumapili Aprili 21 kwenye viwanja tofauti.

Hatua hiyo ya nane bora ambayo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) iliyokuwa kambini kujiandaa na mchezo wake wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake itaendelea katika mzunguko wa Tano(5).

Hatua ya nane bora inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ikishirikisha timu za Panama FC ya Iringa inayotumia Uwanja wa Samora,Evergreen Queens ya Dar es Salaam inayotumia Uwanja wa Karume,JKT Queens ya Dar es Salaam wanaotumia Uwanja wa Mbweni,Alliance ya Mwanza wanaotumia Uwanja wa Nyamagana,Mabingwa watetezi Mlandizi Queens ya Pwani wanaotumia Uwanja wa Mabatini,Baobab ya Dodoma wanaotumia Uwanja wa Jamhuri Dodoma,Kigoma Sisters ya Kigoma wanaotumia Uwanja wa Lake Tanganyika na Simba Queens wanaotumia Uwanja wa Karume.

Huu ni msimu wa pili wa Ligi ya Wanawake kuchezwa ambapo katika msimu wake wa kwanza timu ya Mlandizi Queens ndio waliibuka na ubingwa.

Ligi hiyo inadhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lite yenye ladha maridadi.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

SERIKALI HAITAKUWA NA SIMILE KWA WANANCHI WATAKAOKAMATWA WAKIJIHUSISHA NA KUINGIZA BIDHAA ZA MAGENDO MKOANI TANGA

April 10, 2018



MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim




Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa



PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akizungumza wakati akiwakaribisha wageni kwenye sherehe hizo zilizofanyika kwenye viwanja v ya Bandari Jijini Tanga


Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akifuatilia matukio mbalimbali kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire
Afisa Tehama wa Bandari ya Tanga Ally Isaka akimueleza kitu Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Bandari leo akiwa ameambatana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdallah na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akisalimiana na wafanyakazi wa Bandari ya Tanga

Sehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Sehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

Zoezi la utoaji wa damu likiendelea kwenye sherehe hizo

SERIKALI mkoani Tanga imesema kuwa haitakuwa na simile na wananchi watakaokamatwa kujihusisha na kuingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu kwani wanachangia kuikosesha mapato serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo.

Alisema kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia bandari bubu kupitishia bidhaa za magendo ambazo sio salama kwa matumizi ya binadamu.

“Katika hili hatutakiwa na msamaha wala kumuonea mtu haya tukikukamata chombo tutakitaifisha pamoja na mali zake huku muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheri nilazima wananchi wajifunzi kuona umuhimu wa kutumia bandari rasmi”alisema DC Mwilapwa.

Aidha aliitaka Mamlaka ya usimamizi wa bandari Mkoani Tanga kuhakikisha utendaji kazi wao unaendana na kasi ya maboresho ya bandari hiyo unaofanywa na serikali kwa sasa.

Awali Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama alisema kuwa maboresho ya vifaa na vitendea kazi katika bandari hiyo yameweza kusaidia kuongeza ufanisi wa kuhudumia shehena za mizigo kutoka siku kumi hadi nne.

Alisema kuwa kuhudumia shehena za mizigo katika kipindi kifupi kumesaidia kupunguza gharama kwa wateja wanaohudumiwa na bandari hiyo . “Licha ya kuhudumia mizigo kwa awamu mbili lakini uwepo wa vifaa umesaidia kuboresha uwezo wa bandari yetu ya kuhudumia mizigo kwa ufanisi zaidi”alibainisha Mkuu huyo.

Sherehe hizo zinakwenda sambamba na kauli mbiu Bandari za TPA ni chachu ya uchumi Viwanda na Ustawi nchini Tanzania.

MPINA AFUFUA KIWANDA CHA NYAMA SHINGANYA

April 10, 2018
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina  akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Kiwanda cha nyama cha Shinyanga  iliyoharibiwa  na  kutolewa  mabomba  ambapo pia vitasa vya mlango vimetolewa alipofanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda hicho leo.  (Picha na John Mapepele)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina(Mwenye Miwani) akioneshwa eneo la kiwanda cha nyama Shinyanga na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Jones Mwalemba(aliyenyoosha mkono) Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Asimwe Lovince kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Wilaya a shinyanga wa CCM. (Picha na John Mapepele)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga ( Mwenye Miwani) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakari Mkadamu akivunja kufuli la mlango mkuu wa kuingilia katika kiwanda cha nyama Shinyanga mara baada ya waziri Mpina kufanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda hicho. (Picha na John Mapepele)Na John Mapepele, Shinyanga

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa siku saba kwa wawekezaji wa kiwanda cha nyama Shinyanga cha Kampuni ya Triple S Beef Limited na Agri Vision kuwasilisha hati zote za umiliki hati ya eneo la kiwanda na eneo la kuhifadhia mifugo baadha ya kushindwa kukiendeleza kwa miaka 11.

Akizungumza katika kiwanda hicho leo Mpina amuagiza Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji Jones Mwalemba kutoka Hazina kuhakikisha kwamba ifikapo Juni 30 mwaka huu kiwanda hicho kiwe kimempata mwekezaji ambaye ataanza kazi mara moja ya uchinjaji ili kutoa ajira na kuliingizia taifa mapato.

Aidha amemuagiza Msajili wa Hazina kuanza uhakiki wa mali zote za kiwanda hicho baada ya kubainika wizi uliokithiri katika kiwanda hicho.

Pia Mpina ameamuru mmliki wa Kampuni inayolinda kiwanda hicho kukamatwa mara moja na kufikishwa katika mikono ya sheria kwa ajili ya kujibu mashitaka wa wizi wa mali za kiwanda hicho ambapo amemtaka Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuanzia sasa kiwanda hicho kilindwe na vyombo vya Serikali badala ya makampuni binafsi.

Waziri Mpina alisema hatua ya Kampuni ya Triple S kuuza kiwanda na kuingia mkataba mpya na Kampuni ya Agrovisioni ni kinyume na mkataba wa awali ilioingia na Serikali.

“Huu ni ukiukwaji wa masharti ya Mkataba kulingana na kifungo cha 16.1 ambapo sasa kinauondoa umiliki wake katika kiwanda hiki” alisisitiza Mpina

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Lovince Asimwe kiwanda kilianza ujenzi wake mwaka 1975 na kwamba kimegharimu dola za kimarekani milioni tatu na kilijengwa na Serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Alisema mwaka 2007 kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa mwekezaji Tripple S Beef Limited lakini kutoka na na matatizo ya uendeshaji kiwanda hicho kilifungwa mwaka 2017 na kukabidhiwa kwa Serikali.