MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB DK. CHARLES KIMEI ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA 2016

July 08, 2016



Dk. Charles Kimei akifurahia huduma za Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Habiba Kisaka akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB juu ya huduma wanazotoa.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB pamoja na maofisa wa benki hiyo.


Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Habiba Kisaka akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei alipotembela banda hilo.
Dk. Kimei akisaini kitabu cha wageni katika banda la LAPF.
Ofisa wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Lucia Chuwa akimkaribisha Dk. Kimei.

MZEE MALECELA AMUOMBA MKUU WA MKOA WA DODOMA KUFUFUA ZAO LA ZABIBU NA KUONDOA TATIZO LA NJAA KWENYE MKOA WA DODOMA

July 08, 2016

Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu Mzee John Samwel Malecela amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana kufufua zao la Zabibu Mkoani humo kwa kuzishughulikia changamoto zinazodidimiza kilimo cha zao hilo.

Mzee Malecela pia amemtaka Mheshimiwa Rugimbana kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Magufuli la kuondoa Tatizo la njaa Mkoani Dodoma kwa  kuzifuatilia skimu zote za kilimo zinazolegalega na zile zilizokosa uongozi imara.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki walipoambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana kwenye ziara ya kukagua skimu ya umwagiliaji ya zabibu ya Chinangali II yenye jumla ya ekari 1,250 iliyopo Chamwino ambayo kwa sasa inalegalega na kumtaka Mkuu wa Mkoa kuingilia kati kunusuru skimu hiyo inayokabiliwa na changamoto za kukosa uongozi imara na uendeshaji wa kilimo usio zingatia kanuni za kilimo bora.

Aliitaka serikali kusaidia wakulima wa chama cha CHABUMA wanaomiliki skimu hiyo ya zabibu ya Chinangali ili waweze kuanzisha kiwanda cha kusindika mchuzi wa zabibu na kusema kuwa kufanya hivyo kutawaepusha wakulima wa zabibu dhidi ya wafanyabiashara walanguzi wanaowalalia wakulima wakati wa mavuno ya zabibu.

Katika hatua nyingine, Mzee Malecela amemtaka Mheshimiwa Rugimbana kuondoa tatizo la njaa kwenye Mkoa wa Dodoma kwa kufufua skimu zote zilizokufa na zile zinazolegalega Mkoani hapa ili ziweze kuzalisha chakula na ametaka mkazo mkubwa uwekwe kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Mkoa wa Dodoma una maji mengi chini ya ardhi.

Amesema serikali inaingia gharama kubwa sana kuanzisha skimu za umwagiliaji lakini nyingi zinakosa ufuatiliaji na uongozi imara matokeo yake zinakufa akitolea mfano skimu ya Mgangalenga iliyopo Mpwayungu Chamwino yenye zaidi ya Ekari 20,000. Kwa mujibu wa Katibu Tawala msaidizi wa Uchumi na Uzalishaji Bi. Aziza Mumba amesema Mkoa wa Dodoma una skimu za umwagiliaji zipatazo mia tatu (300).

Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Rugimbana amekubali ushauri huo na kuahidi kuufanyia kazi kwakuwa agizo la kuondoa njaa ni moja ya maagizo aliyopewa na Mheshimiwa Rais Magufuli. Amesema kwanza atakua mlezi wa skimu ya zabibu ya Chinangali, na kuwa atafanya jitihada za kutafuta wafadhili kwa lengo la kuwezesha mradi wa kiwanda cha kusindika mchuzi wa zabibu.

Pamoja na   kutembelea skimu hiyo ya Chinangali, Mkuu wa Mkoa ameahidi atazitembelea skimu zote mia tatu (300) ili kubaini changamoto za kila skimu na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi ili zote ziweze kuzalisha kisasa na kusaidia katika jitihada za kuondoa tatizo la njaa.

Rugimbana amesema tayari ameshaunda kikosi kazi kwa ajili ya kushughulikia masuala ya uzalishaji katika miradi ya Kilimo na Mifugo na moja kati ya jukumu kubwa alilokipa kikosi kazi hiko ni kubaini changamoto za skimu hizi za umwagiliaji, kuhakikisha kinakua nazo karibu na kuzijengea uwezo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uongozi wa skimu hizo zote na uzalishaji kwa ujumla.
Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana wakisalimiana na Viongozi wa skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki.
Afisa Kilimo Wilaya ya Chamwino Ndg. Godfrey Mnyamale akiwasilisha taarifa ya mradi wa skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali II kwa mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mzee Malecela (hawapo pichani) wakati walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana (kushoto) changamoto zinazo didimiza kilimo cha Zabibu Dodoma na kumtaka kufanya kila awezalo kufufua zao hilo sambamba na kuondoa tatizo la njaa Dodoma wakati viongozi hao walipotembelea skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali II mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akiahidi kufufua zao la zabibu Mkoani humo na kuondoa tatizo la njaa kwa kufufua skimu zote za umwagiliaji zinazolegalega na kukosa uongozi imara wakati akizungumza na viongozi wa skimu ya umwagiliaji wa Zao la zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua mitambo ya kusukuma maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua miundombinu ya maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana wakikagua shamba la zabibu la Chinangali II Chamwino linalotumia teknolojia ya Umwagiliaji wa matone wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana jinsi tatizo la fangasi linavyoshambulia zao la zabibu wakati wakikagua shamba la zabibu la Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Sehemu ya Skimu ya zabibu ya Chinangali II iliyopo Chamwino inayotumia teknolojia ya umwagiliaji wa matone, kwa sasa skimu hiyo na nyingine baadhi Mkoani humu zinalegalega kutokana na kukabiliwa na Changamoto kadhaa wa kadhaa ambazo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kuzitafutia ufumbuzi.
Sehemu ya kitalu cha kuzalisha miche kwenye Skimu ya zabibu ya Chinangali II iliyopo Chamwino, kwa sasa skimu hiyo na nyingine baadhi Mkoani humu zinalegalega kutokana na kukabiliwa na Changamoto kadhaa wa kadhaa ambazo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kuzitafutia ufumbuzi.

RAIS MSTAAFU DK. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA NMB SABASABA

July 08, 2016
 Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa  (kushoto), akimkaribisha Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete  alipotembelea banda hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
 Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa  wafanyakazi wa benki hiyo.
 Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akitoa maelezo kwa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete (katikati), akitoka katika banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016  yanayoendelea katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo . Kulia ni Meneja wa banda hilo, Josephiner Kulwa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka. Maonesho hayo yatafikia tamati kesho kutwa.

MWENDA AISA JAMII KUSAIDIA WATOTOTO YATIMA NA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

July 08, 2016

Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akigawa chakula kwa watoto  wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam katika kusherekea sikukuu ya Iddi.

Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akijumuika pamoja katika chakula cha pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam .<!--[if gte mso 9]>

MILIMA YA RORYA MKOANI MARA

July 08, 2016
Na BMG
Ni muonekano wa milima ambayo inapatikana katika Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Mita chache Kutoka Mto Mara ukiwa unatoka au unaelekea wilayani Tarime, ukitokea maeneo mbalimbali katika barabara ya Musoma-Tarime.

Maajabu ya milima ambayo iko pande zote mbili za barabara si kwamba yanatisha, la hasha. Ni maajabu ambayo ni ya kufurahisha kiukweli hususani ukiwa safarini ambapo ukiitazama utaona namna inavyorudi nyumba na kufanya abiria kuhisi uumbaji wa Mungu uliotukuka katika hii dunia.

Ujenzi wa barabara iliyopinda mithiri ya nyoka katikakati ya milima hii huifanya kuwa kivutio kingine japo kwa abiria waoga wakifika katika milima hii sara huwa inaongezeka maana si mchezo hususani likija suala la mpando huwa ni mpando kweli, na likija suala la mtelemko huwa ni mtelemko kweli kwani ikiwa wewe ni muoga basi huweza hata chungulia nje japo ukweli ni kwamba ukichungulia nje utaona uzuri wa kipekee katika milima hiyo.

Kikubwa tunaomba shughuli za kibidanamu zisiiathiri milima hii (mfano katika picha) maana ni tegemeo kwa wanamara na sote twajua umuhimu wa milima kama hii ambayo ina uwepo mkubwa wa mistu ya asili.
Tazama HAPA Picha Zaidi

WASHINDI WANNE WANYAKUA ZAWADI KATIKA KAMPENI YA FAIDIKA NA AMANA BANK

July 08, 2016

Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi,Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo .
Zawadi ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE (Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo. 
Mshindi wa nne amepata zawadi ya Table Feni ya kisasa yenye AC pia.Pichani ni Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi Bwana HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya Faidika na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi za kitanzania Million Tano 

Katika kuadhimisha kilele cha kampeni ya FAIDIKA NA AMANA BANK,Bank imezawadiwa wateja wake waliobahatiika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao na Benk hiyo leo siku ya kilele cha maonyesho ya saba saba Tarehe 7/7/2016.

Wateja hao walichaguliwa kitaalam katika droo iliyochezeshwa ndani ya viwanja vya saba saba katika banda la amana bank na kupewa taarifa ya kufika kupokea zawadi zao kutoka uongozi mkuu wa bank hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji DR MUHSIN SALIM MASOUD.

Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti za akiba binafsi kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za vifaa vya matumizi ya nyumbani kama Luninga,Jokofu,Microwevu,Pamoja na Table Feni yenye AC Pia.
Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa 
Akizungumza na wanahabari mapema leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo kwa washindi hao meneja masoko wa Bank hiyo Ndugu DASSU MUSSA amesema kuwa bank ya amana imejipanga kuendelea kuwafikia na kuwapatia watanzania wote huduma bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao mbalimbali,huDuma pia ambazo zinafwata misingi ya sheria ya kiislamili kuwapatia faida iliyo halali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.

Aidha amewahamasisha watanzania wote kujijiengea na kudumisha utamaduni wa kujiwekea akiba ya pesa kwa ajili ya malengo mbalimbali katika benk ya amana ili wapate kufurahia huduma bora zitowelewazo kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.
Meneja masoko wa Bank ya Amana Ndugu DASSU MUSSA akifafanua jambo kwa wanahabari ambao walifika kushughudia Utoaji wa zawadi hizo katika Banda lao lililopo katika maonyesho ya saba saba ambayo ndiyo yanaelekea ukingoni 

Ameongeza kuwa kampeni ya faidika na amana bank ni mwanzo tu wa kampeni za bank hiyo zitakazohusisha wateja kuweka fedha na kujishindia zawadi mbalimbali kutoka amana bank ukiachia faida nyingine zipatikanazo kwa wateja kujiwekea akiba huku akisema kuwa wanatarajia kutangaza kampeni nyingine kubwa itakayowezesha wateja wengiine Zaidi kujishindia zawadi lukuki kutokana na kujiwekea utaratibu wa kuweka akiba zao amana Bank Bank ambayo inafwata misingi ya kiislam kikamilifu.
Zawadi ambazo zimetolea kwa washindina Bank ya Amana ambazo jumla zimegharimu kiasi cha shilingi million Tano 

Aidha akiwahamasisha watanzania kujiunga na Bank hiyo amesema kuwa watanzania wengi wamekuwa wakidhani Bank hiyo ni kwa ajili ya waislam jambo ambalo sio kweli huku akitanabaisha kuwa Bank hiyo inahusisha wateja wa Dini zote bila kubagua hivyo watanzania wajiunge kwa wingi katika Bank hiyo,

Washindi waliojishindia zawadi mbalimbali katika hitimisho la Kampeni hiyo ya Faidika na Amana Bank ni pamoja na Pikira Nlongane aliyejishindia zawadi ya Televission kwa kuwa mshindi wa kwanza,Shakira Ibrahim aliyeshika nafasi ya pili na kujishindia zawadi ya Friji kubwa,Khamis Said aliyejishindia Microwave huku mshindi wa nne akiwa ni Hemed Suleiman aliyejishindia Table Feni katika droo hiyo.
Picha ya Pamoja maafisa wa Bank ya amana wakiwa na washindi wa Zawadi mbalimbali za kampeni ya Faidika na Amana Bank mara baada ya utoaji wa zawadi hizo katika maonyesho ya Saba saba 

Bank ya amana ni bank inayoongozwa kwa ustadi mkubwa na misingi ya Dini ya kiislam huku ikiwahudumia watanzania wapatao Elfu 34 katika matawi yake saba nchi nzima hadi sasa.

MKURUGENZI MKUU WA PSPF, ADAM MAYINGU ATEMBELEA BANDA LA SIDO KUJIONEA SHUGHULI ZA VIWANDA, PIA ATEMBELEA MABANDA MENGINE YA WASHIRIKA

July 08, 2016

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakitazama gari Kaparata kwenye banda la Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Gari hilo limebuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob Luis, wa Kaparata Engineering.
 Mbunifu wa gari hilo, Jacob Luis, akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu ubunifu huo
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, ametembelea banda la Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 yanayoendelea pale viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mayingu alitembelea banda hilo ili kujionea na kupata maelezo ya kina jinsi shirika hilo linavyoendeleza viwanda vidogovidogo ambavyo vinahitajika sana kwa sasa ukizingatia mkakati mkubwa wa serikali ya awamu ya Tano ambayo iemdhamiria kuifanya bTanzania kwua nchi ya viwanda na hivyo kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania.
Mkurugenzi Mkuu huyo amabye alifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alipokelewa na Msimamizi Mkuu wa banda hilo, Kalumuna Benedicto, na alitembezwa maeneo mbalimbali na kujionea mashine mbalimbali zilizobuniwa na kutengenezwa na watanzania.
Pia alipata fursa ya kujionea gari lililobuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob Luis, wa Kaparata Engineering.
Gari hilo lina injini yenye ukubwa wa CC 900 na linatumia mafuta ya petrol, likitumia lita moja ya petrol kwa kilomita 15 na linabeba watu watano na mzigo wa kilo 500.
Kwa mujibu wa maelezo ya mbunifu Jacob Luis, gari hilo ni maalum kwa shughuli za shamba, kubeba maharusi, shughuli za kijeshi, polisi na zile za kiulinzi.
Mkurugenzi huyo pia alitembelea mabanda washirika wa PSPF, likiwemo lile linalokusanya wajasiriamali wanawake kutoka nchi nzima ikiwemo Zanzibar, hali kadhalika Mkurugenzi Mkuu huyo alitembelea Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF, LAPF, GEPF NA PPF.
 Maelezo kuhusu gari Kaparata
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati akikagua mashine zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda hilo la SIDO
 Muangalizi Mkuu wa banda la SIDO, Kalumuna Benedicto, (kushoto), akimpatia maelezo, Mkurugenzi Mkuu Mayingu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi kuhusu mashine hizi
  Muangalizi Mkuu wa banda la SIDO, Kalumuna Benedicto, (kushoto), akimpatia maelezo, Mkurugenzi Mkuu Mayingu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi kuhusu mashine hizi
 Mayingu akizungumza jambo mbele ya wafanyakazi wa WCF, wakiongozwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi, Fulgence Sebera, (watatu kulia) wakati akitembelea banda la Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF)
 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), akimpatia maelezo ya kiutendaji ya Mfuko huo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, alipotembelea banda la PPF akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akitembelea banda la NSSF
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akiangalia bidhaa zinazozalishwa na mjasiriamali huyu kutoka mkoani Dodoma
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu akipata amelezo kutoka kwa mjasiriamali wa mkoa wa Manyara
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF akitembelea banda la LAPF
 Mayingu akitembelea banda la wajasiriamali kutoka Kigoma lililoko kwenye jengo la EOTF
Mkurugenzi Muu Mayingu (wapili kulia), akitembelea banda la GEPF kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango