Tunafuatilia kwa umakini mkubwa

May 15, 2013
WAANDISHI wa habari nguli kutoka Kampuni ya Mwananchi Comunication Limited (MCL) kushoto ni Paskal Mbunga wa gazeti la Citizen na Salum Mohamed wa Mwananchi,Picha na Oscar Assenga,Tanga.

Nauliza hivi

May 15, 2013
MWANDISHI wa gazeti la Habari leo mkoa wa Tanga,Anna Makange akisisitiza jambo kwenye semina hiyo kulia kwake ni Mwanachama cha Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Tanga(Tanga Presse Club)Augustino Karia picha na mwandishi wetu.

Tupo makini na semina

May 15, 2013
MWANDISHI Mwandamizi wa Gazeti la Mtanzania mkoa wa Tanga,Sussan Uhinga akifuatilia kwa umakini semina elekezi mapema hii leo kushoto kwake ni mwandishi wa kituo cha Radio huruma jijini Tanga,Peter Mtulia nae aifuatilia.

Tunasikiliza kwa umakini

May 15, 2013
KATIBU wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Tanga,Lulu George akifuatilia semina hiyo leo.

Maelekezo ya Semina elekezi leo kwa waandishi wa habari Tanga.

May 15, 2013
MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga(Tanga Press Club)Hassani Hashim akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kuhusu uchangiaji wa damu iliyofanyika katika ukumbi wa chama hicho,kushoto kwake ni Mratibu  wa huduma za maabara mkoa wa Tanga,Mussa Juma Kayanda na kulia kwake ni katibu mkuu wa chama hicho Lulu George,Picha na Mwandishi Wetu.
Bombo yakabiliwa na upungufu wa damu.

Bombo yakabiliwa na upungufu wa damu.

May 15, 2013

Na Mbonea Herman Tanga.

HOSPITALI ya Mkoa wa Tanga Bombo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu jambo ambalo linaweza kuchangia kuongezeka kwa vifo vya wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika hospitali hiyo.

Kufuatia jambo hilo,Club ya waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga(TPC)imeamua kufanya kampeini ya kuwahamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiari.

Mratibu wa Huduma za Maabara Mkoa wa Tanga,Mussa Juma alisema kwamba uhitaji wa hospitali hiyo ni Unit 15 kwa siku wakati wanapatiwa wakati mwingine Unity ishirini kwa wiki kiwango ambacho hakilingani na mahitaji.

“Sisi tunapokea mgawo wa damu kutoka kituo cha kanda ya hospitali ya rufaa KCMC kiwango hicho ni kidogo lakini haya yote yanatoana na uhaba wa damu uliopo katika kituo hicho,”alisema Juma.

Juma alisema kama wananchi wangejengewa utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari taifa lingeweza kuondokana na tatizo hilo ambalo kwa sasa linaonekana kugharimu maisha ya watanzania waliowengi.

Juma alisema pia kwamba kitendo cha hospitali kutegemea vituo vya damu salama vya kanda kinachangia upatikanaji mgumu wa damu katika hospitali zile ambazo zipo mbali na kituo hicho.

Aidha Mratibu huyo alishauri kuwa na vituo vya damu salama ngazi ya Mkoa ili kuondokana na adha ya kuifuata damu umbali mrefu wakati yupo mgonjwa mahututi nayehitaji huduma hiyo kwa haraka.

Akizungumzia uhaba wa damu nchini Mwenyekiti wa (TPC)Hassan Hashim alisema katika kukabiliana na swala hilo waandishi wa habari watajikita katika kuihamasicha jamii kupitia vyombo vyao kama sehemu ya kumaliza tatizo hilo,

Naye Katibu wa Club hiyo Lulu George alisema kazi hiyo itaanza May 21 mwaka huu katika Wilaya za Moa wa Tanga.

MWISHO.