RAIS KIKWETE AMPONGEZA RAIS MTEULE DKT JOHN POMBE MAGUFULI, MAMA ANNA MGHWIRA WA ACT WAZALENZO ATUMA SALAMU ZA PONGEZI

RAIS KIKWETE AMPONGEZA RAIS MTEULE DKT JOHN POMBE MAGUFULI, MAMA ANNA MGHWIRA WA ACT WAZALENZO ATUMA SALAMU ZA PONGEZI

October 29, 2015

ma1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015
mag2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsomea sms za pongezi kutoka kila pembe ya dunia  mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015
mag3
Mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea salamu za pongezi kutoka kwa mgombea Urais Mwanamke Pekee kwa tiketi ya ACT Wazlendo Mama Anna Mghwira mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza rasmi  matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni. Dkt Magufuli amemshukur sana Mama Mghwira na kumwita mkomavu wa siasa na mwana-Demokrasia wa mfano jioni hii Oktoba 29, 2015
mag4
mag5 mag6 mag7 mag8
Mama Salma Kikwete akimpongeza mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tais kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni 
jioni hii Oktoba 29, 2015
mag10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015
Picha na IKULU
Safu mpya ya Makatibu na Naibu Makatibu wakuu Nishati na Madini yakabidhiwa ofisi

Safu mpya ya Makatibu na Naibu Makatibu wakuu Nishati na Madini yakabidhiwa ofisi

October 29, 2015

ch1
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (kulia), akibadilishana Nyaraka za Makabidhiano na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo (Kushoto). Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
ch2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo (Kushoto), akisaini Nyaraka za Makabidhiano sambamba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
ch6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo (kulia) akipokea Shada la maua kutoka kwa Mary Mkwaya Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, mara baada yakuwasili wizarani. Wanaoshuhudia nyuma ni Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja na Mkurugenzi wa Utawalana RasilimaliWatu, Mrimia Mchomvu.
ch5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) akipokea shada la maua kutoka kwa Cecilia Mrope Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
ch4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo, akiongea jambo na Wajumbe wa Menejimnenti wa Wizara baada ya kuwasili wizarani hapo. Katibu Mkuu alitumia kikaohicho kuwaeleza wajumbe masuala muhimu ambayo atayasimamia kikamilifu katika sekta za Nishati na Madini.
ch3
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akimpongeza, aliyekuwa Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
…………………………………………………………………………….
  • Makatibu wapya wataja vipaumbele
  • Kuzingatia 4Us, Uendelezaji Wachimbaji Wadogo
Teresia Mhagama na Asteria Muhozya
Katibu Mkuu mpya na Naibu Katibu Mkuu  walioteuliwa kuiongoza Wizara ya Nishati na Madini wameanza majukumu yao na kusisitiza watumishi wa Wizara na Taasisi zake kuzingatia Uadilifu, Ubunifu, Uwajibikaji, na Uwazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wakizungumza  na wajumbe  wa menejimenti ya Wizara ya Nishati na Madini, viongozi hao walisisitiza  baadhi ya masuala yatakuwa  kipaumbele  kuwa ni uwepo wa umeme wa uhakika na bei nafuu ili wananchi watumie nishati hiyo kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Vipaumbele vingine ni kuongeza mchango wa sekta madini katika pato la Taifa, uwepo wa kiwanda cha kusindika gesi asilia, na suala la uwezeshaji wazawa (Local Content) katika sekta za Nishati na Madini.
Vilevile, vipaumbele vingine ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanasaidiwa katika masuala ya fedha na utaalam na kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi.
Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo, pamoja na kumshukuru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa, alitoa wito wa ushirikiano kati ya uongozi huo mpya na wafanyakazi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja pamoja na kuainisha vipaumbele mbalimbali  vya utekelezaji amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete kwa kumteua kushika nafasi hiyo   na kueleza kuwa, imetokana na kuridhika na utendaji wake wa kazi wakati aliposhika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kuwa Kamishna wa Madini nchini.
Alitoa wito kwa wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini kutoa ushirikiano kwa uongozi huo ili kwa pamoja waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katka uendelezaji wa sekta za Nishati na Madini.
Kabla ya kukabidhi nyaraka za makabidhiano, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi  ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, aliwashukuru watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa ushirikiano waliompa wakati wa kipindi cha uongozi wake na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya.
Vilevile, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, aliwaasa Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana, kuzingatia taratibu, sheria na kanuni, kuzingatia muda na kuimarisha mawasiliano.
Kabla ya kushika nyadhifa hizi Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Manyara na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja alikuwa Kamishna wa Madini nchini.
JAJI DAMIAN LUBUVA AMTANGAZA DK.JOHN POMBE MAGUFULI KUWA RAIS MTEULE WA KITI CHA URAIS TANZANIA

JAJI DAMIAN LUBUVA AMTANGAZA DK.JOHN POMBE MAGUFULI KUWA RAIS MTEULE WA KITI CHA URAIS TANZANIA

October 29, 2015

????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akifafanua baadhi ya mambo mapema leo jioni  kabla ya mawakala wa vyama kusaini fomu namba 27 iliyosainiwa na mawakala wa vyama vya siasa  baada ya majumuisho ya kura kwa wagombea urais kabla ya kutangaza rais mteule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo Dk. John Pombe Magufuli ametangazwa mshindi kwa kura  kura 8.882.935 sawa na asilimia 58.46 huku mpinzania wake kutoka Umoja wa Vyama vya  Upinzani kupitia chama cha Chadema Edwald Lowasa akipata kura 6.072.848 sawa na asilimia 39.97.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akisaini fomu namba 27 mara baada ya mawakala wa vyama vya siasa kusaini kabla ya kumtangaza rasmi rais mteule kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam leo ambapo Dk. John Pombe Magufuli ametangazwa kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi wa Tume hiyo Ndugu Kailima Ramadhan na kushoto ni Jaji Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi 
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM nakala ya fomu namba 27 ambayo mawakala wa vyama wamesaini mara baada ya kukamilisha majumuisho ya kura za wagombea urais kabla ya kutangaza matokeo mapema leo katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  Jaji Mstaafu Hamid Mahmod.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akitangaza matokeo hayo kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya mawakala na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa waliohudhuria kushuhudia matangazo hayo yaliyokuwa yakitolewa na tume ya uchaguzi ya taifa leo kwenye ukumbi wa kimataifa wa JNICC jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Maofisa mbalimbali wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na serikali wakifuatilia matangazo hayo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na wageni mbalimbali wa ndani na nje waliohudhuria ili kushuhudia Rais mteule akitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
????????????????????????????????????
Assa Mwambene Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Mhariri  Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSM Gabriel Nderumaki wakijadili jambo wakati wakisubiri kuanza kwa utiaji saini kwa mawakala wa vyama vya siasa kwenye fomu namba 27 kabla ya kutangaza matokeo ya jumla ya wagombea urais wa Tanzania.
????????????????????????????????????
Baadhi ya mawakala wakipitia fomu namba 25 na 26 kabla ya kusaini fomu namba 27.
????????????????????????????????????
Baadhi ya mawakala wakisaini fomu hizo.

KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET KUISAFIRISHA TIMU YA TAIFA STARS KWENDA ALGERIA

October 29, 2015

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu ya taifa Taifa Stars kwenda nchini, Algeria kwa mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu.
Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu hiyo kwenda nchini Algeria kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedhamini safari hiyo kwa kutoa ndege yake kwa kwenda na kurudi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati na Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.
 Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kudhamini timu ya Taifa Stars kwenda na kurudi  nchini Algeria kwa ndege yake kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda na Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie. 
 Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Dotto Mwaibale KAMPUNI ya Ndege ya Fastjet imetoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha timu ya Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wake na timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi  Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alisema hatua ya kuisaidia timu hiyo ni mwanzotu wa ushirikiano baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
“Kampuni yetu imeanza ushirikiano na TFF katika kukuza michezo nchini na ndio maana tumeanza kuwasafirisha wachezaji hao kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo huo” alisema Kibati
Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda alisema safari ya kwenda nchini humo itakuwa Novemba 16 na kuwa mchezo huo utafanyika Novemba 17.
Alisema gharama za kusafiri na timu hiyo kwa mtu atakayependa kusafiri ni dola 800 kati ya hizo dola 640 ni kwa ajili ya safari na 60 ni malipo ya kodi ya uwanja wa ndege hapa nchini na Algeria.
Alisema safari hiyo itaanza asubuhi na kuwa ndege hiyo watakayosafiri nayo inabeba abiria zaidi ya 150.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)