TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

April 14, 2015


Ktff_LOGO1 
AMATI YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI YA BODI YA LIGI
Kocha Jackson Mayanja wa Kagera Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kutoa lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi yao na Mtibwa Sugar kuwa walipewa rushwa.
Adhabu dhidi ya Kocha Mayanja kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu.
Klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa kuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand United iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.  Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.
Nayo Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar. Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao.
Pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.
Kipa Tony Kavishe wa Polisi Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani kwa kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
KAMATI YA MASHINDANO TFF
Kamati ya Mashindano ya TFF ilikutana jana kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) pamoja na taarifa ya Ligi Daraja la Pili (SDL) iliyomalizika hivi karibuni.
Katika matukio ya SDL, Kamati imeipiga faini ya sh. 300,000 timu ya JKT Rwamkoma ya Mara kwa kusababisha mechi yake dhidi ya AFC ya Arusha kuvurugika. Adhabu hiyo kwa mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya Ligi Daraja la Pili.
Nao makocha wa JKT Rwamkoma, Hassan Makame na Kamara Kadede wamepigwa faini ya sh. 200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi sita kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi namba moja katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 9, 2015.
Wachezaji Shafii Maganga, Saleh Ali, Ismail Salim na Mussa Senyange wa JKT Rwamkoma ambao wanatuhumiwa kwa kushambulia mwamuzi kwenye mechi hiyo suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.
VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja viwili nchini, jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.
TTF YAFUNGUA SEMINA YA WAAMUZI VIJANA
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana wenye umri wa miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.
Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha vijana 27 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa kimataifa baadae.
Vijana hawa mnaowaona hapa wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana nchini, wakikua na kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini kwa sababu watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa habari kabla ya kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.
Mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA barani Afrika, nyuma ya Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda vijana wengi waje kuwa waamuzi wa kimataifa.
Semina hiyo ya siku 5 inatarajiwa kufungwa ijumaa tarehe  17 Mei, 2015 inajumuisha vijana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya, kati ya vijana 37 waamuzi wawili ni wanawake.
Wakufunzi wa semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.
TAMISEMI yatoa ufafanuzi uhaba wa vyakula mashuleni

TAMISEMI yatoa ufafanuzi uhaba wa vyakula mashuleni

April 14, 2015

1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari  (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu baadhi ya Shule za Sekondari za Bweni zilizofungwa kutokana na ukosefu wa chakula ambapo alisema shule hizo zimefungwa kimakosa kwani Serikali imeshapeleka fedha za kununulia chakula kwenye halmashauri zote nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba.
2
Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam mpango wa Serikali kuajiri waalimu wa shule za msingi wenye elimu ngazi ya Stashahada badala ya Cheti kama ilivyo sasa. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
4
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini wakati wa mkutano uliofanyika leo kwenye ofisi za TAMISEMI jijini Dar es Salaam.
Picha na Fatma Salum (MAELEZO)

DC KINONDONI AUNDA TUME HURU KUCHUNGUZA UBOVU WA BARABARA

April 14, 2015

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, kuhusu tume aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza ubovu wa barabara katika wilaya hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………………….
 
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ameunda tume ya wajumbe saba wakiwamo wawili kutoka serikalini kwa ajili ya kuchunguza ubovu wa barabara katika wilaya hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana Makonda amesema amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia ubovu wa barabara katika wilaya ya Kinondoni kuwa zinajengwa chini ya kiwango. Alisema wananchi hao wanasema barabara hizo zinajengwa chini ya kiwango kwani lami inawekwa leo lakini haimalizi miezi sita inabanduka na kuacha mashimo ambayo yamekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa barabara ndani ya wilaya hiyo.
Makonda alisema katika wilaya hiyo barabara nyingi mitaro yake haipitishi maji kama inavyotakiwa, mitaro mingine imechimbwa mifupi kuliko mahitaji halisi, barabara kujengwa nyembamba kutoka kushoto kwenda kulia bna kuwa ujenzi wa barabara hizo hauendani na kasi ya mahitaji na kukua kwa mji.
Alisema kutokana na hali hiyo kwa kuwa si mtaalamu wa masuala ya barabara ameamua kuunda tume huru ya wataalamu itakayojumuisha wasanifu, wahandisi, wataalamu wa mikataba, ugavi na manunuzi na watu wengine kutoka vyombo mbalimbali ili wachunguze.
“Tume hii na vyombo hivyo vingine tumevipatia kazi ya kuchunguza usanifu wa barabara kama unazingatia viwango, taratibu za manunuzi na kutoa tenda kama zinazingatiwa, wakandarasi wetu wazalendo kama wanawajibika ipasavyo au kuna njama yoyote inafanywa ili kuhujumu kazi waliyopewa na kama wahandisi wetu wanatimiza wajibu wao ipasavyo kamtika mchakato mzima wa usanifu na ujenzi ili kuhakikisha ubora wa barabara unafikiwa” alisema Makonda.
Makonda alisema Tume hiyo itafanyafakazi kwa siku 21 kuanzia kesho Aprili 15 mwaka huu na kukabidhi ripoti yake ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari Mei 5 mwaka huu saa 5 asubuhi na kuwa matokea ya ripoti hiyo ndiyo yatakayotoa majibu ya kupanua wigo wa uchunguzi kwenye kandarasi nyingine za ujenzi wa shule za serikali, ofisi za umma za wilaya hiyo.
Wajumbe wanaounda tume hiyo ni Mhandisi Julius Mamilo ambaye atakuwa mwenyekiti , Mhandisi Ronald Rwakatare (Katibu), John Malisa, Abednego Lyaga, Mhandisi Patrick Balozi na wajumbe wengine wawili kutoka vyombo vingine vya serikali vinavyoshughulikia uchunguzi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

WANAFUNZI WA CARMAN AINSWORTH HIGH SCHOOL WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.

April 14, 2015


 Wanafunzi wa Carman Ainsworth High School iliyopo Michigan watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC, na kupata fursa ya kuonana na Mhe balozi Liberata Mulamula.
                      Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mhe, balozi Leberata Mulamula.
                             Mhe, balozi Liberata Mulamula akitoa historia fupi ya Tanzania.
                      Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wageni wake kwa kuchagua ubalozi wa Tanzania kama sehemu mojawapo ya ziara yao hapa mjini Washington DC.