Waziri Mwigulu atoa hoja ya kuidhinishiwa kwa bajeti ya 2016/2017 mbele ya mwalimu wake wa darasa la kwanza.

Waziri Mwigulu atoa hoja ya kuidhinishiwa kwa bajeti ya 2016/2017 mbele ya mwalimu wake wa darasa la kwanza.

May 05, 2016

mw1 
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akitoa hoja kwa Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma huku akishudiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo (hayupo pichani) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)
mw4 
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wake Maria Mnkumbo (katikati) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma.  Kushoto ni mke wa Waziri Mwigulu Neema.
mw2 
Mwalimu msataafu Maria Mnkumbo aliyemfundisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
mw3 
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma.
MATUKIO YA BUNGE LINAENDELEA MJINI DODOMA

MATUKIO YA BUNGE LINAENDELEA MJINI DODOMA

May 05, 2016


1 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo yanayoulizwa na Wabunge leo mjini Dodoma.
2 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akiingia kwenye ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
3 
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwasili viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma
4
5 
Wabunge wakiwasili viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi-MALEZO, Dodoma)

TANAPA KUBADILI MFUMO WA UTENDAJI KAZI KUTOKA KIRAIA KUWA JESHI USU.

May 05, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi (kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuelkea katika uwanja wa Mafunzo katika kambi ya Mlele kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Wahifadhi na Askari wapya waajiriwa wa shirika hilo .
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati akipokea salamu za heshima wakati wa gwaride maalumu la ufungaji wa mafunzo ya awamu ya  mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride la heshima la askari wapya na Wahifadhi waliohitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani)  kwa mwendo wa pole na kutoa heshima wakati  ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa jeshi usu kwa Wahifadhi 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati gwarde likipita mbele ya jukwaa na kutoa heshima,wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori ,Martin Loibooki,Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu,Raphael Muhuga,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Allan Kijazi,Kaimu Mkurugenzi idara ya Wanyama pori,Ndugu Karamaga.
Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani)  kwa mwendo wa haraka wakati  ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi 
Askari wapya waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha umahiri katika kutumia silaha wakati wa kukabiliana na majangili mara baada ya kupata mafunzo hayo katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi. 
Baaadhi ya Wahifadhi Waandamizi na Wafawidhi wakiwa wameshika silaha mara baada ya kupatiwa Mafunzo katika Kambi ya Mlele ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kwenda Jeshi Usu. 
Askari wa Hifadhi akionesha umahiri katika matumizi ya silaha kwa kulenga shabaha wakati wa kuhitimu mafunzo ya  awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo  wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi
Baadhi ya Viongozi na Wageni katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na askari waajiriwa wakifuatilia maonesho yaliyokuwa yakifanywa na wahitimu hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (kulia) akiratibu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .kushoto ni Mkuu wa Mafunzo ,Genes Shayo .
Mhifadhi Sekela Mwangota akisoma risala  ya Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya Mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori,Martin Loibooki akizungumza wakati wa hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .
Baadhi ya Wahitimu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati waa hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Muhuga akizungumza hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa ambapo amegusia juu ya changamoto iliyopo kwa Wafugaji kuingiza Mifugo yao katika Hifadhi pamoja na mapori ya Akiba.
Katibu Mkuu ,Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitoa hotuba yake ya kuhitimisha Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA),Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Baadhi ya Askari Waliohitimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi za Taifa(TANAPA) yaliyofanyika kambi ya mafunzo Mlele mkoani Katavi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko Katavi.

WATOTO OMBAOMBA JIJINI MWANZA WABUNI NJIA YA KUJIPATIA KIPATO.

May 05, 2016
Watoto wanaoishi Mitaani Jijini Mwanza wakiwa katika shughuli ya kufuta magari na kuomba pesa.

AFISA MTENDAJI MKUU DAWASCO AIBUKA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA KITAIFA.

May 05, 2016
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) Mhandisi Cyprian Luhemeja akipokea zawadi ya shilingi milioni 3.5 kutoka kwa Rais wa  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. John Magufuli baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka kitaifa kwenye siku ya Wafanyakazi Dunia, Mei mosi iliyoadhimishwa  kitaifa mkoani Dodoma.

AFISA MTENDAJI MKUU DAWASCO AIBUKA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA KITAIFA.

May 05, 2016
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) Mhandisi Cyprian Luhemeja akipokea zawadi ya shilingi milioni 3.5 kutoka kwa Rais wa  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. John Magufuli baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka kitaifa kwenye siku ya Wafanyakazi Dunia, Mei mosi iliyoadhimishwa  kitaifa mkoani Dodoma.