Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais, Ikulu Bw. Peter Ilomo amewashauri watanzania
kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
ili kujiongezea kipato na hatimaye kuishi ya staha.
Bw.
Ilomo alisema hayo Mjini Bagamoyo wakati wa semina iliyoandaliwa na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa ajili ya Maafisa Rasilimali Watu kutoka
wakala mbalimbali za Serikali
Kutokana
na mabadiliko kwenye sekta ya hifadhi ya jamii, PSPF ilianzisha Mpango
wa Uchangiaji wa Hiari maarufu kama PSS ili kuweza kuwahudumia
Watanzania wote ambao wanahitaji huduma za hifadhi ya jamii ambao
walikosa fursa hiyo huko nyuma.
“Mpango
huu ni mkombozi kwani unazidi kukuongezea kipato na kukufanya uishi
maisha yenye staha sasa na hata wakati wa ustaafu wako. Mpango huu pia
unatoa ruksa kwa mtu asiye raia wa Tanzania lakini anafanyakazi hapa
nchini kihalali kuwa mwanachama” alisema Bw. Ilomo.
Akizungumzia
juu ya ujio ya kanuni moja ya ukokotoaji wa mafao, Bw. Ilomo alisema,
“Kuwepo kwa kanuni moja ya ukokotoaji mafao ni changamoto kwa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii, kwa kuwa kigezo kikubwa cha kuvutia wanachama
kitakuwa ni ubora katika huduma na mafao ya muda mfupi. Hivyo, nawaagiza
watendaji wote wa PSPF kuhakikisha mnatumia vyema fursa hii kutoa elimu
sahihi kwa watendaji hawa muhimu katika utumishi wa umma hapa nchini”.
Kutokana
na Wizara ya Kazi na Ajira kutangaza kuwa Mifuko yote ya Hifadhi ya
itakuwa ikitoa mafao yanayolingana, alisema wanachama wa PSPF
waliokuwepo hadi tarehe 30/6/2014 watalipwa kwa utaratibu wa zamani na
wote walioajiriwa kuanzia Julai 1, 2014 watalipwa mafao yao kwa mujibu
wa kanuni mpya.
Katibu
Mkuu huyo kutoka ofisi ya Rais aliipongeza PSPF kwa kuandaa semina hiyo
na kuongeza, “ Semina hizi ni muhimu kwani zinatoa fursa ya kuonana na
wadau na kutoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwa manufaa ya Mfuko
na wanachama wake”.
Awali
akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu
aliwahakikishia washiriki wote wa semina hiyo kwamba PSPF itahakikisha
inafikia dira yeke ambayo ni kuwa mtoa huduma bora wa hifadhi ya jamii
nchini, na kufanyakazi kwa mujibu wa dhima ya Mfuko ambayo ni kutoa
huduma zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wateja wake
kwa kutumia watumishi wenye ari ya kazi na teknolojia inayofaa.
Katika
kuhakikisha inafikia dira yake na kuishi dhima yake, Bw. Mayingu
aliahidi kwamba PSPF itaendelea kutekeleza majukumu yetu ya utendaji wa
kila siku ikiongozwa na uwajibikaji, wajibu, muitikio, nidhamu, juhudi,
uwazi na unyenyekevu kwa wote.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizunfumza wakati wa
semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa maafisa rasilimali
watu kutoka wakala za serikali iliyofanyika mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Alhamisi Oktoba 16, 2014.
Katibu
Mkuu Ikulu,Peter Ilomo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Semina ya siku moja
iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa maafisa rasilimali watu
huko Bagamoyo mkoani Pwani, Alhamisi Oktoba 16, 2014. Warsha hiyo
ililenga kuwapatia elimu waajiri kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na
Mfuko huo kwa wanachama wake.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo, akizungumza.
Washiriki
wa semina wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na
wataalam wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kuhusu huduma mbalimbali
zitolewazo na Mfuko huo kwa wanachama wake, Semina hiyo ilifanyika mjini
Bagamoyo Alhamisi Oktoba 16, 2014.
Katibu
Mkuu Ikulu, Peter Ilomo, (Kulia), akiongozana na Mkurugenzi wa
Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gabriel Silayo, wakati wa
mapumziko ya chai baada ya kufungua semina ya siku moja iliyoandaliwa na
Mfuko huo kwa maafisa rtasilimali watu huko Bagamoyo mkoani Pwani,
Alhamisi Oktoba 16, 2014.