TANESCO KUWABANA WAWEKEZAJI WABABAISHAJI
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
WIZARA ya Nishati na Madini imesema itahakikisha haitoi mwanya kwa
wawezezaji wababaishaji wanaotaka kuwekeza kwenye nishati ya umeme na
kuwaingiza Watanzania kwenye mgawo wa umeme bila sababu.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi, alitoa kauli hiyo wakati
wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama cha wafanyakazi, TUICO matawi ya
Shirika la Umeme (Tanesco) na viongozi wa wizara.
Alisema asilimia 24 ya Watanzania zaidi ya milion 44 ndio
waliounganishwa na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali vijijini na
mijini.
Maswi alisema kiwango hicho kinaonyesha kwamba kuna watanzania wengi wanaotumia mkaa na kuharibu mazingira nchini.
Kwa sababu hiyo idadi serikali kupitia sekta ndogo ya nishati ya
umeme inadhaniria kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme hadi kufikia
asilimia 50 ifikapo mwaka 2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felichesmi Mramba, alisema
shirika hilo limeanza kufanya vizuri huku akisema ifikapo mwaka 2033
asilimia 75 ya Watanzania watanufaika na huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, alisema mkoa huo
umedhamiria kuinua pato la mtu mmoja mmoja, hivyo anaamini kwamba
kupitia umeme Watanzania wengi watanufaika na huduma bora za shirika
hilo
Chanzo;Tanzania Daima
*MREMBO BORA WA KANDA YA MASHARIKI KUPATIKANA AGOSTI 8 MJINI MOROGORO
Baadhi ya warembo washiriki wa shindano la Miss Kanda Mashariki wakiwa katika pozi,wakati wa mazoezi yao ya maandalizi.
Na Mwandishi Wetu
Mashindano
ya kumsaka mrembo kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014)
yatafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwanue ukumbi wa Nashera Hotel, mkoani Morogoro.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14
kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa
Morogoro chini ya udhamini wa Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari
Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC
Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na
Clouds FM.
Mratibu wa masindano hayo, Alex Nikitas aliwataja warembo watakaoshindana siku hiyo kuwa ni Lucy Julius Diu, Prisca Mengi, Tarchisia Noback Mtui na Angel Shio ambao wanatoka Morogoro.
Warembo wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian Andrew na Leila Abdul Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo kutoka Mtwara ni Nidah Fred Katunzi, Lightness Mziray na Nelabo Emmanuel.
Pia warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary Mpelo
na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa warembo hao watakuwa kambini
kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss
Kanda ya mashariki mwaka jana, Diana Laizer.
RAIS KIKWETE AKAGUA KILIMO CHA KAHAWA MBINGA LEO.
Meneja
wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam
Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche
bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua
shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani
Ruvuma leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la
Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania
leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo
katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima
mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la
kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha
Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga
kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika
vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano
ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
Rais Jakaya Kikwete mpenda watoto, akiwa amembeba mtoto.....Picha na Fredy Maro
RC na RAS nchini kujengewa uwezo na kuhuisha uhai wa utekelezaji wa majukumu yao.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akifungua mafunzo ya
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa nchini leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia akimpongeza Mgeni Rasmi Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd na mara baada ya
kufungua mkutano wa mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa
nchini leo jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akitete jambo na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia wakati wa mkutano wa
mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa nchini leo jijini Dar
es salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa nchini leo jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Eleuteri Mangi-Maelezo)
Eleuteri Mangi-MAELEZO
21/07/2014
Viongozi wa Wakuu wa Mikoa nchini
wameaswa kufahamiana kama viongozi ili kubadilishana uzoefu wa kujenga
mtandao wa mawasiliano na mahusiano kwa ajili ya kupashana habari na
kushauriana.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya Wakuu wa Mikoa (RC) na Makatibu Tawala Mikoa (RAS) nchini leo
jijini Dar es salaam.
“Jengeni mshikamano wa mahusiano
katika utendaji kazi wenu mkiimarisha maelewano miongoni mwenu
mtarahisisha utendaji na kuepuka migogoro isiyo ya lazima” alisema
Balozi Seif.
Balozi Seif aliendelea kusema,
“Tumieni nafasi hii kufahamiana muweze kujenga mtandao wa mahusiano,
mawasiliano mkiimarisha mashirikiano ili kuleta maendeleo katika maeneo
yenu ya kazi kwa manufaa ya wananchi”.
Balozi Seif alisema kuwa kila kazi
inachangamoto zake, katika kutekeleza majukumu yao vizuri na kubainisha
kuwa viongozi hawa baadhi yao wamekuwa na misuguano ya hapa na pale
ambayo husababishwa na mawasiliano yasiyoridhisha.
Balozi Seif alisisitiza kuwa dawa
ya misuguano hiyo itapatikana kupitia mafunzo hayo ya siku tatu ambapo
viongozi hao watakumbushwa mengi waliyoyasahau, watapata mengi ya
kujifunza, kujikumbusha na kujinoa ili kuhuisha uhai wa utekelezaji wa
majukumu yao ambao utaleta mshikamano na umoja miogoni mwa watendaji
hao.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Hawa Ghasia alipokuwa akimkaribisha Mgeni Rasmi alisema kuwa
mafunzo hayo yataimarisha mahusiano na mawasiliano ya viongozi hao
katika kutekeleza majukumu yao ili yapate tija iliyokusudiwa.
Waziri Ghasia amewaasa viongozi
hao kuwa wasipofanya kazi kama timu hawawezi kupata tija katika maeneo
yao ya kazi hasa katika kuwaletea maendeleo wananchi wanaowaongoza na
nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
akimshukuru na kumhakikishia Mgeni Rasmi Balozi Seif kuwa wanamatumaini
makubwa kuimarisha mahusiano kati yao vilevile na wanasiasa wote na
kuahidi kuwa watatoa huduma bora zaidi.
Aidha, mikoa ya Lindi, Mtwara na
Ruvuma viongozi wao hawatashiriki mkutano huo kwa kuwa kwa sasa wapo
kwenye ratiba ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete katika mikoa hiyo.
Wakuu wa mikoa hiyo waunganishwa
kupata mfunzo kama hayo na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa ya
Zanzibar ambayo itapangwa kufanyika hapo baadaye ambapo Serkali ya
Mapinduzi imeahidi kushirikiana na Tasisi ya Uongozi kutoa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yameandaliwa na
Taasisi ya Uongozi kwa lengo la kuwawezesha viongozi hao kufahamu kwa
kina umuhimu wa mawasiliano bora baina ya viongozi wa kisiasa na
watendaji Wakuu wa ngazi ya Mkoa ili kuimarisha utoaji bora wa huduma
kwa wananchi.
MAKAMU MKUU WA MUHAS AONGOZA KUAAGA MWILI WA PROFESA MBWAMBO
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS) Profesa Ephata Kaaya akiuaga mwili wa Mhadhiri wa wa chuo hicho , marehemu, Profesa Zakaria Mbwambo , ambaye ni mume wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi . Joyce Mapunjo leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi. Joyce Mapunjo akifarijiwa na
baadhi ya waambolezaji leo, wakati wa kuuaga mwili wa
marehemu mumewe Profesa Zakaria Mbwambo, ambaye alikuwa ni
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili,
(MUHAS) kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maprofesa wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS), wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Profesa mwenzao , marehemu, Profesa Zakaria Mbwambo , ambaye ni mume wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi . Joyce Mapunjo leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maprofesa wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS), wakiwa katika hali ya huzuni wakati wa kuuaga mwili wa Profesa mwenzao , marehemu, Profesa Zakaria Mbwambo , ambaye ni mume wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi . Joyce Mapunjo leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo
MAUAJI YA VIKONGWE YASHIKA KASI MLELE- KATAVI
Madiwani wakifuatilia kwa umakini wakati mwenzao akichangia hoja katika kikao hicho
(Picha zote na Kibada Kibada –Mlele Katavi)
Na Kibada Kibada –Mlele Katavi.
Wimbi la mauaji kwa watu wenye
umri kuanzia miaka 60 na kuendelea Wilayani Mlele Mkoani Katavi
linaonekana kushika kasi na kutishia hali ya ulinzi na usalama kama
hatua za makusudi hazitachukuliwa.
Hii ni kwa Mujibu wa Taarifa ya
Hali ya ulinzi na Usalama Wilayani humo iliyotolewa na Mkuu wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa wilaya hiyo , Zabron Ibeganisa kwenye
Mkutano Mkuu wa Baraza la Madiwani uliokuwa ukipokea taarifa ya
utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa kipindi cha
mwaka wa 2013/2014.
Subscribe to:
Posts (Atom)