WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI

April 11, 2018

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Roeland van de Geer wakisaini Hati ya Makabidhiano ya nyumba nne (4) kutoka Umoja wa Ulaya zilizopo katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo zimekabidhiwa kwa Wizara na EU baada ya kutumiwa na Umoja huo tokea miaka ya 1975. Baada ya makabiadhiano hayo, Wizara ilizikabidhi nyumba hizo kwa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA). Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani tarehe 11 Aprili, 2018.
Balozi Mushy kwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi. Elius Mwakalinga wakisaini hati ya makabidhiano kama ishara kwa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuzikabidhi kwa TBA nyumba nne (4) zilizopokelewa na Wizara kutoka EU.

Balozi Mushy na Balozi Roeland van de Geer wakibadilishana hati hiyo baada ya kusaini

Balozi Mushy na Balozi van de Geer wakionesha hati hiyo

Balozi Mushy na Mhandisi Mwakalinga wakibadilishana hati hiyo mara baada ya kusaini
Wakionesha hati hiyo

Mhandisi Mwakalinga na Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin wakishuhudia Balozi Mushy na Balozi Roeland (hawapo pichani) wakisaini hati ya makabidhiano ya nyumba kutoka EU

Ujumbe uliofuatana na Balozi Roeland kutoka Ofisi za EU nchini nao wakishuhudia tukio hilo

Balozi Mushy na Balozi Roeland wakiteta jambo

Bw. Batholomeo Jungu, Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Itifaki akitoa maelezo na utaratibu kwa Mabalozi kabla ya kuanza kusainiwa kwa hati hizo za makabidhiano

Picha ya pamoja

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE (JMKF) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

April 11, 2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi kabla ya kuzindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi mara baada ya kumaliza kusoma hotuba yake na kuizindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua. PICHA NA IKULU

DK. KIGWANGALLA AITAKA KAMATI INAYOCHUNGUZA TUHUMA ZA MAUAJI YA TEMBO KATIKA IKOLOJIA YA RUGWA-RUAHA KUTENDA HAKI

April 11, 2018


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mstaafu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye ni Mwenyekiti wa kamati inayochunguza tuhuma za mauaji ya tembo katika Ikolojia ya Rugwa-Ruaha ambazo zilitolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON cha nchini Uingereza, alipokutana na kamati hiyo leo ofisini kwake mjini Dodoma. Wengine pichani ni wajumbe wa kamati hiyo.

Na Hamza Temba-Dodoma


........................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameitaka kamati inayochunguza tuhuma za mauaji ya tembo katika Ikolojia ya Rugwa-Ruaha ambazo zilitolewa mwishoni mwa mwaka jana na kituo cha habari cha ITV London cha Uingereza kufanya kazi hiyo kwa uaminifu na uadilifu mkubwa bila kumuonea mtu ili ukweli ubainike na Serikali iweze kuchukua hatua stahiki.

Dkt. Kigwangalla ametoa rai hiyo leo mjini Dodoma alipokutana na wajumbe wa kamati hiyo ambayo imewasilisha taarifa za awali za kazi ilizoanza kuzifanya za kupitia taarifa mbalimbali kuhusu tuhuma hizo kabla ya kwenda kuzifanyia uchunguzi maeneo husika.

Amewataka wajumbe hao kuchunguza ukweli wa tuhuma hizo ili kubaini kama kweli kuna watumishi wa Wizara waliohusika katika mauaji hayo pamoja na tuhuma kuwa mauaji ya tembo yalikuwa ni makubwa kama ilivyoripotiwa na chombo hicho cha habari.

Dkt. Kigwangalla pia ameitaka kamati hiyo kuchunguza ukweli wa tuhuma kuwa fedha za ufadhili wa mradi wa SPANEST zilizotolewa na Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) zilitumika vibaya kufadhili mauaji hayo kama ilivyoripotiwa na chombo hicho cha habari.

“Msimtafute mtu, wala msimuonee mtu, fanyeni kazi hii kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ukweli ujulikane ili sisi kama Serikali tuweze kuchukua uamuzi unaostahili” alisema Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Kamanda wa Polisi Mstaafu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kamati yake itafanya kazi kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu na kuleta taarifa za ukweli na mapendekezo yatakayoisaidia Serikali kufanya maamuzi sahihi kuhusu tuhuma hizo.

Mapema mwezi Januari mwaka huu, Waziri Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Natalie Boucly wakiwa katika ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam walikubaliana kuunda kamati ya pamoja kuchunguza tuhuma hizo.

Kamati hiyo iliyoundwa mapema mwezi januari mwaka huu inajumuisha wajumbe tisa wakiwemo wawili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na wajumbe wengine kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Ndugu Robert Mande ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Bi. Getrude Lyatuu ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wajumbe wa kamati inayochunguza tuhuma za mauaji ya tembo katika Ikolojia ya Rugwa-Ruaha ambazo zilitolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON cha nchini Uingereza, alipokutana na kamati hiyo leo ofisini kwake mjini Dodoma.

MPINA AWABANA WANAOTOROSHA PUNDA KWENDA NJE YA NCHI

April 11, 2018

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katika) akizungumza na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua, Lifang Yu, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Assimwe Lovince. Picha na John Mapepele.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiangalia zizi la Punda na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua, Lifang Yu aliye kushoto kwake. Picha na John Mapepele.


Punda kwenye zizi la Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua mjini Shinyanga. Picha na John Mapepele.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye miwani) katika picha ya pamoja na watumishi wa Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua. Picha na John Mapepele.



Na John Mapepele, Shinyanga

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewahakikishia wenye viwanda nchini kuwa hakuna mali ya mifugo ya Tanzania itakayotoroshwa tena kwenda nje ya nchi kimagendo kwani Tanzania haiwezi kukubali kugeuzwa kuwa machungio ya mifugo hiyo.

Waziri Mpina ametoa kauli hiyo jana mjini Shinyanga baada ya kutembelea Kiwanda cha Fang Hua kinachojishughulisha na uchinjaji wa Punda ambapo alielezea kuridhishwa kwake na juhudi kubwa zilizofanywa na mwekezaji huyo kuwezesha kuwepo soko la uhakika la mifugo hiyo.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Fang Hua, Lifang Yu alimweleza Waziri Mpina kwamba kiwanda chake kimeshaingia ubia na wafugaji wadogo wapatao 27 ili kuongeza uzalishaji ambapo kinatarajia kuwashilikisha wafugaji wengi zaidi katika mikoa mbalimbali nchini

Waziri Mpina aliwahakikishia wawekezaji wenye viwanda katika sekta ya mifugo kuwa malighafi hiyo itakuwepo ya kutosha kwani Serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. John Pombe Magufuli haitakubali tena mifugo hiyo kuendelea kutoroshwa nje ya nchi na kunufaisha viwanda vya nchi hizo.

Hivyo Waziri Mpina alisema uwekezaji wa aina hiyo wa kuongeza thamani ya mazao ya mifugo ni moja ya vipaumbele vya wizara yake kwa sasa ili kuchochea kwa kasi kufanikisha azma ya Tanzania ya viwanda.

Alisema kiwanda hicho mbali na kuongeza soko la punda pia kimechangia kuchochea uchumi wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na kutatua changamoto ya ajira ambapo hadi sasa kimeajiri wafanyakazi 100 hivyo alimhakikishia mwekezaji huyo kuwa changamoto ya punda wengi kutoroshwa nchini Kenya haitakuwepo tena.

Alisema kwa sasa kuna viwanda viwili vya kuchakata nyama ya punda na kuuza nchini China, ambapo wastani wa mauzo ya nyama hiyo nje ya nchi yalifikia tani 2000 mwaka 216/17

Mpina aliwahimiza wawekezaji hao kuhakikisha wanawasaidia wafugaji katika kuongeza uzalishaji, kupambana na maradhi, upatikanaji wa maji na malisho kwa mifugo.

Aliwataka kuanzisha ranchi ya mifugo na maeneo yakupumzishia mifugo hiyo kabla ya kuchinjwa.

Alisema idadi ya punda waliopo nchini ni 520,000 tu hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuongeza uzalishaji.

Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Lovince Assimwe aliwataka wafugaji kuongeza soko la uhakika.

Alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kubuni mbinu za kuwasaidia wafugaji kwa kuwapatia shilingi elfu tano kila mwezi kwa ajili ya matibabu ya punda.

VIDEO – MZEE ALIYEGUNDUA NA KUOKOA KUTEKETEA KWA MAKAA YA MAWE MGODI WA NGAKA AOMBA KUKUTANA NA RAIS

April 11, 2018



Mzee Benedict Mapunda (Rasha) mwenye umri wa miaka 66 mkazi wa kijiji cha Ntunduwaro ndiye aliyegundua kuteketea kwa moto kwa mgodi wa madini ya makaa ya mawe Ngaka uliopo Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma mwaka 2006.

Mgodi huo hivi sasa unaingiza mabilioni ya fedha kwa Kampuni binafsi ya uchimbaji wa madini hayo ya TANCOAL na serikali inalipwa kodi na ushuru kutokana na kazi ya uchimbaji na usafirishaji wa madini hayo ilioanza tangu mwaka 2011.

Mzee Rasha bado hajatambulika kwa kuokoa rasilimali adimu ya madini ya makaa ya mawe kwa nchi yake ambayo yalikuwa yanateketea kwa moto ardhini kwa miaka kadhaa. Rasha anafanyakazi ambayo haifanani na umri wake katika Kampuni ya TANCOAL kwenye mgodi wa Ngaka.

BANDARI YA TANGA YAPOKEA BOTI YA DORIA

April 11, 2018


MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka hiyo juzi kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akifuatilia matukio kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na kulia ni
MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
sehemu ya watumishi wa Bandari wakifuatilia matukio

Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akipata maekelezo anayefuatia kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama

MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama kulia akimkabidhi zawadi mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa


BANDARI ya Tanga imepokea boti ya doria yenye thamani ya fedha za kimarekani UDS 2,204,100 kwa ajili ya kufanyia doria kwenye ukanda wa bahari

Boti hiyo ambayo imenunuliwa na mamlaka hiyo itakuwa na msaada mkubwa pia kukabiliana na wimbi la biashara haramu za magendo zinazoendelea kufanyika kwa zaidi ya bandari bubu 40 katika ukanda wa pwani mkoani hapa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Bandari Mkoani Tanga Percival Salama kwenye maadhimisho ya wiki ya Mamlaka hiyo Nchini Tanzania(TPA)Mkoani hapa kwa kufikisha miaka 13.

Aidha alisema boti hiyo yenye uwezo mkubwa itakuwa muarubaini kwa ajili ya kukabiliana na wafanya biashara za magendo katika bandari zisizo rasimishwa(bubu) ambapo itakuwa na kazi ya kufanya doria kukabiliana na wimbi hilo la magendo.

“Kweli biashara za magendo zimekithiri hasa katika ukanda wetu wa bahari ya hindi na sasa tayari tumepata boti mpya na ya kisasa kwa ya doria jukumu letu ni kukabiliana na wafanyabiashara hao tu na sivinginevyo”Alisema.

Salama alisema zipo bandari nyingi mkoani hapa ambazo sio rasmi na zinatumiwa na wafanyabiashara ambao si waaminifu kwa Serikali yao jambo ambalo limewalazimu mamalaka husika kutafuta chombokitakachokuwa na uwezo wa kufanya doria nyakati zote.

Alisema mkoani Tanga kuna Bandari mbili ambazo ni Tanga mjini na Pangani ndio ambazo zilizorasimishwa kihalali na mamlaka hiyo kwa ajili ya kufanya shughuli za usafirishajiwa mizigo mbali na zile za kipumbwi,mkwaja,kigombe jasini na nyinginezo ambazo hazitambuliwi kwa mujibu wa sheria.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapwa ambae alikuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo alisema serikali haitakuwa na mjadala na watu wanaojishughulisha na biashara hizo.

Aidha alisema kumekuwepo na wimbi la biashara hizo za magendo katika Bandari bubu ambapo kupitia kamati za ulinzi majeshi yote yataungana kwa ushirikiano na Mamlaka ya bandari kupambana na wafanya baishara hao.

“Labda niseme tu kinachofanyika tanga kama mazoea na sasa vita yakuwakabili wafanyabiashara hao itakuwa kubwa zaidi kama unayosikia kwawenzetu wa Bandari wameleta boti ya kisasa ya doria sisi tutaongeza nguvu ya kijeshi lazma tukomeshe biashara hizo”Alisema Mwilapwa.

Hata hivyo aliwasihi wafanyabiashara kuacha mara moja biashara hiyo ya magendo kutokana na Serikali kutoa maelekezo ya kutaifisha vyombo vitavyo kamatwa na bidhaa zote zitashikiliwa na serikali.