MHE. KAIRUKI AWATAKA VIONGOZI WA TAKUKURU KUZALIWA UPYA KIUTENDAJI

MHE. KAIRUKI AWATAKA VIONGOZI WA TAKUKURU KUZALIWA UPYA KIUTENDAJI

February 15, 2016

SONY DSC
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na viongozi wa TAKUKURU katika mkutano wa kazi na viongozi hao uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza kwa umakini.
MLO2
Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi wa TAKUKURU wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo. 
MLO3
Mmoja wa viongozi wa TAKUKURU akijitambulisha kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb)  (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akifungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akijibu hoja zilizowasilishwa na viongozi wa TAKUKURU katika mkutano wa kazi wa viongozi hao uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wakaguzi wa kanda wa TAKUKURU mara baada ya kufungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.
WAZIRI UMMY APOKEA VIFAA KATIKA WODI YA AFYA YA UZAZI YA MAMA NA MTOTO MUHIMBILI

WAZIRI UMMY APOKEA VIFAA KATIKA WODI YA AFYA YA UZAZI YA MAMA NA MTOTO MUHIMBILI

February 15, 2016

U1
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akipokea vifaa kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa yaTaifa Lauren Rugambwa Bwanakunu vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya Muhimbili Prof Lawerence Mseru na nayefata ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Mpoki Ulisubisya .
U3
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akielekezwa jambo katika nyaraka na katibu Mkuu wa wizara hiyo Mpoki Ulisubisya katika Kitengo cha Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
U4
Baadhi ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mfanyakazi wa Bohari Kuu ya dawa ya taifa (MSD) walishusha baadhi ya magodoro na vitanda vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
U5
U7
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akisaidiana na mmoja  wa kijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kubeba boksi lenye takataka kwenda kuyatupa sehemu husika  wakati wakifanya usafi katika jengo ambalo liliamriwa na Mhe Rais liwe wodi ya  Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
U8
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Zuhura Abubakari mmoja ya wagonjwa waliohamishiwa kwenye wodi mpya ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
U9 
Mafundi wakifunga vitanda katika wodi mpya ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu amepokea vifaa vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni agizo la Mhe.Rais alililolitoa mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika kuhakikisha kuwa wakinamama wanaojifungua hawalali chini.
Akipokea vifaa hivyo Mhe. Ummy Mwalimu amesema anamshukuru sana Mhe Rais kwa kuona changamoto hii ya wakina mama kulala chini wakati wakitoka kujifungua na kumuahidi Mhe. Rais kusilimamia vyema suala hilo na kuwaagiza wakurugenzi husika kumpa taarifa ya kuhusu vitanda na magodoro katika Hospitali zote zilizo chini ya wizara yake.
“ Kuanzia sasa sitolala na natuma salamu kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa fursa hii ni wajibu wao kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya afaya hasa katika vifaa hususan vitanda na magodoro ili kupunguza tatizo hili la wagonjwa katika Hospitali zetu kulala chini wakati tuna uwezo wa kupata vitanda na magodoro”
‘”Mhe.Rais amenifundisha na ametufundisha sote kwamba kutatua jambo sio mpaka mkae vikao au semina ili kujadili ila inawezekana kama mkiweka nia ya kulifanya jambo hilo na kuachana na zile kauli za tunalifanyia kazi, tupo katika michakato na kauli kama hizo zisizotatua tatizo kwa wakati unaotakiwa”alisema Ummy.
Bohari ya Dawa ya Taifa imekabidhi jumla ya vitanda 120, Magodoro 120, Mashuka 480, vitanda vya kuzalishia 10,vitanda 10 vya kulaza watoto ambao hawajatimia Njiti na jumla ya vifaa vyote vina thamani ya shilling Million 100.
Uaandaaji wa wodi hiyo ya akimama wanaojifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umekuja baada ya agizo la Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa hivi karibuni alipokuwa akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es Salam na kutoa siku mbili kwa wizara Ya Afya kuhamisha ofisi zilizokuwepo za kitengo Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto na kuifanya kuwa wodi ya akina mama ili kupunguza tatizo la kulala chini kwa akina mama wanaotoka kujifungua.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA BODI YA CHUO CHA UHAMIAJI CHA KIKANDA (TRITA) MJINI MOSHI.

February 15, 2016

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. Katika hotuba yake Rwegasira aliitaka Bodi hiyo ifanye kazi kwa ushirikiano kwa maendeleo ya chuo. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika mjini Moshi. Watatu kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano.na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma.
 Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Erasmi Francis akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) na wajumbe wa Bodi ya Chuo hicho, kamera inayotumika kuchukua kumbukumbu za usalama kwa ajili ya watu wanaopita katika mipaka ya nchi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Watatu kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Kinemo Kihomano (Wasita kushoto). 
Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Zawad Chazuka akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) albamu yenye hati za kusafiria za mataifa mbalimbali duniani, albamu hiyo inaonyesha alama za kiusalama ambazo zipo katika pasipoti za mataifa mbalimbali. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
 Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Zawad Chazuka akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) albamu yenye hati za kusafiria za mataifa mbalimbali duniani, albamu hiyo inaonyesha alama za kiusalama ambazo zipo katika pasipoti za mataifa mbalimbali. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, wakati alipokuwa anawasili katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi kwa ajili ya kuzindua Bodi ya Chuo hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua maeneo mbalimbali ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. (kushoto) mara baada ya kuzindua Bodi ya Chuo hicho. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa), Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuzindua Bodi hiyo mjini Moshi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

OFISI YA WADOKI SACCOS NA HOTEL YA KIRUMBA RESORT ZA MKOANI MWANZA ZAFUNGWA NA WANACHAMA WA CCM

February 15, 2016
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, leo wamefunga Ofisi ya Taasisi ya Mikopo ya WADOKI (Wadoki Saccos) pamoja na Hotel ya KIRUMBA RESORT kutokana na watajwa kushindwa kulipia kodi ya pango.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid (anaeongea pichani) amesema kuwa wanachama hao wamefikia maamuzi hayo kutokana na kutumia majengo ya CCM katika kata hiyo huku wakiwa hawalipii kodi.

Wanachama wa CCM katika Kata hiyo ya Kirumba wamesema kuwa, maamuzi yao yatatoa fundisho kwa wawekezaji wengine wanaotumia vitega uchumi vya Chama hicho katika maendeo mbalimbali nchini huku wakiwa hawalipii kodi ambapo wametahadharisha kwamba wale wote wenye hulka hiyo wajiandae kutumbuliwa (kuondolewa katika majengo hayo).

Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Juma Wesa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi, wamesema kuwa maamuzi yaliyochukuliwa na wanachama hayo ni sahihi kwa kuwa malalamiko ya wawekezaji hao yaliishajadiliwa hadi ngazi za juu na kuonekana kwamba wawekezaji hao hawatii makubaliano yao ikiwemo kulipa kodi ya pango kwa wakati.

Meneja wa Kirumba Resort hakutaka kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba mzungumzaji ni Mkurugenzi ambae alidai amesafiri huku Uongozi wa Wadoki Saccos ukishindwa kupatikana.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid akitoa kwa wanaccm baada ya wanachama hao kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Acheni Maulidi akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Wesa Juma, akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Jane Masso ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Kirumba (kulia) amesema wanachama watahakikisha vitega uchumi vya chama vinatumika vyema kwa ajili ya maendeleo yao.
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Ofisi ya Wadoki Saccos Kirumba baada ya kuwekewa kama ishara ya kufungwa
Ulinzi wa Askari wa Kutuliza ghasia ulikuwepo ili kuhakikisha hakuna uhalibifu wowote ambao ungeweza kufanyika ambapo suala hilo limefikishwa Kituo cha Polisi Kirumba na kila upande unawasilisha vielelezo vyake ili kutambua wanaokiuka makubaliano ya mkataba wa upangaji.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group
NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YA MT. LUCAS MKOANI IRINGA

NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YA MT. LUCAS MKOANI IRINGA

February 15, 2016

RC IringaMkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza waliokaa kushoto) wakati alipotembelea ofisini hapo. Wengine ni watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (waliokaa kulia).

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla mapema leo Februari 15, ametembelea kambi ya Wagonjwa wa Kipindupindu pamoja na wale waliokumbwa na mafuriko katika kijiji Mboliboli Kata Pawaga Wilayani Iringa ambapo hadi sasa kambi hiyo ina wagonjwa 40 huku zaidi ya wagonjwa 223 walilipotiwa kuugua tangu kipindupindu kimeanza katika eneo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza wakati wa kutoa taarifa yake kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aliyetembea ya Mkuu wa mkoa huyo, alimweleza kuwa kati ya wagonjwa hao 223, wagonjwa 17 ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, Mbali na hao hadi sasa yamesababisha kifo kimoja.
Ugonjwa huo umeelezwa kuwa umewakumba kutokana na mvua zilizonyesha na kubomoa vyoo na kutapanya kinyesi hali iliyopelekea ugonjwa huo kusambaa Zaidi katika makazi ya wananchi hao.
Hadi sasa eneo hilo limekumbwa na maji huku wananchi wakilazimika kuyakimbia makazi yao na hata kuzungukwa na maji karibu eneo kubwa na usafiri wa watoa huduma kuwa wa shida ikiwemo kutumia boti maalum ama chopa.
Mkoa huo ulikumbwa na mvua mnamo Februari 3 hadi leo bado maji yameendelea kuzingira maeneo ya vijiji hivyo.
Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog-Iringa.

RC Iringa

DSC_0468

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa taarifa namna ya kamati yake ilivyopambana usiku na mchana na hatua waliofikia katika kuakikisha kipindupindu kinakwisha katika eneo hilo huku wakiendelea na jitihada za kupambana na mafuriko ikiwemo kuokoa wananchi waliobakia eneo hilo.

kigwanga

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kumaliza kwa mazungumzo na taarifa fupi juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwenye maeneo ya vijiji vya Mkoa huo ambapo hadi leo wamefikia jumla ya wagonjwa 40.

dk kigwanomic

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa tayari kwa kuelekea kupanda Chopa kuelekea kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.

dk kigwangaz

Wakielekea katika Chopa maalum ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwafikia wananchi waliozingirwa na maji ya mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.

Dk kigwaziiNaibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipanda Chopa tayari kuelekea kwenye eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Pawaga, Mkoani Iringa. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Iringa).

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA KIKAO NA MKUU WA WILAYA YA HAI,ANTHONY MTAKA

February 15, 2016
div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako alipofika ofisi ya mkuu huyo wa wilaya na kuzungumza mambo machache na Wakaguzi wa elimu na maofisa elimu wa wilaya ya Hai.
Waziri Ndalichako akitia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Hai,wakiwa katika kikao kidogo na Waziri Ndalichako.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi ,Prof Joyce Ndalichako aliyefanya kikao kidogo na watumishi wa Elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.
Waziri Prof Ndalichako akizungumza na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akimsikiliza kwa makini Prof Ndalichako.
Waziri Prof Ndalichako akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kwa maofisa elimu na wakaguzi wa elimu katika wilaya ya Hai.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

GARI YA WIZI YAKAMATWA NACHINGWEA MKOANI LINDI

February 15, 2016

Gari aina ya NOAH Namba T378 BYH rangi nyeupe imekamatwa huko nachingwe mkoani lindi. Baada ya uchunguzi polisi wamebaini kuwa rangi ya awali ya gari hiyo ni TRIM na mmiliki wake halali ni ABDALA MOHAMED MCHONDA P.O.BOX 1370 DAR ES SALAAM. Namba original za gari ni T 223 CUX. Yeyote mwenye taarifa ya kupotea gari yenye maelezo hayo awasialiane na Polisi Nachingwea kupitia RTO LINDI [0658 376074].Imeandaliwa na RSA na Dj Sek