ASKARI KUTOKA VIKOSI MBALIMBALI VYA PEMBA WAFANIKIWA KUWAKAMATA RAIA SITA WA KENYA.

October 13, 2014
                           
                       NA MASANJA MABULA,PEMBA.
Kikosi kazi kinachojumuisha askari kutoka vikosi mbali mbali vya ulinzi Pemba wamefanikiwa kuwakamata Raia sita wa Kenya wakiendesha shughuli za  uvuvi katika eneo la bahari ya Kisiwa cha Zanzibar kinyume na utaratibu .

Wavuvi hao wakiwa na chombo chenye namba za usajili MV 066 V kikiwa na jina la Samira wamekamatwa siku ya Jumapili majira ya saa nane za mchana na askari hao wakiwa kwenye doria zao za kawaida katika eneo la Rasi Kiuyu .


Taarifa zaidi zinasema kuwa chombo hicho kimekuwa na kawaida ya kuja kuvua katika eneo la bahari ya Kisiwa cha Zanzibar kinyume na taratibu .


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi , Mkuu wa Operation wa kikosi cha KMKM Pemba , Said Ali Ali amesema kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi ndani ya chombo chao kulibaianika kuwepo mishipi 250 pamoja na boksi 5 za samaki .


Amesema kuwa chombo hicho kilikuwa kinaongozwa na nahodha wake Abdilah Kassim Ahmed ( 24) kikiwa pamoja na mahabaria watano ambao wote hawakuwa na paspoti na leseni za uvuvi .

 
Aidha amewatahadharisha wananchi kuwa askari wa kikosi kazi wako makini na wataendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi na kusisitiza mbali na kuzuia magendo ya karafuu pia kazi nyingine na kuhakikisha kwamba vitendo vyote vya hujuma ndani ya nchi havipewi nafasi .


Sheha wa Shehia ya Tumbe Magharibi Massoud Khamis aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi katika kutoa taarifa juu ya wageni wanaoingia hapa nchini ili kuweza kudhibiti kuitokea kwa maafa yanayoweza kuepukika .

Wabunge Duniani wakutana kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiusalama yanayoikabili Dunia

October 13, 2014


Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifatilia kwa makini Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU),unaofanyika mjini Geneva,Uswis.
Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Hamad Rashid Mohamed akiteta jambo na Balozi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Geneva, Uswis, Balozi Modest Mero wakati wa Mkutano wa chama hicho mjini Geneva leo.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa naMhe. Hamad Rashid Mohamed wakishiriki Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) Mjini Geneva, Uswis.

Na Owen Mwandumbya, Geneva
Wabunge kutoka Mabunge wanachama wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wanakutana Mjini Geneva Usiwisi katika Mkutano wa mwaka wa 131 wa chama hicho kujadili na kutafuta ufumbuzi wa namna ya kukabiliana na baadhi ya matatizo yanayoyakumba mataifa mbalimbali duniani ikiwemo usalama pamoja na uvunjaji wa haki za Binadamu.
Katika mkutano huo ambao unahudhuriwa na jumla ya wabunge 700 kutoka nchi wananchama 141 wakiongozwa na Maspika na Manaibu spika kutoka nchi 104 umeanza jana tarehe 12 na unatarajiwa kumalizika ijumaa tarehe 16 Oktoba, 2014 kwa kufanya uchaguzi kumchagua rasi wa chama cha kibunge na ambacho ni kikubwa Duniani.
Katika agenda za mkutano huo, mojawapo ya masuala yanayojadiliwa ni pamoja na kuja na suluhu ya kibunge ya namna ya kukabiliana na kubambana na ugaidi duniani na masuala yote ya imani kali yanayopeleka kuleta machafuko katika baadhi ya nchi hususani za kiarabu kwa kuangamiza maelfu ya watu wasio na hatia. Pamoja na masuala hayo, wabunge hao pia wanajadili namna bora ya nchi wanachama kuwa na sheria madhubuti ya kupiga vita biashara haramu ya usafirishaji wa Binadamu, pamoja na kutambua uhuru wa kila Taifa bila kuingiliwa na mataifa mengine.
Tanzania katika Mkutano huo inawakilishwa na Wabunge wambao ni wanacham wa kudumu katika mkutano huo ambao ni mhe. Hamad Rashid Mohamed, Mhe. Suzan Lyimo na Mhe. Dkt. Pudensiana kikwembe.
Katika mchango wa Tanzania, kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Tanzania Mhe. Hamad Rashid Mohamed akichangia katika Mkutano mKuu w huo ameelezea namna Tanzania inavyounga mkono jitihada za IPu katika kupiga vita masula ya Ugadi ikiwa ni pmoja na jitihada za chombo hicho kutambua uwakilsihi wa wanawake katika masula ya uongozi.
Akisisitiza umuhimu wa mabunge kuwa na sheria rasmi zinazoweza kumlinda mwananke katika ukatili wa kijinsia, Mjumbe kutoka Tanzania Mhe. Suzan Lyimo amesema, takwimu zilizopo zinaonyesha  kuwa mwananmke mmoja katika kila wanawake watatu hivi sasa ni mhanga wa ukatili wa kijinsia unaofanya katika ngazi ya kifamilia na hata utawala hususani na machafuko ya kivita. Ansema bila kujipanga vyema katika ngazi ya kibunge kuwa na sheria na utaratibu madhubuti ya kumlinda mwananke, machafuko yanayotokea duniani hivi sasa yatazidi kumwangamiza mwanamke .
Akitolea mfano wa makundi hatari yanayotokea duniani hivi sasa kama vile ISIS, BOKO HARAM, ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa tishio kubwa kwa usalama wa kimataifa bali hata kwa ustawi wa wanawake duniani kutokana na vitendo vyao vya kuwadhalilisha wanawake.
Mkutano huo unaendelea leo kwa kuangalia masula mengine ya kimataifa na namna mabunge yote duniani yatasaidiana na Serikali zake kutatua migogoro hiii ya kimataifa.
WIKI YA VIJANA YAENDELE KUWA CHACHU YA UZALENDO

WIKI YA VIJANA YAENDELE KUWA CHACHU YA UZALENDO

October 13, 2014
TBR1Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiangalia Jarida katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Dunia (UNFPA – Tanzania) alipotembelea katika Maonyesho ya  Wiki ya Vijana leo mjini Tabora. Kutoka kushoto ni Mchambuzi wa Miradi ya Vijana na Maendeleo wa  UNFPA – Tanzania Bi. Tausi Hassan na Mshauri wa Vijana wa Shirika hiloBw. John Kalimbwabo.

TBR2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Vijana, Jinsia, Wanawake na Watoto ya Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar Bw. Ally Hamisa konyesha nyaraka za vibali na sahihi za Wakuu wa Mikoa alipopita Kijana mzalendo Bw.Abiudi Denis aliyetembea nchi nzima kwa Siku 65 kwa lengo la kuhamasisha uzalendo ikiwemo kupinga Muundo wa Serikali Tatu, Kumpongeza Rais Jakaya Kikwete na Kupinga watu wanaombeza Hayati  Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere leo mjini Tabora wakati alipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa kijana huyo kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Wiki ya Vijana.
TBR3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel  akitembelea mabanda wakati wa Maonesho ya  Wiki ya Vijana yanayoendelea katika Viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Pichana Frank Shija, WHVUM
 Mhariri Gazeti la MTANZANIA akabidhi vyeti Shule ya Salma Kikwete

Mhariri Gazeti la MTANZANIA akabidhi vyeti Shule ya Salma Kikwete

October 13, 2014


1a 
Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya, akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Ahmed Adamu katika mahafali ya tano ya wahitimu wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mwenyekiti wa walimu wa maarifa ya Uislamu Dar es Salaam, Suleiman Gombe.
Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya akizungumza katika mahafali hayo.
………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kutambua wajibu kwa kuhakikisha wanawekeza kwenye elimu kwa watoto wao.
Wito huo ulitolewa Dar es Salam na Mhariri Msanifu wa gazeti la MTANZANIA, Khamis Mkotya alipokuwa akizungumza katika mahafali ya tano ya Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete.
Mkotya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ambapo alisema ni lazima jamii ikubali kuondokana na kulalamika na badala yake iandae mazingira mazuri ya watoto wao kuhakikisha wanasoma kwa bidii.
“Bado siku chache wanafunzi wa kidato cha nne nchini, mtafanya mitihani ya kuhitimu lakini tambueni kumaliza elimu hii kwa ngazi yetu ni chachu ya kutafuta zaidi ya elimu.
“Na mkiwa hamtafanya hivi mtakuwa mmekwenda ninyume na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) ambaye amatutaka tutafute elimu hadi uchina. Na hata leo ukimaliza mtihani wa kidato cha nne na kuona umemaliza tambueni elimu mlionayo sasa ni sawa na elimu ya msingi,” alisema Mkotya.
Alisema ili maendeleo chanya yaweze kupatikana nchini ni lazima jamii ijiandae vema kuyapokea kwa kuwa na mkakati hasa kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii kwenye masomo yao.

RPC KASHAI AELEZA CHANZO CHA MADUKA MANNE KUTEKETEA WILAYANI KILINDI.

October 13, 2014
NA MWANDISHI WETU,KILINDI.
IMEELEZWA kuwa chanzo cha tukio la kuungua moto nyumba mmoja yenye fremu nne za maduka wilayani Kilindi mkoani Tanga ilisababishwa na moto ulikuwa ukitumiwa na mama lishe jirani eneo hilo kusambaa kwenye maeneo yaliyopo sheli hiyo na kuunguza eneo hilo.

Moto huo uliachwa bila kuzimwa baada ya mamalishe hao kumaliza biashara zao za kuuza chakula jambo ambalo lilipelekea kuleta hasara kubwa kwenye maduka hayo ambapo thamani yake bado haijajulikana mpaka sasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai alithibitisha kutokea tukio hilo ambapo alisema lilitokea Octoba 7 mwaka huu katika kijiji na kata ya Negero Tarafa ya Kimbe wilayani humo .

Akielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea Kamanda Kashai alisema kuwa gari lenye namba za usajili T.219 AUC Center yenye tanki la mafuta linalomilikiwa na Adolf Lykundi mkazi wa Handeni lilishika moto na kulipuka wakati likimimina mafuta ya petrol kwenye mapipa dukani kwa Majaaliwa Songomelo.

Hata hivyo,Kamanda Kashai alisema kuwa katika tukio hilo hakuna madhara yaliyotokea kwa binadam.

Wakati huo huo,mkazi mmoja wa Kijiji cha Mafisa Kata ya Mvungwe Tarafa ya Mgera wilayani Kilindi ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya Tumboni, Shingano na Kichwani hali iliyopelekea kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai alithibitisha kutokea tukio hilo ambalo lilitokea Octoba 7 mwaka huu saa 11:30 Marehemu akiwa shambani kwenye kitongoji baina ya Kijiji cha Mafisa wilayani humo.

Kamanda Kashai alimtaja alifariki dunia kwenye tukio hilo kuwa ni Lokoye Machaku (29) kabila Mnguu mkazi wa Maafisa wilayani humo ambayo alichomwa kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali kwenye mwili wake.

Aidha alisema kuwa wakati huo mtu mwengine aliyekuwa ameongozana na marehemu Mohamed Mhina (35) mkazi wa eneo hilo alijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika mkono wake wa kulia.

Kamanda Kashai alisema kuwa tukio hilo lilifanywa na watu wawili wa jamii ya wafugaji na walikuwa wamevaa nguo za kimasai na inasadikiwa kuwa ni wakazi wa kijiji cha Lembapuri wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kugombania malisho ambapo watuhumiwa walilisha mifugo yao kwenye shamba la mabua yaliyokuwa shambani baada ya mavuno katika eneo hilo la mafisa.

Hata hiyo alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kilindi kwa ajili ya uchunguzi wakati jeshi hilo linaendelea na msako mkali kuwatafuta wahalifu waliohusika kwenye tukio hilo.

RAIS KIKWETE ALIPOFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA HOTELI YA PPF MWANZA

October 13, 2014


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa jengo la hoteli ya Gold Crest linalomilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.Wengine pichani toka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo,Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PPF,ndg. Ramadhan Kijjah,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Adam Malima,Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa PPF,William Erio pamoja na Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufuli.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli linalomilikiwa na Mfuko wa PPF jijini Mwanza.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PPF Ndg. William Erio.
Naibu Waziri wa Fedha,Mhe. Adam Malima (Mb) akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli inayomilikiwa na Mfuko wa PPF jijini Mwanza. Ufunguzi huo uliambatana na Rais kutembelea sehemu mbalimbali za jengo hilo la Hoteli.
Jengo la kitega uchumi la hoteli ya PPF Mwanza Gold Crest.
Mamia ya wakazi wa Mwanza wafurika katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli ya PPF Mwanza.
Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF. Pamoja nao ni Waziri wa Ujenzi Mhe. John Magufuli, Naibu wa Waziri wa Fedha Mhe. Adam Malima, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo.
Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya PPF mara baada ya kuzindua jengo la kitega uchumi la hoteli ya PPF Mwanza.
Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa PPF .
Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Ndg. Meshack Bandawe Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa na Mratibu wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli ya PPF Mwanza.

Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya mtoto wa kike yaliyo ratibiwa na WiLDAF yafana jijini Dar es salaam

October 13, 2014
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike yaliyo ratibiwa na Women in Law and Development in Africa - WiLDAF yafana jijini Dar es salaam.

Octoba 11 ya kila mwaka ni siku iliyopitishwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani kote. Maadhimisho haya yalifanyika katika Hoteli ya Double Tree, Dar es Salaam.
Washiriki wa maadhimisho hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mmoja wa washiriki waliofika kwenye hafla hiyo ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto es Kike yaliyoratibiwa na WiLDAF akichangia mada.














WIKI YA MAJANGA KWA VIGOGO "NIGERIA HOI KWA SUDAN.STARS YABUIRUZA BENIN 4-1"

October 13, 2014


BINGWA MTETEZI WA AFCON (NIGERIA) AMEAIBISHWA NA SUDAN KWA KUCHAPWA GOLI 1-


Bingwa mtetezi wa kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), Nigeria, jana ameonja joto la jiwe baada ya kujikuta wakibanwa mbavu na Sudan kwa kuchapwa goli 1-0. Goli hili linaifanya timu ya taifa ya Nigeria chini kocha wa Stephene Keshi kuburuza mkia katika kundi lao lenye timu za Congo Brazaville na Afrika Kusini.

Sudan walipata goli la kwanza na la ushindi mnamo dakika za mwisha wa kipindi cha kwanza ya mpepetano huo kupitia mshambuliaji wao, Bakri Almadina

STARS YAMSHIKISHA ADABU BENIN KWA KUMCHARAZA MAGOLI 4-1 KAMA VILE WALIKUWA WAMESIMAMA


Nahodha wa Stars "Nadir Haroub Cannavaro (kushoto)akishangilia bao lake na Beki wa timu hiyo Oscar Joshua

Watu wengi walikuwa wakiibeza sana Stars kuelekea katika mchezo wa jana dhidi ya Benin, lakini ndiyo hivyo Wahenga walisema, "mdharau mwiba, mguu huota tende" na ndicho kilichowakuta Wa Benin leo katika dimba la taifa licha ya kusheheni nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya kama vile, Stephane Sesegnon anayekipa kunako West Bromwich Albion. 


Magoli ya Stars yalifungwa na beki Haroub Canavaro, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, pamoja naye Juma Luizio. Goli la kufutia kijasho la Benin Lilifungwa na mshambuliaji Sadel akipokea pasi maridadi kutoka kwake kiungo mshambuliaji, Stephane Sesegnon dakika ya 90 ya mchezo huo.
Ushindi huo ni furaha kubwa kwa watanzania ambao walikuwa wamekata tamaa na timu yao ya taifa iliyopo chini ya kocho Mholanzi Mart Nooij kufuatia matokeo mabovu ya hivi karibuni katika michuano ya kuwania tiketi za kupangwa katika makundi ya michuano ya AFCON yatakayo fanyika mwakani nchini Moroco.

KWELI HII NDIO TANGA JIJI, HATA WIKI BADO HEBU JIONEE MWENYEWE

October 13, 2014


KARIBU TANGA, 'WAJA LEO, KUONDOKA MAJALIWA'
Hapa gari likiingia stendi mpya Kange kuchukua abiria kwa ajili ya kufanya safari zake za kawaida

Haya yakiwa yanatoka stendi ya Kange kuelekea mikoani na wilayani

Abiria nao hawakuwa nyuma, hapa wakiwa wamejipumzisha wasipatwe na jua kwenye sehemu za kusubiria magari
  • Huu Ndio Muonekano wa Stendi Mpya ya Mkoa wa Tanga, Kange. KARIBUNI SANA!

VITUO 600 KUTOLEA CHANJO SURUA-RUBELLA TANGA

October 13, 2014


NA EVELINE BALOZI,TANGA.
 ZAIDI ya vituo 600 vya kutolea chanjo vitatumika Mkoani hapa kutolea chanjo ya Surua-Rubella kwa watoto wenye umri wa miezi 9 hadi miaka 15, kampeni itakayoanza tarehe 18 hadi 24 octoba, 2014 kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya, shuleni na vile vitakavyoandaliwa na halmashauri.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni (Mstaafu) Chiku Ghallawa akifungua mkutano wa Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi uliolenga maandalizi ya Kampeni ya chanjo ya Surua-Rubella


Akizungumza kwenye Mkutano wa kamati ya huduma ya Afya ya msingi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga,lLuteni (mstaafu) Chiku Gallawa aliwataka viongozi wa dini wejitolee  kuwahamasisha wananchi katika  maeneo mbalimbali ili waweze kuitikia wito wa kushiriki  katika zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
“Kila mtu kwenye nafasi yake aweke jitihada stahiki kufanikisha zoezi hili, tuwaelimishe jamii kuachana na imani potofu juu ya uvumi kwamba chanjo hizi zinamadhara, serikali ni makini haiwezi kuruhusu chanjo yenye madhara kwa wananchi wake,” alisema Gallawa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Asha Mahita akizungumza kwenye Mkutano huo, muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Gallaawa
Wajumbe wa Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi Mkoa wa Tanga, wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

Wajumbe wa Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi Mkoa wa Tanga, wakifuatilia kwa makini mkutano huo (wawili mbele) pamoja na baadhi ya waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga.


Serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendesha zoezi hilo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na  Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) kwa lengo la kudhibiti magonjwa yayoweza kuzuilika ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuboresha afya za wananchi. 
Nae Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Asha Mahita, alisema pamoja na chanjo hii, watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59  watapatiwa matone ya Vitamini A huku dawa za minyoo zikitolewa kwa wale walio na umri kunzia mwaka 1 hadi miezi 59 na utoaji wa chanjo ya dawa za Matende na Mabusha litawahusisha wananchi wote walio na umri wa kuanzia miaka 5 hadi 100.
Awali mwakilishi wa Wizara ya Afya nchini Dkt Ibrahim Maduhu alisema chanjo hiyo ina umuhimu mkubwa kwa wanawake wenye umri wa kuzaa na wajawazito kwa kuwa itawakinga na athari ya kuzaliwa na ngozi yenye vipele, homa, tatizo la mtoto wa jicho, mtindio wa ubongo, ulemavu na tatizo la Moyo.
Kampeni ya chanjo hii kitaifa itazinduliwa siku hiyo ya Oktoba 18 ambapo zaidi ya asilimia 46 watanzania wanatarajiwa kunufaika ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Linda, Okoa maisha ya Mtoto-kamilisha chanjo”.