KATIBU MKUU UVUVI ATEKETEZA NYAVU HARAMU ZA BILIONI 2.6 MWANZA

February 03, 2018
Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele
Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akishiriki kwenye zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi  zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto kulia mwenye suti ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba akishuhudia,Picha na John Mapepele
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba wa kwanza kulia aliyevaa suti akishirikiana na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana,Mary Tesha zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi  zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara ,Picha na John Mapepele
Na John Mapepele, Mwanza.
Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba ametaifisha na kuteketeza zaidi ya tani mia mbili za shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara .
Mbali na kuteketeza zana hizo haramu, Serikali pia imekusanya zaidi ya shilingi bilioni tano kama sehemu ya adhabu  kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji mwani, samaki na mazao yake nje ya nchi.
Akizungumza na mamia ya wavuvi wakati wa kuteketeza nyavu hizo leo, katika dampo la Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza, Dkt. Budeba amesema hatua hizo kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi kuwaonea wafanyabiashara au wavuvi wanyonge bali zimelenga kuwatengenezea maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali zilizoko ziwani.
Aidha Dkt. Budeba amesisitiza kuwa kikosi hicho kitaendelea na operesheni hiyo bila kuchoka hadi hapo uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi utakapokwisha ndani ya ziwa hilo.
Pia aliwaonya wamiliki wa  viwanda na wafanyabiashara wanaotengeneza na kuuza nyavu hizo ambapo amesema Serikali ikiwabaini itawachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na  kuwafutia leseni zote za biashara zao.
  Alisema rasilimali  zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi viongozi wamepewa dhamana ya kuongoza kazi ya ulinzi tu na endapo uvuvi haramu utakomeshwa wananchi ndiyo watakaonufaika.
Pamoja na kuteketeza nyavu hizo haramu, Dkt Budeba alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) mwaka 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6  hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Fatma Sobo amesema Idara itaendelea kutumia Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na Sheria  nyingine za Mazingira ili kudhibiti Uvuvi haramu nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha alisema Serikali ya Wilaya hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi haramu ili kulinda rasimali  hiyo muhimu waliyopewa na Mungu.
Kwa upande wao baadhi ya wavuvi walimuomba Dkt. Budeba kuwasiliana na Wizara ya Viwanda na Biashara, ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa ambazo zinatengenezwa viwandani na baadae kuuziwa wavuvi.
Hivi karibuni watendaji wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana  na kikosi kazi kilichoundwa na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi  wameweza kukamata  nyavu haramu, meli za uvuvi kutoka nje ya nchi zinazovua bia kufuata taratibu na mazao ya uvuvi yanayotoroshwa nje ya nchi ikiwemo  mwani na samaki yenye mabilioni ya fedha huku Waziri Mwenye dhamana ya sekta hiyo Luhaga Mpina kuahidi kuwa  operesheni hizo zitakuwa za kudumu hadi uuvi haramu utakapokoma.

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO ATATUA MGOGORO WA LESENI YA MADINI ULIODUMU KWA MIAKA 10

February 03, 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018. Picha zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya uchimbaji baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018

Na Mathias Canal, Shinyanga

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametatua mgogoro wa leseni uliodumu kwa takribani miaka kumi kwa kuamuru kupitia haraka eneo la leseni ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine.

Mhe Biteko ametoa agizo hilo Jana 3 Februari 2018 wakati akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama kufuatia malalamiko ya Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe Ezekiel Maige sambamba na malalamiko ya wachimbaji wadogo waliyoyawasilisha Wizara ya Madini Mjini Dodoma Januari 26, 2018.

Alisema kuwa wananchi walifunga safari mpaka ofisi za madini kwa ajili ya kupata uhalali wa kupimiwa eneo lao kwa kutumia GPS lakini Kaimu Afisa madini mkazi Wilaya ya Kahama akawabadilishia Nukta (Coordinator) ambazo baadaye zilionekana kuwa za eneo jingine ambalo ni mbuga isiyokuwa na madini huku eneo hilo likihamishiwa kwa ntu mwingine.

Mhe Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya madini Prof Simion Msanjila kumchukulia hatua za haraka za kinidhamu aliyekuwa Kaimu Afisa madini mkazi Wilaya ya Kahama aliyehusika na upotoshaji wa leseni na kuzua mgogoro wa usumbufu usiokuwa na sababu dhidi ya wananchi na serikali.

Alisema kuwa hakuna sababu ya Wizara ya Madini kukumbatia mgogoro huo wa leseni uliodumu kwa miaka kumi kwa sababu ya eneo ambalo lilipotoshwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya madini kwani jukumu la serikali ni kuwatumikia wananchi ikiwemo utatuzi wa kadhia mbalimbali zinazowakabili katika jamii.

Mhe Biteko kwa msisitizo mkubwa amewataka wachimbaji wadogo kuwa waaminifu na kufichua baadhi ya wachimbaji wanaoficha madini kwa kutorosha bila kulipa kodi kwani kufanya hivyo itakuwa njia pekee ya kuisaidia serikali na kuinusuru katika mtego wa wizi wa rasilimali hizo.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli haitawafumbia macho wamiliki wa leseni hizo ambao leseni zao zimedumu kwa muda mrefu bila kuzifanyia kazi kwani hawazalishi ajira yoyote wala kulipa kodi Hivyo serikali imekusudia kuzifuta na kuwapa watu wengine ambao watazifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuongeza tija kwa sekta ya madini katika uchangiaji wa pato la Taifa.

Akitoa mfano katika eneo la Kahama kuna leseni 249 lakini zinazofanyiwa kazi ni 18 tu huku wenye leseni zisizofanya kazi wakisubiri wachimbaji wadogo wavumbue madini kisha huja kuwaondoa kwa kisingizio cha umiliki wa leseni. Leseni hizo zikiwa zimedumu kwa muda mrefu bila kuendelezwa.

Aidha,  alisema kuwa kuna maeneo makubwa manne ambayo yameshaamuliwa na serikali kutengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo ikiwemo eneo la Nyang'wale lenye hekari 996, eneo la Nyangarata lenye hekari 1074, Eneo la Buzwagi kilometa za mraba 53.4 na eneo la Kinamyuba kilomita za mraba 33.3

Alisema kuwa jukumu la serikali ni kutatua kero za wananchi sio kuwaongezea kero wananchi hivyo watendaji wote wa serikali wanapaswa kutimiza ndoto ya Rais Magufuli kwa kuwatumikia wananchi kwa imani na matendo imara kwa kuwanufaisha watumishi na rasilimali zao.

Sambamba na hayo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amewataka wananchi kuendelea na uchimbaji wakati taratibu zikifuatwa kukamilisha kumaliza mgogoro huo huku akiwahakikishia kutoondolewa tena na endapo kama watakuwa wanahitaji maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo wanapaswa kufuata taratibu za kisheria zilizoainishwa.

Awali mbunge wa Msalala Mhe. Ezekiel Maige alimweleza Mhe. Naibu Waziri kuwa watu wake wameonewa kwa muda mrefu na yeye akifuatilia mgogoro huo bila mafanikio.

"Ni kwasababu ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kimbilio la wanyonge, mheshimiwa Naibu Waziri nilikua nimekata tamaa" Alikaririwa Mhe Maige aliyekuwa akizungumza kwa hisia huku akishangiliwa na mamia ya wachimbaji wadogo waliokisanyika kwenye mkutano huo.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI ILI KURAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA ZAKE

February 03, 2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (MB), akizungumza kwenye warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma Februari 3, 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, na katikati ni Mwenyekiti wa Warsha hiyo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamatui ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Najma Giga.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, DODOMA

KUANZISHWA kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo kuna ongezeko la maeneo ya uzalishaji hususan viwanda kunakokwenda sambamba na ongezeko la matukio ya athari zinazotokana na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewaambia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa wabunge kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), mjini Dodoma Februari 3, 2018.

Mhe. Mhagama alisema warsha hiyo ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria  kutaka wabunge wajengewe uelewa wa shughuli za Mfuko huo.

Akifafanua zaidi Mhe. Waziri alisema Mfuko uliundwa Julai 2015 chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 ili kulipa Fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kwa mujibu wa mkataba.
Alisema, Serikali ilianzisha Mfuko huo  kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata Mafao bora ya Fidia tofauti na Sheria ya zamani ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo viwango vyake vya Mafao ya Fidia vilikuwa vya chini mno.
“Mathalan viwango vya juu vya Fidia kwa Mfanyakazi aliyepata ajali kazini ilikuwa ni shilingi 108,000/= huku Mfanyakazi aliyefariki katika ajali ama ugonjwa kutokana na kazi anayofanya kwa mujibu wa Mkataba wa ajira yake ilikuwa ni shilingi 83,000.” Alibainisha Mhe. Waziri.
Alisema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, mafanikio mbalimbali yamefikiwa ikiwa  ni pamoja na kupata hati safi kwa hesabu za mwaka 2015/2016 na 2016/2017 zilizokaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), usajili wa waajiri 12,546 hadi kufikia Januari 31, 2018, na kulipa Fidia kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kwa wafanyakazi 1,144.
"Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17) na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambavyo vinatekelezwa kwa kasi kubwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinalenga kukuza uchumi wa viwanda na kuboresha maisha ya Watanzania na hatimaye kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025." Alisema Mhe. Waziri.
"Katika kuhakikisha Mfuko unaendelea kuboresha huduma zake na kuhakikisha wadau wanapata huduma kwa urahisi zaidi na katika ufanisi wa hali ya juu, Mfuko utafungua ofisi mikoani kwa awamu." alisema.
Kwa sasa Mfuko unatekeleza majukumu yake mikoani kwa kutumia Maafisa Kazi wa Mikoa.  
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema, katika mazingira yab sasa ambapo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda, jukumu la Mfuko halitakuwa kulipa Fidia pekee bali pia kubuni, kukuza na kuendeleza mbinu za kupunguza ama kuzuia kabisa ajali katika maeneo ya kazi.
“Ili kuwezesha kufanikisha hilo, Waheshimiwa wabunge mnao umuhimu wa kipekee katika kutoa uelewa sahihi wa madhumuni, majukumu na uendeshaji wa Mfuko.”
Matarajio ya Mfuko ni kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau wote, (Waajiri, wafanyakazi, Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, hospitali na vyombo vya habari, alifafanua  Bw. Mshomba.
Akizungumzia majukumu muhimu ya Mfuko, Bw. Mshomba alitaja kuwa ni pamoja na kusajili waajiri na wafanyaakzi, kukusanya michango kutoka kwa waajiri, kulipa fidia stahiki kwa mfanyakazi na wategemezi na kuwekeza ili kujenga uwezo wa kulipa fidia.
Katika warsha hiyo ya siku moja, waheshimiwa wabunge walipata fursa ya kuelimishwa juu ya utaratibu unaotumika kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi aliyoajiriwa kwa mujibu wa mkataba ili hatimaye Mfuko utoe Fidia stahiki.
Lakini pai wabunge walielezwa muundo wa Mfuko huo ambapo umezingatia mfumo jumuishi, kwa maana ya kuwa na bodi ya uwakilishi wa makundi mbalimbali ili kukidhi malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko.
 
  Mhe. Najma Giga(katikati), akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, iliishauri serikali juu ya umuhimu wa waheshimiwa wabunge kukutana nna wataalamu kutoka WCF ili kuwajengea uelewa wa shughuli za Mfuko. 
 Mhe. Andrew Chenge, akizunhgumza kwenye warsha hiyo.
 Baadhi ya waheshimiwa wabunge na viongozi wa WCF wakifuatilia warsha hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya  uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya  uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.

 Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Mhe.Mama Salma Kikwete, akisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba wakati wa warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter akitoa mada juu ya muundo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na uongozi na bodi ya wadhamini ambayo ni shirikishi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar, akitoa mada kuhusu utaratibu unaotumika kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi aliyoajiriwa kwa mujibu wa mkataba kabla ya Mfuko kutoa Fidia.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, akizungumza.

Baadhi ya waheshimiwa wabunge kwa shauku kubwa wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa WCF.

Kutpka kushoto, Mhe. Jenista Mhagama, Mhe. Andrew Chenge na Mhe. Najma Giga, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Timu ya wataalamu wa WCF, kutoka kushoto ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba,  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter, Mkurugenzi wa Huduma za Fedha na Utawala, Bw.Bezil Kwala, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar na Mkuu wa Huduma za Sheria Bw. Abraham Siyovelwa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Mhe. William Lukuvi, (katikati), akibadilishana mawazo na  Meneja Madai (Claims), wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, (kushoto na Meneja Matekelezo, (Compliance), Bw.Bw.Victor Luvena mwishomi mwa warsha hiyo.
Wabunge juu na chini wakipitia vipeperushi vyenye maswali na majibu kuhusu shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, 9WCF), wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa kuhusu Mfuko huo.





Mbunge wa Nkasi, Mhe. Ali Kesy(kulia) na mbunge mwenzake wakiwa kwenye warshan hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Fedha na Utawala, Bw.Bezil Kwala, akizungumza mbele ya waheshimiwa wabunge.
Meneja Madai (Claims), wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, akizunguzma kwenye warsha hiyo ya wabunge.

Mbunge  wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe.Ndugu Cosato David Chumi, akizungumza kwenye warsha hiyo.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, (Kusbhoto), akiteta jambo na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, (katkati) na Mhe. Mbunge ambaye jina lake halikupatikana wakati wa warsha hiyo.
Mhe. Waziri na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, wakiwa katika picvha ya pamoja na uongozi wa WCF.
Mhe. Waziri Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula, (wapili kulia), Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wabunge na viongozi wengine wa Mfuko, wakiwa katika picha ya pamoja
Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, akipeana mikono na Mkuu wa Mkuu wa Huduma za Sheria Bw. Abraham Siyovelwa. 

Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Mshomba na viongozi wengine wa Mfuko huo. 
-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com

RAIS DK.MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAOFISA WAPYA 192 JWTZ,WAMO PIA WA NCHI MARAFIKI

February 03, 2018
 AmiriJeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pamoja na Maafisa kadhaa kutoka nchi marafiki katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakivalishana vyeo mara baada ya Kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakila Kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kutunukiwa Kamisheni.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli (TMA) Meja Jenerali Paul Peter Masao katika picha ya pamoja  na Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki mara baada ya kuwatunuku Kamisheni.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati Bendi ya Jeshi la Ulinzi ilipokuwa ikitoa burudani katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kuisha kwa shughuli za Kutunuku Kamisheni.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kutunuku Kamisheni katika Viwanja vya Ikulu
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki. PICHA NA IKULU
RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ, AWAAPISHA MWANASHERIA MKUU, NAIBU WAKE NA MAJAJI WAWILI LEO IKULU DAR ES SALAAM

RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ, AWAAPISHA MWANASHERIA MKUU, NAIBU WAKE NA MAJAJI WAWILI LEO IKULU DAR ES SALAAM

February 03, 2018
michu 3 (1)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Paul Joel Ngwembe Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018
MICHU 4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Gerson J. Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018 
MICHU1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia Viongozi hao wakila kiapo mara baada ya kuapishwa
michu3c
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018
m1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Mhe. George Mcheche Masaju  akiongea machache baada ya kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama kuu   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018
m2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Mhe. Gerson J. Mdemu akiongea machache baada ya kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama kuu   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018 
m3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi  akiongea machache baada ya kumwapisha   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018 
m4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Naibu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Mhe. Paul Joel Ngwembe akiongea machache baada ya kumwapisha   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018 
m5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe. Gerson J. Mdemu baada ya kumuapisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018. Kushoto ni  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi  na kulia ni  Jaji wa Mahakama kuu  Mhe. George Mcheche Masaju    Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018  
m6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mama Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, waziri wa katiba na sheria Profesa Palamagamba Kabudi,  Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika picha ya kumbukumbu na walioapishwa  ma-Jaji wa Mahakama kuu  Mhe. George Mcheche Masaju na Mhe. Gerson J. Mdemu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Paul Joel Ngwembe baada ya kuwaapisha  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018
Picha na IKULU