Kampuni ya matangazo ya Kwanza yatangaza neema kwa watangazaji na wachapishaji

September 18, 2017

 Meneja Bidhaa  wa Kwanza Advertising Network, Leon John akieleza namna ya jukwaa hilo litakavyofanya kazi ambapo mtandao huo utaunganisha kampuni za uzalishaji, wachapishaji mtandaoni na wate
Baadhi ya wachapishaji (Blogers) wakifuailia kwa makini uzinduzi huo katika hafla iliyofanyika mapema leo katika Hoteli ya Hyatt 
Meneja wa Masoko ya Digitali kutoka kampuni TECNO ambayo ni miongoni mwa kampuni zilizomo kwenye jukwaa hilo, Bw. Kelvin Boniface(wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi mtendaji wa KONCEPT na katibu wa Tanzania Blogers Network  Bw. Krantz Mwantepele (wa kwanza kulia) akichangia jambo kuhusu uelewa wake juu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa upande wa Blog.Meneja bidhaa kutoka Kwanza Advertising Network, Leon John (wa kati kati)


Meneja Mawasiliano wa  Kwanza Advertising Network, Herman Mkamba akieleza vigezo vitakavyotumika kuchagua mitandao na Blog zitakazo jiunga kwenye jukwaa hili.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kwanza Edwin Bruno (mwenye suti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waaalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Kwanza Advertising Network mapema leo katika Hoteli ya Hyatt Regency.
 Meneja Bidhaa  wa Kwanza Advertising Network, Leon John akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa Kwanza Advertising Network.

Dar Es Salaam Septemba 18, 2017: Kampuni ya matangazo ya Kwanza Advertising Network, leo imezindua huduma mpya, itakayowezesha biashara mbali mbali na watangazaji kuwafikia mamilioni ya wateja kupitia simu za mkononi, tovuti na mtandao wa intaneti

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018

September 18, 2017
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah katikati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga leo kuhusu bei elekezi ya korosho msimu wa 2017/2018 kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Maokola Majogo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)Hassani Jarufu    

Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia
 Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Mbaruku Yusuph wa Gazet la Tanzania Daima,Amina  Kingazi wa Gazeti la The Guardian mkoani Tanga,Burhan Yakub wa Mwananchi
 Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kulia ni Sussan Uhinga wa gazeti la Mtanzania Tanga,Pamela wa Tanga One Blog wakifuatilia
 Mwandishi wa gazeti la Habari Leo mkoani Tanga Anna Makange akiuliza swali kwenye mkutano huo
 Mwandishi wa Clouds TV Mkoani Tanga Gift Kika akiuliza swali kwenye mkutano huo kulia ni Amina Omari wa gazeti la Mtanzania
BODI ya Korosho Tanzania imetangaza bei elekezi kwa msimu 2017/2018 kwa kilo moja ya Korosho ghafi daraja la kwanza (Standard Grade) kitakuwa ni sh.1,450 huku kilo moja ya daraja la pili itakuwa ikiuzwa kiasi cha sh.1,160.

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Anna Abdallah wakati  akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu ufunguzi rasmi wa soko la  Korosho msimu wa mwaka 2017/2018.

"Niseme tu bei hii elekezi ya korosho imetangazwa na bodi hiyo kwa mamlaka waliopewa chini ya kifungu cha 5(3)(d) ambapo bei hiyo imefikiwa baada ya utafiti wa kupata gharama halisi za kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi na kuongeza asilimia 20 kama faida ya mkulima "Alisema.

Alisema kwa msimu huu gharama ya kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi ni 1,208.39 na  asilimia 20 ya faida kwa kilo ni sh.241.68 .

Aidha alisema katika mjengeko wa bei ya korosho ghafi msimu wa 2017/2018 ambapo magunia na kamba vitatolewa na serikali kupitia CBT huku chama cha msingi kikipata sh.90.00,Halmashauri ya wilaya ikipata asilimia 3 ya sh.43.50,mfuko wa wakfu ukipata sh.10.00 ambapo jumla ya gharama ni 143.50 wakati bei elekezi ikiwa ni 1,450.00 na mjengeko wa bei ukiwa ni tsh.1,593.50.

Aliongeza kuwa katika msimu wa ununuzi wa korosho 2017/2018 utafunguliwa rasmi Octoba Mosi mwaka huu huku akiwahimiza wadau wote wanaohusika na uuzaji na ununuzi wa zao la korosho kukamilisha maandalizi ya msimu kabla ya ununuzi kuanza.

"Wadau hao ni pamoja na Sekretarieti za mikoa,halmashauri za wilaya,Wakulima,Vyama vya Ushirika vya Msingi,Vyama Vikuu vya Ushirika,Wakala wa Vipimo,Bodi ya Leseni za Maghala,Waendesha Maghala,Wasafirishaji,Wanunuzi,Mamlaka ya Bandari,Mabenki na wengine ambao wanahusika kwa namna moja au nyengine"Alisema.

Akizungumzia suala la utoaji wa leseni za ununuzi wa korosho, Mwenyekiti huyo alisema  bodi hiyo inatumia fursa hiyo kuwahamasisha wanunuzi wa zao hilo wa ndani na nje kuomba leseni ya ununuzi kwa ajili ya msimu wa 2017/2018.

"Leseni hii itatolewa bila malipo yeyote,Fomu namba 2 ya maombi ya leseni za ununuzi wa korosho ghafi inapatikana kwenye tovuti ya bodi ya korosho Tanzania (www.cashew.go.tz) na kwenye ofisi zake zilizopo Mtwara(Makao Makuu) na kwenye matawi yake ya Dar es Salaam,Tanga na Tunduru "Alisema

Hata hiyo alisisitiza umuhimu wa wauzaji,wanunuzi na wadau wa korosho kufuata mfumo wa stakabadhi  ghalani wa kuuza na kununua korosho huku akitoa wito kwa yeyote atakayekiuka sheria,kanuni na mwongozo namba 1 wa mwaka 2017/2018 wa mauzo ya korosho,atachukuliwa hatua kali ikiw ni pamoja na kutaifishwa korosho.


SEND OFF YA DKT CHRIDA DUNCAN NDANSHAU YAFANA

September 18, 2017

  Mandhari ya ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku
 Bibi wa Bi Harusi Mtarajiwa akitoa wasia kwa mjukuu wake katika ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku. Wazazi wa Dkt. Chrida wakisikiliza kwa makini
  Bibi wa Bi Harusi Mtarajiwa akitoa wasia kwa mjukuu wake katika ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku. Wazazi wa Dkt. Chrida wakisikiliza kwa makini
 Dkt. Chrida Duncan Ndanshau alivyotokelezea  Jumamosi usiku. 
TANZANITE YAREJEA DAR KUIVAA NIGERIA

TANZANITE YAREJEA DAR KUIVAA NIGERIA

September 18, 2017
Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 (Tanzanite), Sebastian Nkoma, amekipongeza kikosi chake kwa kiwango walichokionyesha kwenye mechi dhidi ya Nigeria iliyofanyika Jumamoisu kwenye Uwanja wa Samuel Ogbemudian mjini hapa.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Nkoma, alisema kuwa kufungwa ni sehemu ya mchezo, lakini aliweka wazi vijana wake walipambana ila hawakuwa na bahati ya kupata matokeo waliyoyatarajia.
Kocha Nkoma alisema anaamini watafanya vizuri katika mechi ya marudiano itakayofanyika jijini Dar es Salaam huku akisema wana nafasi ndogo ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Mchezo wa marudiano utafanyika Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, uliko Chamazi, Dar es Salaam.

"Kazi haijamalizika, mmefanya kazi kubwa na mmewashangaza wote walioiangalia mechi hii, waliamini wangepata ushindi mnono zaidi ya huu, naamini tutafanya vyema katika mechi ya marudiano," alisema kocha huyo ambaye pia anafundisha timu ya wakubwa ya wanawake ‘Twiga Stars’.

Mkuu wa Msafara, Amina Karuma, alisema kuwa mapambano bado yanaendelea na anaamini kikosi chake kitashinda katika mechi ya marudiano itakayochezwa baada ya wiki mbili.

"Msife moyo wanangu, huu ndio mpira na unamatokeo ya aina tatu, naamini mtawashangaza tena tukia nyumbani," alisema Karuma ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake Tanzania (TWFA) .

Aliongeza kuwa anashikuru wachezaji wote ni wazima na wataendelea na kambi ili kujiandaa na mchezo wa marudiano huku akiahidi kuwatafutia mechi ya kirafiki kabla ya kuwakaribisha Nigeria.
LHRC kuwanoa kisheria wasichana Shinyanga kupambana na maambukizi ya VVU

LHRC kuwanoa kisheria wasichana Shinyanga kupambana na maambukizi ya VVU

September 18, 2017
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la IDLO kimezindua mradi wa Kuwajengea Uwezo wa Kisheria Wasichana na Wanawake Wadogo mkoani Shinyanga ili Kuweza Kuiwajibisha Jamii Kutoa Huduma Bora za Afya ya UKIMWI.
Katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika Septemba 14 katika manispaa ya Shinyanga na Septemba 15 katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, makundi lengwa ya mradi huo ikiwemo wasichana na wanawake wadogo, wazazi, viongozi wa serikali na Jamii kwa ujumla yameonyesha kuvutiwa na malengo na matokeo tarajiwa ya mradi huo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakati wa kuzindua mradi huo Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Bw. Charles Maugila amesema ujio wa mradi huo katika Manispaa ya Shinyanga ni wa kufurahiwa kwani mkoa wa Shinyanga kwa ujumla unakabiliwa na changamoto kubwa ya kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI hususani kwa wasichana na wanawake wadogo. “Kumekuwa na miradi mingi inayolenga kukabiliana na ukatili wa kijinsia na UKIMWI lakini mradi huu ni wa kipekee kwa vile unalenga kuwajengea uwezo wa kisheria wasichana na wanawake wadogo ambao ndio wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI  waweze kuwajibisha jamii kwa kudai huduma bora za afya ya UKIMWI” Alisema Maugila.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Bw. Anthony Ndanya ameitaka Jamii ya Kahama kushiriki kikamilifu na kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo na kupata matoke tarajiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bw. Ezekiel Massanja alisema “kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2016, ukatili wa kijinsia ukijumuisha ukatili wa majumbani, ukatili wa kingono, mimba za utotoni, ndoa za utotoni pamoja na vitendo vingine vya kikatili kwa watoto na wanawake vimezidi kuongezeka maradufu mbali na kuwepo kwa sheria zinazolinda kundi hilo. Moja ya matokeo ya changamoto za ukatili kwa wanawake ni kuambukizwa virusi vya UKIMWI”.
“Sambamba na ongezeko la vitendo vya kikatili, Jamii inakosa uwezo wa kuwawajibisha watekelezaji wa vitendo vya kikatili na kushindwa kukabilianan na madhara ya ukatili wa kijinsia kutokana na ukosefu wa elimu ya sheria na namna ya kudai upatikanaji wa huduma bora za afya” – Aliongeza Massanja.
Mradi huu ni moja ya miradi mingi ya Dreams Innovation Challenge inayotekelezwa nchini.  Mradi umejikita kuwajengea uwezo wasichana wa miaka 15 hadi 24 na jamii kwa ujumla juu ya masula ya kisheria, afya na ukatili wa kijinsia. Mradi unalenga kuwapa uwezo wasichana kuiwajibisha jamii pale haki zao za msingi zinapokosekana hasa kwenye masuala ya afya ya UKIMWI.
Lengo kuu la mradi ni kuimarisha uwezo wa jamii kuboresha huduma za afya ya UKIMWI kwa wasichana na wanawake wadogo kupitia mbinu ya uwezeshaji kisheria na uwajibikaji kijamii.
Mradi unalenga kufikia jumla ya wasichana 1000 wenye umri kati ya miaka 15 – 24. Wasichana 500 Shinyanga na 500 wilayani Kahama. Wanufaika wengine ni pamoja na wanaume ambao ni wapenzi wa wasichana hao, wazazi, watoto, vyombo vya sheria, wahudumu afya pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Inline image 1
Baadhi ya wasichana na wanawake wadogo watakaofikiwa na mradi katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wilayani Kahama.
Inline image 2
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Bw. Charles Maugila akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Dreams Innovation Challenge wilayani humo.

Mobile: +255789147255
Information Officer
Legal and Human Rights Centre

"For a Just and Equitable Society"