TANESCO SUMBAWANGA YAPOKEA JENERETA YA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 10.

February 07, 2018
  NA SAMIA CHANDE, SUMBAWANGA
KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta  ya kufua umeme yenye uwezo  wakuzalisha MegawatI 10 zitakazoimarisha uzalishaji wa umeme mkoani humo.
Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo, Meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Bw.Herini Muhina, alisema, hali ya uzalishaji umeme itakuwa bora zaidi na hivyo kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga, Laila, Kalambo na Nkasi kuwa bora zaidi.
“Nimatumaini yetu kuwa ongezeko hilo la umeme, litasaidia kwenda sambamba na mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kwani umeme wa uhakika utakuwepo na hivyo kufanya Mkoa wa Rukwa kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza kwenye sekta hiyo ya viwanda.” Alitoa hakikisho Bw. Muhidin.

  Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali Watu wa TANESCO Makao Makuu, Bw. Nathan Daimon (watatu kushoto), akipta maelezo kutoka kwa mdhibiti na mwendeshaji mifumo ya umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw.Halfan R. Seba  kuhusu jenereta ujio wa jenereta yenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 10 kwenye kituo hicho.

Bw. Daimon akipewa maelezo zaidi ya uendeshaji shughuli za TANESCO mkoani Rukwa.
 
 

-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com

MPINA APANGUA HOJA ZA WABUNGE KUHUSU NAMNA WIZARA YAKE INAVYOPAMBANA KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU NCHINI

February 07, 2018
 Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina,  Injinia Arcard Mutalemwa (Mwenye shati jeupe), kufanya tathmini ili kujua  uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) akikabidhi  ripoti ya kazi hiyo jana  kwa Waziri Mpina na viongozi wakuu wa Wizara hiyo. Mhe. (Picha na John Mapepele)
 Picha ya pamoja  baina ya Kamati iliyoundwa na Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye suti nyeusi na miwani) kufanya tathmini ili kujua  uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) kushoto kwake ni  Injinia Arcard Mutalemwa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Maria Mashingo Katibu Mkuu wa Mifugo, kulia ni Naibu Waziri Abdalah Ulega na Mtendaji Mkuu wa NARCO,Profesa  Philemoni Wambura (Picha na John Mapepele)
 Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina,  Injinia Arcard Mutalemwa (aliyesimama), kufanya tathmini ili kujua  uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) akisoma na kuwasilisha  ripoti ya kazi hiyo jana  kwa Waziri Mpina na Viongozi wakuu wa Wizara hiyo.(Picha na John Mapepele)
Mtendaji Mkuu wa NARCO,Profesa  Philemoni Wambura akichangia hoja kwa Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina,  kwenye kikao cha kukabidhi taarifa ya kamati ya kufanya tathmini ya uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) jana.(Picha na John Mapepele)
Na John Mapepele, Dodoma
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepangua hoja zilizotolewa na wabunge kuhusu namna Wizara yake inavyopambana kutokomeza uvuvi haramu ili kunusuru  kupotea kabisa kwa samaki na kuchochea kufa kwa viwanda vya  samaki na kusababisha kupungua kwa ajira nchini.
Waziri Mpina alitoa ufafanuzi huo wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge bungeni  Mjini Dodoma ambao walikosoa hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo katika kupambana na uvuvi haramu hususan katika Ziwa Victoria pamoja na kudhitibi utoroshaji wa samaki na mazao yake nje ya nchi.
 “Mimi na Wizara yangu tutahakikisha hili tunalisimamia kwa nguvu zote, hizi ni rasilimali za taifa na haziwezi kugawanwa kwa ukanda, rasilimali hizi zinapashwa kunufaisha nchi nzima kwa hiyo kama Wizara inayosimamia Sheria zilizopitishwa na Bunge hili tutahakikisha kwamba hakuna kabisa uvuvi haramu katika nchi yetu, hakuna mfanyabishara atakayejihusisha na kuuza wala kusambaza nyavu haramu, hakuna kiwanda kitakachochakata samaki wasioruhusiwa, hakuna mtu yoyote atakayevua kwa vyavu haramu wala kufanya biashara haramu ya mazao ya uvuvi ni lazima mali zetu tuzilinde kwa nguvu zote” alisisitiza.
Akifafanua hoja hiyo alisema  Wizara  yake katika kupambana  na suala la uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi inatumia Sheria  ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009, Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 1998, na marekebisho yake  ya mwaka 2007,Sheria ya Mazingira namba 20 ya Mwaka 2004, Sheria ya Uhujumu Uchumi (Economic and organized crime Act Cap 200 CE 2002 as amended  by Act no 3 of 2016) na Sheria ya  Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu namba 29 ya mwaka 1994. 
Wabunge hao waliokuwa wakichangia taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ni pamoja na Joseph Msukuma wa Geita Vijijini, Constantine Kanyasu na Geita mjini na Dk Raphael Chegeni wa Busega
Mpina alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Wizara yake samaki aina ya Sangara wanaoruhusiwa kuvuliwa wenye urefu wa kati ya sentimita 50 mpaka 85 wamebaki asilimia 3 samaki wazazi wamebaki asilimia 0.4 samaki wachanga wasioruhusiwa kuvuliwa chini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6  kwa mantiki hiyo hatuna samaki wanaofaa kuvuliwa katika Ziwa Victoria.
Alisema Kamati hiyo imezungumzia juu ya viwanda vya samaki kufungwa ambapo kabla uvuvi haramu haujashamiri kulikuwa na viwanda 13  vilivyokuwa na uwezo wa kuchakata tani 1, 065 na kutoa ajira 4,000 katika ukanda wa Ziwa Victoria lakini kutokana na kuendelea na uvuvi haramu vimepungua na kubaki 8 vyenye uwezo wa kuzalisha tani 171 na kusababisha kubaki na ajira 2,000 tu.
Mpina aliongeza kuwa Kamati ya Bunge imetoa msukumo mkubwa kwa Wizara hiyo kupitia katika ukurasa wa 32 wa taarifa yao kwamba Serikali iongeze bidii katika kupambana na uvuvi haramu sambamba na kuhakikisha wale wanaotorosha samaki na mazao yake wanawadhibitiwa vilivyo.
Aidha, Mpina alisema katika operesheni hiyo, maamuzi hayafanywi na mtu mmoja katika kutafsiri mambo mbalimbali ikiwa ya vipimo vya nyavu za ngazi mbili au tatu badala yake timu nzima ya wataalamu inachambua na kuishauri Serikali hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Aliongeza kwamba Kamati hiyo imejuisha Maafisa Uvuvi, Maafisa kutoka Baraza la Mazingira la Taifa(NEMC), Jeshi la Polisi,Ofisi ya Rais, Tamisemi, Idara ya Uvuvi .
“Lakini mheshimiwa Mwenyekiti mambo tuliyoyaona kwenye operesheni hii yanatisha zipo gari za waheshimiwa wabunge tumezikamata na samaki haramu,wapo wenyeviti wa halmashauri ,wapo wenyeviti wa vijiji, madiwani, watendaji wa Serikali  tumewasimamisha kazi  kwa hiyo katika operesheni hiyo tulipokagua viwanda tukakuta viwanda vyote  vinachata samaki wasioruhusiwa, tumekamata viwanda vya nyavu haramu”alisema.
Aidha baadhi ya Wabunge akiwemo  Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba kwa nyakati tofauti walimtaka Waziri Mpina kutaja hadharani majina ya wabunge hao wanaotuhumiwa kufadhili uvuvi haramu. 
“ Waziri amesema katika shughuli hii ya kutokomeza uvuvi haramu kuna magari ya wabunge yamekamatwa na samaki ambao wamevuliwa kiharamu,kuna wenyeviti wa halmashauri ambao magari yao yamekamatwa na samaki ambao wamevuliwa kiharamu hawa watu ni wabaya wanaangamiza Taifa letu nakuomba mheshimiwa Waziri uwataje watu hawa ili tuwalaani” alisema Serukamba.
Aidha Waziri Mpina alisema kwa sasa timu yake inakamilisha taarifa ya awamu ya kwanza ya operesheni Sangara mwaka 2018 inayoendelea ambayo iko mbioni kumaliza na kwamba ataifikisha mbele ya kamati na baadae taarifa hiyo itaingia bungeni.
Kufuatia mjadala huo,Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu aliwataka wabunge kuacha kumpa taarifa Waziri Mpina kwani tayari ameshaeleza kuwa taarifa ikikamilika ataiwasilisha kwenye kamati. 
“Waziri ameeleza vizuri ,tuhuma za watu amezitaja taarifa inaandaliwa itawasilishwa kwenye muda muafaka end of the story sasa ninyi mnakataa nini hatupigi daku hapa kuanzia sasa hakuna taarifa yoyote mhe Waziri maliza..”alisema Zungu.
Aidha Waziri Mpina alisema Serikali imekamata zaidi ya kilo 133,000 ya samaki aina ya kayabo na dagaa zikitoroshwa kwenda Rwanda, Burundi, Kongo na Kenya, pia wamekamatwa samaki wachanga kilo 73,000 ambazo rasilimali hizi zote za nchi zinachezewa kwa kiasi huku operesheni hiyo ikiwakamata hadi raia wa kigeni kutoka Rwanda, Kenya na Burundi wakiwa ndani ya visiwa wakishiriki uvuvi na kununua samaki jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Pia walikamata viwanda vya mabondo 22 vinafanya biashara lakini vilivyokuwa na leseni halali ni viwili tu hivyo Serikali ikisema inapambana na uvuvi haramu inapambana kweli kweli huku akisisitiza kuwa operesheni hiyo haina mwisho hadi uvuvi haramu utakapomaliza hapa nchini
Kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu  Waziri Mpina alisema tayari Serikali imeshapata meli ya kufanya doria kwani ilizoeleka meli hizo zinakuja kuvua na kuondoka huku taifa letu linaachwa halina chochote.
“Tunashindwa kukusanya chochote na ndio maana kwa mara ya kwanza tumekamata meli na kuipiga faini  milioni 770 nilitegemea Bunge hili litapongeza jitihada hizi kubwa za Wizara ambazo zinalinda rasilimali hizi leo hii mkakati wa kulinda uvuvi wa bahari kuu tutazikagua meli zote zikiwa zinavua huko huko hakuna mtu atakayeondoka kwenye maji ya Tanzania akiwa amebeba rasilimali za watanzania”alisema. 
Alisema Serikali itaongeza meli mbili za doria katika ili kuhakikisha uvuvi wa bahari kuu pamoja na bahari nzima unalindwa kwa nguvu zote na kuhakikisha kwamba rasilimali  nchini mwetu zinanufaisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Hataruhusiwa mtu yoyote na niseme Mheshimiwa Mwenyekiti kama mtu atajishughulisha na uvuvi haramu aache mimi Mpina hata Mzee Mpina mwenyewe ninyi doria mkamateni kama anajishughulisha na uvuvi haramu hatuwezi kuongelea kwa maneno mepesi mambo makubwa ya mstakabali wa taifa letu’alisema.
Waziri Mpina  alisisitiza  timu yake ya doria kufanya kazi kwa weredi kwa kufuata sheria  na kutokumwonea mtu yeyote wakati wa operesheni hii.
Aidha alisema katika ulinzi wa rasilimali za taifa Serikali ni walinzi tu hivyo mlinzi ukikutwa mlango wa tajiri umevunjwa atakuwa na shida .
“Mimi ni kibarua wenu kazi yangu ni kuhakikisha katika wizara mliyonipa rasilimali zinalindwa kwa nguvu zote na kazi hiyo mimi na wizara yangu tutaifanya usiku na mchana lakini nasema kama kuna hoja ya msingi wabunge wasituhumu kwa ujumla yawezekana kuna mtendaji akakosea katika kuchukua hatua, unasema katika eneo fulani katika kijiji fulani kuna jambo hili na hili limefanyika Mpina lishughulikie hata sasa hivi ukiniletea nitafanyia kazi na kuchukua hatua mara moja ”alisema.
Alisema rasilimali za taifa zimetoroshwa vya kutosha na kwamba Bunge  muda wote limekuwa likilia juu ya makusanyo hafifu  yatokanayo na uvuvi ambapo Serikali inakusanya wastani wa bilioni 20 tu ukiwaondoa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivyo  ni wakati sasa wa Bunge  kuisaidia Wizara kuinua sekta hiyo .
Kuhusu Ranchi za Taifa (NARCO) Waziri Mpina alisema Kamati ilishauri Serikali ifanye tathmini ili kujua  uwekezaji uliopo katika ranchi hizo unatija  ili ije na  mapendekezo sahihi ya namna bora ya kuwekeza katika ranchi hizo ambapo alisema tayari Wizara imeshaunda kamati hiyo inayoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Mstaafu wa DAWASA, Arcard Mutalemwa.

ZAIDI YA WATU KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO BIASHARA CHA PAPAI SALAMA

February 07, 2018
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kulia), akibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Spice leo  makutano ya Mitaa ya Narung'ombe na Lumumba Dar es Salaam leo.Taasisi hizo zitashirikiana katika nyanja za teknolojia na Kilimo kwa lengo la kuunganisha nguvu za umoja ili kuwapunguzia wananchi umasikini. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Seleman Msuya

ZAIDI ya wanachama 500 wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), wanatarajiwa kushiriki mafunzo maalum ya kufungua msimu wa kilimo cha Papai salama.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mkikita, Adam Ngamange wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Ngamange alisema mafunzo hayo yatafanyika Februari 24 mwaka huu yatabeba ujumbe 'Papai salama open speech' kwa lengo la kuunganisha walaji, wazalishaji na wataalam wa kilimo hicho.

Alisema baada ya tafiti kufanyika wamegundua mkanganyiko mkubwa wa taarifa hivyo kupitia mafunzo hayo ni wazi mabadiliko katika kilimo cha Papai yatatokea.

"Tafiti zinaonesha watalaam wanatofautiana kwenye idadi ya miche, uchimbaji wa mashimo, umwagiliaji maji na utiaji mbolea hivyo mafunzo haya yataweka washiriki kwenye mstari ili kukidhi ubora na ulinganifu wa soko la ndani na nje," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema mafunzo hayo yatawakutanisha wabobezi na watendaji mbalimbali katika kilimo hicho kipya cha Papai salama yatakuwa  na awamu tatu tofauti ili kujenga misingi imara katika kuleta unafuu wa uzalishaji papai.

Alisema Mkikita imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha wakulima wa Tanzania hasa wanaolima papai, mchaichai, mhogo na pilipili kichaa.

Aidha, Ngamange alisema pamoja na mafunzo hayo wanatarajia kupokea ugeni kutoka nchini Uturuki kutambua fursa za zao la papai nchini.

Pia alisema wanachama wa Mkikita wanatarajia kufanya ziara ya mafunzo Nchini Israel kuanzia Machi 11 mwaka huu na kugharimu dola za Marekani 2,000.

Halikadhalika Mkikita imesaini makubaliano ya ushirikiano  na Taasisi ya Hope For All ambayo ina wanachama zaidi ya 5,000 ili waweze kushirikiana kwenye nyanja za teknolojia na kilimo.

Akizungumzia makubaliano hayo Mkurugenzi wa Hope For All Edgar Mwamfupe alisema matarajio yao ni kuona mkulima anaheshima katika jamii.

Mwamfupe alisema kupitia Mkikita wanachama wao watafikia kwenye umilionea kwa kuwa kuna fursa za soko na biashara.


 Ngamange akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya semina ya mafunzo ya Kilimo biashara cha Papai Salama.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe akizungumza katika mkutano na wanahabari  na kuelezea ni kwa nini wameamua kuingia ushirikiano na Mkikita kuwakomboa wananchi masikini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe akizungumza katika mkutano na wanahabari  na kuelezea ni kwa nini wameamua kuingia ushirikiano na Mkikita kuwakomboa wananchi masikini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui na Adam Ngamange.
 Mratibu wa Ziara ya Utalii Kilimo Israel, Bw. Kizito (kulia), akielezea umhimu wa ziara hiyo  pamoja na faidha watakazozipata watakaokwenda.
 Mfanyabishara Adamjee (kulia) akielezea kuhusu kilimo cha pilipili kichaa na faida zake. Adamjee amekubali kujiunga na Mkikita ili kusaidiana kutafuta masoko ya zao hilo ndani na nje ya nchi.
 Ngamange akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui akielezea kazi mbalimbali za mtandao huo
 Askofu Mwamfupe na Adam Ngamange wakitliana saini makubaliano ya ushirikiano

 Mtaalamu wa Kilimo cha Zao la Pilipili Kichaa, akielezea faida ya zao hilo  pamoja na matumizi mbalimbali ya pilipili
 Ofisa Uhusiano wa Mkikita, Neema akielezea taratibu za wanachama na wasio wanachama  jinsi ya kushiriki kwenye semina ya Kilimo cha Kisasa cha Papai Salama.
Mmiliki wa Spice Hotel Ltd, Mwangaba (kulia) akizungumza na uongozi a Mkikita uliokutana naye baada ya kufanya mkutano na wanahabari kwenye hoteli hiyo ya Kisasa.

JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO

February 07, 2018
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
MKUU  wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wachezaji wa Gofu wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha heshma ya jeshi kwa kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora wanaowakilisha nchi kimataifa.

Aliyasema hayo Makao Makuu ya Jeshi Upanga  jijini Dar es Salaam  wakati akiagana na wachezaji Sita wa Gofu wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano ya wazi ya wanawake nchini  Nigeria IBB Ladies Open Championship  2018 yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Jenerali Mabeyo amesema kama ilivyokuwa katika michezo ya iiadha na ngumi sasa tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu hii ya Gofu ya Wanawake kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.

“ Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema na Jeshi kwa ujumla tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji  wa Gofu na hata Michezo mingine kuhakikisha jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa chachu kwa wengine,” alisema  Jenerali Mabeyo.

Ameongeza licha ya matumaini yake katika Gofu lakini pia katika Soka licha ya mchezo huo kutawaliwa na Simba na Yanga lakini sasa walau mwanga unaonekana baada ya ya Timu ya Jeshi ya Green Worriorrs kuifurusha Timu ya Simba katika Michuano ya Kombe la Shirirkisho.

“Ushindi ule ulikuwa Mwanzo mzuri wa kupunguza Ubabe wa Simba na Yanga na Ushabiki wa Simba na Yanga hata miongoni mwa wachezaji hivyo nanyi kama mlivyofanya vyema katika mashindano Uganda sasa tunatarajia Ushindi toka Nigeria,"amesema Jenerali Mabeyo.

Kwa Upande wa mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo  Mstaafu amewataja wachezaji hao kuwa ni Nahodha Ayne Magombe, Sara Denis , Sophia Mathius ,Hawa Wanyenche ,Christina Charles  na Angel Eaton huku mkuu wa Msafara akiwa ni Kapten Japhet Masai.

“ Nina matumaini makubwa na Kikosi hiki tunachokituma Nigeria naamini kitarejesha furaha kwa Klabu ,jeshi na Watanzania kwa ujumla ukizingatia uwezo Binafsi wa Wachezaji Mazoezi na Historia kutokana na michuano iliyotangulia” amsema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.

Kwa Upande wake mwenyekiti wa Chama cha Gofu nchini TGU Joseph tango amelipongeza jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa jitihada katika kuendeleza michezo hasa mchezo wa gofu ambao klabu ya Lugalo imekuwa kielelezo.

Amemuomba mkuu wa majeshi ya ulinzi na Mlezi wa Klabu ya Lugalo kuendelea kuisaidia Klabu hiyo ambayo ndio klabu yenye mashindano mengi kwa mwaka ukilinganisha na Klabu nyingine nchini ikiwemo kusaidia utekelezaji wa Ujenzi wa Uwanja makao makuu ya nchi Dodoma.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza February 8 na kuchukua siku tatu yanatarajiwa kushirikisha nchi mbali mbali za Afrika ikiwamo Kenya,Uganda na Zambia.
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo  akimkabidhi Bendera  ya taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi l Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB  nchini Nigeria Hivi karibuni ( Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo  akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB  nchini Nigeria Hivi karibuni.
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo  akiwa katika Picha ya Pamoja na Wachezaji na Viongozi wa  Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Wakuu wa Matawi na Wachezaji wanaotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB  nchini
Nigeria hivi karibuni.
Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo  akisalimiana na Afisa habari wa Klabu ya  Gofu ya Jeshi ya Lugalo  Luteni selemani Semunyu (Kulia) mara baada ya kukabidhi Bendera  kwa Nahodha wa Timu ya Wanawake
ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la  Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB  nchini
Nigeria Hivi karibuni.

MAMA MITINDO AELEZA UKWELI KUHUSU KUSTAAFU KUANDAA LADY IN RED!

February 07, 2018

Baada ya tetesi kuvuma zilizo jaa ukweli kuhusiana na Mama wanamitindo maarufu hapa Tanzania, Asya Idarous Khamsin kustaafu kuandaa jukwaa la ‘Lady In Red, sasa leo  6/Feb/2018 Asya amedhibitisha  tetesi hizo kama ifuatavyo.

 Akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa King Solomon Asya amesema kuwa Jukwaa la Lady in Red mpaka sasa limedumu kwa muda wa miaka 15 likiwa chini yake.  Pia alifafanua  dhamira ya jukwaa la Lady in Red ambapo alisema jukwaa hilo lilianzishwa kwa lengo la kukuza vipaji vipya kwenye Tasnia ya Mitindo hapa Tanzania, ndio maana jukwaa asilimia kubwa huwa linapandisha upcoming Designers maana ndio jukwaa lao la kujidaia.

Aidha aliongeza kuwa kustaafu kuandaa jukwaa la Lady in Red haimaanishi kwamba ataachana na mambo ya ubunifu, “siwezi kuacha maana ndio kazi inayo niweka mjini” alisisitiza Asya.  “Kilicho kikubwa nimeamua kutoa fursa kwa wanamitindo ambao wamekulia kwenye jukwaa hilo”.

Kumbuka Lady in Red 2018 itafanyika 9/Feb/2018 katika ukumbi wa King Solomon uliopo Dar es salaam- Namanga. Siku hiyo ndipo Asya atakapo jivua kuandaa na kukabidhi Designers wengine jukwaa hilo usikose. Kwako mdau wa mitindo endelea kuisambaza kwa walimwengu wote asante.


KATIBU WA UWT JUDITH LAIZER KUTATUA TATIZO LA VYOO KATIKA SHULE YA YA MSINGI ILULA NA ISOLIWAYA ZILIZOPO KILOLO

February 07, 2018
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiongea na baadhi ya viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Isoliwaya wakatika wa kukabidhi msaada huo kwa ajili ya kujengea vyoo ya walimu wa shule hiyo
 Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho Leah Moto na Nancy Nyalusi walikuwa kwenye ziara ya kusherekea miaka 41 ya chama cha mapinduzi 
 Hili ni moja ya jengo lashule ya msingi Ilula iliyopo katika tarafa ya mazombe wilayani kilolo mkoani Iringa 
 Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiwa katika kusherekea miaka 41 ya kuzaliwa chama chao kwa kufanya shughuli za kijamiii


Na Fredy Mgunda,Iringa. 

WALIMU wa shule ya msingi Ilula na Isoliwaya zilizoko katika kata ya Ilula Wilaya ya Kilolo wanakabiriwa na magonjwa ya Mlipuko kwa kukabiliwa na changomoto ya choo.
 
Shule hizo zilizotenganishwa baada idadi kubwa ya wanafunzi, walimu 49 wanalazimika kutumia choo Chenye matundu mawili hali inayohatarisha usalama wa afya zao.

Akizungumza mbele ya Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer, mwalimu Msaidizi wa shule ya Msingi Isoliwaya, Huruma Mbena alisema hali hiyo inahatarisha afya za walimu kutokana na changamoto hiyo.

Mbena alisema kuwa baada ya shule hizo kutenganishwa vyoo vya walimu vilibaki kwa shule ya Ilula hivyo kutokana na idadi kubwa ya walimu wanalazimika kutumia vyoo hivyo licha ya kutotosheleza kutokana na idadi kubwa ya walimu.

Aidha alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya nyumba za walimu ambao hadi sasa walimu 21 wanaishi katika nyumba za kupanga hali inayowaletea ugumu wa maisha zaidi.

Alisema kuwa changamoto nyingine wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa ofisi za walimu na ofisi ya mwalimu mkuu na kulazimika kutumia moja ya darasa kama ofisi na kupunguza idadi ya madarasa.

Akijibia hoja zilizopo kwenye risala Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer alisema kuwa umoja huo umewaleta mifuko ya saruji kumi na tano (15) na bati saba kwa ajili ya kusaidia kujenga vyoo vya walimu ili kupunguza adhabu wanayoipata.

“Kweli ukikosa huduma ya choo bora walimu hawezi kuwa huru kufundisha wanafunzi maana anaenda chooni huku akijua kuwa wanafunzi wake wanamtazama kwa mtazamo tofauti na ukizingatia maisha ambayo wanaishi majumbani kwao” alisema Laizer

Laizer alisema kuwa changamoto nyingine kama ukosefu wa nyumba za walimu,upungufu wa vyumba nane vya madarasa na ukosefu wa ofisi ya walimu atazifikisha kwa viongozi wa wilaya na kwa mbunge wa jimbo hilo Vennace Mwamoto.

“Hizi changamoto zenu zinatatulika kwa kuzingatia kuwa vingozi wa wilaya hii ni wachapakazi na waadilifu kuwatumikia wananchi nauhakika kuwa watakuja hapa na kuzitafutia ufumbuzi hizi changamoto kwa kuwa nitazifikisha kama nilivyozichukua hapa” akisema Laizer

Lakini Laizer aliwataka viongozi wa bodi ya shule hilyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu na wazazi wa shule hiyo kwa kuhakikisha wanaanza ujenzi wa nyumba za walimu pamoja na kujenga vyumba vya madarasa na mwishoni mbunge na halmshauri watamalizia sehemu iliyobaki.

“Naombeni nyie viongozi kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi hao bila kuwashirikisha walimu kwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kama alivyoagiza kuwa elimu bure bila malipo” alisema Laizer

Laizer aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kufanya kazi kubwa ya kufaulisha kwa wastani unaolidhisha na kuwaomba kuongeza bidii kufundisha huku wakibuni mbinu mpya za ufundishaji.