BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, PIA AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA KATIKA NCHI ZA MISRI NA ZAMBIA

November 28, 2017

Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke alisema kukamilika kwa utanuzi wa ujenzi wa Eneo la Maegesho ya Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar utatoa fursa ya kuongezeka kwa huduma za usafiri wa anga baina ya Zanzibar na Mataifa mengine Duniani.


Alisema matayarisho ya ujenzi huo katika hatua za awali za Awamu ya Pili aliyoyashuhudia baada ya kushuka kwenye Uwanja huo wa Ndege wa Zanzibar yamempa faraja yeye pamoja na Uongozi mzima wa Benki ya Kimataifa ya Exim ya Nchini China iliyoridhia kugharamia Mkopo wa ujenzi huo.

Balozi Wang Ke alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo wa Kidiplomasia.

Alisema Zanzibar inaweza kurejesha Heshima yake ya kuwa Kituo cha Kibiashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki chenye uwezo wa kutoa huduma za Kibiashara kupitia mfumo wa kisasa wa Mawasiliano kupitia usafiri wa anga badala ya ule uliozoeleka wa Baharini.

Alieleza kwamba zaidi ya Watalii 70,000 kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China wanaweza kuitembelea Zanzibar kila Mwaka kupitia usafiri wa anga na hata ule wa Baharini iwapo yataandaliwa mazingira mazuri katika Sekta ya Utalii baada ya kuongezeka kwa huduma za Mawasiliano ya usafiri.

Bibi Wang Ke aliyeanza majukumu yake Nchini Tanzania Mwezi Mmoja sasa aliahidi kwamba Nchi yake iliyopiga hatua kubwa Kiuchumi ndani ya kipindi cha Miaka 30 itaendelea kuiunga mkiono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika kuona maendeleo ya Kiuchumi yanakua na kushirikisha wananchi wote siku hadi siku.

Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza faraja yake katika kuona Viongozi wote waliiopo hivi sasa kati ya China na Tanzania bado wanaheshimu ushirikiano wa Mataifa hayo mawili ulioasisiwa na waanzilishi wake Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere na Hayati Mao Tse Tung.

Balozi Seif alisema mchango mkubwa unaoendelea kutolewa na China kupitia Makampuni na Mashirikia yake mbali mbali umeiwezesha Tanzania kukuwa Kiuchumi na kustawisha Jamii mambo yanayokwenda sambamba na kupungua kwa kasi ya ukali wa Maisha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza na kumuomba Balozi huyo wa China Nchini Tanzania kwamba Zanzibar bado inaendelea kuhitaji Wawekezaji pamoja na Watalii kutoka Nchini China katika azma yake ya kuimarisha uchumi hasa kwenye Sekta ya Utalii.

Balozi Seif ameishukuru Serikali ya China kwa misaada yake mikubwa inayotowa na kumuhakikishia kwamba uhusiano wa Kihitoria uliopo wa Mataifa hayo rafiki utaendelea kudumu kila Mwaka.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Mabalozi Wapya Wawili wa Tanzania Nchini Misri na Zambia walioteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Mabalozi hao ni Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor anayeiwakilisha Tanzania Nchini Misri na Balozi Abdulrahman Kaniki anayekwenda Nchi jirani ya Kusini mwa Tanzania ya Zambia.

Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliwakumbusha Mabalozi hao kuzingatia zaidi suala ya Doplomasia ya Kiuchumi ambalo kwa sasa limechukuwa nafasi ya pekee tofauti na lile ya Kisiasa lililozoeleka katika mabadiliko ya Kiuchumi yaliyopo Ulimwenguni.

Alisema matunda makubwa ya uwakilishi wa Mabalozi hao yataonekana katika kasi ya ongezeko la Miradi ya Uwekezaji kutoka katika Mataifa wanayokwenda kufanya kazi.

Mapema Balozi wa Tanzania Nchini Misri Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor kwa niaba ya Mwenzake Balozi Abdulrahman Kaniki anayekwenda Nchini Zambia alisema wanaahidi kuitanga Tanzania katika Mataifa hayo rafiki yenye Uhusiano wa muda mrefu.

Meja Jenerali Nassor aliziomba Taasisi zinazozimamia Sekta ya Utalii Nchini kuwa wazi kwa masuala yanayohitajika katika kuimarisha Sekta hiyo kupitia Wawekezaji na Mikataba ya uanzishwaji wa Miradi ya Hoteli.

Baadae Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioongozwa na Naibu Waziri wake Dr. Suzan Kolimba.

Katika mazungumzo hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Suzan alisema wako Zanzibar kufuatilia Rasimu ya Matayarisho ya Ripoti ya Utawala Bora Barani Afrika kwa upande wa Zanzibar inayotakiwa kutayarishwa na Wizara zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dr. Suzan alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Ripoti ya Utawala Bora Barani Afrika itakuwa ndio Mpango Kazi kwa Maraisi wa Mataifa ya Bara la Afrika watakayoiwakilisha katika Kikao cha Umoja wa Afrika {AU} kinachotarajiwa kufanyika Mwezi Febuari mwaka 2018.

Alisema hatua ya awali ya matayarisho ya Ripoti hiyo imeonyesha mafanikio kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa mfano bora wa Rasimu yake ya Utawala Bora kiasi cha Wataalamu wa masuala ya Kisiasa wa Bara la Afrika kushauri iwe kigezo cha kuigwa na Mataifa mengine Barani Afrika.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
28/11/2017.

Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha Rasmi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mabalozi wa China Nchini Tanzania na yule aliyepo Zanzibar.
  Balozi Seif akiagana na Ujumbe wa Kidiplomasia wa Ubalozi wa China Nchini Tanzania na Ule wa Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA

November 28, 2017
 Msimamizi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam, Sylvester Sikare (kulia) akielezea maendeleo ya ukamilishaji wa kituo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) mara alipofanya ziara katika kituo hicho tarehe 27 Novemba, 2017.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Kigamboni, Mhandisi Richard Swai (kushoto mbele) akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) katika ziara hiyo.
 Moja ya transfoma zilizopo katika kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni  kilichopo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akisalimiana na baadhi ya watendaji mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akisaini kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani kabla ya kuanza kuwahutubia wakazi wa Kata hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga.
 Sehemu ya wakazi wa Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).
 Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akifafanua jambo kwa wakazi wa Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Mkazi wa Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani, Mohamed Masinike akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara.

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa kata za Kigamboni, Vijibweni, Tungi zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika  kufuatia kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mgalu aliyasema hayo  tarehe 27 Novemba, 2017 kwenye ziara yake katika kituo cha kupoza umeme Kigamboni na katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kata za Kisiju na Mkamba zilizopo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja kutoka 6,000 hadi 12,000 na kuongeza kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati  itahakikisha  vituo vingine vya kuboresha  hali ya umeme ndani ya jiji la  Dar es Salaam  vinakamilika mapema Desemba 15, 2017 na kuondoa  tatizo la  kukatika kwa umeme mara kwa mara lililokuwa linajitokeza.

MKURUGENZI MKUU MSD AFANYA ZIARA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM

November 28, 2017
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya  ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo na  Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo, ili kubaini changamoto zilizopo za  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola.
 Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)
 Mkutano ukiendelea.
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.
 Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Sinza baada ya kufanya nao mazungumzo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.


Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amewatembelea wateja wa MSD wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Dar e's Salaam ukiwa ni pamoja na Hospitali ya Mwananyamala na Sinza kubaini changamoto zilizopo katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuzipatia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo iliyofanyika jumanne jijini Dar es Salaam Bwanakunu amewataka wateja hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha Msd kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa Manunuzi maalumu.

Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.

Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na wamedata msaada wa magari kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.

Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.

"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu na changamoto kubwa " alisema Bwanakunu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola alisema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo kwa sasa ni asilimia  80 .

"Changamoto iliyopo ni uhaba wa vitendanishi vya maabara na vifaa vya macho na meno ambavyo tunapata chini ya kiwango hivyo havikidhi mahitaji tuliyonayo," alisema.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Daniel Mkungu alisisitiza haja ya ushirikiano baina ya Hospitali hizo na MSD ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Ziara hiyo ya mkurugenzi huyo itaendelea tena kesho katika baadhi ya hospitali zilizopo jijini Dar es Salaam.


TIGO YATANGAZA DILI YA PEKEE YA SIMU ZA SMARTPHONE

November 28, 2017
Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari   (hawapo pichani) mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael. 
Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akifafanua jambo kwa   waandishi wa habari  mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo.Kulia ni Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh.
Shirika la Kivulini lasaidia uanzishaji wa Kiwanda katika Shule ya Wasichana Bwiru Mwanza

Shirika la Kivulini lasaidia uanzishaji wa Kiwanda katika Shule ya Wasichana Bwiru Mwanza

November 28, 2017
Shule ya Wasichana Bwiru iliyopo Jijini Mwanza imezindua kiwanda cha mfano, fuatilia hafla ya uzinduzi huo ambayo imefanyika jana ikiwa ni sehemu ya "Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia" ambayo huadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10. [embed]https://youtu.be/uVnE_X4U-EU[/embed] Uzinduzi wa kiwanda kidogo katika shule ya wasichana ya kidato cha tano na sita Bwiru iliyopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. Mgeni rasmi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akikagua bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa shuleni hapo. Mgeni rasmi akijionea picha mbalimbali zinazochorwa shuleni hapo Mgeni rasmi akijionea utengenezaji wa sabuni pamoja na dawa za chooni. Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza kwenye uzinduzi huo. Mkuu wa shule ya wasichana Bwiru, Mwalimu Mackrida Shija akizungumza kwenye uzinduzi huo. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga akizungumza kwenye ufunguzi huo ambapo aliahidi ushirikiano katika kuendeleza kiwanda hicho. Mwanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru, Dorophy James (kushoto), akisoma risala ya ufunguzi. Kulia pia ni mwanafunzi wa shule hiyo Delvina Mollel. Wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirika la Kivulini, Yassin Ally kwenye uzinduzi huo Viongozi mbalimbali. Maafisa wa ulinzi.
 MWANZA WAZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI WA MKOA

MWANZA WAZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI WA MKOA

November 28, 2017
MKOA wa Mwanza umefanya Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji ambao umeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF). Mwongozo huo ni sehemu ya ripoti tatu zilizotokana na agizo la mkoa wa Mwanza la kutaka kuwekewa pamoja taarifa sahihi zinazogusa uwekezaji mkoani humo ili kurahisisha na kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje. Ripoti nyingine ni Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials Report), na Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report) . Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, Mashirika ya Umma, Sekta binafsi na mashirika ya kimataifa, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella, alisema walilazimika kuwatafuta wataalamu wa ESRF, kuwasaidia kuweka pamoja fursa zote za mkoa katika mpangilio mmoja unaobainisha fursa zilipo. Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa chini ya ufadhili wa UNDP katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.[/caption] Alisema katika kukabiliana na changamoto hizo waliiomba Taasisi hiyo kufanya utafiti na uchambuzi wa kina ili kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa huo na ndio wakatoka na ripoti tatu ikiwa Mwongozo huo. Alisema kazi hiyo ilifanyika kwa miezi 4 kwa msaada wa kifedha kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuanzia mwezi Julai 2017 hadi Novemba 2017. Mongela alisema: wawekezaji wamekuwa wakipata taabu namna ya uoanishaji wa taarifa zinazotolewa kwao kutoka mamlaka moja hadi nyingine. Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa taarifa kuhusu uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Mwanza ulioandaliwa na taasisi yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa mwongozo huo uliofanyika jijini Mwanza.[/caption] Alisisitiza katika hotuba yake kuwa wawekezaji walikuwa wanapata majibu tofauti katika maswali yao walipofika katika mkoa huo kutoka kwa watendaji tofauti ambao ilikuwa lazima kuwaona ili kukamilisha nia yao ya kuwekeza . Alisema kutokana na hali hiyo waliomba ESRF kuwasaidia kuweka pamoja takwimu zote na kuwavutia wawekezaji kwa kuwa na majibu ya maswali muhimu wanayotakiwa kuyajua kabla ya kuwekeza. Mongela alisema kwamba mwongozo uliotengenezwa unakwenda sanjari na dira ya maendeleo ya Tanzania na kuwataka wawekezaji wa kigeni na nchini kuwekeza katika mkoa huo. Mkuu na Mtaalamu wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bw. Amon Manyama akitoa salamu za UNDP katika hafla fupi ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi za Mkuu wa Mkoa huo jijini Mwanza.[/caption] Alisema wakiwa katikati ya nchi za Afrika Mashariki, zenye soko la watu wapatao milioni 230, Mwanza ni sehemu muhimu na njema kabisa kwa uwekezaji. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi waliyopewa Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) alisema pamoja na kukabidhi mwongozo huo, Ripoti zote zilithibitishwa na Mkoa Septemba 15, 2017 katika warsha maalum iliyoandaliwa na Mkoa (Validation Workshop). Tayari ESRF imeshandaa na kuzindua Mwongozo kama huo Mkoani Simiyu mwanzoni mwa mwaka huu. ESRF imeshakamilisha kuandaa Miongozo ya Uwekezaji katika Mikoa ya Mara na Kilimanjaro ambayo inatarajiwa kuzinduliwa ndani ya wiki mbili zijazo. Miongozo hii itasaidia sana katika kupata Mwongozo wa Uwekezaji wa Taifa utakaoonyesha fursa zilizopo nchini na katika kila mkoa.” Alisema Dkt Kida. Mshiriki Mtafaifiti wa ESRF, Dkt Hoseana Lunogelo, akiwasilisha fursa za uwekezaji mkoani Mwanza walizoziona wakati wa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwongozo huo jijini Mwanza.[/caption] Miongozo hiyo ya Uwekezaji, alisema Dkt. Kida inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016 – 2021) unaosisitiza ujenzi wa Tanzania ya Viwanda ili kuifikisha nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025. Pamoja na kutoa maelezo ya kazi Dk Kida alishukuru uongozi wa mkoa wa Mwanza na taasisi zake mbalimbali kwa kuwezesha ukusanyaji wa takwimu na kuandaa muongozo huo. “Kwa namna ya pekee napenda kuushukuru Uongozi wa Mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa John Mongella, Katibu Tawala wa Mkoa – Kamishna wa Jeshi la Polisi Bw. Clodwing Mtweve na viongozi wengine wa mkoa na wilaya zote kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu wetu wakati wanapita kutafuta maoni, taarifa na takwimu mbalimbali za kutayarishia Mwongozo huu.” Alisema Dkt. Kida na kuwashukuru pia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)

KAMPUNI YA BIMA YA RESOLUTION YAWAKUTANISHA MADALALI WA BIMA, WARUDISHA SHUKURANI KATIKA JAMII.

November 28, 2017
Mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma ambaye ni Meneja Mkazi wa Africa Practice mshauri  akitoa shukurani zake za dhati kwa Kampuni ya Bima ya Resolution kwa kuwakutanisha Madalali wa Bima 'Insurance Brokers' toka sehemu tofauti nchini ambapo kwa kufanya hivyo itaongeza zaidi ufanisi na ushirikiano baina yao na Kampuni ya Bima ya Resolution.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mambo mbalimbali kuhusiana na kampuni hiyo na kuwashukuru madalali wa Bima kwa kwa kuungana nao katika chakula cha usiku, pamoja na hayo alisema kuwa wapo Kenya, Uganda na Tanzania, kwa Tanzania wapo Dar es salaam na Arusha lakini hivi karibuni watafika Zanzibar na Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo akieleza kwa ufupi kuhusiana na tukio hilo la kurudisha shukurani, ambapo pia alizitaja baadhi ya huduma wanazozitoa ikiwa nipamoja na; Travel Plan, Medical plan, Liability plan,Home Insurance,Marine insurance na Motor Private Insurance 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo (aliye simama nyuma) akiwatambulisha viongozi wa Idara mbalimbali katika kampuni ya Bima ya Resolution wa nchini Tanzania.
Bwana Melkizedech Nyau ambaye ni mtakwimu wa Bima kutoka kampuni ya Bima ya Resolution akielezea bima ya Afya Bora kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini kuanzia mwaka 0 hadi 64 ambao ni kama Bodaboda, Mama ntilie,wauza maandazi pamoja na makundi mbalimbali yanayofanana na hayo. Alieleza kuwa ili kujiunga na Bima hiyo itakuwa vizuri watu wawe katika kundi au Vikoba waweze kupata kwa pamoja huduma hiyo bora kutoka kampuni ya Resolution.
Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku ambaye pia ni Mchekeshaji maarufu hapa Nchini Tanzania akiendelea kutoa taratibu mbalimbali wakati wa  chakula cha usiku kilicho andaliwa na Shirika la Bima la Resulution katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku akiwauliza maswali mbalimbali kuhusiana na bima.
Bi. Mailda William(Kushoto) kutoka Aste Insurance Brokers ambao walishinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Msichana ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution

Bi. Jenifa Projest (Kulia) kutoka Aste Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma baada ya  kushinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Salvation Army  ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution
 Bi. Fauzia Bairu (Kulia) kutoka Pioneer Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati baada ya  kushinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Sustainable Education ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution.
 Bw. Emmanuel Mkindi, Meneja wa Maendeleo ya Biashara- Biashara kwa ujumla kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution akitoa neno la shukurani kwa madalali wote wa bima waliofika katika tukio lao la 'Appreciation Dinner' ambapo kaulimbiu yao inasema 'Protecting what you value' yani tunalinda unachokithamini.
Madalali wa Bima wakiwa katika hafra ya chakula cha usiku iliyo andaliwa na Kampuni ya Bima ya Resolution kwa ajili ya kurudisha shukurani kwa jamii.