VIDEO:MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA

February 27, 2018

Manaibu Waziri, Mhe. Antony Mavunde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, (wapili kushoto), na  Mhe.  Dotto Biteko, kutoka Wizara ya Madini, (wapili kulia), wakipatiwa maelezo na Mjiolojia Mkuu wa mgodi wa Al-Hilal Minerals Limited wa mjini Shinyanga, (aliyenyoosha mkono), wakati wa ziara ya kushtukiza ya viongozi hao ili kubaini kama mgodi huo unazingatia sheria katika kutekeelza majukumu yake, Ziara hiyo waliifanya Februari 27, 2018

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SHINYANGA

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, na mwenzake wa Madini Mhe. Dotto Biteko, leo Februari 27, 2018 wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye mgodi wa almasi wa Al-Hilal Mineral Ltd ulioko kilomita 60 kutoka mjini Shinyanga, ili kubaini kama wamiliki wa mgodi huo wanatekeleza sheria za uendeshaji.
Wakati Mheshimiwa Mavunde alikuwa akifuatilia kama mgodi huo umejisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), ikiwa ni pamoja na jinsi mgodi huo unavyotekeleza Sheria ya ajira na mahusiano kazini,
Mhe. Biteko yeye alikuwa akifuatilia kwa nini mgodi huo haujawasilisha wizarani mpango wa ukarabati wa mazingira (rehabilitation plan) na mpango wa uwajibikaji wa shirika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR).
Kwa upande wake Mhe. Mavunde alibaini kuwa Mgodi huo bado ulikuwa haujajisajili na Mfuko na badala yake uongozi ulipeleka michango siku moja kabla ya ziara ya Naibu waziri.
“Serikali inataka waajiri wazingatie sheria, na ninyi mmevunja sheria kwa kutojisajili, ingawa mmelipa michango yenu jana, ninachoweza kusema, agizo la serikali la kuwafikisha mahakamani waajiri ambao hawajajisajili nchi nzima liko pale pale, ni juu yenu kutekeleza hilo kabla hamjapelekwa mahakamani.” Alisema Mhe. Mavunde.
Ziara ya Naibu Waziri ni muendelezo wa ziara yake iliyoanza Februari 26, 2018 jijini Mwanza ambapo aliagiza kufikishwa mahakamani waajiri watatu jijini Mwnaza.
Mhe. Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko. “Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.­­

Naibu Waziri Mvunde, akiwasikiliza wafanyakazi wa mgodi wa almasi wa Al-Hilal Minerals Limited wa mjini Shinyanga.
Mhe.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, (kushoto), akiwa na mwenzake wa Madini Mhe. Dotto Biteko, wakati akizungumza kwenye kikao cha pamoja baina ya uongozi wa mgodi huo kwenye ziara hiyo ya kushtukiza Februari 27, 2018
 Mhe. Biteko, (kulia), akiwa na Mhe. Mavunde, wakati akizungumza katika kkikao cha pamoja na uongozi wa mgodi huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw.Anselm Peter, (kushoto) na Naibu Kamish Idara ya Kazi, Bi.Rehema Moyo.
 Kutoka kushoto, Bw. Anslem Peter, Bi. Rehema Moyo, na Bi. Laura Kunenge 

 Mhe. Naibu Waziri akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo.

Mwanasheria wa WCF, Bw. Deo, (kushoto), Afisa Kazi Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, na Bw. Anslem peter
 Naibu Waziri Mvunde akizungumza na baadhi ya manesi wa hospitali ya Kolandoto.
 Naibu Waziri, akiongozana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kolandoto, Dkt. Maganga Ngoi (katikati) na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, wakati akitoka hospitalini hapo baada ya ukaguzi.
 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe.Josephine Matiro, (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (wakwanza kushoto), na Afisa Kazi Mkoa wa Shinyanga, wakimsikiliza Bw. Anslem Peter.

Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, akifafanua masuala yahusuyo  Sheria ya ajira na mahusiano kazini, Kulia ni Bw. Anslem Peter.

 Naibu Wazuiri Mavunde, akizungumza mbele ya viongozi wa Hospitali ya Kolandoto mjini Shinyanga.
 Manaibu Waziri Biteko, na Mavunde wakitoka mgodi wa Al-Hilal baada ya ziara yao ya ghafla.
Mwanasheria wa WCF, Bw. Deo Ngoi, (kushoto), akimsimamia Afisa Mwajiri wa Hospitali ya Kolandoto kujaza fomu za kujisajili na Mfuko huo.


-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com

WACHUUZI WA NAZI SOKO LA MGANDINI WAELEZA SABABU ZA BIDHAA ZINAZOTOKA MOMBASA KUKUBALIKA

February 27, 2018
Chama cha wauza nazi katika soko la Mgandini Jijini Tanga wameeleza sababu za nazi zinazotoka Mombasa nchini Kenya kukukabilia kuliko za Tanga kutokana na ubora zilizokuwa nazo na kubwa.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa chama cha Wauza Nazi katika soko hilo (Coconut Group) Kassim Mohamed katika mahojiano na Blog hii ambapo alisema sababu nyengine ni wakulima nchini humo kuiweka nazi hiyo muda mrefu shambani kwa kufuata utaratibu kuliko ilivyo kwa wengine.

Alisema hali hiyo imezifanya nazi zinazotoka huku kuonekana kupendwa na wafanyabiashara wengi ambao wamekuwa wakifika kwa ajili ya ununuaji wa zao hilo kwenye soko hilo kuliko ilivyo za mkoani Tanga hali inayotajwa kuchangiwa na wakulima.

“Kwa mfano utakuwa mkulima wa nazi mkoani Tanga anavuna nazi mapema shambani kutokana na shida alizokuwa nazo lakini wa Mombasa nchinio Kenya wamekuwa wakiziweka muda mrefu na hivyo zinavunwa zinakuwa kubwa na wenye ubora”Alisema

“Lakini pia wanasema uharakishaji wa uvunaji wakulima hao zao hilo wamepeleka kupata nazi ndogo ambazo sokoni zimekuwa na changamoto kubwa kuliko ambazo zinatoka nchi jirani ya Kenya kwani hizi za Tanga unaweza kuwa nazo unauza reja reja “Alisema.

Alisema sababu inayopelekea wakulima hao kupata nazi ndogo inatokana na kushindwa kuendeleza zao hilo kwa kuipanda mingine kwani iliyopo hivi sasa ni ya zamani ambayo wamerithi katika maeneo yao.


“Lazima watambue kuwa hata kama utakuwa umerithi mnazi unapaswa kutambua umuhimu wa kupanda mingine kwani inapokaa muda mrefu inapelekea kuzalisha nazi ndogo.

Naye mchuuzi kwenye soko hilo,Akida Juma aliwataka wakulima wa zao hilo mkoani hapa kubadilika kwa kulima kisasa ili kuondokana na kutegemea minazi ya zamani ili waweze kuvuna jambo ambalo linaweza kuwapeleka kukosa soko kabisa kutokana na ushindani uliopo.

“Ndugu zangu tunajua minazi mingi watu wamerithi kutoka na kupandwa miaka ya nyuma hivyo hakikisheni mnaipanda mingine kwa kufuata taratibu mzuri na baadae mnaweza kupata mafanikio kuliko sasa “Alisema.

MANAIBU WAZIRI, MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI EL - HILAL SHINYANGA

February 27, 2018
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko, leo Jumanne Februari 27,2018 wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye mgodi wa almasi wa El – Hilal Minerals Limited uliopo katika kijiji cha Maganzo kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. 

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI YA ZANZIBAR ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO

February 27, 2018

Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania Bara na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar zimeweka mkakati wa pamoja wa kuimarisha ushirikiano wa usimamizi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii kwa maslahi ya pande zote za Muungano. 

Hayo yameelezwa  na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi baada ya mkutano wa pamoja wa wizara hizo uliofanyika hivi karibuni katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku moja uliongozwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Joseph Meza.

Akifungua Mkutano huo wa siku moja,  Maj. Gen. Milanzi alisema pamoja na Wizara hizo kutokuwa za muungano imekuepo haja kubwa ya kukutana kwa ajili kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha sekta ya maliasili na utalii na kukabiliana na changamoto zinazogusa sekta hiyo katika Muungano.

"Tumejadiliana kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya biashara ya mazao ya misitu, biashara ya Wanyamapori inayohusiana na mikataba ya CITES na mikataba mingine ya ndani na ya Kimataifa.

"Tumekubaliana pia kuhuisha sheria zinazokinzana katika usimamizi wa sekta tunazozisimamia ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza katika utekekezaji na hivyo kuathiri Muungano wetu," alisema Maj. Gen. Milanzi. 

Alisema katika mkutano huo wa siku moja wataalamu kutoka pande zote za Muungano waliagizwa kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendesha biashara ya mazao ya misitu na kupendekeza utaratibu wa kufanya biashara kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo.

Alisema kupitia mkutano huo Wizara hizo zimeunda kamati maalum ya kuratibu utekelezaji wa maazimio ya pamoja ya kuimarisha usimamizi bora wa sekta hizo na utatuzi wa changamoto zilizopo kwa kuandaa mapendekezo ya kimkakati ya muda mfupi na mrefu.

"Kamati hiyo itaongozwa na Afisa Mipango Mkuu Msaidizi kutoka Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka (DFNR), Saleh Kombo Khiari na Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii, Mugure Wambura," alisema Milanzi.

Mbali na hayo alisema kutakuwepo na vikao mbalimbali vya kuimarisha Muungano kupitia Wizara hizo katika ngazi ya wataalamu, Makatibu Wakuu na Mawaziri ambapo kikao kingine kinatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe 30 Machi, 2018.

TIGO NA MILVIK TANZANIA ZACHAGULIWA KUWANIA TUZO ZA GSMA ZA UVUMBUZI WA SIMU ZA MKONONI KATIKA SOKO LINALOCHIPUKIA

February 27, 2018

live it love it
DAR ES SALAAM, FEBRUARY 2018. Milvik Tanzania na Tigo wamechaguliwa katika tuzo za Uvumbuzi Bora wa simu za mkononi katika soko linalochipukia katika kundi la Ubora kwa jamii (Social good) katika Tuzo za Simu za Mkononi za GSMA. Tuzo hizi za heshima zinalenga kutambua na kusherehekea mchango uliotolewa katika sekta ya simu za mkononi inayoendelea  kubadilika duniani kote. 
Tuzo za Uvumbuzi Bora wa simu za mkononi katika soko linalochipukia zinatambua uvumbuzi halisi katika jitihada za simu za mkononi ambazo zinalenga kutambua mchango unaotolewa na makampuni katika ushirikishaji, upatikanaji na uhai wa masoko yanayochipukia. Uteuzi huo unalenga kutambua juhudi za Milvik na Tigo kwa jamii kwa kuwapatia wateja ambao mwanzo walikuwa wamesahaulika katika huduma za bima ya afya kwa gharama nafuu.
Milvik imeleta gharama ndogo za upatikanaji wa huduma ya bima Afrika kwa masoko yanayochipukia (3% tu) kwa kuunganisha pamoja nguvu ya teknolojia ya simu za mkononi na makampuni ya simu kufungua upatikanaji mpya wa huduma nafuu za mawasiliano, na kuunganisha jamii za pembezoni zilizokuwa zimesahaulika katika huduma muhimu za bima kwa lengo la kuleta ushirikishwaji jumuishi wa kifedha. 
Milvik na Tigo wameanzisha mfumo wa kwanza wa kidigitali wa bima katika simu za mkononi kwa kuunganisha mfumo wake wa bima katika simu za mkononi na miundombinu ya teknolojia ya makampuni ya simu, jambo ambalo linawawezesha wateja  kujiunga na kulipia bima kupitia simu zao za mkononi.
Nchini Tanzania, Milvik inashirikiana na Tigo kuleta huduma za bei nafuu za bima kwa wateja wa Tigo ambapo wataweza kulipia bima zao kwa kutumia fedha zilizoko katika simu.  Ushirika huu wa Tigo/Milvik kwa sasa unatoa moja kati ya huduma kubwa zaidi ya bima ya kulipia kupitia simu za mkononi duniani. 
Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, amesema: “ninafuraha kwamba kazi ambayo Tigo na Milvik wamefanya katika kuleta ushirikishwaji wa kifedha kupitia uvumbuzi huu unaanza kutambulika. Kwa kuwezesha upatikanaji wa bima kupitia simu za mkononi, wateja ambao kwa kawaida wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kupata huduma za kifedha kupitia taasisi zingine, kwa sasa wataweza kupata ulinzi wa kifedha, wao na familia zao. Tunajisikia furaha kushirikiana na Milvik kutoa bidhaa zenye thamani kubwa za bima kwa wateja wetu pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla.”
Tom Chaplin, Meneja wa Milvik Tanzania, kwa upande wake alisema: “Kupitia mfumo wetu wa bima kwa simu za mkononi na ushirika wetu na Tigo, tumeweza kusambaza huduma rahisi ya bima na yenye bei nafuu kwa watu wengi na kuwezesha upatikanaji wa bidhaa za msingi za kifedha. Kadri ambavyo huduma za simu zinavyozidi kujipenyeza katika masoko yanayochipukia, tunaona fursa nyingi katika kushirikiana na makampuni ya simu na kuwapatia watu zana za kifedha wanazohitaji kuhakikisha mafanikio yajayo ya kiuchumi na familia zao.”
Mshindi wa Tuzo hizo atatangazwa katika Kongamano la Simu za Mkononi Duniani (Mobile World Congress) Barcelona, litakalofanyika kuanzia tarehe 26 Februari mpaka tarehe 1 Machi mwaka huu.

TANZANIA YADHAMIRIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE NCHINI

TANZANIA YADHAMIRIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE NCHINI

February 27, 2018

????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi
????????????????????????????????????
Wadau wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB)  wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
…………………..

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 huku lengo likiwa ni kuondoa tatizo hilo nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
“Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani na kuimarisha afya ya wanawake Tanzania na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Ocean Road Saratani ya Mlango wa kizazi zinazoongoza nchini kwa Asilimia 36 huku ikifuatia na saratani ya matiti, huku jumla ya wagonjwa wa Saratani nchini katika kila wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti.
Aidhe, Serikali imepanga kuanza na wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri wa chini, huku ikitegemea kuchanja zaidi ya wasichana 610,000 katika jitihada za kutokomeza kabisa tatizo hili la Saratani ya mlango wa kizazi nchini,
Mhe Ummy alisisitiza kuwa Chanjo hii itatolewa katika vituo vyote vya Afya nchini  vya Serikali, vya watu binafsi na vikundi mkoba bure, na kuwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha mabinti zao wanapata chanjo hii ili kujikinga na ugonjwa huo.
Nae Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Dafrossa Lyimo aliendelea kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza juu ya umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya duniani na mamlaka ya chakula na viodozi nchini (TFDA).

DK MWANJELWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA, ATETA NA KINA MAMA WANAOJITEGEMEA 'SINGLE MOTHERS'

February 27, 2018
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea machache na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Pamoja naye (kushoto) Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga viongozi wa wasaidizi wake mkoani humo. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogs)

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na mmoja wa wageni alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kulia) alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Kulia kwa Naibu Waziri ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga.


 NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiagana na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Amina Masenza baada ya kufanya naye mazungumzo ofisini wakati wa kuanza kwa ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey.


NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akikagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Katikati ni mwenyeji wao, Mhe Amina Masenza Mkuu wa Mkoa.










NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiwabadilishana mawazo na wakina mama wanajitegemea 'Single mothers' baada ya kukagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 mkoani Iringa kwa ajili ya kilimo cha biashara maalum kwa ajili yao, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. 

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF

February 27, 2018
TWIGA STARS KUCHEZA NA ZAMBIA AFCON YA WANAWAKE
Timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) itacheza na Zambia katika mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake zitakazochezwa Ghana baadaye mwaka huu.
Twiga Stars inatakiwa kucheza mechi zote mbili kati ya April 2 na April 10,2018.
Mchezo huo ni wa raundi ya kwanza.

NGORONGORO HEROES KUCHEZA NA DR CONGO  KUFUZU FAINALI ZA AFRICA
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes) imepangwa kucheza na DR Congo kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba.
Mchezo wa kwanza utachezwa Tanzania kati ya Machi 30,31 na April 1,2018 na ule wa marudiano utachezwa Congo kati ya Machi 20,21 na 22.
Mshindi katika mchezo huo atacheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 11,12 na 13,2018.

YANGA KUCHEZESHWA NA WAAMUZI KUTOKA BURUNDI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Yanga ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya
Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17,2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Africa Kusini Gay Makoena.
SIMBA YAPANGIWA WAAMUZI WA AFRICA KUSINI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7,2018 Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.
Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.
CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO
Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi 18,2018 Madagascar.
Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine
Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo
Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola.
KAMATI YA MAADILI YAWAFUNGIA VIONGOZI MVUVUMWA KWA KUGHUSHI LESENI ZA WACHEZAJI
Kamati ya Maadili ya TFF ilIyokutana Februari 3, 2018 na Februari 17,2018, katika ofisi za TFF Karume,Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa pia ilipitia na kutoa hukumu ya tuhuma za kutoa taarifa zisizo sahihi na kughushi leseni za usajili zilizowakabili watuhumiwa mbalimbali walioletwa mbele yake.

Tuhuma hizo zilitokana na mechi namba 26 kundi A Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika 29 Oktoba 2017 kati ya Mvuvumwa FC na Friends Rangers ambapo katika mchezo huo timu ya Mvuvumwa FC iliwachezesha wachezaji watano (5) ambao ni Elias Costa Elias (aliyevaa jezi namba 5), Lukwesa Joseph Kanakamfumu (jezi namba 7), Dunia Abdala Dunia (jezi namba 1), Doto Justine Kana (jezi namba 12) na Mwarami Abdala Mwarami (jezi namba 8).

Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliwafungulia mashtaka watuhumiwa
  1. Dr. Yared Fubusa – Mwenyekiti na Mmiliki wa timu ya Mvuvumwa FC
  2. Ramadhani Kimilomilo – Katibu wa Mvuvumwa FC
  3. Joseph Kanakamfumu – Kocha na Mratibu wa Mvuvumwa FC
  4. Elias Costa Elias – Mchezaji wa Mvuvumwa FC
  5. Lukwesa Joseph Kanakamfumu – Mchezaji wa Mvuvumwa FC
  6. Dunia Abdala Dunia – Mchezaji wa Mvuvumwa FC
  7. Doto Justine Kana – Mchezaji wa Mvuvumwa FC
  8. Mwarami Abdala Mwarami – Mchezaji wa Mvuvumwa FC
  9. Yusuph Makoya – aliyekuwa mratibu wa mwanzo wa Mvuvumwa FC na mmiliki wa nyumba ambayo timu hiyo ilipanga kwa ajili ya kuweka kambi jijini Dar es Salaam.

    TUHUMA ZILIZOWASILISHWA
    Watuhumiwa 4 (Dr. Yared Fubusa, Ramadhani Kimilomilo, Joseph Kanakamfumu, na Yusuph Makoya) ambao ni viongozi wa Mvuvumwa FC walishtakiwa kila mmoja kwa makosa mawili;
·         Kutoa taarifa zisizo sahihi/udanganyifu ili kufanikisha usajili wa wachezaji kinyume na kifungu cha 41(12) ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza toleo la 2017. Kama ilivyo ainishwa kwenye Kanuni za Maadili Toleo la 2013 kifungu cha 5.
·         Kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.


Watuhumiwa 5 (Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdala Dunia, Doto Justine Kana, Mwarami Abdala Mwarami) ambao ni wachezaji wa Mvuvumwa FC


·         Kushiriki mechi namba 26 kundi A Ligi daraja la kwanza iliyofanyika 29 Oktoba 2017 kati ya Mvuvumwa FC na Friends Rangers, huku wakijua usajili wao haujakamilika ikiwa ni kinyume na kifungu 37(14) cha Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza toleo la 2017.
·         Udanganyifu na kugushi leseni  wakati wa usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.

MAHOJIANO NA WATUHUMIWA
Kamati ilifanya mahojiano na watuhumiwa Ramadhani Kimilomilo, Joseph Kanakamfumu, Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu na Yusuph Makoya. Wachezaji Dunia Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami walishindwa kufika wa sababu mbalimbali huku Dr. Yared Fubusa akigoma kuja kuhojiwa na Kamati.

Katika mahojiano hayo Kamati ilibaini mambo yafuatayo;
  1. Uendeshaji wa timu ya Mvuvumwa FC umekuwa usioridhisha hasa baada ya kuhamisha michezo yake ya Ligi Daraja la Kwanza kutoka kituo cha Kigoma na kuja Dar es Salaam. Licha ya kuhamishia makazi yake Dar es Salaam, viongozi wakuu waliendelea kubaki Kigoma na hivyo timu kuonekana kama imetelekezwa. Majukumu ya timu alikabidhiwa Ndugu Idd Thabiti ambaye katika taarifa ya mwamuzi wa Mechi Na. 26 aliorodheshwa kama Meneja (Team Manager). Ndugu Idd Thabit, anayejulikana kwa jina maarufu “Omba” ndiye alikuwa mratibu wa timu ikiwa Dar es Salaam. Hata hivyo hakuna taarifa zozote zilizowasilishwa mbele ya Kamati kuonyesha kama “Omba” alitambulishwa kama mmoja wa viongozi wa Mvuvumwa FC.

    Baadaye Uongozi wa Mvuvumwa FC ulimteua Ndugu Joseph Kanakamfumu kuwa kocha na mratibu wa timu kupitia barua pepe (email) ya tarehe 12 Oktoba 2017, na kama ilivyothibitishwa na Ndugu Ramadhani Kimilomilo Katibu wa Mvuvumwa FC alipohojiwa na Kamati. Hata hivyo Kamati haikuonyeshwa nyaraka zozote kuthibitisha makabidhiano ya timu kati ya Ndg. Joseph Kanakamfumu na “Omba” aliyekuwa mratibu kabla yake. Aidha Kamati ilithibitishiwa na Ndg. Kimilomilo kuwa hakuna mkataba wowote kati ya Ndg. Joseph Kanakamfumu na Mvuvumwa FC unaoinisha haki na majukumu ya kila upande. Mazingira kama haya yanatoa mwanya wa kutowajibika kwa pande zote.


    Kutokana na kukosekana kwa mfumo unaozingatia taratibu, viongozi wake (Dr. Yared Fubusa – Mwenyekiti na Mmiliki; Ndg. Kimilomilo – Katibu; na Ndg. Kanakamfumu – Kocha na Mratibu) waliendelea kuendesha timu kiholela. Kutokana na kutozingatiwa kwa taratibu, sasa hivi kuna mgogoro kati ya Ndg. Yusuph Makoya, mmiliki wa nyumba ambayo Mvuvumwa FC iliweka kambi mara baada ya kuhamishia michezo yake kituo cha Dar es Salaam. Ndg. Makoya, ambaye aliieleza Kamati kwamba alikuwa anasaidiana na viongozi kuendesha timu, aliingia mkataba wa kuipangisha Mvuvumwa FC kwenye nyumba yake iliyopo nguvu kazi ( Chanika )kwa kipindi cha Miezi 6.Hata hivyo timu hiyo ilihamishwa kinyemela bila yeye kutaarifiwa wala kulipwa madai yake na kusababisha upotevu/uharibifu wa mali zake. Suala hili limefikishwa katika vyombo vya dola.
  2. Uhamishaji wa timu ya Mvuvumwa kutoka kituo cha Kigoma kuja Dar es Salaam haukuwa na uwazi wala kufuata taratibu zinazotakiwa. Alipoulizwa sababu za kuhamishia timu Dar es Salaam badala ya Kigoma ilikosajiliwa Ndg. Kimilomilo alisema kuwa timu yao inapigwa vita kule Kigoma. Kitendo cha kuhamishia timu Dar es Salaam bila kuzingatia taratibu ndicho kilisababisha iendeshwe kiholela na kuwapa mwanya wa kufanya mambo kienyeji ikiwamo kugushi leseni za wachezaji.
  3. Usajili wa wachezaji watano wa Mvuvumwa FC, ambao ni Elias Costa Elias (leseni namba 51992), Lukwesa Joseph Kanakamfumu (leseni namba 51995), Dunia Abdala Dunia (leseni namba 51994), Doto Justine Kana (leseni namba 51997), na Mwarami Abdala Mwarami (leseni namba 51995) haukuwa halali; hakuna rekodi yoyote ya leseni hizo TFF. Hivyo wachezaji hao walishiriki Mechi Na. 26 isivyo halali.

    Wachezaji hao walisajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo na kupewa leseni zilizotolewa tarehe 28 Desemba 2017 zenye namba: Elias Costa Elias (950307002), Lukwesa Joseph Kanakamfumu (980509002), Dunia Abdala Dunia (970625006), Doto Justine Kana (970417002), na Mwarami Abdala Mwarami (970914003). Huu ni uthibitisho kuwa kulikuwa na udanganyifu kwa vile mchezaji hawezi kusajiliwa mara mbili ndani ya msimu mmoja kwa timu ile ile.
  4. Taarifa ya mwamuzi wa Mechi Na. 26 inaonyesha kuwa namba ya leseni za wachezaji Lukwesa Joseph Kanakamfumu (aliyevaa jezi namba 7) na Mwarami Abdala Mwarami (jezi namba 8) ilikuwa na moja: 51995. Katika mazingira ya kawaida namba za leseni za usajili wa wachezaji wawili haziwezi kufanana kwa tarakimu zote.
  5. Ndg. Joseph Kanakamfumu aliieleza Kamati kuwa wakati anakabidhiwa timu na “Omba” aliikuta ikiwa na wachezaji wachache. Hata hivyo wakati anakabidhiwa timu anasema kuwa alipokea kadi za wachezaji hao watano ingawa hawakuwepo kambini. Wachezaji waliofika mbele ya Kamati (Elias Costa Elias na Lukwesa Joseph Kanakamfumu) waliithibitishia Kamati kuwa hawakukamilisha usajili baada ya kutolipwa fedha za usajili. Alipoombwa kutoa uthibitisho wa kupokea kadi za wachezaji hao watano kutoka kwa “Omba”, Ndg. Joseph Kanakamfumu hakuweza kutoa nyaraka zozote kuonyesha makabidhiano hayo. Aidha alipoulizwa na Kamati kwanini hakutaka kujiridhisha kama wachezaji hao wamesajiliwa kwa kuangalia kumbukumbu zilizoko TFF hakuweza kutoa majibu yoyote.
  6. Kwa mujibu wa maelezo ya Ndg. Kimilomilo, wachezaji hao watano hawakuwemo katika orodha aliyokabidhiwa Ndg. Joseph Kanakamfumu, hivyo hawakupaswa kuwemo katika orodha ya timu wala kushiriki Mechi Na. 26 kwa vile walitakiwa kusajiliwa kipindi cha dirisha dogo. Kamati ilipata uthibitisho kuwa wachezaji hao wanatoka katika Kituo cha Mpira wa Miguu (Football Academy) inayoendeshwa na Ndg. Joseph Kanakamfumu; hivyo ni wazi kuwa alikuwa anafahamu kila kilichokuwa kinaendelea.
  7. Kuna uwezekano wa udanganyifu kufanyika ndani ya mfumo wa usajili pale inapotokea baadhi ya maafisa wa TFF wasiokuwa na uaminifu kushirikiana na viongozi wa vilabu. Kwenye maelezo ya baadhi ya watuhumiwa ilionekana kuwa usajili wa Mvuvumwa FC ulifanywa kwa kiasi kikubwa na mfanyakazi wa TFF aliyejulikana kwa jina la Michael. Kamati ilipofuatilia ilielezwa kuwa mtumishi huyo aliondolewa na uongozi mpya wa TFF.

    HUKUMU
  1. Wachezaji Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami
    Kamati haikuwakuta na hatia yoyote wachezaji hawa kwa vile walishiriki Mechi Na. 26 baada ya kupotoshwa na viongozi wao kwa kuaminishwa kuwa usajili wao ulikamilika na wakapewa sehemu ya fedha walizoahidiwa kwa ajili ya kusaini. Vile vile wachezaji hawa hawahusiki na suala la usajili, hivyo hakukuwa na uwezekano wa wao kugushi leseni.

    Hata hivyo Kamati inawakumbusha wachezaji wote kuwa makini wakati wa kufanya makubaliano na timu zao kwani mpira ni ajira kwao. Suala kama hili linaweza kuwanyima fursa ya kukitumikia kipaji chao na kuwasababishia matatizo ambayo yanaweza kuepukwa kwa wao kuwa makini. Endapo wanakutana na vikwazo au kuhisi mazingira ya ubabaishaji ni vizuri waombe ushauri na msaada TFF.

  2. Ndg. Joseph Kanakamfumu – Kocha na Mratibu wa Mvuvumwa FC
    Kamati imemtia hatiani kwa makosa yote mawili; Kutoa taarifa zisizo sahihi/udanganyifu ili kufanikisha usajili wa wachezaji kinyume na kifungu cha 41(12) ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza toleo la 2017 na kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
    Katika kosa la kwanza, Ndg. Kanakamfumu, akiwa kocha wa Mvuvumwa FC aliwaorodhesha wachezaji Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami kushiriki Mechi Na. 26 huku akijua kuwa hawana leseni halali kutoka TFF. Wachezaji wote hao walitoka katika kituo (academy) anayoiendesha, hivyo ni dhahiri kuwa alijua alichokuwa anafanya.
    Katika kosa la pili, Ndg. Kanakamfumu aliamua kuwaongeza wachezaji hao baada ya kukabidhiwa timu kwa vile alifahamu uwezo wao na inaonekana alitumia uzoefu wake katika mpira wa miguu kupata leseni hizo za kugushi.

    Kwa makosa hayo, Kamati inamfungia Ndg. Joseph Kanakamfumu kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5). Adhabu hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.

  3. Ndg. Ramadhani Kimilomilo – Katibu wa Mvuvumwa FC
    Kamati imemtia hatiani kwa kosa kushiriki kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
    Ndg. Kimilomilo akiwa kama Mtendaji Mkuu wa Mvuvumwa FC alishindwa kusimamia timu yake ipasavyo na kusababisha ichezeshe wachezaji wasio na leseni. Aidha Ndg. Kimilomilo hakutoa taarifa TFF wala Bodi ya Ligi au kuchukuwa hatua zozote kwa Ndg. Joseph Kanakamfumu licha ya kukiri mbele ya Kamati kuwa wachezaji hao hawakuwemo katika orodha ya Mvuvumwa FC. Hii inamaanisha kuwa alishirikiana na viongozi wenzake kugushi leseni ili kuiongezea nguvu timu yake.
    Kwa makosa hayo, Kamati inamfungia Ndg. Ramadhani Kimilomilo kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5). Adhabu hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.

  4. Dr. Yared Fubusa – Mwenyekiti na Mmiliki wa Mvuvumwa FC
    Kamati imemtia hatiani kwa kosa la kushiriki kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
    Dr. Yared Fubusa akiwa Mwenyekiti na Mmiliki wa Mvuvumwa FC amehusika kwa sehemu kubwa katika uendeshaji mbovu wa timu hali iliyosababisha matatizo mengi ikiwa suala la kugushi leseni za wachezaji Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami.
    Kwa mujibu wa maelezo ya Ndg. Joseph Kanakamfumu, kulikuwa na mawasiliano kati yake na Dr. Fubusa kuhusiana na uendeshaji wa timu. Hata suala la kuongeza wachezaji ili kuimarisha timu liliwezekana baada ya kupatikana fedha za kuwalipa kwa ajili ya kupata saini zao. Maelezo hayo yalithibitishwa na Ndg. Kimilomilo, Katibu wa Mvuvumwa FC. Kamati inaona kuwa Dr. Fubusa, ambaye alikuwa anatoa fedha za uendeshaji wa timu, alikuwa anapewa taarifa zote za matumizi yake. Aidha kama Mwenyekiti na Mmiliki alipaswa kujua kila kinachoendelea katika timu yake.
    Alipopewa taarifa ya wito wa kufika mbele ya Kamati ya Maadili, Dr. Fubusa alinukuliwa akisema kwa njia ya simu kuwa “TFF ni wapumbavu, mimi siwezi kuja huko. Kwanza mimi ndiyo mhanga”. Kauli hiyo ni ya dharau na ni kinyume na Kifungu cha 73(5) & (8) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
    Kwa makosa hayo, Kamati inampa adhabu zifuatazo;
  • Kwa kosa la kukaidi wito huku yeye akiwa mwanafamilia ya mpira wa miguu, Kamati inamfungia kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni tatu (Sh.3,000,000.00). adhabu hii ni kwa mujibu wa 73(5) & (8)(a) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
  • Kwa kosa la kusaidia kugushi leseni za wachezaji wa Mvuvumwa FC ili washiriki Mechi Na. 26, Kamati inamfungia kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5). Adhabu hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.
    Adhabu zote mbili atazitumikia kwa pamoja