MAELEZO YA SHUKURANI YA MWENYEKITI ALIYEMALIZA MUDA WAKE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF - KWA VIONGOZI NA WADAU WA SOKA NCHINI

July 19, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
1.Kama wote tunavyofahamu jana uongozi wangu wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulifikia tamati kama mlivyotangaziwa na Rais wa TFF. Kwa heshima kubwa naomba kutumia fursa hii kuwashukuru viongozi na wadau wa soka kwa ushirikiano mkubwa nilioupata kutoka kwao wakati nikitekeleza majukumu mbalimbali ya TFF.

2.Kwa kushirikiana na viongozi wa mpira wa miguu katika TFF na mikoa yote Tanzania Bara, pamoja na wadau wa soka, nimepata fursa kulitumikia soka la nchi yetu kwa nafasi mbalimbali. Kwa pamoja tumetekeleza majukumu ya ujenzi wa misingi ya uongozi bora katika TFF na wanachama wake.

 3.Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF:
(i) kwa kuniteua kuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, (Jan 2005 - Jan 2007). Nawashukuru pia wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mhe. Said El-Maamry kwa kunichagua kuwa Katibu wa Kamati hiyo. Ushirikiano mlionipatia ulioniwezesha kulitumikia taifa katika soka na kwa pamoja kurejesha nidhamu kwa kiwango kikubwa.

(ii) kwa kuniteua kuwa mjumbe wa Kamati Maalumu, iliyochunguza mkasa wa timu yetu ya Taifa ya wachezaji wa umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) mwezi Juni 2005. Nawashukuru wajumbe wa kamati  hiyo chini ya Dr. Hamad Ndee Mkuu wa Idara ya Michezo ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, kwa kunichagua kuwa Katibu wa kamati hiyo iliyoandaa taratibu za mashindano ya vijana  ambazo ni msingi  wa mashindano ya vijana wa umri chini ya miaka 17  hapa nchini.

(iii) kwa kuniteua kuwa Mjumbe wa Kamati Maalumu iliyotayarisha Programu ya kuendeleza Timu ya Taifa kwa kipindi cha miezi 15 (April 2006 hadi Juni 2007). Progamu iliyochangia Tanzania kiinua kiwango cha ubora wa soka kutoka nafasi ya 165 duniani mwezi Februari 2006 hadi nafasi ya 89 mwezi Desemba 2007.

(iv) kwa kunipa fursa ya kuwa mjumbe wa Kamati Maalumu ya kuboresha mapato ya TFF mwaka 2009. Nikiwa mjumbe na Katibu wa Kamati hiyo nilipata ushurikiano mkubwa kutoka kwa wadau wa soka nchini  na nje ya nchi.  Nina imani kuwa TFF itakamilisha utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati na ya wadau wa soka ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia tiketi za elektroniki.

(v) kwa kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kwa  vipindi viwili; Februari 2009 - Machi 2011 na kuniteua tena kuiongoza Kamati hiyo kwa kipindi cha pili Machi 2011 hadi jana tarehe 18 Julai 2013. Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF kwa imani kubwa iliyoonyesha kwangu na wanakamati wenzangu.

4.Nawashukuru wajumbe wote wa wa Mkutano Mkuu wa TFF, kwa ushirikiano mkubwa mliotoa kwangu na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kushiriki kwa amani na utulivu na kuzingatia Katiba za vyama vyenu, Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi na hivyo kufanikisha zoezi la chaguzi za viongozi katika wilaya zote na Mikoa yote ya Tanzania Bara na hivyo kuwezesha kuwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu, ambao  katika kikao chake cha kwanza baada ya chaguzi hizo kimefanya jambo la kihistoria kuweka nguzo za  Mwenendo, Maadili  na Miiko ya uongozi wa soka la nchi yetu. Nilifarijika kuwa sehemu ya Mkutano Mkuu huo nikiwa mwalikwa.

5.Nawashukuru viongozi na wafanyakazi wote wa Sekretarieti ya TFF, wajumbe wa Kamati zote za TFF, Wajumbe wa Kamati zote za Uchaguzi za wanachama wa TFF na wanachama wao, kwa ushirikiano mkubwa na wa dhati uliowezesha kuwatumikia wadau wa soka kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

6.Nawashukuru sana wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ushirikiano niliopata kutoka kwao kwa muda tuliofanya kazi pamoja. Si jambo rahisi kusimamia chaguzi za mikoa yote na klabu zenye wanachama za Ligi Kuu, hata hivyo kwa kushirikiana na wadau mbalimali wa soka ambao nachukua fursa hii kuwashukuru, kwa pamoja tumeweza kutimiza jukumu hilo kikamilifu. 

7.Nawashukuru sana Wandishi na Wahariri wa habari za michezo na pia Wahariri Watendaji wa vyombo vya habari, kwa ushirikiano mzuri nanyi, ushirikiano na uhusiano wa uwazi ambao haukuwa na mikwaruzo ya aina yoyote kwa kipindi chote (Jan 2005-Jul 2013) tulichoshirikiana kwa pamoja kulitumikia soka la nchi yetu.

8.Namshukuru sana Rais wa TFF Ndg. Leodegar Tenga kwa imani kubwa aliyonayo kwangu na kwa wanakamati niliokuwa nao katika kutekeleza majukumu ya umma. 


Miaka ishirini na tisa (29) iliyopita nilipata fursa ya kufanya kazi ya mpira miguu kwa mara ya kwanza na Ndg. Tenga, nikiwa nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Desemba 1984, wakati Ndg. Tenga alipojitolea kuifundisha timu ya Chuo Kikuu cha DSM. Tangu wakati huo hadi sasa imani  na  ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya umma niliopata kutoka kwa Ndg. Tenga haujawai kutetereka hata kwa siku moja. 

Ni faraja kubwa kwangu kufanya kazi hizi za umma chini ya kiongozi anayeheshimika na kuaminika na wadau wa soka hapa nchini, Afrika Mashariki na Kati, Afrika na familia ya soka Duniani kwa ujumla.

9.Mwisho, kwa viongozi na wadau wote wa mpira wa miguu, nawashukuru na nawatakia kheri, baraka  na mafanikio katika Uchaguzi Mkuu wa TFF na  ujenzi wa  soka la nchi yetu..

 

WAZIRI akataa kupokea mradi wa Maji wa zaidia ya Milioni 400 jimboni kwake.

July 19, 2013
Na Mwandishi Wetu,Bumbuli
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambae pia ni Mbunge wa Bumbuli January Makamba amekata kupokea mradi wa maji wa zaidi ya Sh Mil 400 ambao ungehudumia vijiji vinne vilivyoko kwenye Jimbo la Bumbuli kutoka na kujengwa chini ya kiwango.

Hayo aliyasema wakati akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha stendi jimboni humo,alisema licha ya mradi huo kutengewa fedha nyingi na wahisani lakini haukutekeleza vile ulivyotakiwa.

Alisema mradi huo ulikuwa uanze kutoa huduma zake kuanzi kijiji cha Kwamanolo ambao ulikuwa ujenzi unaanzia pamoja na kujenga tanki lenye uwezo wa kuchukuwa lita lakimoja na thelathini na tano lakini tanki lilijengwa linachukuwa lita 90 tu

“Nimekata kuupokea mradi wa maji katika Jimbo langu kutoka na kutoridhishwa na ujenzi wake lakini pia nimemuomba waziri wa Maji Jumanne Maghembe atusaidi kuingiza kijiji kimoja katika mradi wa maji uofadhiliwa na Benki ya dunia wa kuhudumia vijiji kumi ili kupunguza shida ya maji Bumbuli”alisema Makamba.

Nae Diwani wa kata ya Bumbuli Tulo Guga alisema kuwa mradi huo ulikuwa unufaishe vijiji vya Bumbuli Mission,Bumbuli Kaya,Mboki na Kwamanolo lakini makubaliano ilikuwa kule eneo mradi unapoanzia nilazima maji yaanze kupatika na pamoja na ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji.

Aliongeza kuwa yote hayo mkandarasi hakuyatekeleza licha ya kazi ya ujenzi kukamilika kwa wakati ,lakini kikubwa zaidi ni kujenga tanki ndogo la kuhifadhia maji ambalo halitaweza kuhudumia wananchi wengi kwa wakati mmoja.

Hivyo aliiomba Halimashauri ya Wilaya ya Lushoto kuupokea mradi huo na kujaribu kurekebisha mapungufu kabla ya kuukabidhi tena kwenye Hlamshauri ya Bumbuli ili wananchi waweze kunufaika na mradi huo na kuondokana na kero ya maji .
 
Viongozi wa Dini waaswa

Viongozi wa Dini waaswa

July 19, 2013

Na Mwandishi Wetu,Tanga
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya  dini wametakiwa kuhamasisha mafunzo ya  kuzingatia maadili na matendo mema kwa umini wao kama ambavyo vitabu vya dini hizo  yalivyoamrishwa  ili kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya UKIMWI kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Rai imetolewa na Naibu Meya wa Jiji la Tanga Muzamin Shemdeo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu UKIMWI na Jinsia kwa makundi ya mbalimbali ya kijamii yaliyoratibiwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia programu ya UKIMWI iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa mipango miji jiji hapa.

Alisema viongozi hao wanajukumu la kuhaisaidia jamii iepukane na ngono zembe kwa kutoa mafunzo yanayohusia na matendo mema ili kuisaidia jamii isiendelee kuangamika katika gonjwa hilo ambalo kwa sasa idadiya maambukizi   inazidi kukua kwa kasi.

“Tunatambua kuna jamii  inayoamini mafundisho ya dini na wengine hata uwaeleze vipi hawana imani hivyo ni vema viongozi wa dini tukashirikiana  katika kuelimishana,na nyie wanahabari tumieni taaluma yenu katika kutoa habari sahihi za ugonjwa huu ili jamii ielimike”alisema Shemdoe.

Nae Mkufunzi wa mafunzo hayo Desideri Joseph alisema mabadiliko ya kijamii yanayotokea ulimwenguni pamoja na nguvu za kiuchumi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuathiri maadili  na tamaduni zetu  kama watanzania .

Alisema stadi za maisha zimekosekana pamoja na hali ya uchumi kuwa duni katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla imekuwa ni kikwazo kikubwa cha udhalilishaji wa kijinsi hali inayopelekea kuchangia maambukizi ya UKIMWI katika jamii nchini.

Hata hivyo Shekhe Shariff Mohamed Yahya alisema uhamasishaji kutumia  wa kondom ilikujilinda  licha ya dini kupinga ndio umekuwa kuhamasisha ngono na kuchangia kasi ya maambukizi mapya kila siku hivyo ni vema jamii ikamrudia mungu ili kupata salama katika gonjwa hilo.

Vilevile Mratibu wa UKIMWI Jiji la Tanga Moses Kisibo alisema kwa sasa kiwango cha maambukizi ni 7.8% huku waathirika wengi wakiwa ni wanandoa na vijana walio katika umri kuolewa ndio kundi linalofuata.

Mafunzo hayo ya siku moja yalihusisha makundi mbalimbali ya watu wakiwemo Viongozi wa dini kutoka taasisi mbalimbali,nakundi ya vijana,wazee,wanasiasa pamoja na waandishi wa habari kwalengo la kuihamasisha jamii juu ya kutambua wajibu wao katika mapambano ya ugonjwa huo.
MWISHO