KATIBU WA NEC IDARA YA SUKI, NGEMELA LUBINGA AMNADI MGOMBEA WA CCM JIMBOLA SINGIDA KASKAZINI LEO

January 09, 2018
Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kushoto) akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Singida Kaskazini ndg:Justine Monko (kulia) wakati wa mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini  Bi Grace Shindika Akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida
.Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (katikati) akizungumza na Mgombea Ubunge Jimbo ;la Singida Kaskazini ndg: justine Monko (kwanza kushoto) pampoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Ndg:Juma Kilimba.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe: Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida mhe: Martha Mlata  akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida ndg:Juma kilimba akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akizungumza na kumnadi Mgombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida
 Viongozi wakifurahia jambo
Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini Ndg:Justine Monko akijinadi katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

DK.KIGWANGALLA ATEUA KAMATI BONDE LA MTO KILOMBERO

January 09, 2018

*NI kamati maalum itakayochunguza athari za bonde hilo na kumpatia majibu
*Akagua maeneo mbalimbali ya bonde hilo na kuhushudia athari zaidi
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ameteua Kamati maalum ambayo itaishahuri Serikali namna ya nini kifanyike katika kushughulikia  athari za bonde la Kilombero lililopo Mkoani Morogoro.

Waziri Dk Kigwangalla amebainisha kuwa Kamati hiyo aliyoiteua,  ndio itamshahuri juu ya bonde hilo litasimamiwa vipi pamoja na namna bora ya hatua za kuchukua ili kulinda bonde hilo ambalo lina mahitaji makubwa ikiwemo chanzo kikubwa  cha maji yanayotengeneza Stiegler’s Gorge ambako Serikali imeamua kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme unaotarajiwa kufikia megawatts 2100 huku pia bonde hilo likiwa na utajiri wa kuwepo na aina zaidi ya 400 ya ndege pamoja na mnyama anaina ya Puku ama Sheshe ambaye hapatiani duniani kote zaidi ya Tanzania pekee.

"Hii ndio Kamati yangu, itakayonishahuri juu ya bonde ili litasimamiwa vipi.

 Hii ndio Kamati ambayo itanishahuri mimi na kwamaana hiyo Serikali kwa ujumla wake juu ya namna bora ya uhifadhi hususani katika eneo lile la Pori tengefu.

Hapa kuna vitu viwili vya kuzingatia: Ardhi Ohevu (Ramsar site) ambalo lina eneo lake huku pia eneo la pori tengefu nalo kichukua nafasi kubwa zaidi" Amesem Waziri Dk Kigwangalla wakati wa kuteua Kamati hiyo.

Kamati hiyo inaundwa na  wajumbe mbalimbali ambao wataongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Ndugu Andrew Napacho, Pia wajumbe ni  Brig. Gen. (Mst.) Edmund Mndolwa, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Mstaafu, Suleiman Kova, Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha wafugaji Bwana  Semkae Kilonzo (Policy Forum).

Wengin ni  Dk. Simon Mduma, Prof. Jaffar Kideghesho, Ruzika Muheto, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, MKuu wa Wilaya ya Kilombero na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi.

Wengine ni Mwenyekiti Halmashauri Ulanga, M/Halmashauri Kilombero, M/Halmashauri Malinyi  na M/Halmashauri Ifakara.

Pia yupo  Mtendaji Mkuu wa KPL, Mtendaji MKuu wa Illovo, Mkuu Kikosi JKT Chita. Wengine ni  Dk. Aggrey Mlimuka, Mwakilishi kutoka mamlaka ya maji Bonde la Kilombero, Mwakilishi kutoka Wizara ya ardhi.

Wajumbe wengine ni Ndugu.  Innocent Kylogeris, Dk. James Wakibara pamoja na Mkurugenzi Mkuu TAWA ambaye atakuwa Katibu wa Kamati hiyo.

Hatua hiyo inafuatia Waziri Dk Kigwangalla kufanya ziara maalum kwenye bonde hilo la kilombero ambapo ameweza kushuhudia athari kubwa zaidi zilizofanywa na wavamizi wakiwemo wakulima na wafugaji ambao wameonekana kuvamia maeneo makubwa  ndani ya pori tengefu la bonde pamoja na Kwenyeeneo ohevu ndani ya bonde hilo.

TFC YAPAKIA TANI 200 ZA MBOLEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK. JOHN MAGUFULI

January 09, 2018
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili jana na leo jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo,  Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji,  Sagar Shah na Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
 Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipakia mbolea hiyo kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda mikoani.
 Malori ya JWTZ yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
 Shehena ya mbolea hiyo ambayo inasafirishwa kwenda mikoani kwa wakulima
 Mbolea ikibebwa kuingizwa kwenye malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.
 Malori yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.

 Maghara ya kampuni ya Premium Agro Chem Limited yenye mbolea hiyo.

 Na Dotto Mwaibale


KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo. 

Waandishi wa Habari  jana na leo wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo hilo. 

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu juzi, waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori) ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). 

“Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba. 

Mkumba aliongeza kusema kwamba, kutokana na uzito wa agizo hilo lililotolewa na Rais Magufuli, wameongeza nguvu ya magari, yanayoelekezwa mikoa ya Katavi na Rukwa, ambako mahitaji ya mbolea hiyo ni makubwa kwa sasa. 

Alisema nusu saa baada ya tamko la Rais Magufuli, alipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage, akimtaka kuhakikisha wakulima kwenye maeneo husika wanatulia kwa kupokea mbolea. 

“Mbolea hii inapelekwa kwa wakulima kote nchini na itauzwa kwa bei elekezi ya szerikali, na ninawashukuru hawa wenzetu wa kampuni ya Premium Agro Limited kwa kuwa tayari kushirikiana kwa maslahi ya wananchi na Taifa letu,” alkisema Mkumba. 

Mkumba alisema wameamua kuingia makubaliano na kampuni binafsi ya Premium Agro Chem Limited, kupeleka mbolea hiyo kwenye maeneo hayo na mengineyo nchini yenye mahitaji, lakini akiamini kuwepo kwa unafuu kwenye maeneo mengine. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Primium Agro Chem Limited, Sargar Shah, alisema kwamba makubaliano na TFC ni kupakiwa kwa zaidi ya tani 1000 za mbolea hiyo kwenda katika mikoa ambayo wo hawana mawakala na kurahisha upatikanaji na pia kwa bei elekezi ya serikali. 

Meneja Biashara wa Primium Agro Chem Limited, ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia zoezi hilo Brijesh Barot, alisema wamejiandaa vizuri kufanya kazi hiyo mchana na usiku kwa nia ya kufikia malengo ambayo serikali imeyahitaji. 

Barot alisema kampuni hiyo tayari kuanzia mwezi Septemba, imesambaza kwa wakulima kupitia kwa mawakala wao zaidi ya tani 19,500 za mbolea ya kupandia aina ya Urea, ikiwa kwenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50. 

Barot aliongeza kusema kwamba, kampuni yake imeendelea kusambza na kuuza kwa wakulima mbolea zaidi kwa bei elekezi, licha ya kuwa tayari walimaliza kuuza tani 3,500 zilizoagizwa na serikali na kutakiwa kuuzwa kwa bei elekezi. 

“Sisi ni watanzania, wafanyabiashara wazalendo kwa nchi hii, hatutaki kufanyakazi kwa ajili ya kutafuta faida,badala yake tunaungana na Mheshimiwa Rais Magufuli, kuisaidia jamii kwa kufanya kazi ” alisema Barot.

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI(MIFUGO) DK MARIA MASHINGO AHIMIZA NGOMBE WENYE UMRI WA MIEZI SITA NA KUENDELEA KUPIGWA CHAPA

January 09, 2018
 KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akiwaeleza na wafugaji wa Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umuhimu wa zoezi la kupiga chapa ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu. 
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
Na Kumbuka Ndatta, KASULU
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo ameagiza ng’ombe wote wenye umri wa kuanzia miezi sita na kuendelea kuhakikisha wamepigwa chapa kabla ya kufikia tarehe ya mwisho ya upigaji chapa Januari 31 mwaka huu, kwani zoezi hilo sio la hiari bali ni la lazima na linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria.
Dk. Mashingo ametoa kauli hiyo wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa Wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.  

Dk Mashingo aliwaambia wafugaji hao kutambua kuwa zoezi hilo linasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na  ufuatiliaji wa mifugo  Na. 12 ya Mwaka 2010 na kuwasititiza kuwa haijulikani Serikali itaamua nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa hadi kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa ya Januari 31 mwaka huu.
Aidha Dk. Mashingo alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wafugaji sehemu maalum ambayo  ng’ombe anapotakiwa kupigwa chapa mwilini mwake ili kutoharibu ngozi yake inayotegemewa kwa  matumizi mengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali  Mstaafu Emanuel Maganga amesema zoezi la upigaji chapa linaendelea vizuri na mwitikio ni mkubwa kutoka kwa wafugaji ambapo jumla ya ng'ombe 93,182 wameshapigwa chapa kati ya ng'ombe 345,469 waliotambuliwa ambao ni sawa na asilimia 27.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Fatima Laay amemweleza Katibu mkuu kuwa jumla ya ng'ombe 7,552 kati ya 10,000 wenye umri wa zaidi ya miezi sita na kuendelea tayari wameshapigwa chapa ambao ni sawa na asilimia 75.52.
Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko alikiri kuwepo tatizo la Ng'ombe kupata vidonda vikubwa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo jambo lilochangiwa na wafugaji kutoelimishwa sehemu sahihi ya kupiga chapa mifugo.
"Mimi ng'ombe wangu bado hawajapigwa chapa,waliopigwa chapa walipata vidonda vikubwa kwa hiyo kama wataalam wetu ngazi ya vijiji wameelimishwa vizuri jinsi ya kupiga chapa basi haina shida nitawapeleka ng'ombe wangu wakapigwe chapa na kuhamasisha wananchi wengine kuunga mkono zoezi hili "alisema Nsanzugwanko.

WAZIRI PROFESA MBARAWA AVAMIA BANDARINI USIKU ABAINI MADUDU

January 09, 2018

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwa simu na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisini kwake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiondoka katika eneo linalotolewa huduma za kibenki bandarini jana usiku mara baada ya kukagua kama huduma zinatolewa saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakimuhoji mmoja wa wafanyakazi kwenye ofisi za wakala wa Meli ambaye ilibainika hawezi kutoa huduma zote zinazostahili.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakishuhudia moja ya wakala wa meli akiwa amefunga ofisi kinyume cha maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi saa 24.
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa jana usiku  amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini mawakala wa meli wanaotoa huduma katika bandari hiyo hawafanyi kazi saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.

Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mawakala wote waliokiuka agizo la Serikali la kutoa huduma bandarini kwa saa 24.

"Kati ya Mawakala wa Meli nane ambao tumewatembelea usiku huu ni wakala mmoja tu ndiye tuliyemkuta akitoa huduma kwa saa 24 hivyo SUMATRA katika kipindi cha siku saba hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa wote wanaokiuka utaratibu huu na nipewe ripoti ya hatua zilizochukuliwa," alisema Waziri Prof. Mbarawa.

"Katika ukaguzi huu tumegunduwa kuwa mawakala wengi wanaacha watoa huduma wasiostahili, wakiwemo walinzi kufanya kazi nyakati za usiku ambao hawawezi kutoa huduma inayostahili usiku na kuendelea kutoa huduma asubuhi jambo ambalo sio sahihi," amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na huduma zinazotolewa na taasisi za Serikali pamoja na benki, isipokuwa kwa taasisi ya Atomiki Enegy ambayo ameitaka ijieleze kwanini haifanyi kazi kwa saa 24 kama Serikali ilivyoagiza.

Profesa Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana 
bandarini hapo kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoingia na kutoka na mapato yanayopatikana katika huduma hiyo ya maji kujulikana.

Waziri Mbarawa katika ziara yake ya kushtukiza aliambatana na maofisa wa SUMATRA ili kujionea wenyewe ukiukwaji wa agizo la Serikali na kusisitiza nia ya Serikali kuitaka Bandari ya Dar es Salaam kufanya kazi saa 24 ni kuiwezesha kushindana na bandari nyingine katika ukanda wa Bahari ya Hindi na kuongeza mapato.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

SHAKA AWASILI SINGIDA LEO,KUMNADI MGOMBEA UBUNGE WA CCM SINGIDA KASKAZINI.

January 09, 2018
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka (Kulia) Akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ndg:Peter Monko  Alipowasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Singida leo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akisain kitabu cha wageni  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Singida (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Ndg Juma Kilimba.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  dkt. Denis Nyiraha akimkaribisha  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka alipowasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Singida.
''Tutashinda na tutashinda kwa sababu mtaji wa ushindi tunao lengo ni lile lile kuhakikisha Singida kaskazini inaendelea kuwa ngome ya CCM''Alisema Shaka wakati akizungumza na Viongozi wa CCM Alipowasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Singida leo.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

MHASIBU HALMASHAURI YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA AJISHINDIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA TATUMZUKA

January 09, 2018
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 50 mwishoni mwa wiki kwa Mkazi wa wilaya ya namtumbo mwenye umri wa miaka 31,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma,ndugu Jacob Ndee aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 50 .
Akielezea kwa furaha za kushinda kitita cha milioni 50 za mchezo huo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Jacob alisema kuwa ndoto yake kubwa siku akipata fedha za kutosha atazitumia kwa Kilimo,Anasema kwa sasa anaona ndoto yake imetimia baada kupata fedha hizo,hivyo atazitumia katika kilimo.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Kitita cha Milioni 50 cha TatuMzuka Ndugu Jacob Ndee pamoja na baadhi ya Wadau wengine,ambapo pia walionekana kuuufurahia ushindi wa Jacob,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

MPINA ATAKA MNADA MLUSAGAMBO KUFUNGULIWA KUDHIBITI UPOTEVU WA MILIONI MIA MOJA

January 09, 2018





Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akipata maelezo ya hali ya sekta ya mifugo na Uvuvi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denis Mwila (mwenye  suti  nyeusi) alipotembelea kituo cha mpakani cha Mutukula  leo.





Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akipokea  maelezo ya changamoto za ukaguzi mazao ya mifugo na Uvuvi  kutoka kwa Afisa Uhamiaji Konstabo, Rahabu Joel alipotembelea kituo cha mpakani cha Mutukula  leo.





Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akiangalia mabondo ya samaki aina ya Sangara yaliyokamatwa katika kituo cha mpaka cha Mutukula  mkoani Kagera. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya  Uvuvi Mwanaidi Mlolwa  katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Missenyi Limbe  Maurice. Kilo120 zilikamatwa katika kituo hicho.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akifungua mlango wa gari lililokamatwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato zenye  thamani ya shillingi 20,850,000/=  kwenye mpaka wa Mlusagamba wilayani Ngara tarehe 03/12/2017

Na John Mapepele


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina ya  Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kuhakikisha inafufua mara moja mnada wa Mlusagamba ifikapo mwezi Februari mwaka huu ili kudhibiti zaidi ya milioni mia moja zinazopotea kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali ya kusafirisha mifugo nje ya nchi kwa kupita njia za panya.
Waziri Mpina aliyasema haya leo alipokutana na uongozi wa Halmashauri hiyo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara katika kituo cha mpaka cha Rusumo baina ya Tanzania na Rwanda kukagua shughuli mbalimbali za sekta za Mifugo na Uvuvi  baada ya kutokea katika kituo cha Mutukula mkoani Kagera ambapo pia alifanya ukaguzi kama huo na kukamata kilo 120 za mabondo ya samaki aina ya Sangara yaliyokuwa yakitokea nchi jirani ya Uganda bila kufuata utaratibu.
“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya sekta ya mifugo na uvuvi naelekeza kwamba ifikapo Februari mwaka huu nataka miundo mbinu yote iwe imeboreshwa na mnada wa Mlusagambo uwe unafanya kazi katika kiwango cha mnada wa upili na mimi mwenyewe nitahakikisha ninakuja kuuzindua”lisisitiza Mpina
Waziri Mpina alisema kutokuwepo kwa Mnada wa Mlusagambo kunaipotezea Serikali mapato makubwa ambapo mifugo mingi imekuwa ikiuzwa katika nchi jirani na Serikali kuambulia kiasi kidogo cha fedha kutokana na wafanyabiashara kupita njia za panja na kufanikiwa kukwepa kulipa kodi malimbali za Serikali.
Alisema taarifa inaonyesha kuna idadi kubwa ya Ng’ombe  wanaopita njia za panya ambao hawatozwi  ushuru wa kushafirishwa  jambo ambalo amelilalamikia kuwa ni  hujuma  na kuendekeza rushwa  baina ya watendaji wa Serikali.
Aidha amesema Wizara inakusudia kuomba Serikali kupandisha ushuru wa kusafirisha mifugo (movement permit) kufikia shilingi 50,000/= badala ya shilingi 20,000/= ya sasa kwa kuwa hailingani  na hali halisi ya soko na gharama za utunzaji wa mifugo hiyo.
“Tutahakikisha tunaiomba serikali ibadili ushuru huu kwa kuwa mfugaji anatumia gharama kubwa za kumfuga na kumnenepesha mfugo kwa zaidi ya miaka mitano halafu anakuja kupata shilingi 20000 tu ni jambo lisilokubalika” alisisitiza Mpina
Aliongeza kwamba baada ya kukamilika kwa mnada huo Serikali itaweka vizuizi katika njia zote za panya ambapo pia alisisitiza watendaji wa Serikali na wananchi kwa ujumla  kuwa waadilifu  na kuwa walinzi  badala ya kutegemea   viongozi wa kitaifa wa Serikali kulinda utoroshaji wa raslimali za taifa ikiwa ni pamoja na mifugo, samaki  na mazao mbalimbali yatokanayo na sekta hizo.
Aidha alisema katika njia zote za panya inashangaza kuona kuna wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, kata, vyombo vyote vya serikali vya ulinzi na usalama pia kuna Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya lakini utoroshaji unaendelea bila wahalifu hao kukamatwa, ambapo aliwataka watendaji wote kuwa waaminifu na kumwagiza Mkuu wa Wilaya kuwachukulia hatua za mara moja watendaji watakaobainika kujihusisha na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na rushwa.
Akitolea mfano wa jinsi alivyokamata kilo 65,600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia hivi karibuni, alisema  zoezi hilo lilifanikiwa baada ya yeye kupata taarifa kutoka  kwa raia mwema ambapo aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye kuwakuta  samaki hao wakiwa wameanikwa chini katika kisiwa hicho.
“Naomba kusema raia mwema huyo alitoa taarifa siyo kwa sababu alilipwa fedha  bali alikuwa na uchungu na uzalendo wa dhati kwa taifa lake baada ya kuona kwamba  raslimali ya taifa inatoweka” alihoji Waziri Mpina
Aidha, Waziri Mpina alisema Wizara inapambana kuhakikisha kwamba kunakuwa na kodi ya mifugo ambapo kila mfugo utatakiwa kulipiwa kodi tofauti na mfumo wa sasa ambapo hakuna kodi ya moja kwa moja inayotozwa kwa mifugo.
Alisema  uanzishwaji wa kodi ya mifugo utasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya mifugo katika kipindi kifupi kijacho  kwa kuwa fedha itakayokusanywa itatumika katika kununua madawa ya ruzuku kwa mifugo, chanjo, kuboresha  malisho na miundombinu mbalimbali ya mifugo ikiwa ni pamoja na majosho na malambo ya kunyweshea  maji mifugo hiyo.
Alisema taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 30 ya mifugo yote nchini inateketea nchini wakati wa jua kali kipindi cha kiangazi kwa sababu ya kukosa maji na malisho bora jambo ambalo  ni hasara kubwa kwa taifa.
Mbunge wa jimbo la Ngara, mheshimiwa,Alex Raphael Gashaza alipendekeza wafugaji kutambuliwa kwa kulipa kodi ya mifugo na kuanzisha vitalu maalumu vya ranchi za mifugo ili kuthibiti magonjwa na kuinua ubora wa mifugo.
Alisema utaratibu huo pia utapunguza migogoro mingi inayojitokeza sasa baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ambapo ambapo pia ameipongeza Serikali kwa juhudi inazofanya katika zoezi linaloendelea la kupiga chapa mifugo.
Akitoa ufafanuzi Waziri Mpina alisema Serikali inaruhusu uanzishwaji wa ranchi  ndiyo maana suala hilo limezingatiwa katika sheria mbali mbali za tasnia ya mifugo ikiwa ni pamoja na Sheria ya Utambuzi, Usajili  na Ufuatiliaji Mifugo Namba 12  ya Mwaka 2010, Sheria ya Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo Namba 13 ya Mwaka 2010, na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo namba 4 ya Mwaka 2012.
Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele  alimweleza Waziri kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2017 jumla ya kilo 903,018 za mazao ya uvuvi kutoka katika maeneo ya Mwanza,Mganza,Kagera, Kigoma na Dar es Salaam yenye thamani ya shilingi  bilioni mbili yalikaguliwa na kuhakikiwa na kuruhusiwa kusafirishwa kupitia kituo cha mpakani cha Rusumo.
Aidha alisema kituo cha Rusumo katika kipindi hicho kimekusanya shilingi 7,058,300 kama mrahaba kwa mazao ya uvuvi yanayokwenda nje ya nchi.
Akiwa katika ziara hiyo Waziri Mpina alipata fursa ya kuliona na kukagua  gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter lililokamatwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato zenye  thamani ya shillingi 20,850,000/=  kwenye mpaka wa Mlusagamba wilayani Ngara tarehe 03/12/2017 saa tatu asubuhi ambapo aliwaelekeza watendaji kuhakikisha taratibu zote za kisheria zinafuatwa ili kuweza kulitaifisha gari hilo  kulingana na Sheria  ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2012 na 2015.
Katika tukio hilo Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana  Ayoub Ngoma  na dereva  wa gari hilo Ayoub Sanga  walishikiliwa na polisi ambapo Ngoma alisimamishwa kazi mara moja kupisha uchunguzi.
Aidha Mshauri wa Uvuvi wa Mkuu wa Mkoa, Efrazi Mkama na  maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya Muleba Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki hao.