MIUNDOMBINU YA UMEME ITAKAYOENDESHA TRENI YA MWENDO KASI (SGR) KUKAMILIKA JANUARI 2024

November 16, 2023

 





Leo tarehe 16 Novemba, 2023 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Kilumbe Shaban Ng'enda imetembelea na kukagua miundombinu ya umeme iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya kuendesha treni ya kisasa ya mwendokasi (SGR) pamoja na mitambo ya uzalishaji Umeme wa Gesi Asilia ya Kinyerezi I (MW 150), Kinyerezi II (MW 240) pamoja na Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kinyerezi (MW 185) iliyopo Dar es Salaam.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Shaban Ng'enda, amesema kuwa ziara hiyo ilianza tarehe 11 Novemba, 2023 kwa lengo la kuangalia namna ambavyo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia Wizara ya Nishati limekuwa likitekeleza mradi wa miundombinu ya umeme itakayoendesha treni ya mwendokasi (SGR), wakianza na vituo vya Morogoro na kuhitimisha kituo cha Kinyerezi.


*"Sisi kama Kamati tumeridhishwa na maendeleo ya kazi hii, kwasababu mradi huu kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umekamilika kwa asilimia 100 na Morogoro hadi Kintiku mkoani Singida kwa asilimia 99.Tumeridhishwa na tunawatia shime wafanyakazi wote wa Wizara ya Nishati na TANESCO kwa ujumla kusimamia kazi hii kwa umakini mpaka itakapokamilika"* Amesema Mhe. Ng'enda


Amesisitiza kuwa, TANESCO kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC ) kuwa na mitambo ya akiba (backup) itakayosaidia endapo kutakuwa na dharula kwenye Grid ya Taifa ili treni ya mwendo kasi iendelee kufanya kazi.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha fedha takribani bilioni 76 ili kufanikisha miundombinu ya umeme kwa ajili ya mradi wa treni ya mwendokasi.


*“Sisi Wizara ya Nishati tumeshirikiana na Wizara ya Uchukuzi kuhakikisha miradi hii inatekelezwa vizuri na sasa tumekamilisha kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Kingorwila, Morogoro. Tunamshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jwmhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maelekezo yake, vile vile kwa kutenga fedha kwa ajili ya miradi hii ambayo ina maslahi kwa maendeleo ya Tanzania. Sisi kama Wizara ya Nishati tukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko tutasimamia miradi hii kwa ufanisi mkubwa na kuhakikisha inakamilika kwa wakati"* Amesema Mhe. Kapinga


Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amewashukuru wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana pamoja katika kufanikisha utekelezaji wa mradi wa miundombinu ya kuendesha treni ya SGR. Amesema kuwa hadi sasa wanategemea kupokea vichwa vya treni ya mwendo kasi na kufanya majaribio ili kujiridhisha na utendaji kazi wake ambayo itatembea kwa mwendo wa kilomita 160 kwa saa.

NEC YAKUTANA NA VYAMA VYA SIASA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

November 16, 2023

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza na wawakilishi kutoka Vyama vya Siasa kuhusu majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yanayotarajiwa kufanyika katika Kata za Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora na Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

Vyama vya siasa vimehimizwa kushiriki kwenye majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yanayotarajiwa kufanyika katika Kata za Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora na Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele ametoa wito huo leo tarehe 16 Novemba, 2023 wakati akifungua mkutano wa Tume na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam.
 
“Vyama vya siasa kwenye zoezi hili vitashiriki kwa kuweka wakala mmoja katika kila kituo cha kuandikisha wapiga kura, lengo ni kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika wakati wa majaribio ya uboreshaji wa Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Amenongeza kuwa majaribio ya uboreshaji yanafanyika kwa lengo la kupima uwezo wa vifaa na mifumo itakayotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kufanyika nchi nzima kwa tarehe zitakazopangwa na kutangazwa na Tume.
 
Majaribio ya uboreshaji yatahusisha kuandikisha raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na atakayetimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
 
Kundi lingine litakalohusika kwenye zoezi hili ni; wapiga kura wanaoboresha taarifa zao ambao wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo lingine, waliopoteza au kadi zilizoharibika, wanaorekebisha taarifa zao na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari.
 
Majaribio ya uboreshaji yatafanyika katika vituo 16 vya kuandikisha wapiga kura. Kati ya hivyo, vituo 10 ni vya Kata ya Ng’ambo na vituo sita (6) ni kutoka Kata ya Ikoma. Vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
 
“Tume inatoa wito kwa wakazi wa Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika majaribio ya uboreshaji wa Daftari na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hili muhimu kwa mustakabali wa Taifa,” amesema Jaji Mwambegele.
Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa vikishiriki katika mkutano huo wa Tume na Vyama vya siasa.

Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa vikishiriki katika mkutano huo wa Tume na Vyama vya siasa.
Viongozi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) nao wakiwa katika mkutano hao.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa majaribio wa Daftari La Kudumu la Wapiga Kura. 
BVR Kits zenye vifaa mbalimbali vinavyowasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura BVR Kits za sasa ambazo zinatumia programu ya android tofauti na BVR Kits za awali ambazo zilikuwa zinatumia programu ya Microsoft Windows.

BENKI YA NMB INATOA MPAKA BILIONI 340 KWA WAWEKEZAJI WAKUBWA

November 16, 2023

 

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus akielezea fursa za benki hiyo wakati wa Kongamano la Uwekezaji wa Biashara na Utalii lililofanyika kwenye ukumbi wa Regail Naivera Jijini Tanga ambalo lilifunguliwa na Waziri wa Uwekezaji na Mipango Profesa Kitilya Mkumbo ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus akielezea fursa za benki hiyo wakati wa Kongamano la Uwekezaji wa Biashara na Utalii lililofanyika kwenye ukumbi wa Regail Naivera Jijini Tanga ambalo lilifunguliwa na Waziri wa Uwekezaji na Mipango Profesa Kitilya Mkumbo ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus akielezea fursa za benki hiyo wakati wa Kongamano la Uwekezaji wa Biashara na Utalii lililofanyika kwenye ukumbi wa Regail Naivera Jijini Tanga ambalo lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitilya Mkumbo ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kasim Majaliwa 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitilya Mkumbo ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo wakiwemo watumishi wa Benki ya NMB mara baada ya kufungua kongamano hilo
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitilya Mkumbo ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo wakiwemo watumishi wa Benki ya NMB mara baada ya kufungua kongamano hilo


Na Oscar Assenga,Tanga,

BENKI ya NMB imeshirikiki Kongamano la Uwekezaji wa Biashara na Utalii katika Mkoa wa Tanga huku wakibainisha kwamba kwa hivi sasa mwekezaji mkubwa anaweza kuchukua mkopo mpaka bilioni 340 kwa mkopaji mmoja.

Hayo yalibainishwa leo na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus wakati wa Kongamano la Uwekezaji wa Biashara na Utalii lililofanyika kwenye ukumbi wa Regail Naivera Jijini Tanga ambalo lilifunguliwa na Waziri wa Uwekezaji na Mipango Profesa Kitilya Mkumbo ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.

Alisema kwamba hivyo kupitia hilo wawekezaji wanaweza kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo ili kuweza kujikwamua kiuchumi ambao utakuwa chachu ya kukuza pia mitaji yao na hatimaye kuweza kuchochea ukuaji wa biashara zao.

“Wenzetu wa Simba kama mtaji ni changamoto karibuni sana lakini uwekezaji huo wa Tanga hauwezi kuwezekana bila kuwa na upatikanaji wa huduma za kifedha na wana matawi ya benki zaidi ya 12 kwa wilaya zote nane na wilaya nyengine wana matawi mawili na hivyo hii ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha tunazoziongelea”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba benki hiyo wamejipanga vizuri na itaendelea kushirikiana na Serikali ili kuchangiza maendeleo muhimu kwa watanzania .

Meneja huyo wa Kanda aliwaeleza wawekezaji watanzania waliopo mkoani Tanga kwamba benki hiyo inajivunia kushiriki kwenye kongamano na wanataka kuwaambia wawekezaji wa Tanga kwamba inajivunia uwezo wake mkubwa kuwahudumia sekta mbalimbali za uwekezaji na wameanza kuhudumia sekta ya biashara za kati na wadogo kwa kuwa na muda mrefu wa kuwahudumia.

Hata hivyo alisema kwamba pia benki hiyo imeendelea kukuza mtaji wake na niwaambie wawekezaji kwamba benki ina uwezo mkubwa wa kutoa mitaji ambayo itachagiza uwekezaji ambao unaozungumziwa leo ambao umekuwa mkombozi kwao.