Mtanzania Alphonce Simbu anyakua nafasi ya 5 London Marathon

Mtanzania Alphonce Simbu anyakua nafasi ya 5 London Marathon

April 23, 2017
pic+simbu
Alphonce Simbu Balozi wa DStv na Mshiriki pekee kutoka Tanzania aliyeshiriki mashindano ya London Marathon yaliyofanyika leo jijini London ameibuka mshindi wa tano huku akivunja rikodi yake kwa kutumia muda wa 2:09.10 ambao ndio muda wake bora zaidi tangu aanze kushiriki mashindano ya kimataifa. Kabla ya hapo rekodi yake ilikuwa muda wa 2:09.21aliyoiweka mwaka jana kwenye mashindano ya Lake Biwa Marathon nchini Japan.
Simbu ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu wa Mumbai Marathon ameonyesha umahiri mkubwa katika mashindano hayo hasa ikizingatiwa kuwa mashindano hayo yalikuwa yanashirikisha vinara wengi wa riadha ulimwenguni wakiwemo Muethiopia Kenenisa Bekele  wakenya Daniel Wanjiru, Bedan Karoki na Abel Kirui.
Mara baada ya ushindi huo salamu za pongezi zimekuwa zikimiminika huku mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akisema kuwa kampuni yake imeridhishwa sana na ufanisi aliouonyesha katika mashindano hayo. Amesema uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo katika kumdhamini Simbu umezaa matunda kwani kiwango cha mwanariadha huyo kimekuwa kikiimarika siku hadi siku. “Tumefurahishwa sana na kiwango alichoonyesha Simbu kwenye London Marathon. Hii ni ishara nzuri sana na tunaamini atafanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London mnamo mwezi Agosti mwaka huu”
Kwa upande wake, meneja wa mwanariadha huyo Francis John amesema kuwa ameridhishwa na kiwango alichoonyesha Alphonce Simbu na kwamba punde tu atakaporejea wataanza maandalizi kwa ajili ya ushiriki wake katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika mwezi agost mwaka huu.
Katika mashindano hayo nafasi ya kwanza imechukuliwa na Mkenya Danie Wanjiru (2:05:48) akifuatiwa kwa karibu na Kenenisa Bekele (2:05:57) na Bedan Karoki (2:05:41)
Harusi ya John Focus na Bi. Bernadetha Munishi ilivyofana

Harusi ya John Focus na Bi. Bernadetha Munishi ilivyofana

April 23, 2017
Bwana harusi, John Focus Lyimo akimlisha ndafu mkewe kwenye hafla ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni kabla ya hafla hiyo. Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akimlisha keki mumewe John Focus Lyimo kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni. Bwana harusi, John Focus Lyimo (katikati) akiandaa ndafu maalum kwa ajili ya kumlisha mkewe ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani mara baada ya ndoa yao. Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi pamoja na wapambe wao wakiwa kwenye hafla hiyo.  Bwana harusi, John Focus Lyimo (wa pili kushoto) akimtambulisha mkewe Bi. Bernadetha Munishi (wa pili kulia) kwa wageni waalikwa kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Waliokaa ni wapambe wa maharusi.  Dada na mashemeji wa bwana harusi.. Bwana harusi, John Focus Lyimo (kushoto) akipita meza hadi meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akipita meza kwa meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Maharusi wakiwaongoza wageni waalikwa kwenye maakuli... Wanajumuiya wenzake na bwana harusi, John Focus Lyimo kutoka Temboni wakiongozwa na Mr&Mrs Msafiri wakishiriki katika hafla hiyo Kulia ni MC Leopold Sondoka (mwenye kipaza sauti) akitoa maelekezo kwa Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi kwenye hafla hiyo. Wazazi wa Bwana harusi wakiongozwa na mwakilisha wa Baba ndg, Pius Elias (kushoto) wakizungumza machache kwenye hafla hiyo. Wazazi na ndugu wa bibi harusi wakipata picha ya ukumbusho. Familia ya bwana harusi ikiongozwa na mwakilisha wa baba ndugu, Pius Elias wakigonganisha glasi kwa furaha Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi wakionesha furaha yao kwa kugonga chiaz... Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya harusi hiyo wakigonga chiaz kwa furaha kubwa baada ya kufanikisha shughuli hiyo. Kutoka kushoto ni Mrs. Machonchoryo na Mrs Oscar Munishi. Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi wakiwalisha vipande vya ndafu 'mades' wao kama ishara ya kuwashukuru. Wanakamati wakinyanyua keki waliopewa na maharusi kama shukrani kwa kujitoa na kufanikisha hafla hiyo... Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi (kushoto) wakimkabidhi keki ya asante Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia). Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia) akiwatambulisha wajumbe mbalimbali wa kamati yake. Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi
UZINDUZI WA MRADI WA GARI 8 ZA CCM JIMBO LA MFENESINI UNGUJA.

UZINDUZI WA MRADI WA GARI 8 ZA CCM JIMBO LA MFENESINI UNGUJA.

April 23, 2017
mag1
Gari nane (8) aina ya Dyna  zilizonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Mfenesini  Mhe.Col.Mstaafu Masoud Khamis ambazo leo amezikabidhi kwa Chama cha Mapinduzi CCM zitakazotumika na kutoa huduma katika Matawi ya Chama cha CCM katika jimbo hilo,ambazo zimegharimu jumla ya shilingi za kitanzania Millioni Mia moja na Tisiini na Mbili,[Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
mag2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Mbunge wa Jimbo la Mfenesini  Mhe.Col.Mstaafu Masoud Khamis alipowasili  katika viwanja vya   Z. Ocean Hoteli  iliyopo Kihinani Jimbo la Mfenesini leo katika sherehe za Uzinduzi wa Mradi wa Gari nane (8) za Chama cha Mapinduzi CCM ikiwa ni ahadi ya Mbunge wa jimbo hilo, [Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
mag3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanaCCM wa Jimbo la Mfenesini wakati alipowasili katika  viwanja vya Z. Ocean Hoteli  iliyopo Kihinani Jimbo la Mfenesini Wilaya ya Magharibi leo katika sherehe za Uzinduzi wza Mradi wa Gari nane(8) za CCM  zilizotolewa na Mbunge wa jimbo hilo Col.Mstaafu Masoud Khamis,ikiwa ni ahadi ya  kwa Wananchi, [Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
mag4
Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mfenesini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza katika sherehe za Uzinduzi wa Mradi wa Gari Nane (8)za CCM zilizokabidhiwa leo kwa Rais ikiwa ni ahadi ya Mbunge wa jimbo hilo Col.Mstaafu Masoud Khamis,ikiwa ni ahadi ya  kwa Wananchi hafla iliyofanyika katika ukumbi wa   Z. Ocean Hoteli  iliyopo kihinani Jimbo la Mfenesini,[Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
mag5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akipokea kadi za Gari Nane (8) aina ya Dayna ambazo Rais amezindua Mradi huo wa CCM zitakazotumika  katika Matawi ya Chama Jimbo la Mfenesini,Gari hizo ini ahadi aliyoitoa  Mbunge Mhe.Col.Mstaafu Masoud Khamis katika ukumbi wa Hoteli ya Z. Ocean iliyopo kihinani Jimbo la Mfenesini leo katika sherehe Jimboni humo, [Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
mag6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akitoa hutuba yake wakati  sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa Gari 8 za Chama cha Mapinduzi CCM zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mfenesini Col.Mstaafu Maoud Khamis ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa kwa jimbo,hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Z.Ocean Kihinani Wialaya nya Magharibi Unguja, [Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
mag7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akitoa hutuba yake wakati  sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa Gari 8 za Chama cha Mapinduzi CCM zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mfenesini Col.Mstaafu Maoud Khamis ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa kwa jimbo,hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Z.Ocean Kihinani Wialaya nya Magharibi Unguja, [Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
mag8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Gari Nane(8) ya CCM aina ya Dyna ikiwa ni ahadi ya Mbunge wa  CCM wa Jimbo la Mfenesini Col.Mstaafu Masoud Khamis (wa pili kulia) katika viwanja vya Z. Ocean  Hotel iliyopo kihinani Wilaya ya Magharibi Jimbo la Mfenesini leo, [Picha na Ikulu] 23/o4/2017.

MSANII WA BONGO FLEVA 'NILLAN' AMPONDA SHILOLE KWA KUHARIBU SHOW SIKUKUU YA PASAKA

April 23, 2017
 Na Mwandishi Wetu

MSANII wa Bongofleva anayetamba na kibao cha ‘Njenje’ Gilbert Paul maarufu kama ‘NILLAN’ (pichani kulia) ameponda kitendo kilichofanywa na msanii  mkubwa katika  tasnia hiyo Zuwena Yusufu ‘Shilole’ cha  kuharibu Show iliyotarajiwa kufanyika mkesha wa siku ya mkesha wa Pasaka na hivyo kusababisha hasara kwa promota.

Nillan aliyetarajiwa kufanya show siku pamoja na msanii mwingine Nuhu Mziwanda alisema kitendo kilichofanywa na Shilole siyo cha kiungwana kutokana na heshima kubwa aliyonayo msanii huyo kwa Taifa hili.

“Ukweli kitendo hicho mimi kama msanii chipukizi kimeniumiza sana, sikutaraji kingeweza kufanywa na msanii mkubwa na maarufu kama Shishi, namuheshimu kama dada yangu lakini kwa hili amejishushia heshima” alisema Nillan.

Show hiyo iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya  Merry Merry Entertainment, ilishindwa kufanyika baada ya Shilole kuchelewa kufika ukumbini hali iliyosababaisha mashabiki waliofika mahali hapo kulalamika warudishiwe fedha zao na baadae kuondoka.

Akizungumzia baada ya tukio hilo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Merry Mussa mbali na kulaani kitendo hicho cha Shilole alisema  ni lazima sharia itafuata mkondo wake kwa msanii huyo kulipa hasara yote iliyotokana na kitendo alichokifanya.

“Haiwezekani mtu tukubaliane afike  ukumbini saa  2 usiku, yeye anakuja  muda anaotaka, na hapo hapo hata kushuka kwenye gari hakushuka, hiyo ni dharau na kamwe sikubaliani na kitendo hicho hata kidogo” alisema Merry.

Shilole aliyetarajiwa kutoa burudani  siku hiyo ya mkesha wa Pasaka katika ukumbi wa Heinken uliopo Kijichi, aliwasili ukumbini hapo saa 7 za usiku tofauti na makubaliano na Promota aliyeandaa show hiyo.

Hata hivyo alipotafutwa Shilole kuzungumzia suala hilo alidai kufika ukumbini hapo kama taratibu zilivyo za wasanii kufika kwenye show mbalimbali hivyo haoni kama kuna kosa lolote alilifanya kuhusiana na show hiyo.
Kwa upande wake Nuhu Mziwanda aliyewah kuwa mahusiano na msanii huyo alikwenda mbali na kusema kitendo kilichofanywa na mpenzi wake huyo wa zamani ni ushamba na kumtaka kurudisha fedha alizochukua kutoka kwa promota.
Alisema anashangazwa kwanini Shilole alikubali kupokea fedha hizo na kuahidi kufanya show lakini badala yake akaingia mitini na kuibukia ukumbini muda ambayo show ilipaswa iwe mwishoni.


Akizungumzia suala hilo Meneja wa kampuni ya Ochu Entertainment  inayomsimamia msanii Nillan, Felix Mkuya alisema kitendo kilichofanywa na Shilole ni cha kushangaza na hakipaswi kufanywa na  wasanii wa hapa nchini.

“Imagine watu wametumia gharama kubwa kuandaa ile Show, kila msanii alishapewa hela yake mkononi, sasa kwanini yeye afanye vile, Nuhu Mziwanda alifika ukumbini mapema saa 12 jioni, alikadhalika kwa Nillan…sasa vipi Shilole afanye vile” alihoji Mkuya.

HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS IJUMAA

HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS IJUMAA

April 23, 2017
SERENGETI-BOYS-1
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Gabon. Fainali hizi zitafanyika kufanyika kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017.
TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust (DTB).
Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.
TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi.
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz, kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.
Aidha wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao siku hiyo ya Ijumaa.
TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Serengeti Boys
MAJALIWA:MABALOZI WA TANZANIA TANGAZENI VIVUTIO VYA UWEKEZAJI NA UTALII

MAJALIWA:MABALOZI WA TANZANIA TANGAZENI VIVUTIO VYA UWEKEZAJI NA UTALII

April 23, 2017
KASSIM-MAJALIWA
Waziri mkuu Kassim Moajaliwa amekutana na mabalozi wa Tanzania wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki kati ya nchi  wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania kiuchumi,ikiwa ni pamoja na kueleza fursa za uwekezaji na utalii  zilizopo nchini.
Mabalozi wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kuwakilisha  Tanzania nnje ya Nchi,wamefika ofisi ya waziri mkuu mjini Dodoma kwa lengo la kumuaga na kwenda kuanza majumukumu yao katika nchi walizopangiwa.
Waziri mkuu amewaleeza mabalozi hao kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji Na jukumu lao  la kwanza la  Mabalozi hao  ni kuvitangaza vivutio vilivyopo ili kuleta wawekezaji wengi TANZANIA .
Suala la ushirikishwaji sekta binafsi pia waziri mkuu amesema Tanzania imelipa kipaumbele
Waziri Mkuu alizungumzia sula la watanzania waishio nje ya nchi , aliwataka Mabalozi kuwakutanisha na kufanya nao mikutano mara kwa mara ilikujua kama wanamatatizo yanayoyapata katika nchi wanazoishi ilikuangalia jinsi gani wanaweza kusaidiwa,
Mabalozi hawa wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi za QATAR,UBELIGIJI,AFRIKA KUSINI,UJERUMANI,COMORO,ALGERIA,INDIA NA ,SUDAN.
WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MAELEZOTV

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MAELEZOTV

April 23, 2017
mae1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.Televisheni iyo itaonyesha kazi mbalimbali za Wizara,Taasisi na Idara za Serikali.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Anastazia Wambura.
mae2
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas wakifurahi mara baada ya kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.
mae3
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Harrison  Mwakyembe akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo(Hawapo Pichani) na kuipongeza Idara ya habari kwa kuwa wabunifu.Kulia kwake ni Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas.
mae4
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akiangalia mahojiano yaliyofanyika kati ya Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo Hassan Abbas na Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassan Suluhu kuhusu maadhimisho ya Muungano yatakayofanyika mjini Dodoma.Mahojiano hayo ni ya kwanza kupitia televisheni ya mtandaoni ya Idara ya habari-MAELEZO.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.
……………………………………………………………………..
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza Idara ya Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa  katika kuitangaza Serikali.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.
“Napenda nichukue fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara hii  kwa mara ya kwanza katika historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na” Alisema Waziri Mwakyembe.
Amesema kuwa kwa kazi ya kwanza ambayo imeonekana katika televisheni hiyo imeonyesha weledi wa hali ya juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara hiyo kuiga mfano mzuri na kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina vipaji na ubunifu wa hali ya juu ikiwemo timu yetu ya Vijana ya Serengeti Boys na n.k
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,amesema  kuanzishwa kwa televisheni hii ya mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko mbalimbali na uzinduzi wake wa mapema utasaidia kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii husika.
“Sisi kama Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake”,Aliongeza Dkt Abbas.
Mbali na hayo amesema kuwa kipindi cha kwanza kabisa kuwekwa katika televisheni hii itakuwa mahojiano ya maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya muungano  waliyofanya na Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Hassan Suluhu.

WILAYA YA HANDENI YAZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

April 23, 2017

Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa wanawake wa Wilaya ya Handeni  kwenye ukumbi wa maount Ilulu uliopo Kabuku mjini lenye ujumbe wa “Wezesha wanawake kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda”.
Jukwaa hili linalengo la kuwakutanisha wanawake pamoja na kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli nyingine za kiuchumi katika Wilaya ya Handeni.
 Akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni  Bw. John Mahali aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alisema kuwa jukwaa la wanawake hilo  litasaidia  kuongeza uelewa kwa wanawake katika upatikanaji  wa mitaji , sheria za nchi katika masuala ya kiuchumi na jinsi ya kujitegemea.
Aliongeza kuwa wanawake wamekuwa hawapati fursa za kutosha za kiuchumi hapa Nchini hata na duniani kote kutokana na kutokuwa na usawa katika fursa , uwezo wa kupata mitaji.
“jukwaaa litasaidia kuondoa matabaka na sheri ambazo zitasaidia kupunguza ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake, ambalo ni jambo la muhimu sana katika kuleta maendeleo ya usawa katika pato la Taifa, jamii na familia” alisema Bw. John.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe alisema kuwa  jukwaa hili litafanya kazi ya kutambua shughuli za kijasiliamari katika kutoa elimu kuhusu upatikanaji wa mitaji, kusajili biashara, kuwezesha kiuchumi na kutafuta masoko.
Aidha, alisema katika suala la utoaji mikopo vikundi vitakavyopewa kipaumbele ni vile viliyojidhatiti kwa kusajiliwa, vyenye utawala unaoeleweka, miradi inayoonekana na zenye hesabu za kifedha zinazoweza kukaguliwa na kukosolewa inapobidi.
Uzinduzi huo ulipambwa na maonesho ya bidhaa za kijasiliamari ya vikundi mbalimbali kutoka kata mbalimbali. Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga itaratibu shughuli zote za uchumi kwenye Wilaya zote ndani ya Mkoa na kuhakikisha kunakuwa na majukwaa ya Wilaya/Halmashauri zote ambayo yatafanya  vikao vyake kila baada ya miezi sita (6).
  
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw William Makufwe wakwanza kulia akifuatiwa na Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali wakitazama Moja ya bidhaa ya vikapu vinavyotengenezwa na kikundi cha wanawake tupendane cha segera
 Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali akizungumza na wanawake waiojitokeza kwenye Uzinduzi wa jukwaa Hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe akionesha katiba waliyopewa viongozi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya itakayowasaidia Katika Uongozi wao
 Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akipokea katiba kutoka Kwa mgeni rasmi Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali.
 Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akishukuru wanawake waliompa dhamana ya kuwaongoza.
 Baadhi ya vikundi vya wanawake waliojitokeza kuonesha bidhaa zao wakati wa Uzinduzi.
 Baadhi ya wanawake wakishiriki wa Uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya  ya Handeni
Viongozi wakipata maelezo kutoka vikundi vya kinamama.

TAMISEMI YABARIKI MICHUANO YA COPA UMISSETA 2017 – COCA-COLA KUENDELEA NA UDHAMINI KAMA KAWA

April 23, 2017
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na SerikalizaMitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa mishindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bw Yusuf Singo akizungumza na washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa wamishindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni yavinywajibaridiya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo. Katikati ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoana SerikalizaMitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akiwa pamoja na Afisa Msimamizi wa Copa Cola-Cola, Pamela Lugenge (kushoto). Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.
Afisa Msimamizi wa Copa Cola-Cola, Pamela Lugenge (kushoto) akizungumza na washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo. Katikati ni Naibu Waziri wa Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bw Yusuf Singo (kulia). Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akiteta na viongozi mara baada ya kumalizika kwa semina.
Meza kuu.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''