NAIBU WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA WATAALAMU WA UGAVI JIJINI ARUSHA

December 02, 2014

Mwandishi wetu,Arusha

WIZARA ya Fedha, imeitaka Bodi ya Wataalam wa Ugavi na Manunuzi nchni  (PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia thamani halisi ya fedha na kuwataka waajiri kuacha mara moja kuwaajiri watu wasio na sifa kufanya kazi hizo

Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua mkutano wa tano wa mwaka wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la Mikutano la AICC jijini Arusha ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao.

Amesema katika bajeti ya mwaka 2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni 20 kati ya hizo asilimia 65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee katika kudhibiti mapato ya serikali yasitumike vibaya.

Awali Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya mkutano huo “Thamani halisi ya fedha za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha serikali inapata huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua uchumi wa nchi.

Amesema Bodi hiyo imezalisha wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali ambayo ni sawa na asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri watumishi wasiosajiliwa na Bodi hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa Siku mbili unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC, jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa Siku mbili wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)  unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC jijini Arusha.
Baadhi ya Maafisa Ugavi na Ununuzi wakisoma nyaraka mbalimbali za mkutano huo leo jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Clemence Tesha(kulia)akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima kwa hotuba nzuri.
Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wazi wa Fedha
 Air Seychelles yazindua safari za ndege Mahe – Dar es Salaam

Air Seychelles yazindua safari za ndege Mahe – Dar es Salaam

December 02, 2014
unnamed
unnamed1
Shirika la Ndege la Taifa la Shelisheli, Air Seychelles limeanza kufanya safari zake kati ya mji mkuu wa nchi hiyo, Mahe na Dar es Salaam ambapo leo, Desemba 2, 2014, ndege yake ya abiria HM 777 ilifanya safari yake ya kwanza ya uzinduzi kwa kutua Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Ujio wa shirika hilo la ndege unafanya mashirika ya ndege yaliyoanzisha safari zake kuja Dar es Salaam kwa siku za hivi karibuni kufikia matatu, Air Seychelles, Flydubai ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Rwandair ya Rwanda. Shirika lingine la ndege, Etihad la Abudhabi (UAE) linatarajiwa kuanza safari zake mwaka 2015.
Uzinduzi wa safari za ndege ya Air Seych elles ulifanywa na Naibu Waziri
RAIS KIKWETE AMUAPISHA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI LEO IKULU

RAIS KIKWETE AMUAPISHA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI LEO IKULU

December 02, 2014

Rais Jakaya Mrisho kikwete akimuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam
  leo ni Disemba 2 2014
unnamed1 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akimuangalia Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad akiweka sahihi yake
kwenye nyaraka baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo ni Disemba 2, 2014 unnamed2 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akitia sahihi yake kwenye nyaraka
baada ya kumuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa
Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo ni Disemba 2, 2014
unnamed4 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akimkabidhi vitendea kazi baada ya
kumuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Musa
Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo ni Disemba 2, 2014 unnamed5 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad baada ya kumuapisha  Ikulu
jijini Dar es salaam leo ni Disemba 2, 2014
unnamed6 
Rais Jakaya Mrisho kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib
Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande
Othman, Spika Anne makinda na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad
Ikulu jijini Dar es salaam leo ni Disemba 22, 2014 unnamed7 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na familia ya  Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini
Dar es salaam leo ni Disemba 2, 2014 unnamed8 
R
ais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na CAG Mstaafu Bw. Ludovick
Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo ni Disemba 2, 2014
unnamed10 
Rais Jakaya Mrisho kikwete katika picha ya pamoja na Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na
wafanyakazi wa ofisi ya CAG  Ikulu jijini Dar es salaam leo ni Disemba 2, 2014
PICHA NA IKULU

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF

December 02, 2014
MIKOA MITANO YATAKIWA KUWASILISHA USAJILI COPA 2014
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitaka mikoa mitano kuwasilisha usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu.

Mikoa hiyo ambayo haijawasilisha usajili wake hadi sasa kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza Desemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni Arusha, Dodoma, Katavi, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Mjini Magharibi na Simiyu.

Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya michuano hiyo, mkoa ambao hautawasilisha usajili wake kwa ajili ya uhakiki wa umri wa wachezaji utakaonza Desemba 10 mwaka huu utaondolewa katika fainali hizo zitakazomalizika Desemba 20 mwaka huu.

Wachezaji watakaobainika kuzidi umri hawataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya michuano kuhusu idadi ya wachezaji, kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 20 na wasiopungua 16.

Hivyo, kila timu inatakiwa kuhakikisha inakuwa na idadi hiyo ya wachezaji, kwani kikanuni wakipungua 16 itaondolewa kwenye mashindano.

Timu 16 kwa upande wa wavulana zitashiriki katika fainali hizo wakati kwa upande wa wasichana ni timu nane. Mikoa iliyoingiza timu za wasichana kwenye fainali hizo ni Arusha, Dodoma, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Mwanza, Temeke na Zanzibar.

MANDAWA MCHEZAJI BORA WA VPL NOVEMBA
Mshambuliaji wa timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja.
Mandawa ambaye kwa mwezi huo alichuana kwa karibu na mshambuliaji Fulgence Maganda wa Mgambo Shooting ya Tanga na nahodha wa Simba, Joseph Owino atakabidhiwa zawadi yake na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.

Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo inatarajiwa kufanyika wakati wa mechi ya raundi ya nane ya ligi hiyo kati ya Simba na Kagera Sugar itakayochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KOZI YA UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA SASA MACHI
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limesogeza mbele kozi ya ukufunzi ya utawala wa mpira wa miguu iliyokuwa ifanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa FIFA, kozi hiyo sasa itafanyika Machi mwakani katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

TFF imepokea maombi ya zaidi ya washiriki 40 kwa ajili ya kozi hiyo itakayoshirikisha washiriki 30. Kutokana na maombi kuzidi idadi ya nafasi zilizopo, FIFA itafanya mchujo wa washiriki.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

 MKUTANO KATI YA DR. SHEIN NA MABALOZI WETE KISIWANI PEMBA JANA

MKUTANO KATI YA DR. SHEIN NA MABALOZI WETE KISIWANI PEMBA JANA

December 02, 2014
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Map[induzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi alipofika katika Viwanja vya Jamhuri  Holl  kuzungumza nan a Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika mkutano  wa kuimarisha  Chama  cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Wete  leo Mkoa wa Kaskazini Pemba.[Picha na Ikulu.] unnamed1 
BAADHI ya WanaCCM  wa Wilaya ya Wete Pemba wakimkaribisha   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipofika kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa  Maskani  wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba katka ukumbi wa Jamhuri akiwa katika ziara za kuimarisha Chama .[Picha na Ikulu.] unnamed2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akitia saini kitabu cha wageni alipofika katika ukumbi wa Jamhuri Wete  kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara za Kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba leo .[Picha na Ikulu.] unnamed3 
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Wilaya ya Wete wakifuatilia kwa makini taraatibu za Mkutano huo uliofanyika leo katik na a Ukumbi wa Jamhuri  ikiwa ni katika kuimarisha Chama ,[Picha na Ikulu.] unnamed5 
BAADHI ya WanaCCM  wa Wilaya ya Wete Pemba wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa  Maskani  wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba katka ukumbi wa Jamhuri akiwa katika ziara za kuimarisha Chama .[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea Utenzi  baada ya kusomwa  na Asha Msanif wakati wa  Mkutano wa kuimarisha Chama alioufanya leo kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya  Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.[Picha na Ikulu.] Kaskazini Pemba.[Picha na Ikulu.] unnamed8 

TMF YAFADHILI WANAHABARI TISA KWENDA ACCRA NCHINI GHANA KUPATA MAFUNZO

December 02, 2014
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)
 Mkufunzi wa Masuala ya Biashara za Habari kutoka Accra Ghana,  Nuamah Eshun (katikati), akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanahabari hao Dar es Salaam leo asubuhi, kabla ya kuondoka  kwenda nchini humo kwa mafunzo hayo ya siku 10. Eshun atakuwa ni mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Misaada wa TMF, Alex Kanyambo na  Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.
 Baadhi ya wanahabari waliopo katika safari hiyo ya mafunzo.
 Wanahabari hao wanaosafiri wakimsikiliza Mkufunzi wa Masuala ya Biashara za Habari kutoka Ghana,  Nuamah Eshun.
Wanahabari hao wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya 
kuanza kwa safari hiyo.
Wanahabari hao wakienda kupanda gari, tayari kwa safari ya kwenda Accra nchini Ghana kwa mafunzo ya siku 10 kwa ufadhili wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF).
 
Dotto Mwaibale
MFUKO wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), umewafadhili wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini kwenda Accra nchini Ghana kupata mafunzo. Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo katika maeneo ya utawala na uongozi, biashara, masoko na kuboresha maudhui katika vipindi vyao kama namna ya kuchochea mabadiliko ya kimfumo katika vyombo vyao.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanahabari hao wapatao 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TMF Upanga Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TMF, Ernest Sungura alisema TMF imekuwa ikiwawezesha wanahabari kupata mafunzo ya aina mbalimbali ndani nan je ya nchi.
Alisema wanahabari hao wanakwenda nchini humo ambapo watapata mafunzo kwa siku 10 kuanzia Disemba 2 hadi 13 mwaka huu.
“Waliochaguliwa kwenda kupata mafunzo hayo ni baadhi ya wakuu wa vitengo kutoka vyombo vya habari, mameneja, wamiliki wa vyombo vya habari na maofisa masoko na mauzo na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio” alisema Sungura.
Aliongeza kuwa tangu mwaka 2008 TMF imeweza kufadhili vyombo zaidi ya 120 na wanahabari zaidi ya 500 kupitia aina ya ruzuku mbalimbali. Kati ya vyombo 120 vilivyofadhiliwa na TMF, 31 vimepewa ruzuku inayolenga kuimarisha utendaji wao katika masuala ya utawala na uongozi, biashara, masoko na kuboresha maudhui katika vipindi mbalimbali.
Alisema katika safari hiyo vituo vya redio vitano vimebahatika kuchaguliwa ambavyo ni CG Fm (Tabora), Standard FM (Singida), Kahama FM (Kahama), Triple A FM (Arusha) na Jogoo FM (Songea)-(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)

DR.SHEIN NINAAMINI TUME YA UTUMISHI SERIKALI ITATEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA MUJIBU WA SHERIA.

December 02, 2014
Masanja Mabula -Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema anaamini kuwa Tume ya Utumishi Serikalini inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kama kuna malalamiko dhidi yake Serikali itafuatilia.

Akizungumza na viongozi wa mashina na wenyeviti wa maskani wa wilaya ya Wete , Dk. Shein alisema kuwa kuanzishwa kwa Tume ya Utumishi ni sehemu ya utekelezaji ahadi ya Chama cha Mapinduzi ya kuimarisha utawala bora.

“Ni ahadi ambayo tuliiweka hivyo tulipounda serikali tulilazimika kuunda Wizara hii kubwa na taasisi zake ambazo zinatekeleza suala hilo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa”, Dk. Shein alieleza.

Alisema yeye binafsi haamini kuwa Tume za utumishi zinapendelea bali zinatekeleza sheria ya utumishi wa umma ambayo wananchi wengi hivi sasa hawajaielewa vyema.

“Kuundwa kwa Taasisi hizi isiwe tatizo kwetu, haya ni mambo yetu wenyewe tuliyoyaanzisha kwa mujibu wa Katiba yetu na kama kuna watendaji hawatekelezi majukumu yao ipasavyo ni wajibu wetu kuwawajibisha” Dk. Shein alisema

Katika mkutano huo baadhi ya viongozi walilalamikia mfumo wa ajira serikalini hivi sasa kwa madai kuwa kuna upendeleo.

Wakati huo huo Dk. Shein aliwataka viongozi hao kutokuwa na wasi wasi kuhusiana na suala la amani na utulivu katika uchaguzi mkuu ujao, akiwahakikishia kuwa huu si wakati tena wa kutishana na wasibabaishwe na watu waliozea kuwatisha wananchi hasa wakati wa uchaguzi.

“msiwe na wasiwasi, tutaweka ulinzi wa kutosha wakati wa uchaguzi, wakati wa kutishana ulikomeshwa na Mapinduzi ya mwaka 1964” na kuwataka wananchi wasikubali kutishwa kwa kuwa watu hao “hawana mamlaka ya kufanya hivyo” Dk. Shein alieleza.

Aliongeza kuwa hivi sasa nchi inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwamba hakuna mwananchi aliye juu ya sheria hivyo kila mmoja anapaswa kufuata sheria na kinyume chake sheria zitafuata mkondo wake

Alirejea ahadi ya serikali ya kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao utakuwa wa haki na huru na kwamba uimarishaji wa ulinzi na usalama ni sehemu ya maandalizi hayo.

Alisema wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Jeshi la Polisi imebuni sera ya ulinzi shirikishi na kupata mafanikio makubwa katika suala zima la ulinzi wa usalama wa raia na mali zao, viongozi hao wa CCM nao wanaweza kubuni mbinu zitakazosaidia ulinzi ndani ya chama hicho dhidi ya watu wasiopendelea maendeleo yake.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri  mjini Wete, Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwataka wana CCM kuendeleza kasi ya kuimarisha chama chao ili kuwahakikishia ushindi katika uchaguzi ujao.

“Tuendelee kujiimarisha ili kuendeleza historia ya chama chetu ya kushinda kila uchaguzi ” Dk. Shein alisisitiza.

Mapema akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa alisifu utekelezaji wa Ilani katika mkoa huo na kueleza kuwa matokeo ya utekelezaji huo umeleta mabadiliko katika maisha ya kila siku ya wananchi.

“Ujenzi wa barabara mbalimbali katika mkoa wetu umeleta mabadiliko katika hali za maisha ya wananchi ikiwemo makaazi kwa wananchi kuhamaiska kujenga nyumba bora” Mzee Mberwa alieleza

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai aliwaeleza viongozi hao kuendelea kuelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa kama vile suala la Katiba inayopendekezwa

Alisema upinzani walitaka Katiba ambayo itavunja  muungano badala ya kuimarisha na ndio maana wamekuwa wakitumia muda mwingi kupotosha wananchi kwa mambo yasiyo ya msingi.

 Dk. Shein anatarajiwa kuendelea na ziara yake hiyo ya kichama kesho kwa kuzungumza na viongozi wa chama hicho katika wilaya ya Micheweni.