Msafara
wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukipokelewa kwa farasi
wakati alipowasili katika kijiji cha Mikocheni TPC wakati alipoanza
ziara yake ya kukagua na kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM katika jimbo
la Moshi Vijijini akitokea jimbo la hai ambapo alimaliza ziara kama
hiyo jana, Kinana akiwa katika jimbo la Moshi vijijini atashiriki
shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na wananchi na kuhimiza uhai wa
Chama Cha Mapinduzi CCM jimboni humo akiongozana na Nape Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MOSHI VIJIJINI- KILIMANJARO)
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana
na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika kijiji cha Mikocheni
TPC, Kulia ni Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Mh. Dk Cyril Chami.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisalimiana na Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Kilimanjaro Mh. Betty Machangu.
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Mh. Cyril Chami kulia wakati alipowasili katika kijiji cha Mikochenzi.
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na wananchi mara baada ya kupokelewa.
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea eneo la mkutano ambapo amezunguza na wananchi baada ya mapokezi.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Mh. Dr. Cyril Chami akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mikocheni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mgorole kama ishara ya heshima ya wazee wa Kijiji cha Mikocheni wa jamii ya kimasai.
Ktibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi waliofurika kumpokea katika kijiji cha Mikocheni jimbo la Moshi Vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aki
akiwasili katika ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya
kushiriki mkutano wa wajumbe wa halmashauri kuu ya Moshi vijijini, kulia
ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na kushoto ni Iddi Juma
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro.